Pages

Wednesday, June 14, 2017


JE UNAJUA BAADHI YA WATEULE WAMESHAPIGWA NAMBA YA MPINGA KRISTO AMBAYO NI NAMBA 666 KUPITIA MAJIRA YA SAA?


UFUNUO 13:18

Shalom watu wa MUNGU wa mataifa yote walio wateule wa kwenda mbinguni na wale wote ambao hawajajua habari za YESU wa Nazareti, nikimaanisha ambao hawajaokoka. Hiki ndicho kipindi cha neema, bado kitambo kidogo tu Mwana wa pekee atarudi kuja kuwanyakua wale ambao wamekubali kuishi maisha Matakatifu na siyo ya dhambi. Ufunuo 13:18 “18Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu  ya kibinadamu. Na hesabu yake  ni mia sita, sitini na sita”.

Na katika mwaka huu wote ambao nawaandikia mimi Nabii Hebron, watu wote wa dunia yote  ili mjielewe na muweze kupona na kuikataa hii namba 666 ambayo imeletwa kwa njia ya kubadilisha majira ya saa. Mnamo mwaka 2009, nikuwa katika kazi aliyonipa BWANA kwa muda, ili aniandae kwenda kumtumikia, pasipo mimi kujua, mpaka pale alipokuja kunijulisha, ndipo baada ya mwaka nilianza kuongea na malaika Gabriel, nikiwa jiji la Arusha wakati natokea Sanawari kupitia barabara ya AICC (Arusha) kuelekea mjini, nilipofika eneo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa, pale kwenye mzunguko (round about),  nilishikwa na butwaa na sikuweza kumweleza mtu yeyote yule mpaka  leo hii ndio nawaeleza, mengine bado muda wake wa kuyasema, wakati huo nilikimbiwa na kukataliwa hata na baadhi ya watu katika familia yangu, marafiki na ndugu wa karibu. Maisha yalikuwa yameharibiwa na wachawi, kazi zangu zote ziliharibiwa, yamkini walitaka nife kimwili lakini ikashindikana, wachawi walitaka kunitoa kafara na mambo mengine mengi mabaya waliyokuwa wamenipangia hayakuwezekana. Baadhi ya hao walikuwa wakijiita watumishi wa MUNGU kumbe walikuwa ni watumishi wa shetani. MUNGU alinitenga nao kwa sababu MUNGU alikuwa na kusudi na mimi, na mengi MUNGU alikuwa ananieleza lakini sikuweza kumjibu mtu kitu, na wakati hayo yalipokuwa yakitokea sikuwa na mbele wala nyuma. Nilikuwa nimehifadhiwa kwa mtu ambaye MUNGU ndiye aliyemwandaa, lakini pia hata yeye pamoja na familia yake hawakulijua hilo, ila MUNGU ambariki sana na tayari alishabarikiwa pamoja na familia yake.

Sasa siku hiyo, majira ya saa yangu ya mkononi yalionyesha 2:30pm (two thirty), yaani saa nane na nusu mchana, lakini cha ajabu Malaika Gabriel aliniambia majira halisi na kwa namba au tarakimu za kiswahili na akaniambia atakuja kuongea na mimi wakati mwingine, tena kwa muda wa masaa ya Afrika Mashariki lakini sikumwelewa, na siku nyingine nikiwa na watalii wa kijerumani katika eneo la Ngorongoro kuelekea Lake Natron alisema na mimi na huyo alikuwa ni Malaika mwingine Mikael, akasema, tupo na wewe Hebron katika safari hii tokea muda fulani, kwa majira ya nchi yako, na safari hiyo ilikuwa ina ugumu kwa sababu  shetani alijua kuwa nitakuwa nani hapo baadae,  hivyo alitaka nianguke na gari wakati nikipita katika mlima Natron, mlima huo mrefu  sana, wenye kona nyingi wakati ukitokea Lobo kupitia Loliondo kuelekea ziwa Natron na kisha unafika katika mji wa Natron, lakini nilifika chini salama  na nilimaliza safari na wageni wangu salama.

Malaika Mikaeli alikuwa amevaa saa yake iliyokuwa mkononi  haisemi uongo,  au kwa lugha nyingine tulifundishwa shuleni eti saba ndio saa moja (7am), na moja ndio saa saba (1pm) na alikuwa akionyesha majira lakini cha ajabu alikuwa hataki kabisa kuangalia saa yangu, nilidhani kuwa labda kwa vile ilikuwa ya bei rahisi au haifai, kwa maana ya kwake ilikuwa ni ya gharama,  la hasha, kumbe ni kwa sababu saa yangu ilikuwa ikisoma majira tofauti na ya Mbinguni.

Malaika Mikaeli alipokuwa akija alikuwa anapewa muda wa kuongea na mimi, muda aliopewa na MUNGU, na alipokuwa akianza kuongea na mimi alikuwa akiangalia muda na dakika kila mara, na zilipokuwa zimebakia dakika chache alikuwa ananiaga, kuwa muda wake ulikuwa umekwisha, lakini akili yangu ilikuwa ni ya kijinga, nilikuwa naonyeshwa na kufundishwa kuhusu majira ya saa lakini sikuelewa. Ilipofika wakati wake nilimwona YESU akija kwenye gari la wageni nililokuwa naendesha, na alikuwa ananiambia vua saa yako, halafu ndio anaanza kuongea na mimi, hata kwa masaa mawili, nikiwa naendesha gari kwenye mapori ya wanyama na ilipofika mwaka 2010, akaniambia kuanzia sasa saa yako isome kwa namba za Kiswahili kama ilivyo saa moja ni saa moja, saa mbili ni saa mbili na saa tatu ni saa tatu. 

