JINSI
YA KUMJUA MTUMISHI ANAYEONGOZWA NA MIUNGU YA KIKRISTO
BWANA YESU ASIFIWE! Hapa
naongelea mtumishi ambaye anaongozwa au kutumikia au ameitwa na miungu ya kikristo au yule ambaye
aliitwa na KRISTO halafu akarudi
nyuma. Huyu mtumishi ambaye aliitwa na KRISTO
na baadaye akarudi nyuma huwa anachukuliwa na miungu ya kikristo na ndipo miungu hiyo huanza kumwongoza kufanya
kazi za injili kwa njia ya miungu ya kikristo, wapo wengine wanajijua kabisa kwamba
wao si watumishi wa YESU, na wapo
wengine wanatekwa na miungu kwa kufuata mapokeo ya kurithi elimu ya wanadamu. Kama
unaongozwa na mtumishi wa jinsi hii na wewe
muumini unakuwa mfuasi wa miungu ya kikristo, kwa sababu jinsi alivyo
kuhani na ndivyo alivyo muumini kiroho.
WANAOONGOZWA
NA MIUNGU YA KIKRISTO HUFANYA YAFUATAYO:
§ Kuwaombea
watu kwa kuwatoza pesa, wanakuwa na ma-partner
ambao anawachagua yeye ili kuendeleza hiyo huduma akitumia jina la YESU.
Atawabatiza watu kwa ubatizo ambao sio kama aliobatizwa YESU. Watabatiza
ubatizo wa kisima, ubatizo wa kikombe, kulipindua Neno, kubarikia watu wazima
badala ya kubarikia wakiwa watoto wadogo kama YESU alivyobarikiwa. Huchanganya
mafundisho ya uongo na ukweli, huwaeleza waumini waandike sadaka zao majina, kiwango
walichotoa, anwani (address) au barua
pepe (email address) na huwapa waumini
stakabadhi (receipts) wanapotoa sadaka.
Hufuata watu nyumbani au ofisini kukusanya sadaka ambazo waliwalazimisha
waumini watoe. Wengine hukopa benki na kuwalazimisha waumini walipe mikopo hiyo
wakati MUNGU yeye anasema usije toza mtu
RIBA. Kanisa linapoenda benki kukopa
hiyo inakuwa ni miungu ya kikristo ndio inaenda kukopa kwa sababu yenyewe ni
maskini, haina fedha wala dhahabu, bali YESU
wa mbinguni Yeye anavyo vyote hivyo na kazi zake anazifungulia njia mwenyewe na
wala si kwa njia ya madeni na kukopa.
§ Katika
nyumba za ibada hufanyika harambee, katika nyumba za ibada huzikwa viongozi wao.
Kwa njia hiyo watu wanakuwa wanaenda kusali kaburini kwa sababu kaburi lipo
ndani ya hekalu. Hata kibinadamu kaburini ni mahali panapotisha, wapo mapepo au
maroho ya giza. Hata YESU mwenyewe hakuzikwa kanisani alizikwa mbali na hekalu,
sasa iweje leo mtu anazikwa kanisani? Jibu ndio hilo, miungu ya kikristo
inafanya kazi yake ya injili ya miungu ya kikristo. Injili ya kikristo ikiwa
inampinga MUNGU katika kweli yake, mfano imeandikwa usimpe mtu kilevi na hapo
hapo utaona pombe inabarikiwa, tena bila aibu anatajwa Bwana YESU, sasa uelewe
wakati huo ni yesu wa miungu ndiye anayekuja kulewa kwa sababu yeye ulevi na
uovu ni mambo yake anayotaka wanadamu wayafuate.
§ Watumishi
wanakuwa ni wachawi au wanachama wa freemason kabisa na hata katika
matendo yao, ndiyo sababu hata baadhi yao huvaa misalaba ili waonekane ni
wafuasi wa YESU wa mbinguni. Cha ajabu utaona mtu fulani amejiunga na freemason lakini amevaa msalaba, yamkini
ni mchezaji au mwanamziki, wala usishangae huyo anakuwa amepewa hivyo vitu na
miungu ya kikristo na hapo anakua anaitambalisha. Baadhi ya makanisa yanakuwa
na bendera zake, wamezibuni, ila siri anaijua kiongozi na zile bendera, ni lazima
aziweke zipepee kwa sababu kila moja inaashiria mfalme aliyepewa kwa ajili ya
kulitawala hilo kanisa ili lipoteze watu na yeye afaidike. Huomba watu
waliokufa wawaombee ikiwemo hata kuwataja wanafunzi wa YESU kwa majina yao,
huabudu sanamu na mengine mengi, ila endelea kusoma makala haya utajifunza
mengi na utakuwa huru kwa jina la YESU.
§ Hutoa
makafara na kuwapinga wale watumishi ambao wameitwa na MUNGU ambao husema kweli
kama ilivyo. Wanao umoja katika ulimwengu wa roho, hawa watumishi wa miungu ya
kikristo hata kama hawajuani kimwili kiroho wanakua pamoja kabisa wakiwa na
waganga, wachawi, majini na mapepo, hao wote ni roho za ufalme mwingine.
Jina la YESU limekuwa
likitukanwa na watu kwa muda mrefu kwa sababu ya watumishi wanaoongozwa na
miungu ya kikristo, wanafanya kinyume na YESU aliyoyaagiza, wanasababisha watu wanakwazika
hata hawamtaki YESU. Mie nawaeleza hao ni wa miungu ya kikristo. Inawezekana
wewe huipendi ila ulikuwa huelewi, sasa unaelewa, achana nayo hiyo miungu ya
kikristo na mkimbilie YESU wa mbinguni na Yeye atakuponya utakuwa salama.
NABII
HEBRON.