MAOMBI YA MTUMISHI
YA KUMLALIA MUUMINI AU MTU KIFUANI KWA NINI WANAYAFANYA?
Yapo maombezi yakutia aibu kiasi fulani
yanawafanya watu wengi kutokutetea habari za YESU sababu ya makwazo hayo na
mengineyo, mimi nawaeleza haya siyo ya YESU hayo ni ya maagano na YESU hana
maagano yoyote juu ya kichawi na ya giza au uchafu. Sasa kuhusu kufanyiwa
maombi unaambiwa ulale chini mwanamke, halafu mtumishi analala katika kifua
chako amekushika mkono kama vile watu wanavyozini na ameweka miguu yake
katikati ya mwanamke halafu anafanya maombi akimuombea mtu, na mtu sababu ya
shida ya kutaka kuombewa au kufunguliwa katika jambo fulani anaamini ndivyo
ifanyikavyo; nawaeleza dunia yote hivyo siyo, hayo ni maombi ya uchawi,
anakuzika, anakuwa juu ya maisha yako na baraka zako, majini yakimsaidia kuiba
vtu vyako na zaidi maombi hayo hufanywa kwa siri. Sasa uwe na akili, kwanini
asifanye katika nuru? Jibu giza hukumbia nuru. Unapofanyiwa hivyo ni lazima
ufunguliwe upya; umengamizwa maisha yako tena umebaki mwenyewe.
Yapo maombi mengine watu wananyonywa
viungo vya siri na wengine pastors baadhi wamewanyonya wanawake maziwa na
wengine wamewanyonya waumini mate eti ndio wanawafanyia deliverance na wengine wanafanyiwa deliverance
kwa njia ya zinaa iwe wanaume au wanawake. Nawaeleza mmeangamizwa watu hao, kwa
njia hiyo anachukua vitu vyako na baraka zako wewe unabakia kuchoka maisha
yako.
Wapo wengine wamenyolewa au
kukatwa kucha, hayo yote ni maombi ya kuwaangamiza kabisa, hivyo YESU anajua
wengi wanamtafuta, mnampenda lakini wakati mwingine mnamtafuta shetani na siyo
yeye. Yeye siyo mchafu. Funguka akili
msikubali maombi ya jinsi hiyo ikiwemo na maombi ya kufukia BIBLIA, watumishi
wote wa jinsi hii huongozwa na nguvu za majini na uchawi wa kununua, hivyo
unaweza ukafikiri ni kazi za MUNGU kumbe ni za majini zimejengwa katika maeneo
mengi kiroho na kimwili.
NOTE:
Mambo haya yote hufanyika sababu
wanatafuta pesa na wameamua kumchukia MUNGU kutoka katika mioyo yao na kumpenda
shetani na kuamua kuziingiza sheria zake na kuzilinda na kuzisambaza zifanye
uchafu. Nasema washindwe kila mahali kwa JINA LA YESU WA NAZARETI
NABII HEBRON