Pages

Saturday, May 13, 2017


 

                            NINI MAANA YA PASAKA NA EASTER DAY?
                                              (Easter ni mungu mke)
 

SHALOM, BWANA YESU ASIFIWE,  tutasoma  neno la MUNGU,  kutoka katika kitabu cha KUTOKA 12:11-14 neno la  MUNGU linasema;   11 Tena mtamla hivi; mtakula mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka ; ni Pasaka ya BWANA .  12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza  wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami  nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri. 14 Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.

Leo tutajifunza habari ya Pasaka si habari ngeni na wengi tunaijua Pasaka, lakini nataka tujifunze kuhusu Pasaka, je! Pasaka ina faida gani na Pasaka ni nini?

Pia tunasoma neno la MUNGU, kutoka katika kitabu cha MAMBO YA WALAWI 23:7-8. 7 Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye yoyote ya utumishi. 8 Lakini mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.

BWANA YESU ASIFIWE, maana wako wengine wanasema Jumamosi ni Pasaka lakini Biblia inasema siku ya saba, hii inatukumbusha kwamba Pasaka kuna sadaka yake, na ile siku ya saba pia. Lakini lengo kubwa hapa nataka tujifunze kuhusu pasaka na Pasaka ni nini?  Maana MUNGU aliponiita aliniambia nataka ukarejeshe ulimwengu kama ninavyotaka mimi maana umeharibika kwa asilimia kubwa sana.

 Neno Pasaka  limetoka kwenye neno la kiingereza PASS OVER yaani MUNGU alipita juu ya wana wa Israeli;  kuanzia alipokuwa kule jangwani  na waliponywa kupitia damu ya wanyama ambapo walichinja wakaweka kwenye milango kwa hiyo MALAIKA WA BWANA alipopiga usiku aliondoa mauti kwa wana wa Israeli,  wale ambao walikuwa hawajaweka walikufa, hiyo ndiyo Pasaka  ya kwanza.

 Biblia inasema muifanye kila mwaka vizazi na vizazi kwa hiyo na YESU alipozaliwa aliikuta kwa hiyo na yeye alikula Pasaka kwa miaka 32 YESU alikula Pasaka hiyohiyo, lakini Pasaka ya mwisho ambayo MUNGU ametupa ni BWANA YESU, baada ya BWANA YESU kuja tukawa hatumwagi damu za wanyama tena, wala kuchinja na kuweka juu ya milango kwasababu DAMU YA YESU ilimwagika na kumaliza kila kitu  ikatuondolea mauti, alikufa, akazikwa, akafufuka tumekuwa na ushindi yaani kuwa hata tukifa tutafufuka.

 BWANA YESU ASIFIWE, lakini nataka nikuulize hivi wewe huwa unasherekea Pasaka au Easter? Sasa leo tutamchambua easter vizuri, sidhani kwamba ulipokuwa ukisoma Biblia ulishakuta mahali umeambiwa usheherekee easter? Tafuta kwenye Biblia ya kiarabu, ya kijerumani, ya kiingereza hakuna kusheherekea kitu kinaitwa easter ni PASS OVER yaani Pasaka kwa Kiswahili. BWANA YESU ASIFIIWE lakini kuna mahali shetani alifanya mambo yake, lakini sasa nataka Pasaka irejee kama vile MUNGU alivyotaka na anavyotaka iwe katika Dunia nzima, haya mambo ya easter kuanzia leo hayatakuwepo tena.

Lakini nataka nikufundishe, na uelewe kuwa  unaabudu kitu usichokijua sio ESTA, kuna ESTA ya kiingereza, na kuna easter, sasa nikuulize kuwa ni sehemu ipi katika Biblia imeandikwa kila mwaka mtakuwa mnakumbuka easter? Wasomi wa Biblia ya kiingereza kasomeni, haijaandikwa hivyo.

