UNABII
WA NCHI YA TANZANIA NA DUNIA ITAKAVYOKUWA 2018
BWANA
YESU ASIFIWE, Mfalme wa wafalme, Mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai. Napenda
kuwajulisha watu wote wa mataifa yote yale niliyoelezwa na MUNGU kwa mwaka 2018 kuhusu nchi ya Tanzania katika baadhi
ya maeneo ambayo niliyoruhusiwa kuyasema na mengine ni ya kwangu. Napenda
mtambue kuwa MUNGU ameiandaa Tanzania kama ndiyo nchi yake ambayo hata ile siku
ya mwisho mwanae atashukia katika anga la Tanzania katika unyakuo, na pia ndiyo
Edeni ya sasa.
Ukirejea
katika makala ya blog
ya Nabii Hebron kupitia tovuti (website) www.prophethebron.or.tz kuanzia
mwaka 2014 na 2015, kuhusu unabii alionieleza MUNGU umetimia, kuanzia kumpata
rais huyu wa sasa ambaye MUNGU alimficha na hakujulikana wala kutazamiwa,
kuhusu shirika la ndege kuinuliwa, kuhusu bandari, kuhusu mgodi wa Tanzanite
kurejeshwa kutoka AFGEM na kupewa watanzania, kuhusu uchumi kuinuliwa juu,
kuhusu usalama wa jeshi la nchi kuwa bora na mengine mengi aidha uliyasoma au
utayasoma na yametokea. Na mwaka huu 2018 yapo mambo mengi ambayo MUNGU
atafanya njia kwa kuwatumia watu wake waaminifu.
1. UCHUMI WA TANZANIA
· Uchumi
wa nchi ya Tanzania MUNGU ataunyanyua mpaka utakuwa ni uchumi namba moja katika
bara la Afrika, myaonapo hayo mtukuzeni MUNGU na yeye tayari yupo kazini.
· Kuna
wizi mkubwa sana ambao haujawahi kufichuliwa aidha na watanzania au serikali
tokea nchi hii ipate uhuru, ni mali ya Tanzania iliyofichwa na baadhi ya watu, wengine
wapo hapa Tanzania na wengine wapo nje ya nchi hii, ni vitu vyenye thamani ya
pesa nyingi ya ajabu. MUNGU atawafichua.
· Pesa
nyingi za nchi zilizoibiwa zitarejeshwa.
· Kuhusu
viwanja vya ndege nilishaeleza 2013/2014, bado kasi itaendelea zaidi wala
hakuna atakayeweza kuzuia au kukwamisha, jicho la MUNGU lipo hapo.
· Kuhusu
madini ya Tanzanite: Madini ya Tanzanite yatapotea katika nchi za nje na hivyo
watakuja wenyewe kununua hapa nchini.
2. MUUNGANO
WA TANZANIA
Tanzania
itabakia kuitwa Tanzania tu milele yote. Mimi Hebron tokea MUNGU aniite na
nimfahamu, nilipokuwa naongea naye hajawahi kuniambia omba kwa ajili ya Tanganyika
au nimekuita unitumikie katika nchi ya Tanganyika. Nilishasema muungano
hautavunjika kamwe, hiyo ni sauti ya MUNGU na ni mpango wa MUNGU, na katika
upande wa Zanzibar patatokea soko kama lile la Dubai au China, nilishaelezea,
hii yote ni MUNGU anatengeneza nchi yake iwe Eden kwa ajili ya utukufu wake.
Upo usemi usemao, watu ni sauti ya MUNGU, mimi napenda kuwaeleza, siyo kila
usemi au sauti za watu ni sauti za MUNGU, sauti nyingine ni sauti za shetani.
Kama
wewe ni msoma Biblia mzuri, YESU alipokuwa anasulubishwa katika nchi ya uyahudi
zaidi ya miaka 2018 iliyopita je wale watu waliokuwa wanasema asulubishwe tena
ni wengi je zile sauti zilikuwa ni za MUNGU au sauti za shetani? Jibu ni kwamba
zile zilikua ni sauti za shetani. Hata hapa Tanzania sauti hizo za shetani
zitaendelea kusikika ila hazitafanya kitu, sababu shetani yeye hapendi mpango
wa MUNGU utimie Tanzania, ila utaona, itatimia tu.
