Pages

Sunday, January 13, 2019


UNABII WA NCHI YA TANZANIA 2019.
MAMBO YATAYOENDA KUFANYIKA KWA NCHI YA TANZANIA KWA WANANCHI WAKE.

BWANA YESU ASIFIWE Watanzania na watu wote wa mataifa yote katika nchi hii aliyoiumba MUNGU mwenyewe na aliyeniita kutoka katika nchi hii, nchi hii MUNGU anaiita EDENI yake ya sasa tokea aliponiita alinieleza mpango wake kuhusu nchi hii na nimeshaelezea katika blog na YouTube, TV na redio mbali mbali. Vitu vilivyokuwa vimekufa atavifufua na ameshafanya ikianzia na ndege, shule (wanafunzi kusoma bure), madini kurejeshwa kwa Watanzania, kuweka rais 2015 aliyemchagua yeye na amefanya na mengine mengi.

Tarehe 11.01.2019 MUNGU aliniambia kuhusu umeme katika nchi hii utakuwa ni bure kwa wananchi wale ambao wapo katika nyumba zao ila watakao lipa ni viwandani, umeme unaotumika katika sehemu za biashara yeyote ile hautakuwa ni wa bure MUNGU atafanya njia hivyo msishangae mrudishieni MUNGU utukufu. Tarehe 13.01.2019 nilipokuwa nakaribia kusimama kuanza kuhubiri kanisani akaniambia “Hebron Nabii wangu usifanye jambo lolote bila mimi kukujulisha, mengine useme na mengine ni siri yako wewe kama wewe, hii ni Edeni yangu, nataka mataifa yote waje wanijue mimi na kuniabudu, mwanangu YESU karibia anarudi sasa kwa unyakuo kuanzia tarehe hii nimeshasema na ndivyo ilivyo. Katika shule zote nchini Tanzania pamoja na Zanzibar watakuwa wanapelekwa mashuleni na mabasi pamoja na kurudishwa nyumbani kwao itaanzia primary mpaka sekondari kwa wale wanaoenda kusoma na kurudi yaani (day school) na itakuwa ni bure, mimi MUNGU ndiye ninayeyafanya hayo yote kwa utukufu wangu.”

“Na pia kuhusu maji yatatolewa bure kwa kila mwananchi isipokuwa katika sehemu za biashara au wanaonyeshea hao watalipia, watu wasijiulize itakuwaje mimi ni MUNGU nisiyeshindwa njia zangu hazichunguziki mimi ndiye ninaye jua nguzo za kushikilia dunia zilipo hili ni jambo dogo kwangu. Hebron yote niliyokueleza kuhusu nchi hii yametimia” (yapo katika blog ya Prophet Hebron- www.prophethebron.or.tz) uaangalie unabii wa Tanzania kuanzia miaka mitano, wengine miaka tisa mpaka sasa. Na bado ataendelea hatua kwa hatua kwa utukufu wake, maneno haya ni ya MUNGU na siyo ya kinywa cha Nabii Hebron, mimi ni chombo cha kuyafikisha duniani na yamefika, hivyo hivyo ni neema nyingine kwa Watanzania, MUNGU anafanya sasa kwa utukufu wake kila eneo siku baada ya siku. Haya ni machache nitaendelea kuyaleta kwenu kila anaponieleza kwa utukufu wake.

MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU uokoe watu wote kwa utukufu wako.

PROPHET HEBRON.