Pages

Sunday, February 25, 2018


BILA KUZIKWA NA KUFUFUKA KWA NJIA YA UBATIZO WA MAJI MENGI; HUWEZI KUFUFUKA KAMA YESU

Bwana YESU asifiwe, katika somo hili la kufufuka kama YESU utasoma katika kitabu cha Warumi 6:1-6 neno linasema je damu katika dhambi, mstari wa 4, tunapobatizwa kwa maji mengi hapo ndipo linapotokea tendo la kuzikwa na kufufuka na YESU na ufufuko huu ninao waelezea ni kufufuka kiroho na kimwili, unaweza ukapata ufufuko wa giza bila kujua au kupenda, badala ya kupata ufufuko wa nuru ya kweli ambao aliuagiza MUNGU ili watu wote ili ufuatwe na watu wote ili siku moja wamuone yeye na wafufuke na kupaa mbinguni.

Aliponiita YESU, alinieleza na kusisisitiza “ukafundishe kuhusu ubatizo, wa kweli kwa wote na watu wabatizwe,ili wawe watu wangu na kwa sababu watu wengi wanao ubatizo wa giza, na wanajiita wakristo na hawafuati njia zangu katika ubatizo wengine hawajui na wengine wanajua kabisa kuwa wanafanya makosa na wapo upande wa mpinga kristo.

Neno linasema mkabatizwe kwa mfano wangu mimi niliobatizwa sasa jiulize! Je ni mfano upi? Je! YESU alibatizwa ubatizo upi? Mataifa hebu jiulizeni. YESU yeye alibatizwa katika maji yanayotembea tena ya mtoni, ukisoma biblia hutaona kuwa kama kuna aina yeyote ya mfano wa ubatizo ambao YESU alibatizwa nao, na MUNGU alijua kuwa neno lake litabadilishwa,  na mwanae YESU alisema watatuumia jina langu kuwapoteza hata wateule  wake kwa kufundisha mambo ya uongo,  na yasiyo ya mfano wake, mimi Hebron hapo awali kabla sijapata neema hii,  nilishabatizwa kwa mfano ambao haukuwa wa YESU, na sijui mfano huo ulitokea wapi na nilikuwa mtoto mchanga na sikuwa na ufahamu na nilimwagiwa maji kichwani.

Ninajua kuwa watu wengi ni wasomi  “maana ya Neno Ubatizo ni Kuzamishwa” sasa inakuwaje leo unamwagiwa maji kichwani na uitwe kuzamishwa? Hauni kuwa huo ni uongo na kama ni uongo basi unakuwa unapokea nuru ya ufufuko wa giza, utafufuliwa na hilo giza na hatima yake unapokea nuru ya ufufuo wa giza na giza hilo litakufufua na ila siku ya mwisho utaenda kwenye giza la shetani kwa sababu unacho kiapo hicho. Tafuta kwenye biblia, hakuna mfano wowote ambao ambao unaeleza ubatiizo mbadala wa ule ambao alibatizwa YESU, hakuna. Soma 2 Wakorintho 4:2,4 jambo lingine baadhi ya watu katika Mataifa mengine wanabatiza wakifuata madhaifu ya baadhi ya Mitume, badala ya kufuata yale mazuri tu na hao walikuwa ni wanadamu na wapo waliokosea kama YESU alivyotaka katiba baadhi ya Mambo, mfano: Paulo alipobatiza ndugu zake kwa vumbi lile ni kosa, na natumaini alitubu ndio maana yuko mbinguni. MUNGU anataka dunia yote ifuate kama vile alivyoonyesha YESU katika ubatizo na sio kamaa mwingine yeyote,  na ndio sababu yeye YESU aliitwa njia ya kweli.