BWANA YESU ASIFIWE nilikuwa nimekaa na MUNGU nikasikia ananiambia Hebron easter vipi? Hivi easter ni nini? Sasa akishaniambia hivyo najua ni wakati muafaka wa mimi kuwaeleza jinsi ambavyo MUNGU anataka iwe, kama hajaniambia sizungumzi,  aniuliza  je! mimi ni easter? YESU akaniambia Hebron hivi easter ni nini? Nami nikamuuliza kwa nini? akaniambia ni wakati wake sasa wa kuwafundisha  ulimwengu,  kwamba mimi siyo easter mimi ni Pasaka, nitakutafsiria kwa kiingereza, mpaka easter ilivyokuja na ikatolewa Pasaka.

Tunadanganyana hapa na makanisani wanasema happy easter badala ya heri ya Pasaka, ni  jinsi ulimwengu ulivyopotea muda mrefu ziko Pasaka  za kweli, ziko pasaka za kipagani, na ziko za kimiungu.

Pasaka ya kwanza ni ile ya wana wa Israeli walivyokuwa jangwani, Pasaka ya pili ni ile ya BWANA YESU mwenyewe, sasa kwanini Pasaka  isiitwe PASSOVER? wazungu wakabadilisha na kuiita easter? Soma Biblia ya kiingereza je kuna kitu inaitwa easter? Wala Pasaka haiitwi jina lingine easter hakuna. BWANA YESU ASIFIWE lakini nitakufundisha kidogo ,  na  pia unaposoma Biblia  haijasema tuabudu easter jamani uliza hata wazungu inaitwa ni PASSOVER sasa kama MUNGU ameleta PASSOVER yaani Pasaka sisi tunaleta easter nani kichaa hapa? Biblia inasema wanadamu wameangamia kwa kukosa maarifa je? nani kaileta hii easter?

Je sisi tumeletewa easter au tumeletewa Pasaka? Sisi tumeletewa Pasaka,  sasa kwanini  huwa tunasema happy easter? Uthamani wa neno Pasaka ulifichwa na shetani ndipo tukaletewa easter. BWANA YESU ASIFIWE sidhani kama  mnanielewa; lakini bado nataka tuichambue easter vizuri nataka uelewe, unajua mimi napenda mtu aelewe, maana jambo hili lina madhara makubwa sana , hata mimi Hebron nimeikuta, sikujua na mimi nilikuwa nasema happy easter kumbe nimepokea na kushiriki pasaka ya kipagani, Waisraeli wenyewe ni wajanja hawajakubali kusema happy easter, wamesema Pasaka tu BWANA YESU ASIFIWE,  YESU hajakuta inaitwa easter, amekuta inaitwa Pasaka tu MITUME WA YESU hawajawahi kusema easter wamesema Pasaka  tu lakini akaja anayeitwa mungu wa kughushi. (kufoji), na kuifanya Easter itapakae dunia nzima.

 Katika karne ya nane, kasisi mmoja akaibadilisha maana zamani ulikuwa ukiletewa Injili ya mahali Fulani, kuna wafalme  nao wana miungu yao, sasa yuko mungu anaitwa mungu easter yuko huko ujerumani . Kwa hiyo ile siku ya Pasaka yuko mungu wa kijerumani anaitwa mungu mke, mungu wa kike alikuwa anaabudiwa na wafalme huko ujerumani zamani BWANA YESU ASIFIWE.

 Mnanielewa jamani kwa hiyo walipokuwa wakianziasha jambo jipya lazima lipitie kwake, BWANA YESU ASIFIWE kwa hiyo wakaiba Pasaka wakaiita easter, sasa easter ina maana ya Mashariki kwa kijerumani ostern BWANA YESU ASIFIWE, hii easter shetani bado akaichezea chezea ina maana ni Mashariki sasa ikaongezwa “r” pale wakaondoa “n” ingekuwa “n” ingeitwa easten watu wangeshituka kuwa mbona ni Mashariki. BWANA YESU ASIFIWE sasa nikuulize jamani MUNGU alizunguka Mashariki au alizunguka juu? Unaona wanadamu wanavyoangamia, unaona sasa  kwahiyo miaka na miaka hata mataifa ya Ulaya na wenyewe ile sherehe ikaanza kubadilika easter sasa mnaelewa?  tukapigwa uvuvio wa kutupumbaza kama na mimi pia nilivyopigwa na uvuvio huo nikaamini easter ndio Pasaka na nimesoma na nimeelewa kama na wewe ulivyosoma, ukisoma Biblia, ukichambua unakuta kabisa MUNGU hakuleta easter alisema Pasaka.

