Pages

Thursday, September 28, 2017

JIFUNZE NA UELEWE NI KWA JINSI GANI MKRISTO ANAWEZA AKATUMIKA KUMSULUBISHA YESU.

BWANA YESU ASIFIWE! Katika mada hii tutaona jambo ambalo watu wengi pasipo kujua na wengine kwa kujua linawafanya wamsulubishe YESU katika roho na kumsaliti au kumwaibisha au kulichafua Neno lake Takatifu kwa kulichanganya na uongo na hata watu wakaliamini na kufanyika kuishika njia ya jehanamu kwa kujua na wengine pasipo kujua.

Neno “kusulubisha” lina maana nyingi ikiwemo kuua, kumpiga, kumwaibisha, kumchukia, kumteketeza ili asionekane tena katika ulimwengu huu. Ingawa YESU alifanyiwa yote hayo lakini aliyashinda na mpaka leo anaonekana akitenda na akitawala. Baada ya YESU kuondoka, shetani akatengeneza mbinu nyingine ya kulisulubisha Neno lake YESU, akiwatumia wanadamu kwa njia ya mapokeo ya uongo na kila anayeshiriki mafundisho ya uongo na yeye anakuwa ameshiriki katika kusulubisha injili ya YESU na Neno lake. Wote tunajua kuwa yupo MUNGU wa haki ambaye atamtendea haki yake kila anayemsulubisha YESU kupitia Neno lake na kumchanganya YESU na uongo au kulitumia Jina lake kutafutia pesa au kulitumia Jina lake na uchawi au mizimu ili kutengeneza makanisa au huduma ambazo zinatumia nguvu za giza. Kama mnavyoelewa watu wa jinsi hiyo hawana tofauti na wale Wayahudi ambao walimsulubisha YESU pale Golgotha. Unaweza ukasema unawachukia wale wayahudi waliomsulubisha YESU, jiulize na jiangalie, je wewe katika ukristo wako haujamsulubisha YESU?

Ifuatayo hapa chini ni baadhi ya mifano itakayo kuwezesha kujua kama unamsulubisha YESU au hapana:

  •      Angalia ubatizo, je ni ule wa maji mengi ya mtoni? Kama umebatizwa ubatizo tofauti na ule wa kwenye Biblia ulioletwa na Yohana, jiulize je hapo upo sawa?

         Ikiwa ni wa kikombe, kisima, tenki au kwa jina la mchungaji hapo uelewe                unayo haki ya kwenda jehanamu, kwa sababu unamsulubisha YESU katika                eneo hilo na MUNGU, Hakimu Mkuu atatenda haki.

  •          Mtumishi yeyote anayefanyia michango (harambee) nyumba ya ibada au sikukuu ya mavuno (miradi), wote pamoja na waumini mnaunganishwa kuwa ni adui wa MUNGU. Tazama Yeye aliyakataa (Marko 11:15-17) sasa hauoni ni unafiki hamtaki kumfuata YESU, je hayo hayajakatazwa na YESU? Kwenda kinyume ni sawa sawa na kumtukana MUNGU au kulidharau Neno lake na amri zake.

  •       Mtumishi anapowatoza watu pesa za maombezi tayari anamsulubisha YESU kupitia neno lake, analiua halafu analeta neno lake la kuwatoza watu pesa kwa sababu hilo ndilo shetani analolipenda na siyo mapenzi ya YESU.

  •          Kutozwa pesa kwa ajili ya kumwona mtumishi au unatozwa pesa kiasi fulani na ukilipa ndio unapewa upendeleo ukifika hapo kanisani unapewa kiti karibu na mtumishi kwa kiwango cha pesa yako uliyoitoa. Nawaeleza kwamba hapo mnakwenda kumwona shetani wala YESU hayupo kabisa katika huduma ya jinsi hiyo. Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie.

  •      Unapoabudu sanamu unakuwa unamshusha YESU thamani, unaiona hiyo sanamu ni bora kuliko Yeye aliyepo mbinguni na kupitia hiyo sanamu ndani ya moyo wa huyo mtu, sanamu ndiyo anakuwa anaishi na siyo YESU. Ndio sababu imeandikwa msiabudu sanamu na wala Yeye hafananishwi hata na dhahabu wala fedha. Sasa mataifa hamuoni hapa hakuna ujanja mbele za MUNGU, siku ya hukumu utaonekana ni adui na utapelekwa jehanamu!

  •     Majina kuandikwa katika sadaka au taarifa zako za matoleo kuchukuliwa kanisani na kuwekwa katika file lako au kupewa cheti cha hongera kwa kuwa wewe ni mtoaji maarufu. Hapa hakuna anayemtolea MUNGU wa mbinguni sadaka bali wanawatolea miungu kwa sababu hizo ni taratibu za miungu. Utaratibu wa MUNGU unaelekeza sadaka iwe ni siri yako, sasa wameisulubisha siri yako, wameigeuza kutokuwa siri yako na kuamua ni lazima wajue unachokitoa na kama wanataka wajue basi uelewe unawatolea hao, na usipotoa utachukiwa na hata kunyimwa huduma za kiroho. Sasa swali jiulize je YESU hakusema mmepewa bure nanyi mtoe bure?

Sasa baadhi yao wameua na kugeuza ile BURE, wameleta malipo na kama ni malipo basi uzidi kuelewa unayeshiriki, bado na wewe unaunganishwa na laana hiyo ya kuliua Neno lake alilolipiga muhuri akasema lifuatwe (Ufunuo 22:18-19).

  •      Unapofanya ibada tofauti na kumtukuza MUNGU aliyeumba mbingu na dunia ikiwemo matambiko au ibada za wafu au kuabudu viumbe vyake hapo unakuwa unalisulubisha Neno lake na kufanyika adui wa MUNGU.

  •       Kukanyaga sadaka za watu na miguu.

  •          Mtumishi anayezika Biblia ni wakala (agent) mkubwa wa shetani, aliyepewa agano hilo ili aongoze vyema kuwateka wanadamu kuwapeleka kwa shetani. Sisi sote tunajua kuwa Neno lipo ili liishi na siyo life, sasa Biblia ni Neno la MUNGU na kitu chochote kinachozikwa ni mfu na Biblia inapozikwa madhabahuni, yakupasa uelewe kwamba watu wote wanaosali hapo nguvu ya Neno la MUNGU imekufa na kubakia ni hadithi (story) tu hapo, hakuna udhihirisho wa kweli, na kama Biblia ilizikwa katika nyumba yako, hapo wewe muumini unafanyika kulisulubisha Neno la MUNGU lisiwe hai ndani yako milele, bali yale mapokeo ya mwanadamu ndiyo yanakuongoza kwa njia hiyo ambayo inasababisha mtu kumfukuza MUNGU kwake. Kwa mtumishi anayefanya hivyo, yeye anakuwa anainuliwa na shetani kwa sababu anaua roho yako na kupanda mauti ndani yako. Ameng’oa uzima wa YESU wa kweli. Mtumishi wa jinsi hiyo akiwa anafundisha mahali popote iwe ni katika redio, TV, semina au kuhubiri, kila anayelipokea neno lake, madhara atakayoyapata ni kuuawa kiroho pasipo yeye kujua. Japo wakala (agent) huyo wa mpinga kristo yeye anajua anachofanya ni nini.

Mataifa muwe makini nyakati hizi ni za hatari mbwa pori wamejaa katika ulimwengu wote, MUNGU akulinde ili using’atwe na mbwa pori wa kiroho.

NABII HEBRON.