Pages

Friday, September 29, 2017

JE INA MAANA GANI UNAPOTOA SADAKA KANISANI HALAFU KANISA LINAKUPA RISITI ILI URUDISHIWE NA SERIKALI (GOVERNMENT).

BWANA YESU ASIFIWE,  watu wote wa Nchi zote, siku chache zilizopita nilikuwa nikiongea na YESU kuhusu jambo hili ambalo baadhi ya wakristo katika nchi zao wamejiwekea mfumo ambao sio wa Mbinguni au wa kutokubarikiwa na MUNGU, akaniambia huo sio mfumo wa BABA yake yaani MUNGU, na haijalishi  kama jina la mtu  limetajwa hapo hayo ni machukizo kwake makubwa sana.

Kwa mtu asiyejua;  ngoja nikuelezee, katika baadhi ya nchi wakristo wanapotoa sadaka zao mfano dola 10, atapewa risiti ya kuonyesha kuwa ametoa dola kumi kwenye kanisa (Sadaka) hivyo huzitunza hizo risiti mpaka mwisho wa mwaka kisha huzipeleka katika serikali husika, kisha zitajumlishwa zote – kwa mfano jumla ya fedha ambazo umetoa zimefika dola 2000 au kiasi fulani ambacho umetoka kwa mwaka mzima, serikali husika huwa inamrudishia mhusika fedha  zake. (Yaani sadaka ambazo umetoa kwa mwaka mzima kanisani).

Sasa nataka ujiulize, unapomtolea MUNGU si unategemea kubarikiwa na MUNGU Mbinguni? Hivyo ndivyo ambavyo  baadhi ya wakristo  walivyopigwa chini na shetani, sasa mtegemee serikali hizo ndizo ziwabariki au kwa lugha nyingine hambarikiwi na MUNGU kwa sababu mnarudishiwa na Kaisari.Ndio sababu mateso hayaishi na pia ni sababu ambayo imelifanya kanisa kuwa sehemu ya kubadili fedha(Money exchange).

Nawaandikia na kuwatangazia kuwa habari hii inamuudhi sana YESU, Malaika wote na Mbingu yote kwa sababu ya mfumo huo, na mimi Hebron nawaeleza wala sipunguzi amesema “ Waeleze kuwa hawaniletei mimi bali wanajiwekea akiba zao kwa Kaisari, ili wapewe baada ya muda, wengi wanaomba wananiambia nizikumbuke sadaka zao waulize ni zipi ambazo wamenitolea mimi?  Waeleze Abel  aliponitolea sadaka yake ilienda Mbinguni kupitia moshi (Mwanzo 1:2-15)”.
Hata  kipindi chaYESU alipokuwa hapa ulimwenguni alikuwa akitoa sadaka lakini hakuwa anapewa risiti ili baadae akadai kwa kaisari, hivyo basi mdaini kaisari baraka na mengineyo kwa sababu mlimpa yeye. 

Cha kustaajabu, hata wapo baadhi ya waumishi wengine ambao wanalifahamu jambo hili kuwa sio sawa, na  wamekataa kulisema ili watu wasipone na wasione baraka zao na mengine yamefichwa  ikiwa inamaana mmemshukuru shetani au wametekwa fikra zao na shetani au wamekuwa vipofu. Na kupitia jambo hili hizi ni dalili kuwa vipofu ni wengi wanaongoza watu na watu hawaoni njia, na tayari wametumbukia katika mashimo, wapo baadhi ambao wanajua na wengine wanaiga mifumo ya vipofu.

MUNGU anaheshimiwa na Mataifa yote, (TAHADHARI (ONYO)) Huo mfumo uachwe mara moja na uachwe na mengineyo hivyo ndivyo ninavyoelezwa mda huu ninahimizwa ujumbe huu. Utayesikia sikia  hii ni dhambi kutoa sadaka halafu unaidai serikali ikurdishie hapo umetoa kwenye serikali ya kaisari.

Note:
Na zaidi ibada bila sadaka siyo ibada kamili hivyo basi kwa mfumo huo wa kutoa sadaka halafu mwisho wa mwaka unaenda kudai ofisi za Serikali (Government) ili wakupe cheque ya marejesho ya fedha ulizozitoa hapo hakuna ibada yeyoye ambayo anafanyiwa MUNGU wa Mbinguni bali unakuwa unamfanyia kaisari ibada.


NABII HEBRON WILSON KISAMO.