Ubatizo mwingine ambao utafanya watu wasiende mbinguni ni  ubatizo wa kisima au shimo huo bado sio ubatizo wa mfano YESU mwana wa MUNGU, sasa cha kujiuliza je! Mnafuata ubatizo wa mfano ule ule wa YESU au ubatizo wa mifano ambayo hajabatizwa YESU? Jibu unalo na ni demokrasia yako ila kama ulikuwa hujui sasa sasa uelewe na upate uponyaji. Japo upo ubatizo wa maji mengi ya mtoni lakini kabatizwa kwa jina la YESU na la mchungaji kwa jina lake(mfano. Mchungaji anaitwa X na muumini A, mchungaji anakubatiza “Nakubatizwa A, kwa jina la baba, mwana na roho mtakatifu na kwa jina lake X)  huo ni ubatizo wa giza, imeandikwa kwa jina la YESU tu  na sio la mtu yeyote.

Shetani aliwapofusha watu wasiielewe biblia, na wanaofundisha hivi ni sawa na mwanafunzi anayesoma sana halafu asiielewe anachokisoma katika kitabu, biblia watu wanazo lakini baadhi hawaelewi na shetani na shetani anatumia njia hiyo kama mlango wa kuwafelisha Wakristo, ili wasiende mbinguni na zaidi wapo mawakala wa shetani wakijiita kuwa ni watumishi wa MUNGU, ila wametumwa kuiharibu hii dunia, na watu wake waangamie kwa kulipindua neno la MUNGU,  na kama Neno lilivyoandikwa linapobadilishwa au kuongezwa, na watu tayari linakuwa sio lile alilosema MUNGU, sasa maneno  ya watu yakachanganywa na ya MUNGU, hapo ndipo palipo haribika na mtu akiamini neno lililoharibika na yeye ndipo anapoharibika sababu anapokea uharibifu, na analazimika au kulazimishwa kuona ndio sahihi.

Sasa ili ukamilishe mpango wako wa kufa na kufufuka na YESU kwanza ni lazima uokoke yaani umpokee yeye awe BWANA NA MWOKOZI WAKO na pili, ubatizwe kwa mfano wake na kuwa na uhuru, mtu mzima anayo akili timamu; lakini mtoto mdogo mchanga yeye haelewi, hajui chochote, ingelikuwa ni mpango wa MUNGU kuwa watoto ndio wabatizwe basi YESU angebatizwaga na maji ya kumwagiwa kwa kikombe lakini siyo mpango wa MUNGU na mapenzi yake Mwenyezi MUNGU, hayo ni makosa na ni dhambi na ndipo Warumi 1:7 inaongea na wewe. Mamilioni wamebatizwa kwa uongo; baadhi wakijua na baadhi hawajui kuwa ni wa uongo, sasa hiki ni kipindi chako cha Neema, ijue kweli nayo itakuweka huru, Fuata ubatizo wa kweli na kwa mfano ule ule ili siku ya mwisho utafufuliwa na wewe utafufuka na utakuwa unajiunganisha na ile nguvu ya kupaa katika unyakuo

Sasa cha ajabu shetani anajua siri hii na kuamua kuwatumia baadhi ya watumishi  kuwaongoza watu jehanamu pasipo wao kujua, wapo  Wakristo kwa kuwadanganya kama anavyofanya, kiasi kikubwa , mtafufuka lakini hamtapaa mawinguni sasa ufanye maamuzi kuwa Mkristo tu bila wokovu ni bure,  na pili bila kubatizwa kwa maji mengi ya mtoni bado ni kazi bure,(unapobatizwa tofauti unauchafua tu mwili wako)  kama unataka kupona fuata kama yeye njia (YESU ) ya kweli.

Kwa kweli itakuwa ni siku ya kilio kwa wengi, kwa ambao hamtaendelea kubatizwa kama YESU, na cha ajabu ni pepo gani hilo ambalo linawafunga watu ufahamu wasimtii YESU na kuamua kutengua njia zake? Amenituma kwa mataifa yote, ili mbadilike, mje mbatizwe kama yeye, na sio kwa mfano wa tofauti na yeye, ili mpone yeye anawapenda, mrejee, hiki ni kipindi cha neema(Grace Period) itafika wakati mtatafuta neno la kweli hamtaliona, wala mafundisho ya kweli hayataonekana, ndipo watu watakumbuka haya maneno, mda uliobakia ni mchache sana yupo njiani anarudi, kuwachukua wale walio wake, jitahidi usiwe na shitaka , kabatizwe sasa.


Nabii Hebron Kisamo.