Nataka
muelewe ya kwamba, siyo watumishi wote ni wa YESU, haijalishi hata wakisema
amewaita wengi, wao ni waongo na ni mawakala (agents) wa shetani ila
MUNGU ameshawazimisha, na wale wa MUNGU wa kweli wataendelea kudumu na hawataporomoka.
Wapo walioitwa hapo mwanzoni lakini baadaye wakamkataa YESU, wakajiunga na
miungu na freemason.
3. KUHUSU
NGOs
Baadhi
za NGOs (taasisi zisizo za kiserikali) zilizopo hapa Tanzania siyo za mpango
wa kunufaisha watanzania bali zimefunguliwa na baadhi ya watanzania kwa ajili
ya kujifaidisha kwa kutumia watanzania, zitafungwa.
4. KUHUSU
WATUMISHI WASIO WAAMINIFU
Watumishi
ambao watakuwa wezi na wengine wasio waaminifu au kujipatia nafasi hizo kwa
njia ya nguvu za giza watashangaa wanaachishwa kazi tu, kwa sababu MUNGU
anataka aitengeneze nchi, na yeye hafanyi kazi na mchawi, kwa sababu mchawi yupo
katika ufalme mwingine, labda mtu huyo atubu na aache.
5. KUHUSU
WANACHAMA WA FREEMASON
Wanachama
wa freemason, katika mwaka 2018, japo
siyo rahisi kujulikana na wengi ni watu matajiri na maarufu, wengi watakufa, ku
paralyze na wasiamke tena, hili
litafanyika katika dunia.
6. KUHUSU
UMOJA WA MATAIFA
Katika
Umoja wa Mataifa kutakuwa na mpasuko mkubwa katika yale mataifa kiongozi, na
baadhi ya nchi zitavunja uhusiano na nchi nyingine, na pia maafa makubwa zaidi
yatatokea katika dunia ambayo haijawahi kutokea, yatakuwa ni ya aina yake
ajuavyo MUNGU, mimi naleta taarifa tu.
7. MBUGA
YA LOLIONDO
Mbuga
ya Loliondo itarudishwa katika mikono ya nchi ya Tanzania.
8. KUHUSU
WANAO ITAKIA TANZANIA MABAYA
Wapo
ambao wanaitakia nchi ya Tanzania mabaya, MUNGU atawazimisha kama mshumaa. Nikimaanisha
kwanza wale wanao watakia mabaya viongozi, watu aliowaweka MUNGU, hao ni
watumishi wake, ikiwemo kiongozi wa nchi hii. Asifanyiwe mabaya, mtapigwa na
MUNGU, na wapo wengine tayari wameshapigwa na MUNGU japo hawaelewi. Yeye
ameteuliwa na MUNGU, ni mtu wa MUNGU, anaongozwa na MUNGU ili aijenge nchi hii
kwa utukufu wa MUNGU, haijalishi anajijua au halijui hilo.
9. KUHUSU
UCHAGUZI WOWOTE
Hapa
namaanisha kuanzia hata chaguzi za ubalozi wa mtaa, katika sector binafsi, serikalini, katika vyama vya siasa hata vyama vya
mpira, vyama vya wafanya kazi, wakulima, na wengineo. Alichoniambia MUNGU, “sipendi wizi wa kura, Mimi ni MUNGU mwenye
haki natenda haki. Waeleze wasiibe kura kwa mtu yeyote ili apate nafasi ya
uongozi kwa ajili ya kuwaongoza watanzania. Mimi MUNGU nitamnyima amani mtu
huyo atakayeiba kura au kununua ushindi, hata pata amani katika maisha yake,
pili mauti itamfuata ili aondoke nimweke mtu aliyepata kwa uhalali, ili niweze
kumtumia kuongoza watanzania”. Yatakapomtokea mtu asishangae na msione ni
mzaha ndivyo ilivyo na haibadiliki.
ANGALIZO:
Yapo
mengi ila nitayatoa wakati atakaponiruhusu MUNGU mwenyewe kwa wakati wake na
sehemu husika.
MUNGU
IBARIKI TANZANIA.
NABII HEBRON.