Pages

Thursday, April 11, 2019


MBINU ALIZOTUACHIA YESU TUZIJUE ILI TUKIAMBIWA KRISTO YUPO HAPA AU KULE TUSISADIKI (USIENDE).

MATHAYO 24: 23-24, 26
Neno linasema:
23wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu: wapate kuwapoteza kama yamkini, hata walio wateule. 26Basi wakiwaambia, yuko jangwani, msitoke, yumo nyumbani, msisadiki.”

BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote na kwa kila anayependa kufika mbinguni siku moja akalakiwe na BWANA YESU mbinguni.  Napenda kufafanua au kuelimisha wafuasi wa YESU popote walipo kwa wanaoelewa maana ya neno hili na wasioelewa.  Kwa nini YESU alisema watakuja tokea manabii wa uongo na makristo wa uongo na watawapoteza watu wengi hata wateule yaani wale ambao tayari walishaiona nuru ya wokovu halafu wakachanganyika pasipokujua au kwa kujua wakaingia katika madhabahu au sehemu ya ibada au katika mikutano ya injili ambayo YESU hayupo.

Neno hilo limekuwa likitumiwa sana kuwazuia watu wasimfuate YESU na wakati hata mtu mahali alipo unakuta kabisa muumini anaona kwa macho ya nyama na rohoni kuwa anaposali hapana MUNGU anaenda tu basi ila siku akija YESU asiachwe na wakati cha kujiuliza hata hapo ambapo hayupo YESU wala siyo mahali pake unafikiri YESU atakuja hapo?   Jibu, hatakuja haijalishi linatajwa jina lake na ndio sababu anasema watakuja makristo yaani watumishi wa kikristo ambao wapo tofauti na yeye, hao ukiwafuata hautakutana na YESU bali utakutana na makristo na manabii wa uongo (kinywa kisemacho uongo au kinywa kinachotumiwa na baba wa uongo yaani shetani, sasa utalijuaje hilo?  Kinywa ni kupitia yale ayasemayo kimatendo au kulichanganya neno la MUNGU na uongo.

Mfano ambao YESU anapenda muelewe nyie mnaompenda maana yake ni hii. Na hata neno linasema kila anitafutaye kwa bidii ataniona, sasa ni ajabu unaona kabisa mahali ulipo labda YESU hayupo halafu unaridhika tu na kukaa hapo badala ya kuangalia sehemu nyingine au kumuomba MUNGU akufunulie mahali alipo YESU na akakuonyesha.  Maana yake ni hii kweli katika dunia hii kweli katika dunia hii kila sehemu utasikia anatajwa YESU yupo kila miji, barabara hata kwenye redio au runinga hata kwenye mitandao ya kijamii na matokeo yake YESU hayupo.  Nitaelezea kwa ufupi na mtaelewa sababu siku moja alinieleza YESU niwaeleze nchi zote ukweli watu wanijue mimi maana idadi kubwa wananipenda na katika hao wanaonipenda hawanijui na watakaponijua mimi YESU wataniona na nitawaokoa, nenda uwaeleze YESU anaposema ukiambiwa yupo hapo au yupo kule msisadiki, maana yake ni atatajwa YESU sana katika makanisa baadhi na akitajwa ina maana ni yeye anaabudiwa na kumbe yeye hayupo hapo kwa hiyo usiende, sasa utajuaje? Utachunguza mafundisho kama yapo kama alivyoagiza na ikiwa yanapunguzwa au kuongezwa hapo usiende wala usisadiki kabisa yaani usipaamini kabisa usiende.

Nitaelezea kwa mifano michache soma Ufunuo 22: 18-19. Aliposema maneno yasiongezwe ya kitabu hicho ina maana kuwa huko ndiko kuondolewa YESU mahali hapo pa kuabudiwa au kumfukuza YESU sababu yeye neno lake limepigwa muhuri na MUNGU  kuwa linafaa kwa kila kiumbe.