Pasaka kwa kiigiriki ina maana yake, kwa kiebrania ina maana yake kwa kichaga ina maana yake kwa Kiswahili inaitwa Pasaka kwa kiingereza inaitwa PASSOVER sasa mimi nashangaa tunaabudu Mashariki nini wewe unasema furaha ya Mashariki? Unaona tulivyovurugwa? Matokeo yake sasa unaposema happy easter, au unasheherekea easter unaungana na mungu wa kipagani, Je!  Wewe hujaabudu mungu wa kipagani? pale unaposema kwa  kinywa tu unakuwa umeshiriki, sasa utajiuliza mbona makanisani wanasema happy easter? Hivyo ndivyo kanisa lilivyotekwa na shetani katika maeneo mengi, linafanya mambo lisilo yajua ndio maana unaambiwa kwenye Biblia Utukufu wa mwisho ni mkubwa kuliko wa kwanza . MUNGU amenituma kuyafichua yote, utashindwa kwenda Mbinguni ,utashindwa kusheherekea Pasaka kwa kusema happy easter hata Kanisani  kwangu sitaki kusikia hicho kitu.

Sasa Pasaka hii watu wengi wamekula ya kipagani, ni mungu mke wamemsherekea, wewe mwanamke unamuabudu  na huyu mungu mke mpaka sasa hivi kwa wazungu wanavyomsheherekea wanatumiaga sungura maana sungura wanaamini ni mnyama anayezaa sana kipindi cha mwezi wa 3 na mwezi wa 4 BWANA YESU ASIFIWE halafu wanachukua na mayai wanachora msalaba, kwa hiyo sasa wanawapa watu zawadi huku wakiamini kabisa yale mayai ukipewa utapata miujiza na baraka ndipo ikaanza enzi ya miungu mpaka sasa hivi Ulaya wakati wa Pasaka wanatoa sungura na mayai je! nikuulize YESU alileta sungura na mayai?  kwanza sungura ni mnyama ambaye kiroho anatafsiriwa muongomuongo, mjanjamjanja BWANA YESU ASIFIWE  sasa huyu easter akasambaa kila mahali, unakuta mtu ana master au ni doctor amesomea Biblia na yeye bado anasema happy easter na yeye amevurugwa na shetani na akili imepumbazwa muulize kama MUNGU alileta easter?  Hatakuwa na jibu sasa huyu shetani mmbea anakaa pemben ianakushtaki kwa MUNGU, anasema siunaona wanamuabudu easter  huku likicheka hehehee! Huku akisema hawa ni wangu, sasa ndivyo ilivyo kipindi cha Pasaka watu wengi utasikia wakisema happy easter,

Makanisani happy Easter, mapastor happy easter yaani mnakuwa mmesema furaha ya yule mungu mke wa kipagani, jambo hili ni matokeo ya kuwa wakati wa pasaka  watu hawafufuliwi kiroho, sasa kwa kusema neno easter watu hawainuliwi kiroho, wala hawasongi mbele, yule mungu wa kipagani anawamaliza kwa sababu anao mlango,(uhalali nao) sasa wewe nyumbani kwako pambo happy easter kwanini usichukue pambo la heri ya Pasaka?

 Fahamu kwanza  kuwa hii easter ilianzia wapi, ni  kwa jamaa zetu weupe lakini watapona BWANA YESU ASIFIWE hakuna anayeweza kukataa jambo hili  ninalokuambia ndio maana shetani anatamanigi nife mimi “Sitakufa” nitawaambia ukweli tu, kwahiyo  sasa kuanzia leo mwisho kusema happy easter, utasema ninafunga mfungo ili ninyanyuke utanyanyuka kweli? BWANA YESU ASIFIWE .

