Pages

Saturday, June 17, 2017

BAADHI YA NDOA ZA WANADAMU ZIMEUNGANA NA 

SODOMA NA GOMORA


Shalom! Karibu tena katika mafundisho ya ndoa takatifu ili uachane na ndoa ya uchafu au ndoa inayomchukiza Mwenyezi MUNGU aliyekuumba wewe binadamu. 

Nitawaeleza kuhusu ndoa inayomkasirisha Mwenyezi MUNGU kutoka katika kiti chake cha Ufalme. Ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 14 mpaka Mwanzo 20; utasoma kuhusu habari ya Lutu alivyotolewa Sodoma ili asichomwe moto kwa sababu yeye hakufanya huo uchafu au uzinzi wa mitindo ya wanyama (Style za X). Ukisoma katika kitabu cha Waebrania 13:4 na 1Wakorintho 7:4-5, yapo maelezo ya ndoa na maonyo kwa sababu MUNGU alijua kuwa shetani bado anafuatilia ndoa ili zisiwe za MUNGU bali yeye shetani ndio azitawale.

Nitaelezea kwa kifupi yatakusaidia na utaelewa na wewe unayetaka kupona utapona ila hata sasa nasikia katika roho baadhi yao wanaumia roho kwa sababu wanapenda kuingiliana kama mbwa, au kuku au kinyume na maumbile hiyo ndio furaha yao, ikiwa ina maana kuwa pepo Sodoma na Gomora ndilo limejaa katika ufahamu wao na ili waache ni mpaka hilo pepo liondoke na lisipoondoka hawataweza kuacha kukutana kimwili kwa mitindo (style) hiyo ya wanyama na usipoacha hautaenda mbinguni; sehemu yako itakua ni Jehanam, kila unavyoendeleza na hizo style za X, ndivyo unavyozidi kujiunganisha katika safari ya kwenda kuchomwa moto kwa sababu umemkubali mnefili.

            Nashangaa na hata wewe pia ushangae, ni ajabu ukienda katika semina ya ndoa au kabla wanandoa hawajaoana wanaingizwa katika ofisi ya Mchungaji, watapewa mafunzo ya mitindo ya kuingiliana katika tendo la ndoa kwa njia ya Kisodoma badala ya kufundishwa yale anayoyataka MUNGU, sasa hapo unakua umepewa yale ya shetani na unapoyafuata basi ndoa yako au hizo ndoa zinakuwa ni chukizo mbele za MUNGU.  Mfano, eti utaambiwa muwe na mitindo (style) nyingi ili msichokane au mwenzako atakuona wewe ni mshamba, haujui mapenzi, (wakati hayo sio mapenzi bali ni kifo).

Nitaeleza baadhi kwa ufupi:

·        Kunyonyana mate ni dhambi;

·        Kutumia ulimi kunyonya viungo vya kiume au vya viungo vya kike ni Sodoma. Mdomo kazi yake ni kumsifu MUNGU na kula, madhara yake utapokea laana ya kuwa kibogoyo na meno yatang’oka mapema na uthamani wa kinywa chako kuibiwa na shetani. Ulimi hutumiwa na wanyama kama mbuzi, ng’ombe, nyani sasa wewe kwa nini uwe kama mnyama?;

·        Mitindo ya chuma mchicha, mbuzi kagoma, kukutana kama jogoo anayempanda mtetea, mwanamume kulala chini halafu mwanamke anamlalia juu ili kutenda tendo la ndoa;

·        Kunyonya viungo vya siri mpaka mbegu zitoke na zaidi zinamezwa kama chakula, mbegu hizo zinatakiwa ziende mahali pake na siyo kwenye kinywa cha mtu, kwa njia hiyo elewa umerudia matapishi ya Sodoma na Gomora na kukufanya uje uchomwe moto katika siku ile ya hukumu, hivyo ni bora uache kabisa sasa hivi na utubu;

·        Na zaidi utaweza kukuta watu wa jinsia moja wanaoana, mfano mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke na wanafunga ndoa na wanaishi kwa kusudi la kuwa mwili mmoja kwa njia za shetani. Wakristo kama wanampenda MUNGU wafunguke, dunia yote wasikubali kuongozwa na mchungaji shoga, awe wa kike au wa kiume, yeye tayari ameshakuwa mtaji wa Jehanamu na anapokuongoza kiroho na wewe unanajisika katika roho, alipo yeye anayekuongoza na wewe utamfuata huko huko. Jinsi alivyo kuhani ndivyo alivyo muumini. Je! utapenda kuitwa muumini wa shoga?;

·        Kuzini na wanyama;

·        Kufanya punyeto;

·        Kuzini na roboti au sanamu za ngono (artificial sex organs) au sanamu.

Angalizo: Yapo mengi kwa kupitia haya mafundisho yatakusaidia na utapona kabisa ila yakupasa kutubu. Sema, BWANA YESU naomba unisamehe, dhambi zangu zote ikiwamo hii ya Sodoma na Gomora, nakataa mimi siyo mtaji wa Jehanamu, naivunja ndoa ya Sodoma katika ulimwengu wa roho na mwili. Amen.

NABII HEBRON.