·        Aina za ubatizo uliotokea mbinguni alibatiza Yohana, alibatizwa YESU katika mto wenye maji yanayotembea ndio njia aliyotuonyesha YESU ila inahuzunisha sana hata YESU hana furaha kabisa akiangalia huku duniani jinsi watu wanaompenda walivyopotezwa na makristo ili wakachomwe moto, ila kipindi cha neema mrejee mpone mkabatizwe kama YESU na siyo kubatizwa kwa batizo za makristo na wewe utafanyika kuwa mtoto wa makristo na siyo wa YESU pasipokujua au kwa kujua.  Na hata hapa ulimwenguni mtu hutambulika kwa jina lake na kwa sura yake  hivyo hivyo na kiroho YESU hutambulika  kwa jina lake na kwa neno lake kama lilivyo na ikiwa ni jina linatajwa tu halafu sura yake imechanganywa na vitu vingine tayari amekuwa  sio yeye sababu yeye hachangamani na uongo,  giza, mapokeo ya wanadamu au manabii wa uongo au makristo bali yeye anajitegemea kama alivyo ndio sababu anaitwa mwana wa pekee.  Niwa kipekee kwa kila kitu ila baadhi ya watu wanamfanya aonekane siyo wa kipekee kwa kubadilisha ubatizo wa pekee ukawa wa kikombe, ukawa wa maji ya kisima, drum na kubatizwa kwa jina la mchungaji, hapo ndipo shetani alipowateka wanadamu na msifikirie sehemu kama hizo YESU yupo na ndizo sehemu ambazo tulizoambiwa msisadiki msiende huko, lakini imekuwa ni kinyume watu wengi zaidi ndio wapo huko na wanaona wapo na YESU yupo hapo na kumbe anasema usiende hapo kila sehemu yenye mafundisho ya uongo usiyafuate wala kukaa hapo.   Mahali  panapofanyika mambo kama hayo tayari  hapo panakuwa  ni ngome ya shetani, sababu MUNGU yeye ni wa haki na anakaa mahali penye vitu vyake, yeye habadiliki na ikiwa neno limebadilika basi uelewe mahali hapo ni kwa mungu anayebadilika ambaye ni miungu kwa majina yake. Kama nilivyoelezea huzuni ya YESU tokea akiniita 2009, ni kwa watumishi baadhi yao wanaomkataa YESU wameamua kumchagua shetani kama ndiyo baba yao wapo wanaojua kabisa mpaka kimwili kuwa baba yao ni shetani kabisa na wanamwita baba kabisa japo wanahubiri.  Hao ndio wale wakristo sugu na wapo wanafunzi wa makristo wengi wanafuata mkumbo wa uongo wakifikiri wapo na MUNGU na kumbe kuanzia kimwili na kiroho siyo watenda kazi wa YESU asiyebadilika bali ni watenda kazi wa yesu anayebadilika.

·        Mfano mwingine mnajua YESU alikataza watu wasichajiwe  pesa yoyote ili waombewe, sasa cha ajabu sehemu nyingi sana mpaka ni aibu na zinanuka harufu mbaya na anayetumia jina la YESU kuwadai watu pesa yaani ananuka milele mbele za MUNGU pia ni adui wa MUNGU, anapofanya hivyo anakuwa ni mtoto wa baba wa uongo (shetani).  Sasa hili siyo jambo geni siku nyingi dunia hii au kwenye nyumba za watu wanaofanya maombezi au semina au katika mikutano linapotajwa jina la YESU mtashangaa yanafanyika mambo aliyokataa na yakifanyika basi uelewe mwana wa pekee anakataliwa hapo soma Mathayo 22:29, Mathayo 15: 8-9, sehemu hizo ndizo unazoambiwa ni jangwani ukiambiwa yupo hapo usiende ila mahali alipo yeye nenda, YESU anasema mmepewa bure toa bure cha kujiuliza je YESU ni kigeugeu? Je neno na ahadi yake imebadilika?  Jibu hajabadilika.  Mwenye akili na afahamu na aelewe watu wote waseme Amen.

