UNABII WA
KURUDIWA UCHAGUZI WA URAIS KENYA 2017 UMETIMIA.
BWANA YESU ASIFIWE!
Hatimae leo unabii aliyotabiri Nabii Hebron umetimia na
kuelezwa na BWANA YESU mwaka 2013 kuhusu uchaguzi uliyopita. YESU alimwambia
uchaguzi utarudiwa tu na leo umetimia kupitia supreme court ya Kenya, umefuta
uchaguzi wa Kenya wa 2017 na kuamuru urudiwe upya.
Maneno haya YESU alimwambia na akamwambia itatimia na yule
aliyempanga awe kiongozi wa nchi hiyo itatimia. MUNGU ndiye amesimamia haki;
hivyo Utukufu arudishiwe MUNGU na siyo wanadamu. Zaidi utasoma blog ya unabii
huo katika blog ya Nabii Hebron 17th February 2013.
MANENO YA MUNGU WA KWELI HAYAENDAGI BURE, LAZIMA NENO LAKE
LITIMIE, NA LIMETIMIA.
UBARIKIWE!
Nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO wa Nazarethi, aliye hai,
Mfalme wa Wafalme.
Huu ni unabii ambao tayari ndivyo ilivyo na itakavyokuwa, ndiye
Rais atakayeshinda uchaguzi wa rais. Japo kabla ya kumtaja, kwanza kabisa
iliandaliwa mipango ya kuhakikisha hataishi, ila MUNGU ndiye anayemlinda na
hakuna la adui litakalofanikiwa juu yake, ila asijishughulishe na mambo ya
kishirikina atamuudhi YESU na kuachwa, hivyo kusababishwa uchaguzi kurudiwa
upya.
Atakayekuwa rais ni
mgombea ambaye ni waziri mkuu katika nchi hiyo, na huyu kupitia yeye nchi
itainuliwa sana na maisha ya wananchi hao yatakuwa mazuri."
UCHAGUZI
MKUU WA KENYA 2013
Nawasalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareth aliye hai,
BWANA wa Mabwana, MUNGU wa miungu, ambaye ndiye MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na
Yakobo.
Ndugu Wakenya, MUNGU anawapenda sana. Niliyajua haya
nilipowekewa mzigo moyoni mwangu kuombea nchi ya Kenya, hasa ni katika uchaguzi
mkuu 2013. Wananchi wa Kenya, kwa rangi zote, makabila yote, na watu kwa jinsia
zote; nyie wote ni yeye kawaumba na nyie ni mali ya MUNGU, na MUNGU anawawazia
mema na siyo mabaya, ila shetani anaiwazia mabaya nchi yenu. Ila, mkitii haya
niliyoelezwa na MUNGU, shetani atashindwa kuleta machafuko katika uchaguzi wa
mwaka 2013.
MUNGU ameniambia watu wote na vyama vyote anawapenda sana,
japo nitaendelea kuiombea tu ili kusudi la MUNGU lisimame. Watoto wa MUNGU,
kuhusu suala la uchaguzi haswa la Urais, muombeni MUNGU awape kiongozi ambaye
MUNGU ndiye atakayewapa awaongoze. Yeye anamjua yupi atawaongoza vema, na
atakuwa mwema na mwenye hekima, YESU akaniambia, watu wanaomba tu kama
wanavyotamania, ila siyo MUNGU anavyotaka na madhara ya kuomba unachotaka,
utapewa ila usimlaumu MUNGU. Ila mkimuomba wape kiongozi wa kuongoza mzuri
hakika atawapatia, hivyo baadhi wanaomba kwa kumpenda wanayemtaka, ila hawajui
ndani ya moyo atafanyaje. Muache ukabila, kabila zote ni za MUNGU, nay eye
ndiye muasisi wa lugha zote, wekeni ukabila mbali muwe na umoja, upendo na
mshikamano. Nyakati hizi ingieni kwa maombi, mwachieni MUNGU awape rais yeye,
hii ni siri ya MUNGU, japo ninajua kila kitu na matokeo ya uchaguzi wa nchi hii
ila sijaruhusiwa kutamka.
Ujumbe:
Muombeni yeye awachagulie kiongozi mwema, maana wengine
ndani yao hawaiwazii mema nchi, ila yote MUNGU ameyaona, na ameniambia kanisa
lijipange upya kwa kumuomba MUNGU awape kiongozi kutoka kwake na si vinginevyo,
na yeye atafanya. MUNGU ibariki Kenya, wafungue fahamu zao wale wasiojielewa
kuhusu uchaguzi 2013.