KILA
MTU ANAYETAKA KWENDA MBINGUNI NI LAZIMA AOKOKE
BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote ambao mliumbwa
kwa mapenzi ya MUNGU na kwa mapenzi yake ili siku moja mfike tena mbinguni
mahali ambapo ndipo penye makao mazuri ya milele. Ili ufike mbinguni sharti ni moja
tu UOKOKE na umpokee BWANA YESU, uishi
maisha matakatifu na kufuata sheria zake na Neno kama lilivyo katika kweli na
siyo lipunguzwe au kuongezwa mapokeo ya wanadamu au shetani.
YESU anapenda muelewe ukweli kwa sababu wengi mnampenda sana
ila mpo katika njia ya upotevu mkifikiri mpo na yeye kumbe mpo na mpinga kristo
au shetani. Anasema Yeye ndiye njia ya
kweli, na Yeye ni wokovu na ili
umpate yeye sharti uokoke kwanza ndio upate tiketi ya mbinguni, cha ajabu watu
wengi hawana tiketi hiyo wanabakia kuwashangaa wenye tiketi ya mbinguni huku wakipumbazwa
na wasiokoke na kudhani wataenda mbinguni wakati hawaendi. Sisi hapa duniani
tuliookoka ni wapitaji, kwetu ni mbinguni bali kama haujaokoka, wewe umekuwa ni
mkaaji wa hapa hapa, atakapokuja YESU kulinyakua kanisa mtabakia hapa hapa na
shetani na mtachomwa moto. Hivyo basi nyakati hizi ni za hatari sana shetani
anawazuia wanadamu wasikate tiketi za wokovu yaani wasiokoke na wengine
waliookoka wanarudisha tiketi za mbinguni wanarudia tiketi za hapa hapa
ulimwenguni na kuachwa na YESU.
Mara nyingi ninapoongea na YESU anakuwa na huzuni jinsi
ulimwengu unavyopotezwa na mpinga kristo na watumishi wenye maagano na shetani
ya kuwaangamiza watu wa MUNGU kwa kuwaweka katika njia ya uongo katika
ulimwengu wa roho na mwili. Ndio sababu baadhi ya wakristo hawataki kuokoka
kabisa au kwa lugha nyingine hawataki kwenda mbinguni pasipo kujua na wengine
wakijua. Sasa mkristo bila wokovu bado unayo hasara, unakuwa bado haujaupata tiketi
ya mbinguni, kwa sababu mwokozi YEYE alikuja kutuokoa kwa yule atakayependa,
hakuja kusema tuwe wafuasi wake na tusiokoke, hapana. Hili linakupa picha ya
kweli kwamba wakristo wengi zaidi hawajampokea YESU bali hao wanakua ni
wakristo ambao hawataki kwenda mbinguni.
JINSI
YA KUJIJUA HAUENDI MBINGUNI
1. Haujaokoka
mpaka sasa au uliokoka na ukauacha wokovu;
2. Umeokoka
ila matendo yako ni ya dhambi bado;
3. Umeokoka
halafu hautaki kubatizwa kwa maji mengi ya mtoni yanayotembea;
4. Umeokoka
lakini umebatizwa kwa jina la Mchungaji au umebatizwa kwa ubatizo wa maji ya
kisima.
Na mengine mengi soma vitabu vya mafundisho ya Nabii Hebron na makala zaidi za YouTube, utajifunza mengi na utakuwa
huru zaidi.
Angalizo:
Katika ule mwisho wa dunia, YESU ndiye Mtume na Nabii wa
MUNGU pekee ambaye ndiye aliyechaguliwa kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu wote
kwa rangi zao na kwa sura zao, hata manabii wote waliopita hawakupewa kibali
hicho cha kufanyika wokovu na kukupeleka mbinguni. Siku ile ataangalia
aliyemkubali wakati huu na ndiye atakayemchukua aende katika makao aliyoyaandaa
kwa ajili ya waliookoka tu na siyo kwa ajili ya watu ambao hawajaokoka. Dini
nyingine wanamuita Nabii Issa.
YESU ameniambia niwaeleze anawapenda sana na ili mpone na
Jehanamu sharti lazima kuokoka sasa hivi na siyo ile siku ya mwisho akija ndio
watu waseme YESU nakuhitaji uniokoe, atakuambia sikujui sikujui na ndipo litatimia
lile Neno “nitawaambia sikujui sikujui” soma Mathayo 7:22-24 na kuendelea. Sasa je na wewe ni mmoja wao? Jipime
kwa ujumbe huu ndani ya moyo wako, ufanye maamuzi sasa na uokoke kikweli na
siyo uwachukie wanaookoka. Tazama kipindi cha Nuhu akijenga Safina walimcheka.
Na wewe uewacheka wangapi waliookoka? Tubu na uokoke, gharika inakuja itakuangamiza,.
Usidanganyike na neno wanalosema hakuna wokovu hapa duniani ni mpaka ufe, hilo
ni pepo lipo ndani ya mtu likipinga watu wasiende mbinguni, ukifa kama
haujaokoka uelewe unayo tiketi ya jehanamu, na usidanganyike utaombewa toba
uende, kumbuka unapewa muda ukiwa na uhai na akili timamu ili utengeneze na
MUNGU, uokoke tu na siyo kingine.
MUNGU siyo MUNGU wa mizoga, haongei na mizoga. Mizoga inakuwa
tayari inanuka, imeharibika haina uhai, na wala mtu hayupo tena katika ule
mwili huu ni uongo mkatae kabisa. Maneno haya yananirudia sana, hivyo ni lazima
niyaseme ili nipate amani ya MUNGU na wengi mtapona msiyoijua siri hii. YESU
hana dini yeye ni wa watu wote, anawahitaji mumfuate YEYE umkiri kama BWANA na
MWOKOZI wako kuanzia sasa. Si dini, wala dhehebu, wala utajiri, wala umaarufu,
wala jeti au ndege haikupeleki mbinguni ila ni YESU tu. Basi sasa muelewe
hakuna chochote wala binadamu yeyote au Nabii au Mtume aliyeteuliwa na MUNGU
aliyekuumba wewe, ufanye wepesi utii ili usiangamie.
Sema, BWANA
YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniokoe, uniandike jina langu kwenye
kitabu chako cha uzima wa milele kuanzia sasa wewe ndiye Bwana na Mwokozi
wangu, uniongoze milele. Amen.
NABII
HEBRON.