JE
NI SAHIHI KUABUDU KABURI LA YESU?
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE!
Swali, Je ni sahihi kuabudu
kaburi la YESU, au kufanya ibada ndani ya kaburi lake? Kila mtu anajua kaburi la
YESU siyo YESU, kaburi ni nyumba ya kuhifadhia mwili mpaka uoze na usionekane
tena. Ninawaeleza hii ulimwengu wote kwa sababu hata YESU mwenyewe anawashangaa
wanadamu hapa duniani wakiliabudu kaburi lake, wakati hilo kaburi siyo YESU. Shetani
naye akiendelea kuwashtaki kila anayeenda kuabudu hapo kaburini huko Israel na kufanya ibada kama vile hilo
kaburi ndiyo YESU. Mkumbuke moja ya amri kumi usiabudu chochote zaidi ya MUNGU
na wala usiabudu vitu alivyoviumba, na imeandikwa MUNGU yeye siyo MUNGU wa
wafu. Sasa mtu anapoimba kaburini na kutoa sadaka na kupeleka maombi yake,
katika ulimwengu wa roho yapo mapepo
kaburi yanameza na zaidi unakuwa unapata dhambi kwa sababu umevunja amri ya
MUNGU.
Kitu kingine cha kujiuliza, je
ibada ya kaburini ikoje? Jibu ni ibada ya kusindikiza mwili, sasa swali, je
bado YESU anazikwa hata leo? YESU amefufuka yu hai, hivyo unayependa kujua
ukweli, usifanye hivyo. Unapoenda kwenye kaburi la YESU, wewe nenda kutembea tu
kwa kujifunza au kama mtalii, YESU hayupo kaburini, yupo mbinguni. Msitende
tena dhambi hii, kama ulikuwa hauelewi sasa umeelewa na utubu na kuacha. Wakati
mwingine nitaelezea kwa undani zaidi kuhusu kaburi la mfalme wetu BWANA YESU
aliye hai. Hata kibinadamu kwa wale wanaoenda makaburini kupeleka matatizo yao
katika familia pale kufanya ibada kwa yule aliyekufa awasaidie jambo fulani kwa
sababu ni mzoga upo pale na mizimu. Sasa jiulize, je YESU ni mzimu au ni mzoga?
Jibu hapana, YESU yupo hai wala hayupo kaburini tena, yupo mbinguni na BABA
yake, yaani MUNGU. MUNGU ni MUNGU wa wenye uhai na siyo MUNGU wa wafu.
Yapo madhara makubwa na mabaya
endapo utaabudu katika kaburi lolote lile likiwemo la YESU. Madhara yake ikiwemo
kupata dhambi na mengineyo. Na zaidi yupo mungu
aitwaye kaburi huyu ni aina ya miungu
ambaye huwasaidia wanaofanya ibada za makaburi na ndiye anayekuwa kiongozi wao
na kuharibu maisha ya wanadamu. Pia wapo wachungaji
wengi wanaotumia nguvu za giza huongozwa pia na aina ya huyu mungu kaburi, na zaidi utashangaa
utaona baadhi ya watumishi wanajijengea makaburi au minara katika nyumba zao au
katika makanisa yao, na wala hakuna mtu amezikwa hapo. Sasa jiulize, kwa nini
wanajenga na hata wanaweza wakasema tujenge kaburi la YESU au la mtume yeyote,
mfano Daudi, Eliya na wengineo, waulize je kazi ya injili waliyotumwa ni kujenga
makaburi ya watoto wa MUNGU? Hawana jibu, kazi ya makaburi hayo ni nyumba za
miungu kaburi, unapoona hayo mwenye akili na aelewe na apone nafsi yake. Watu
wanaoenda hapo wanamezwa katika ulimwengu wa roho na hayo makaburi, na
usishangae imeandikwa kaburi limenimeza na anayeandika yupo hai. Makaburi hayo
ni masharti anayopewa mtumishi ili kuwapeleka watu kwa shetani, na kwa kufanya
hivyo yeye hufanikiwa hapa duniani, ila mwisho wake ni jehanamu.
Wapo wengi ambao tayari
wanajijua, wote watachomwa tu kwa sababu wamekubali kuwa wakala wa shetani.
Hivyo usithubutu kuomba/kufanya ibada katika hayo makaburi wala kutoa sadaka
hata kupeleka mguu wako. Unapoenda kufanya ibada mahali hapo, huyo mungu kaburi
anakumeza na vitu vyako vyote na unabakia na matatizo lukuki (full).
NABII HEBRON.
USISAHAU KUSUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL
YETU YA PROPHET HEBRON KWA KUBONYEZA LINK HII https://www.youtube.com/prophethebron?sub_confirmation=1 KUTAZAMA
VIDEO ZAIDI