Mungu REHEMA
(Hili ni pepo)
Mungu Rehema ni aina ya miungu, yeye hukaa na kuishi katika
makanisa ambayo yanaongozwa na miungu ya kikristo. Mahali ambapo hapana kweli
ya MUNGU au mahali ambapo NENO la MUNGU limechanganywa na uongo
ila Biblia husomwa kama kawaida kabisa.
Kazi ya huyu mungu rehema ni kupumbaza watu pale
wanapoomba toba na msamaha, ambapo watu huamini wamesamehewa dhambi zao. Cha
ajabu utakuta mtu ni mkristo, hataki kuokoka bali anataka asamehewe dhambi
zake, halafu huyo huyo ambaye hajaokoka anaomba asamehewe dhambi zake na
anaamini kabisa amesamehewa na MUNGU, wakati hajasamehewa dhambi yeyote
ile. Biblia inasema TUBU na UOKOKE hapo ndipo utasamehewa dhambi zako, yaani uache
uovu. Siyo kujiita mkristo wa uongo, nikimaanisha haujasamehewa dhambi, bado unakua
ni mkristo mwenye dhambi, unakua unapumbazwa na huyo mungu rehema, cha ajabu
utasikia mtu huyo huyo anaenda kanisani anasema naenda kupunguza dhambi wakati
hajaokoka, sasa anazipunguzia wapi?
Mtu huyo anakuwa amepumbazwa na huyo mungu aina ya
rehema ya kishetani, asiyetaka mtu aokoke kwa sababu anajua akiokoka na kutubu hatampata
tena. Hivyo, mkristo au mtu yeyote, kwa imani yeyote ile, ili usamehewe dhambi
zako ni mpaka uokoke. MUNGU hafanyi kazi ya ujinga, eti watu hawataki kuokoka
halafu wanataka wasamehewe dhambi zao, wakati MUNGU ameshatuwekea namna ya
kutubu na kusamehewa dhambi kupitia YESU, ni lazima uokoke, umkiri ndipo
utasamehewa.
Watu wengi wanakufa bila kuokoka, nataka muelewe kwamba
hao wanasubiri hukumu, na hata wewe ambaye unamkataa YESU sasa, halafu
unadanganywa ukifa utaombewa ili upokelewe, nakueleza hapo unadanganywa, wakati
wako ni sasa, tubu ukiwa hai na ukiwa na akili zako timamu, siyo ukiwa mzoga au
maiti. MUNGU ni wa watu wenye uhai na siyo MUNGU wa watu waliokufa au maiti. Maiti
haiongei. Yakupasa ukiwa una uhai, unaongea na una akili ya kutubu, utubu sasa
na uokoke na kuacha dhambi kabisa. Jitenge na huyu mungu rehema, anawapumbaza
watu wengi na makanisa mengi na watumishi wengi katika dunia yote, ila sasa
awaachie.
YESU amenituma niwaeleze na kuwafundisha mataifa KWELI
YAKE ili waokoke, usirudi tena kwa huyo mungu rehema, atakuangamiza kiroho.
Huyu ni aina ya miungu anayevuvia fahamu za wanadamu ili wazubae na wasitubu
ili atakapokuja YESU kulinyakua kanisa awakute bado wakristo wapo katika milki
ya shetani na ni mali ya shetani, shetani anakuwa anao uhalali kabisa na watu
hao. Sasa ili umnyime shetani uhalali wa maisha yako na nafsi yako, tubu na
uokoke. Ukiwa haujatubu na haujaokoka unakuwa ni mali ya shetani kabisa, kwa kujua
au kutokujua. UKWELI umeujua sasa.
NABII HEBRON