MAMBO
MANNE YA KUJIULIZA KABLA YA KWENDA KANISANI AU KWENYE MAOMBEZI YEYOTE.
BWANA YESU ASIFIWE! Mambo haya ni kwa ajili ya usalama wako
wa kiroho, sasa hivi ulimwengu umebadilika, unaweza ukafikiria utaupata msaada
wa MUNGU katika kanisa unaloenda au katika maombezi na badala yake unakutana na
shetani ndiye umeenda kumwona yeye.
1.
Angalia huyo mtumishi je ni MUNGU ndiye yupo nae
au huyo ni mganga anayetumia biblia akijipa cheo cha uchungaji au mwinjilisti
akitumia nguvu za giza, watu wengi wanakataa mambo ya ushirikina wameamua
kumrudia MUNGU lakini hata sehemu baadhi wanazosikia jina la YESU likitajwa
wakienda wanamkuta pastor ni mganga wa kienyeji nikimaanisha amejenga kanisa
kwa nguvu za uchawi, na anasaidiwa na nguvu za uchawi yeye anaishi kwa maagano,
wapo wanaotoa sadaka za damu kwa shetani na wachawi.
2.
Ikiwa unaenda kukutana na MUNGU hautachajiwa
pesa yeyote na utapokea uponyaji wako na ukiwa unaenda kwa mganga ni lazima
utachajiwa pesa, hata za kuonana na mtumishi uongee na yeye na mengineyo
yasiyompendeza MUNGU asiyoyataka utafanyika kama vile mganga afanyavyo masharti
masharti MUNGU yeye njia zake ni salama.
3.
Jambo la tatu unaenda kulishwa chakula cha
kiroho kilicho salama au sicho salama. Chakula cha roho kilicho salama kwa roho
ya watu ni neno la kweli ambalo halijachanganywa na uongo. Mfano wengine ni
kweli mnafundishwa lakini hakuna kuokoka au umebatizwa ubatizo wa uongo wa
kikombe, wa kisima, jina la mchungaji, zote hizo hata kama hapo ya kweli bado
uelewe unalishwa chakula cha kiroho cha shetani sababu kiapo cha agano la mtu
na MUNGU ni ubatizo uliootoka mbinguni kama alivyobatizwa YESU na ndio huo upo
kwenye biblia. Ufunuo 22:18-19 inaonyesha wazi hauna sehemu yako mbinguni, sasa
umeshajua ukweli ni bora uitafute nafasi yako sasa ya mbinguni ubatizwe
kwa maji mengi (Soma kitabu cha ubatizo
wa kweli kwa ulimwengu wote kilichoandikwa na Nabii Hebron), na jambo ambalo
YESU analiangalia ili uwe umetimiza haja yake uende na yeye ni uokoke umkiri
yeye, na siyo uwe mkristo lakini hautaki kuokoka iwe ni mtumishi au muumini
kama haujaokoka na kubatizwa kama YESU bado haujawa mwanafunzi wake bali ni
mwanafunzi feki; yeye hana feki huo ni mchomeko wa shetani kukupotezea muda na
kukupumbaza ili uje uchomwe moto na yeye. Yapo na mengineyo, usome kitabu Mkristo
usikubali kuwa mpumbavu lipo katika blog.
4.
Jambo la nne je utakutana na chakula cha kiroho
salama, ikiwa mchungaji mwenyewe anaye MUNGU anafundisha kweli na hachanganyi
na uongo, hakuna michango siyo sokoni, watu wote ni sawa, hakuna kulipia kanisa
madeni ya benki, kuwasoma majina waliotoa pesa nyingi hayo yasiwepo, ubatizo
uwe kama wa YESU ulivyo na siyo mwingine, roho mtakatifu atawale au YESU
mwenyewe ndio kiongozi wa kanisa hilo hapo utakuwa upo salama. Hivyo wengi
wakienda hukutana na kuwekewa appointment na waganga wanaotumia biblia
wakifikiri wana nguvu za YESU, madhara yake yule pepo aliyopo ndani yake huiba
vitu vyako na kukufanya kuteseka na ndio sababu wewe chunguza watu wengi
wanapoenda kwenye maombezi huchoka maisha yao kimwili
na kiroho, sababu hawajaenda kukutana na YESU bali wanakutana na mganga wa
kienyeji, na wachungaji wengi sana ni wateja maarufu na waganga wa kienyeji,
kama unabisha tafuta mganga wa kienyeji
atakueleza. Watu wanakuwa wanaongozwa na waganga na jinsi alivyo kuhani wa
kondoo hufanana nao kiroho. Ukiyajua hayo baadhi yatakusaidia na utafunguka
kabisa, sababu hizo ni kamba za kiroho.
NABII HEBRON.