MERRY CHRISTMAS 2018 AND HAPPY NEW YEAR 2019
Ni siku ya furaha Mbinguni na
duniani ya kukumbuka kuzaliwa kwake BABA yetu mpendwa YESU wa Nazareti mwokozi
wetu na rafiki yetu. Siku hii ndiyo chanzo cha wokovu kwa watu wote, kwa wale
ambao watampokea katika mioyo yao na kuokoka, watakao okoka na kufanyika kuwa wana
wa MUNGU.
Mjiandae katika mioyo yenu
kiimani na kimatendo kwa kuokoka na kumkiri Yeye kwamba ni BWANA NA MWOKOZI wa
maisha yako na uzidi kuishi milele katika utakatifu na siyo katika dhambi. Kwa wale
mliopokea neema ya wokovu mzidi kubarikiwa na kwa wale ambao bado hamjaokoka
ukoka sasa kwa sababu ukristo bila kuokoka ni kazi bure. Ili uende Mbinguni
atakachokiangalia ni kama umepokea wokovu wake tu, yaani Yeye YESU.
Mbinguni watu hawaendi kwa kuitwa
wakristo, Mbinguni watu watakao kwenda ni wale waliookoka tu, haijalishi utaisherekea
siku hii ya mfalme vipi ila kama haujaokoka bado utakuwa ni msindikizaji wa
wale watakao kwenda Mbinguni. Hivyo nawasihi mataifa yote kwa wewe ambaye bado
haujaokoka kuitumia fulsa hii kuokoka. Najua mataifa mengi wanajiandaa kimwili
kula na kunywa na kupumzika au kusafiri kwenda sehemu mbali mbali, hii
inapendeza sana ila itapendeza zaidi kwako na kwa YESU na pia Mbinguni kama
ungechanganya na kuokoka kwa sababu unakuwa unasheherekea wewe ukishirikiana na
Mbinguni na utapokea baraka zake YESU. Cha kujifunza hapa, hii inatokana na baadhi
ya watu kutokujua ukweli na kutohubiriwa injili ya kweli inavyotakiwa. Watu
wakazuiwa kuokoka wabakie kuitwa wakristo tu. Nataka muelewe hata Mfalme YESU
akisema anakuja, atawapoteza wengi na ndivyo ilivyo sasa, wakristo wengi zaidi
hawajui ukweli wanampenda YESU bila matendo, tendo ambalo wanaliogopa ni
kuokoka, wamepoozwa na kuridhika kuitwa mkristo tu. Kama vile mpinga kristo,
yeye haokoki wala haokoi. Sasa ni miaka 2018 imepita tokea kuzaliwa kwake Mfalme
ili wewe uokoke na usichomwe jehanamu. Yakupasa sasa uokoke ili siku hii iwe
imeleta ushindi wa milele kwako hapa duniani na siku moja ukashiriki ufalme wa
Mbinguni. Ila uking’ang’ania ukristo tu bila kuokoka utabakia hapo hapo, huo
ndio ukweli na Yeye anakuangalia wewe msomaji na mwanadamu, YESU anasema na
wewe kupitia ujumbe huu, nakusihi umpokee Yeye.
Pamoja na salamu za Christmas
nawatakia pia mwaka mpya mwema 2019, nitaendelea kuwaombea na mtavuka mwaka kwa
ushindi kwa kila atakayesoma ujumbe huu na mengine nikiendelea kuwaombea.
Msisahau huyu Mfalme YESU
anakuja muda wowote kuwachukua wale waliompokea yaani walio okoka. Mpe YESU
zawadi sasa, umkiri yeye, sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu,
uliandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele na uniokoe, mimi
ni mtoto wako sasa na hata milele. Amen.
Nawatakia Christmas njema.
Nawatakia heri ya mwaka mpya 2019, uwe
wa baraka kwako na ushindi mkubwa BWANA awe nanyi nyote. Amen.
PROPHET HEBRON WILSON KISAMO.