MUNGU alimleta Mwanae ili kwamba tukapate kupona lakini unakuta hii pasaka ibada zinafanyika sehemu mbalimbali baadhi, maisha ya watu hayana mabadiliko kwa hiyo kipindi cha Pasaka  ni kipindi cha watu kunyanyuliwa kila mwaka kiwango kingine na kingine kama ni mtumishi kiwango kingine na kingine lakini yuko easter, Mimi sitaki kusikia kwenye Kanisa  langu mtu anasema happy easter. Sasa kwanini wapagani wakawa na mungu mke anaitwa easter?  Zamani walikuwa wanaangalia jua linachomoza Mashariki linaenda Magharibi kwa hiyo wakawa wanaona Mashariki ndiko kunakoanzia mambo mazuri BWANA YESU ASIFIWE kuna shida imani zimekufa, zimekuwa za kipagani, ukija kwenye amri ya MUNGU inasema usiabudu miungu na wewe unasema huabudu miungu je? Hii happy easter je? Message zako za happy easter utachorewa na vinyumba , utachorewa na keki  imeandikwa happy easter sasa heri nyie mnaojua Kiswahili tunasema Pasaka maana huku kwetu haijachakachuliwa sana, sasa ibada zote za kizungu ni happy easter utasikia wakisema today is easter day! Haleluya! anakuambia hawasemi PASSOVER today wanasema ooh receive the bless of easter utachukuwa baraka na kipagani mpaka ukome, sasa tazama ni mataifa mangapi wanasema  happy easter?

 Ukiangalia kwenye TV utaona kwenye matangazo I wish you happy Easter jamani yaani huyu mungu wa kipagani tu ndio anatajwa, mara utasikia karibu dinner ya Easter, kwanini usimwambie karibu Pasaka?  Utamkapo neno hili kwa kujua au kutokujua ujue tayari umemla huyo jamaa, mungu mke; sasa iweje dunia nzima shetani ameirubuni hata watu wasielewe kwamba hiki hakifai? Sasa mnaelewa jamani tafuta kwenye Biblia kama kuna easter ukiangalia kwenye dictionary watakuambia ni Pasaka. (watakuambia easter day kwasababu hawajui) sasa ni lazima NENO LA MUNGU lisibadilishwe lazima litajwe lilelile BWANA YESU ASIFIWE siyo tunaletewa maneno ya uongo uongo halafu tunapokea haya hayajaanza leo yameanza miaka mingi utasikia wafalme wanasema ninawatakia happy easter wananchi wangu, tusiendelee jamani kumuabudu MUNGU kwa kisaniisanii au kikomedikomedi ndivyo watakavyokuja siku ile ya Pasaka MALAIKA wanakuja kukutembelea, ili baraka zako zije kwako,

MUNGU haji kwako MALAIKA hawatembelei maisha yako  kwasababu umemtaja easter hapo unakuwa umemfukuza MUNGU halafu unataka vitu vya MUNGU? ; lazima ulimwengu ujue ukweki sasa, soma Biblia hakuna kitu kinaitwa easter hata wale waanzilishi wa kule jangwani kina Musa hawakusema easter sasa imetoka wapi? Ikaingizwa ndani ya watu ikasambazwa, ile siku sasa ya Pasaka  wanaambiwa happy easter mimi Hebron nimetumwa habari ya kueleza Pasaka, sasa easter ikasambazwa wakatumwa Wamissionary wambeawambea na waongo wakasambaza wakapewa na pesa na magari kutusambazia uongo ni wakati wa kuteketeza ndio maana na wewe umepotea kwasababu umepokea uongo jua kwamba kuna Wamissionary wa uongo kuna washetani wakusambaza kazi za ibilisi kama ilivyo lazima ziondoke, wakati MUNGU amemleta YESU kwa ajili yetu Pasaka hakuileta ichezewe kupitia hili JINA LA BWANA YESU,  BWANA YESU ASIFIWE .

Muulize mtumishi yeyote maana ya easter, hatakuwa na jibu sasa ukiongozwa na kipofu unaenda wapi? Shimoni ndio jinsi ambavyo dunia imeenda shimoni BWANA YESU ASIFI  Sasa nikuulize MUNGU alipita Mashariki ili akuokoe? MUNGU si alipita juu sasa tunakwenda wapi? Imani yako inapotea, unakaa kila mwaka unasema happy easter unapotea hata na yule anayetengeneza kadi anaiga na yeye amepotea, mtaigaiga mpaka mapepo,  YESU alienda kuzimu akanyanyuka sasa amekwenda  kwa ajili yako yaani ili kila mwaka vitu vyako viwe vinashuka kwa ajili yako na kunyanyuliwa lakini unasema happy easter baraka zako zinapita mpaka mwaka mwingine tena BWANA YESU ASIFIWE.

