UKIABUDU SANAMU UNAFANANA NA SANAMU
ZABURI 115: 4-8
ZABURI 115: 4-8
Shalom, katika makala hii ya somo linalohusu sanamu, nitaelezea
zaidi kwanini MUNGU anasema anayezitumainia anafanana nazo.
Kwanza sanamu ni kitu
kilichotengenezwa, hakiongei, hakisikii na kama hakisikii kwanini mnakiabudu kanisani?
kwanini unakiamini kikusaidie? Kama nilivyokwisha kufundisha katika masomo ya
nyuma yapo mengi, niliyowaelezea kuhusu
sanamu ya kuwa hakuna faida mtu atakayoipata ambaye anayeabudu sanamu bali
atapata hasara na kuhukumiwa katika ile siku ya mwisho kama hatatubu sasa na
kuacha na kuokoka.
Ninalo swali kwa wafuasi wa BWANA YESU wa Mataifa yote ,
hivi YYESU ni sanamu? Jibu yeye sio sanamu, au Mariam Mama yake YESU yeye ni
sanamu? Jibu ni hapana na je! wewe unoyesoma makala hii, wewe ni sanamu au mtu?
Cha kujiuliza katika nchi mbalimbali zipo sanamu za aina nyingi, je! umeshawahi
kuona zikiongea au kurukia au zikinusa kwa pua au zikiangalia kwa macho yake?
Jibu hazina lolote. Bali nyakati hizi shetani amebuni njia nyingi za kuwapoteza
hata wateule ili wasiende mbinguni, kwa kuwapofusha imani zao wasijue kuwa YESU
ni MUNGU na yupo hai na kubadilisha
imani na fikra kwa mafundisho ya uongo na baadhi ya wakristo wakamfanya YESU
sanamu na YESU akafananishwa au kufanywa
sanamu au kwa Kiswahili kinyago hii ni dhambi kabisa ya kumtengeneza YESU kama sanamu au kumfananisha kama sanamu,
yeye ni MUNGU hafananishwi na chochote na zaidi anaitwa mwana wa pekee wa MUNGU
hakuna kama yeye duniani na mbinguni hivyo basi kile kitendo cha kuchonga
sanamu na kuiita YESU ni kufuru na pia tendo la kuiabudu na hata kuitolea
sadaka hiyo sanamu au kinyago hicho ni
dhambi kubwa sababu kwa njia nyingine tayari
unakuwa umevunja amri ya MUNGU, usiabudu kitu chochote wala kukisujudia
alichokiumba MUNGU, wala alishokitengeneza mwanadamu au shetani. Huu ni upofu
ulioletwa na mpinga kristo ili kuwaangamiza watu sasa unapoiabudu sanamu
unafanana nayo katika ulimwengu wa roho
na hata kimwili na kufanya usionekane na MUNGU na zaidi ulishafanana na kinyago au sanamu kwa sababu Mbinguni wataenda wale
wanaofanana na MUNGU, kwa mfano wake ila
aliyefanana na sanamu hatakwenda yeye ataenda kwa muasisi wa sanamu ambaye ni
shetani.
Hivyo nilipokuwa naelezwa
na YESU habari hizi ili niwaeleze na kuwafundisha watu wote ili mpate kupona
kwa wale ambao watahitaji kwenda mbinguni waachane na sanamu na kufanya ibada
za sanamu, kwasababu hata wanaotumia sanamu katika ibada zao wanafana na sanamu na
hazifanani na ibada za MUNGU Mtakatifu
hata kama jina lake linatajwa YESU alishasema wengi watapotezwa kwa
kutumia jina lake na waongo au mpinga kristo yamkini wajijua au hawajijui.
Akawaonyesha ulimwengu wote ndio maana mnaona kuwa ni watu
wachache waliookoka ndio wanafanana na MUNGU na watu wengi ambao idadi yao kubwa hawafanani na MUNGU katika
ulimwengu wa roho na sura zao zinakuwa sanamu.
Hivyo akaniambia Hebron
waeleze maana idadi kubwa hawajui madhara yake waeleze wanifuate mimi “YESU” na
wanajiita kwa jina langu halafu hawaokoki, kila mtu anayenipenda aokoke, anipokee,
niwe Mwokozi wake, mimi YESU ni Mwokoziz kila mtu anipendaye aupokee Wokovu wa
kweli na aishi katika utakatifu,
akaniambia narudi kulichukua kanisa na kanisa ni watu sio dini au dhehebu, mimi
ni wa watu wote, wakinipokea watafanana na mimi na wasiponipokea hata nikija sitawachukua sababu hawafanani na mimi. Akaniambia wengi
hawajielewi na nimekutuma usipunguze
wala kuongeza neno langu sema kwa dunia yote waeleze wote wanirejee watubu. Na
hata waliopo katika sanamu (madhabahu za sanamu/ Zenye sanamu) wasibutu kwangu wakiwa huko (Kwenye sanamu)
maana mimi sipo huko kabisa wala sifanani na sanamu wala msalaba.
Na zaidi unapoiabudu au hata kubusu sanamu au kuufuata
au kuweka msalaba kwako au hata kanisani, tayari huyo MUNGU aliyeumba vitu
vyote anakuwa siyo MUNGU wako, kwa sababu tayari wewe unaabudu sanamu na unaongozwa na mungu sanamu haijalishi kuwa
unasoma biblia na unasheherekea krismas na pasaka au unatoa sadaka. Zote hizo unakuwa
kwenye ufalme wa mungu sanamu na
kuwafanya watu kushikiliwa na mungu sanamu,
kwa kujua na kutokujua, na zaidi hata mafundisho ya mila,ibada ya wafu zote hizo ni huwa chini ya miungu na siyo
MUNGU, Tubu mrejee YESU, uokoke na wewe uweze kufanana na YESU na siyo sanamu .
Imeandikwa na
Nabii Hebron Wilson Kisamo.
USISAHAU KUSUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL
YETU YA PROPHET HEBRON KWA KUBONYEZA LINK HII https://www.youtube.com/prophethebron?sub_confirmation=1 KUTAZAMA
VIDEO ZAIDI