·        Runinga na redio nyingi ni za kulitumia jina la YESU kunyanganya watu mali zao, kuomba msaada au kulia shida za mafuta ya generator na gharama.  Napenda muelewe MUNGU yeye hana shida kama ni redio na runinga zenye baraka zake kweli atafungua njia na watu watafanya na watabarikiwa na siyo kwa kuomba watu pesa walipie gharama,  (neno linasema msijisumbue, naamini hivi runinga na redio za jinsi hiyo ni lazima zimeanzishwa na mtu, basi mtu huyo kama alipewa redio hiyo na MUNGU amrudie yeye na atafanya, ila napenda muelewe redio nyingi na runinga nyingi zaidi zinazolitaja jina la YESU ni za maagano ya shetani, ila watu wanafungwa macho na ufahamu waone ni kazi ya MUNGU na kutambua ni vigumu, ila ni mpaka uwe una neema ya MUNGU apende kukujulisha, na endapo utaisikiliza hata kama linatajwa jina la YESU na matendo ya unyang’anyi yakiendelea bado unatakiwa usikilize sababu shetani atakuwa amekufikia direct kwa njia ya sauti ya redio yake hivyo kama ni katika nyumba au gari lako shetani anakuwa amefika kabisa au freemason na kwa njia hiyo utaona unafifia kiroho ndio kufa kiroho, hauoni mabadiliko.  Hata vyombo vyenye kuhubiri na kuchaji watu pesa kwenye vyombo hivyo usisikilize.

·        Makanisa yanayofanyia siasa madhabahuni au wanasiasa kuja kanisani kuomba kura, hilo ni jambo baya.  Mwana siasa akija kanisani aombe MUNGU amwezeshe ushindi na siyo kufanya kanisa au nyumba ya ibada ni jangwani- mahali kama hapo usiende kabisa, kumbuka YESU aliingia kanisani alikataa nyumba ya BABA yake kuwa soko, leo imekuwa ni soko utasikia leo harambee, leo siku ya mnada wa mazao, huko ndipo anapoelezea YESU ukisikia yupo pale au kule wewe usiende, hata sasa YESU anasema na wewe usiende, unafunguliwa ufahamu zaidi.

·        Ili kumwona mtumishi unadaiwa kiasi fulani ili upate private ya kuonana na yeye, huko ndipo anaposema YESU usiende, usisadiki hayupo.

·        Kuandika majina sadaka na kupewa risiti, huko usiende hayupo, hizo sadaka zote haziendagi kwa MUNGU wala hazipokelewi sababu hazifuati mpango wa neno kama lilivyo, bali linafuata mapokeo ya wanadamu na kuwafanya hata watoe sadaka waonekane ni wanafiki mbele za MUNGU wakati wakijua wanamtolea MUNGU (soma Mathayo 15:8-9). Usitoe.

·        Hii dunia ni vizuri mnaompenda MUNGU na mlioujua ukweli mseme ukweli sababu baadhi ya watumishi sasa na makanisa imekuwa ni biashara na inapokuwa ni biashara YESU ndie sababu akasema huko usiende tulia hapo hapo, na ukiwa hapo uombe kwake umuulize wewe upo wapi, je upo kwa mtumishi gani au kanisa lipi yupo? Na pia muelewe YESU anakaa na mtumishi na endapo labda kanisa lina matawi 10,000 kwa kipindi hiki usishangae labda ni matawi 21 tu ndio YESU yupo na watumishi hao tu sasa 9,979 wapo na nani? Na jinsi alivyo kiongozi (mchungaji) ndivyo walivyo waumini- Hivyo basi utatakiwa utoke kwenye hao 9,979 uingie katika moja ya hayo 21 ukikutana na YESU na kutembea na yeye.

·        Wanapoabudu sanamu- usiabudu hapo usiende yeye anakataa na neno linakataza.

·        Usiabudu wafu- huko ndipo usiende wewe.