Shetani akome amebadilisha vitu vingi sana yaani hata siku ya MWANA WA MUNGU kusulubiwa msalabani ametolewa sadaka atubadilishie iitwe Mashariki?  hakikisha kitu unachotamka unakijua sasa Pasaka ikafichwa, lakini yupo MUNGU achunguzaye, endapo kuna shida ipo wapi?  siku ile ya mwisho utasema mimi sikuabudu miungu, ndipo  li happy easter linatoka na mkia wake, linakushitaki kuwa wewe kila mwaka unanitaja, Mara utasikia kongamano la easter, semina maarufu ya easter sasa hapo lazima adhihirike huyo mungu easter kwasababu mmeshamtaja , mimi namjua YESU aliyekufa ndio maana na mimi nina Pasaka,  unajua ukisema kweli watu wananuna wenyewe wanune lakini shetani akome, watu wapone, unajua ukishapenda uongo ina maana na wewe hautaki tena kwenda Mbinguni  unataka kwenda jehanamu, sasa watu wanamuabudu huyu mungu wa kipagani, mungu mwanamke wakati kuna MUNGU MWANAMUME tunamuacha BABA YETU, tunaanza kwenda kwa miungu ya kike, BWANA YESU ASIFIWE sasa nikuulize  Pasaka ni nini na easter ni nini? easter nimekufundisha kwamba ni mungu wa kipagani wa kike akaingizwa kwenye Pasaka ili Pasaka  iishe nguvu ili watu wasiinuliwe, watu wasimuone MUNGU hii  nguvu ya kupumbaza itoke dunia nzima na itoke kama nyie mnavyosoma sasa ni wakati wa kuikataa na lile pepo liondoke hata ninavyokuambia sasa hivi akili yako inavyofunguka ina maana bado ilikuwa imepumbazwa na gundi ya shetani usielewe yanawekwa mapepo ya ulinzi usijue siri hii sasa umejua, umefunga mifungo mingi kwa miaka mingapi? siku arobaini? Je ni kwa MUNGU au kwa easter sasa ashukuriwe MUNGU nimekujulisha ili ukifunga kitu kijibu. BWANA YESU ASIFIWE lakini tunaita easter.

 MUNGU si ametupa Pasaka? Sasa kama si kuchanganyikiwa na kutaja vitu ambavyo vimeingizwa kimchomeko kwenye JINA LA BWANA YESU, sasa haikutosha sasa hivi katika dunia hii bado kuna watu wana pasaka zao wanachinja mbuzi, au kondoo zinachinjwa hivyohivyo,  BWANA YESU ASIFIWE sasa MUNGU akatupa MWANA KONDOO WAKE ndio maana mpaka leo husikii watu wanachinja kwa ajili ya Pasaka kwa hiyo ibada za kuchinja zote zinazofanyika sasa hivi hizo zinakuwa ni makafara si za YESU, YESU alishamaliza kila kitu MUNGU alituletea yeye na ndio maana akasema hivi Pasaka nyingine nitakula nikiwa na nyie nitakaporudi, alikula na wanafunzi wake maana ile siku walimla yeye na yeye YESU akala Pasaka  na wanafunzi wake BWANA YESU ASIFIWE  lakini ilikuwa bado ni mafunuo yamefichwa msielewe

 BWANA YESU ASIFIWE:  MITUME wake wakala Pasaka kama wale walivyo kula Pasaka na ndio wakatuambukiza dunia nzima kufuata  Pasaka, wakaendelea kusema Pasaka NI YESU, lakini haikutosha walivyoondoka na kufa wajamaa wengine wakaanza kubadilisha easter, sasa amenituma kun’goa eastern na mengineyo, unajua shetani anafikirigi MUNGU hana watu wake  ambao amewaandaa watasema kweli sasa ni wakati wakulipiga hili li mungu easter na kulibomoa katika JINA LA YESU, ashukuliwe MWENYEZI MUNGU yeye ambaye ametupa neema ya kujua Neno lake la kweli na jinsi ya kutufungulia tupate kuelewa.