YESU akaniambia, Hebron hivyo ndivyo adui alivyouteka ulimwengu na kuweka uongo na kufanya hata mtu ambaye ananipenda asije akafika mbinguni, ili mradi tu awe nakizuizi, kwa sababu MUNGU yeye ni wa haki na siku ile ya mwisho, shetani anamshitaki kila mtu kuwa hao siyo watu wako sababu wanatembea na namba 666, katika majira yao. Sasa mimi nawaeleza mataifa yote mfanye marekebisho katika saa zenu, iwe za nyumbani, ofisini, katika gari na za mikononi.

Wewe ambaye hupendi namba hii 666, unakuwa umeweka majira ya uongo, kama nitakavyoelezea hapa chini, utaona mwenyewe, utafanya mahesabu utakuta kila saa ni namba 6 badala ya saa ya kweli na zaidi hata ukisoma kwa lugha ya kingereza namba 1 ni one na sio seven, na namba 2 ni two na sio 8. Shetani ni mjinga sana, na je umesha jiuliza ni kwa nini saa saba inakuwa one o’clock, au saa sita kuitwa 12 o’clock? Jibu ndio hilo alilolileta shetani ili kila anayebadili au kuandika saa yake hivyo anakuwa anaishi na kutembea na namba 666 pasipo yeye kujua ila wengine ni kwa kujua.

Nitaeleza kwa kifupi ila kwa ufasaha namna namba hii 666 ilivyotengenezwa na jinsi ilivyofuatwa na dunia yote.

Majina ya namba 666, saa 1 inaitwa 7 na ukitoa 7-1=6

Mfano:

Saa                          

Inaitwa

Ukitoa
1
7
7-1=6
2
8
8-2=6
3
9
9-3=6
4
10
10-4=6
5
11
11-5=6
6
12
12-6=6
7
13
13-7=6
8
14
14-8=6
9
15
15-9=6
10
16
16-10=6
11
17
17-11=6
12
18
18-12=6
13
19
19-13=6
14
20
20-14=6
15
21
21-15=6
16
22
22-16=6
17
23
23-17=6
18
24
24-18=6

Mpaka hapo watu wote wa dunia hakuna anayeweza kubisha kuwa hiyo si namba 666, na cha ajabu hebu jiulize, siku moja ina masaa mangapi? Jibu ni masaa 24, utakuta ni masaa 18 (18 hours) na siyo masaa 24 (24 hours) sasa anza kuhesabu kuanzia 7 mpaka 24, utakuta ni masaa 18 na sio 24, hivyo basi utakuwa unafuata majira hayo ya uelewe na wewe hata siku yako inashikiliwa na 666.

 Nilimshukuru YESU kwa kunifunulia siri hii, japo ziko nyingi za namba 666 na zaidi waulize Warumi walinunua saa zenye namba za kirumi zinazosoma I ni saa 1, II ni saa 2, III ni saa 3, IV ni saa 4, n.k. kwa nini unadanganywa kirahisi? Wapo Wasomi wa mahesabu kwa nini wasifundishe ukweli? Wamefungwa fahamu na kuongozwa na roho, hiyo. Hata mimi Hebron nilifuata huo uongo, ni cha ajabu hata makanisani utaona baadhi  wanaandika majira ya uongo, mfano Ibada inaanza 02:30-20:00 hrs, yaani ibada inaanza saa nane na nusu mchana, mpaka saa mbili kamili usiku, wakati huo ni uongo, ibada zipo katika uongo na kufanya MUNGU na ROHO MTAKATIFU asionekane katika ibada hizo kwa sababu  kibao chenyewe cha ratiba za ibada kinaonyesha majira ya 666. Kwenye maofisi na hata kwenye sehemu za biashara,  angalia saa utakuta inaishi na  namba 666, yaani inaishia na mpinga kristo. Unaweza ukajiona kweli wewe haumpendi mpinga kristo, lakini mbona unaishi naye, unatembea naye na mpaka ukikata roho unatembea na majira ya 666, hicho kinakuwa ni kibali kamili cha kuchukuliwa na ufalme wa giza.

Zaidi fuatilia katika website: www.prophethebron.org; pia ingia katika link ya YouTube na Blog utajifunza mengi na yatakusaidia kufika mbinguni siku moja.

  Karibu kwa YESU umfungulie moyo wako. Sema, Bwana YESU, naomba unisaheme dhambi zangu zote, uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, uniondolee namba 666, sitaki kutembea nayo, nashukuru nimejua ukweli na sasa nachukua hatua kufuata majira ya kweli yanayofuatwa na Mbinguni, sitaki majira ya kuzimu tena. Amen.

Angalizo:  Kwa maana nyingine haya majira ya uongo ndio majira yanayotumika kuzimu, na unapoyafuata unakuwa upo katika majira ya kuzimu au kwa maana nyingine unakuwa umefuata majira ya freemason, au kuishi na majira ya freemason aidha kwa kujua au kutokujua. Huo unakuwa ni mlango wao wa kukuibia vitu vyako, kwa sababu wana uhalali huo wa majira yao ambayo ni ya uongo, ambayo umeyakubali yakuongoze badala ya kukubali majira ya kweli ya mbinguni.

NABII HEBRON