·        Makanisa yanayokopa benki ili kujenga kanisa au kutumia mikopo ya riba kujengea ufalme wa MUNGU,  MUNGU  yeye siyo maskini wala yeye siyo mnyang’anyi.  Anasema kwenye neno lake usichaji riba.  Riba mtu  anaposhindwa huwa anafilisiwa, na usishangae ukasikia kanisa au mradi wa kanisa unafilisiwa na benki, najua yameshafilisiwa na benki mengi tu katika dunia hii, sasa cha ajabu mjiulize je MUNGU ameishiwa mpaka akakopa wanadamu au benki halafu akashindwa kulipa, kwa hiyo MUNGU amekuwa anaonekana ni yeye anafilisika, namtetea YESU 100%, wakifilisiwa hata wakikopa mkopo hizo kazi wala majengo yanakuwa hayana kibali cha MUNGU bali ni kibali cha miungu na makristo na manabii wa uongo.  Ifike mahali sasa hata mabenki yajiulize je yanaweza mchaji MUNGU riba?  Au kumjadili MUNGU kwa njia ya kukopwa na kanisa?  Nitaelezea wakati mwingine, endelea kufuatilia makala haya ya Nabii Hebron, nitaendelea kuufichua huu uovu wote wa kumchezea YESU kila mtu aujue na wateule wapone sababu ukweli unaponya na uongo unaangamiza.

Biblia inasema kama wewe ni mtumishi wangu usijisumbue kwa lolote. Rudi kwangu MUNGU, omba, nitafanya.  Ila neno likasema tena maana ya (KAMA) hili neno lina maana mbili hivyo uelewe nyingine sio kama watumishi wa MUNGU na wengine ni kama watumishi wa MUNGU, mtumishi wa MUNGU siyo jina tu hata mahubiri yawe ni kweli na siyo mchanganyo ikiwa hivyo tayari unakuwa makristo au nabii wa uongo. Huko usiende ndio maana yake, lakini leo hii huko ndiko wengi walipo na ndipo biblia inasema ni kwenye mizoga.

·        Ilitokea habari ya kikombe hapa Tanzania na watu walienda maelfu kwenye mzoga wakachajiwa shilingi 500, jiulize wapi anasema YESU mchajiwe pesa kiasi fulani ndio mpewe dawa ya mizizi?  Jibu hakuna- kila aliekwenda alienda kwenye mzoga akala mzoga wa kiroho- ndio hao huko msiende mtanyanganywa na kufa kiroho hata kama ulikuwa mtu wa kwenda mbinguni, labda ukaombewe upya mahali alipo YESU akutoe mauti uliyoinunua kwa kujua na kutokujua.

·        Mahali mtumishi anajiita yeye ni YESU huko usiende yeye yupo mbinguni na huyo anayejiita yeye hajakufa na kufufuka na zaidi angekuwa yeye ni YESU basi yupo hapa duniani basi ingekuwa ndio mwisho wa dunia, nyota zingedondoka, lakini cha ajabu nyota zipo angani zinang’aa, na cha ajabu anaumwa malaria ana mateso na- huko msiende wala kusikiliza huko ndipo anasema msiende.

·        Wanapotumia uchawi, iwe ni nabii, mwalimu, mchungaji, mwinjilisti, askofu, shemasi, mwimbaji na nyimbo za injili, mtume- hao usiwafuate wote- wanaochaji watu pesa dunia muwakatae kabisa hao ni majangili wa kiroho, ni bora kubadilika sasa moto umeandaliwa juu ya wanyang’anyi.

·        Mtenda miujiza ya kipepo- usimfuate, mkatae.

·        Mhubiri anayelichanganya neno la uongo- mkatae kabisa ni YESU anasema na wewe ili umjue yeye.