 Ukisoma 2WAKORITHO 4:2-4  2 Lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya Neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU 3 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake MUNGU.

Mnaona sasa fikira zimepofushwa tufanywe watu wa dunia hii kupokea injili ambayo si mpango wa MUNGU huku  baadhi ya makanisa na watumishi wametulia tu  hawataki kuongea maana wanakatazagwa na shetani wasiongee hivyo ndivyo shetani alivyolichezea NENO LA MUNGU na kupiga upofu na kulizuia; haya ikaja tena ikikaribia Pasaka watu wanaambiwa msile nyama eti mtakuwa mnamla YESU jamani nyie kuleni nyama YESU YUKO MBINGUNI,  BWANA  YESU ASIFIWE siku ya Pasaka ni siku ya furaha siyo kurudisha tena watu kwenye majonzi eti YESU anakata roho YESU YUKO MBINGUNI.

MBINGUNI hawajui easter wanajua Pasaka sasa wewe unaabudu kitu ambacho kimetolewa kwenye midomo ya watu? Ukisoma ufunuo 22:18-19 ole wake aongezae maneno ya kitabu cha unabii huu, sasa neno easter limeongezwa yaani kwa namna hiyo shetani anapata watu wengi siku ile ya mwisho.

Ukisoma NENO LA MUNGU KATIKA KITABU CHA UFUNUO 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Ibilisi na shetani audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Yule joka audanganyae ulimwengu ametupwa ameudanganya ulimwengu umeacha kusema heri ya Pasaka  unasema happy easter sasa mnaona BWANA YESU ASIFIWE hii yote unapumbazwa ili usikutane na muujiza wako ili kwamba usikutane na ile ahadi MWENYEZI MUNGU aliyoileta kwa ajili ya mtoto wake kwa ajili yako wewe ukanyanyuliwe, sasa wamekuwepo baadhi ya watumishi  ni wahuni wengine ni wachawi wanatumia NENO LA MUNGU huku wanaenda kuzimu, mimi kuzimu nimefika na MBINGUNI nimefika ninawaambia ninachokijua unayesikia sikia utakwenda kupona, BWANA YESU ASIFIWE ,shetani huko  kuzimu wao wanasheherekea easter ndio maana unasikia kuna pasaka ya kuzimu hiyo ndiyo inaitwa easter.

MBINGUNI wanasheherekea Pasaka wanakumbuka vile MUNGU alivyofanya wanampa BWANA YESU hongera kwa kufanya kazi nzuri Haleluya sasa na huko kuzimu wanamwambia easter ulifanya kazi nzuri tumeshawachukua wanadamu husikii wanasema happy easter, sasa fikira zimeharibiwa shetani ameudanganya ulimwengu,  lakini shetani ili afanye kazi na MUNGU ili afanye kazi anamtumia mwanadamu anayemkubali ndio maana mtu anatumia JINA LA YESU anatafuta pesa anakuambia BWANA  amesema lete laki utaponywa mimi namjua huyu MUNGU WA MBINGUNI yeye hachukui pesa anakuponya bure, utasema umemuona nabii kumbe umemuona mchawi.

Ukisoma NENO LA MUNGU kutoka katika kitabu cha 1WAKORINTHO 5:7-8 7 Basi jisafisheni mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani Kristo 8 Basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

Sasa Pasaka iliyochachika ndio unaitaka? easter ndio kuchakachua huko BWANA YESU ASIFIWE imani zimeharibiwa, baraka zimeharibiwa yaani ni kama DAMU YA YESU imechacha ndivyo maisha yalivyokuwa kwa wana wa Israel kule jangwani walikula mikate michachu si ndio?  lakini YESU yeye siyo mchachu usifuate chachu ya zamani  DAMU YA BWANA YESU haijachacha ni fresh BWANA YESU ASIFIWE

Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua na kutokujua ninamkataa shetani na mambo yake yote nakushukuru kwa siku ya leo nimejua ukweli kuhusu Pasaka, na namna ya kutofautisha kati ya Pasaka na easter na maana zake, simtaki tena mungu wa kike katika JINA LA YESU Amen.

NABII HEBRON