JE MAANA YA EASTER
NI PASAKA?
SHALOM, Maana ya Easter siyo
Pasaka na Pasaka haiitwi Easter, bali neno Easter linatumika kulifanya jina
hili lionekane ndio Pasaka katika sherehe ya kufufuka na siku ya kufufuka kwake BWANA YESU, neno hili
lina maanisha mungu wa kike wa kijerumani, ambaye alipewa hiyo nafasi miaka
mingi na watumishi ambao walikuwa chini ya wafalme wa kijerumani ambao
waliongozwa na huyo mungu mke ambaye aliitwa Ostren (yaani Mashariki) na
baadaye ikaendelea katika dunia yote kwa lugha ya kiingereza akaitwa Easter
wakatupiga upofu kuondoa “N” mbele sababu watu wangegundua ni Mashariki na
Mashariki siyo Pasaka.
Hivyo usiseme unasherekea Easter
tena, unaposema unakuwa umemsherekea
huyo mungu wa kike na siyo YESU, na ukitaka kusherekea Pasaka ya YESU wa kweli
sema nasherekea Pasaka, na kwa kiingereza sema happy Passover.
Nashangaa sana, mimi nilishafanya kazi ya utalii na nilishawabeba
Waisraeli wengi sana tena hata katika kipindi cha Pasaka nilipokuwa nipo nao
katika safari za utalii (adventure) kama kiongozi wao, sikusikia wakisema happy
Easter walikuwa wananiambia happy Passover, sasa cha ajabu, huko kuliko anzia
asili ya Pasaka wao bado wanakiri
Pasaka, lakini huko ambapo siyo chimbuko
alikotokea YESU wameghushi (wamefoji) kutupoteza mataifa tuabudu huyu mungu wa
kike,
Huu ni mwisho wa shetani kughushi
(kufoji) vitu vya MUNGU, zaidi soma blog hii prophethebron.blogspot.com nimeelezea zaidi kuhusu Pasaka ni nini na
Easter ni nini?
NABII HEBRON