Pages

Saturday, November 10, 2018


NINI MAANA YA AAMINIYE NDIYE ATAOKOKA NA ASIYEAMINI ATAHUKUMIWA.


Marko 16:14-16
14Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. 15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.  16Aaminiye na kubatizwa ataokoka asiyeamini, atahukumiwa.”

BWANA YESU wa Nazareti asifiwe na azidi kutukuzwa juu sana huyu mwana wa MUNGU wa pekee mwenye upendo na utiifu kuanzia kwa BABA yake mbinguni YESU huyu ndiye aliyeteuliwa na MUNGU yeye afanyike njia na ukombozi wa kila mwanadamu yeyote yule anayetaka kwenda mbinguni na apone na aepuke jehanamu. Hakuna jina lolote la mtumishi yeyote au kiumbe chochote ambacho kimeteuliwa kwa ajili ya watu wote wa mataifa yote. Napenda kukumbusha ulimwengu wote na kwa mliojisahau na wengine kuona kuwa MUNGU hayupo wala huyu YESU hatakuja na wale wanaoamini uongo kuwa hamna mwisho wa dunia; siku chache zilizopita MUNGU akaniambia tena niwaeleze mataifa yote kuwa mwanae wakati wowote anarudi na atawachukua wale waliomwamini na kumkubali tu na atawachukua waliomkubali kiimani na kimatendo.

Nitaelezea sasa kwa ufupi kuhusu maana ya waraka huu na hapa najua mabilioni ya watu hata na wakristo baadhi wanapigwa upofu wanasema na hawaelewi, japo wapo wanaoelewa ila wameamua kuwadanganya wanadamu ili wasije wakafikia ahadi ya MUNGU ya uzima wa milele na badala yake hata sasa wakristo wengi wamepoteza mwelekeo na safari ya mbinguni na wanabakia hawana direction ya mpinga kristo kwa kufuata uongo na kwenda kinyume na neno la MUNGU na wengine hata baadhi yao wanachanganya neno la MUNGU na uongo wakati MUNGU hana ushirika na uongo soma Ufunuo 22: 18-19. 

Ukisoma Marko 16:16 hapo pamebadilishwa kwa kiasi kikubwa neno la MUNGU limegeuzwa na kama limegeuzwa na hao waliogeuza basi maana yake ni nini? Maana yake kwa anayeligeuza na kulipokea pasipokujua au kwa kujua na yeye anakuwa amemgeuza MUNGU akamfuata mwingine. Utasema ni kivipi mtu amemgeuza MUNGU? Katika ubatizo kuna maelekezo ya tendo la ubatizo atakavyo MUNGU na siyo atakavyo ndugu yako, wala dunia, wala dhahabu wala mtumishi yeyote yule wala kiumbe chochote kile. Hapa amri ni neno lifanyike kama anavyotaka MUNGU na siyo mtu yeyote yule, kwanza anapofuata tofauti anakuwa anayo dhambi na zaidi ataipata laana ya milele la kulitengua neno la MUNGU.

Mimi Hebron  sipunguzi chochote kuhusu ujumbe huu, mpone na muelewe hata mnaoficha kweli kuhusu ubatizo. MUNGU anazo njia nyingi usizozijua, hata mawe ni watumishi wake yatahubiri na watu wataokolewa tu, ndivyo alivyonieleza. Shetani aliringa muda mrefu kwa kulidanganya kanisa sasa ni wakati wa MUNGU kufichua siri alizozifunga shetani kuanzia kwenye biblia.

JAMBO LA KUJIULIZA

Fomula ya ubatizo MUNGU anasema uamini kwanza! Umwamini YESU uokoke halafu ndio ukabatizwe. Hivi mbona shetani amedanganya hata wasomi baadhi yao wasielewe hii fomula. Najua unayo akili timamu mwana wa MUNGU, sasa swali je mtoto mchanga anayo akili na ufahamu na kumwamini YESU, jibu ni hana hata kumbukumbu, na je mbona biblia inasema mtu aamini mwenyewe? Sasa baba na mama wa ubatizo ndio wanasikiliza kwa ajili yake na jiulize tokea Yohana aje kubatizwa mpaka YESU kabatizwa je alishatokea wa baba na mama wa ubatizo? Mimi mwenyewe Hebron nilishakua baba wa ubatizo wa baadhi ya waumini wa kikristo, nimetubu, sikujua ila nilipotoshwa, labda na wewe umetumika kwa kujua na kutokujua sasa ili usiachwe tubu sababu na wewe mbele za MUNGU unakuwa unashtakiwa kuwa ni kati ya mmoja wapo anayelibadilisha neno  la MUNGU na adhabu yake ni hukumu ya milele. 