·        Theolojia zilizo changanywa neno na mapokeo ya wanadamu zikatae- siyo za YESU na hata unayezitumia- ule mwisho ipo adhabu ya mateso juu yako ni bora kuiacha kafanye mambo mengine kuliko kujifunza elimu ya mapokeo ya wanadamu pasipo kujua au kwa kujua soma Isaya 30:1-3 tubu na uache kabla ya aibu ya milele itakayokuwa juu ya kila muhubiri wa uongo? Au anayebadili neno, tubu na uachane nayo kabisa  ndio usalama wako kwa MUNGU, hiki ni kipindi cha neema, ila neema ikiondoka milango itafungwa, heri yako uliye hai, sasa hao waliokufa kabla ya kutubu na kuacha tayari wanateseka sababu wamekuwa baadhi yao makristo au nabii wa uongo.


·        Mahali wanapokataza au kutenga mtu aliyeokoka hapo usiende ndipo sehemu asizozitaka YESU japo wanadamu hawajui baadhi ukweli na zaidi maneno haya wapo watumishi  wafrika na wengine wazungu na wengine kwa rangi zao walitumwa waziseme miaka mingi wakagoma na wakamkufuru MUNGU wakakaa kimya hivyo basi shetani asingeweza kuwateka watu wengi hivyo, ila sasa atawakomboa watu wake mwenyewe kwa njia zake kama alivyoniambia na ndivyo ilivyo.  YESU yupo kazini kiroho na kimwili kufanya kazi yake, shetani alijitamba muda mrefu aliwatumia watoto wake waliomkubali ili kuichafua biblia. Sasa ni mwisho ataendelea kuumbuka tu na mataifa watajua ukweli na mtaokolewa kabisa.

·        Imekuwa ni aibu siku hizi baadhi ya watumishi wanafundisha siasa kanisani au katika semina za injili na wengine wanafundisha uchumi badala ya neno sasa cha ajabu ni kujiuliza hivi MUNGU anachanganywa na elimu ya dunia? Na je waalimu wa siasa au uchumi je waliambiwa wafundishe uchumi kanisani? MUNGU anachezewa sana- mambo ya Kaisari apewe Kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU. 

MUNGU hachanganywi na elimu ya dunia hii na hii ndio dalili ya kujua mtumishi aliyeitwa akakubali halafu akarudi kwa shetani.  Petro aliambiwa wacha kuvua samaki twende ukahubiri.  Mimi Hebron nilipoitwa nilikuwa nafanya kazi akaniambia wacha hii kazi sasa utahubiri tu na kupeleka neno langu kila ninakotaka na kuwaponya watu sehemu mbali mbali.  Sasa ikiwa leo naanza kufundisha mambo ya professional tour guide, mambo ya hifadhi, wanyama hivi si mtaona huyu tayari ameshamgomea YESU?  Na hao ndio hivyo hivyo, siasa inafundishwa chuoni, na uchumi pia au hesabu au urubani kuna vyuo vya kaisari, bali kanisani ni habari za mbinguni na watu wamjue YESU sio wajue siasa, uchumi, urubani, hapo siyo mahali pake.

ANGALIZO:
Natumanini watoto wa MUNGU mmeelewa sasa maana yake mkisikia yupo YESU kule uangalie nini na kama upo mahali ambapo hayupo ni bora ukae nyumbani ukiendelea kuomba yeye sababu utazidi kuangamizwa.

Kanisa halitakiwi kuwa na benki- litafilisi watu wakishindwa kulipa na itaonekana ni YESU amenyang’anya na kumbe siyo yeye.

Wahubiri, wavuta bangi, walevi, freemason, wanaotumia mizimu, wanaozika biblia, wanaofanya maagano, kafara, kuzika vitu vya waumini madhabahuni, wahubiri wanaotumia miungu- hao wachana nao msisadiki (na mengineyo mengi ya uongo na uchafu).

Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniandike jina langu kwenye kitabu cha uzima wa milele, unitoe mahali ambapo umesema nisiende wewe YESU unapajua, uniongoze mahali ulipo wewe, nifungue masikio yangu, moyo wangu, macho yangu, nione yaliyofichwa ili nisitegwe tena.  Amen.

Mbarikiwe- umtumie ujumbe huu kwa kila unayeweza kumtumia kwa njia yeyote ile na YESU atakubariki sana, wengi wataponywa zaidi.

NABII HEBRON WILSON KISAMO.