Zaidi mtoto anapobatizwa akiwa hajaamini wala hajui chochote, katika ulimwengu wa roho amechukuliwa na mpinga kristo na kufanyika kuwa mwanafunzi wa mpinga kristo bila kujua au kwa kujua na ndio sababu utaona wahubiri wengi sasa hivi wanahubiri habari za wokovu kwa wakristo huyo huyo ili akiri mwenyewe halafu ndio akabatizwe sababu bado mpaka sasa hajamwamini YESU ndio sababu hajaokoka na imani pasipo matendo imekufa hivyo nawasihi kama MUNGU aishivyo na atakayo kwa kila mwanadamu aamini sasa kama bado alibatizwa akiwa mtoto mdogo hajielewi mpaka sasa bado hujaamini haijalishi utakuwa na moyo mgumu lakini ukweli ndio huo wala hautabadilika.

MUNGU anajua watu wengi wanampenda ila wametokea wakristo wa uongo, uelewe hata injili ya mapokeo ya wanadamu na watu wengi pasipokujua wakaiamini na kuikubali na wakaikataa injili ya kweli. Jambo lingine neno “ubatizo”  maana yake ni kuzamishwa, sasa maji yanayomwagiwa kichwani hivi umezamishwa au umewekewa matone ya maji? Mbona mataifa hamjui huu uongo na muupinge? Sasa matokeo yake YESU mwana wa pekee hana wafuasi wengi japo kimwili wakristo au wanafunzi wake kwa wanoitwa kwa jina lake wanaonekana ni wengi machoni pa watu na kumbe bado hawajamwamini mpaka sasa na wengi hawajui na ndio sababu YESU alisema wengi watalia ile siku ya mwisho na yeye atawaambia sikujui sikujui. 

Ewe mtu wa MUNGU, unayependwa sana na MUNGU mrejee yeye uokoke, hatua ya kwanza na ubatizwe kwa maji mengi yanayotembea, yasiwe ya kisima, wala drum, wala baharini, bado huo ubatizo una dosari na shetani atajiingiza na kushiriki tena katika ubatizo huo tena na mbele za MUNGU bado utaonekana umepinga sheria yake. Hata usikubali kubatizwa kwa jina la mchungaji bado utakuwa siyo mfuasi wa YESU, watu wote nawasihi kwa upendo wa kweli kutoka kwa MUNGU chunguza huu ujumbe utapata jibu la kweli na wengine mmeshuhudiwa na roho wa MUNGU mnabakia na mioyo migumu japo nafsi yako imejua ukweli hivyo.

Nafsi ina nguvu sababu ina agano la mpinga kristo, sasa wewe amini uokoke, ubatizwe na shetani atakuachia, anaushika nafsi yako sababu anaouhalali ulikubali mwenyewe na wapo waliokulelea kuupokea ubatizo au kiapo cha uongo haijalishi likatajwa jina la YESU na roho mtakatifu na haya ndiyo maneno ya kulichanganya neno la MUNGU na uongo na siyo ajabu unajiandaa kumpeleka mtoto akashiriki kuchanganya neno la MUNGU na uongo. Hapo ni lazima ulaaniwe na MUNGU ukivunja neno lake uelewe ipo laana inakufuata juu yako. Watu wote hiki ni kipindi cha neema na shetani anawapiga upofu wakristo ili wakahukumiwe ile siku ya mwisho pasipokujua. Amenituma Nabii wake niwaeleze na niwahubirie kweli yake, kuyafichua yaliyofichwa na shetani. Nakuombea MUNGU akufungue ufahamu atakavyo yeye usije ukahukumiwa.

Ili MUNGU afanye kazi anao watumishi wake na shetani ili afanye kazi  na yeye anao hivyo hivyo mfano Nabii, Mtume,  mchungaji, mwinjilisti, mwalimu, askofu hivyo hivyo, usipokuwa makini utapelekwa jehanamu na hawa watumishi wanaoligeuza au kulipindua neno la MUNGU wengine hawajui wanafundishwa huko college uongo na wanauendekeza sana ila hawajui wanafanya kazi gani. Ulimwengu utaokoka na watu wengi zaidi muda siyo mrefu na waislam wengi sana wataokoka na wataingia mbinguni wakimfuata Nabii Issa.

Tubuni BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, nakuamini wewe ndiwe bwana na mwokozi wa maisha yangu. Amen.

ANGALIZO:
Soma mafundisho mapema ya ubatizo na upate kitabu cha “Ubatizo wa kweli kwa ulimwengu wote” cha Nabii Hebron yapo mengi utaelewa zaidi. Ubarikiwe. Watu wengi hawajaamini, kiri wokovu kwanza

PROPHET HEBRON.