Mungu MNYANG’ANYI (MWIZI) YUKO HIVI….!
Ukisoma katika injili ya Mathayo
Mtakatifu: Soma; Mathayo 10;7-8, Mathayo 22:29-37, inaeleza kwa ufupi. Hivi ulishajiuliza kwa nini MUNGU anasema
katika neno lake nimewapa bure watumishi vipawa hivyo watoe bure, hivyo
wahudumu kwa watu bure bila kuwachaji pesa, au malipo yeyote yale? MUNGU alishajua
ya kuwa ipo miungu mbali mbali watakaotokea na kujifanya kuwa na wao ni MUNGU, na ndio
sababu usishangae akisema usiabudu Miungu mingine, ila mumuabudu yeye peke yake
yaani MUNGU akimaanisha kuwa tufuate na sheria zake kama zilivyo katika biblia
na siyo kupokea sheria za sehemu
nyingine.
Jinsi ya kumjua mtu anayeongozwa na
mungu mwizi, au jambazi au mnyang’anyi, kwa ufupi; utaona anatenda yale yale ya
unyang’anyi, kwa sababu katika ulimwengu wa roho ndivyo anavyoongozwa nafsi
yake (na mungu mnyang’anyi) na haongozwi na
MUNGU ambaye yeye amesema mtoe bure na zaidi iweje MUNGU alisaliti neno
lake? Au iweje MUNGU awe kigeugeu?
Hivyo basi maombezi yote katika dunia
yote kupitia jina la YESU na hata ikiwa ni kwa kupitia Nabii, Mtume, Mchungaji,
Mwalimu, Mwinjilisti, Askofu na wengineo , ambao wanatoza pesa (wanachaji pesa) tena
wanamsingizia MUNGU kuwa kasema toa kiasi fulani ndipo awaponya au watoe kiasi
fulani ndipo wawekewe mikono sababu ya tozo walilodaiwa kutoa ili wapate huduma
ya kiroho. Mimi Nabii Hebron nawaeleza
kuwa mambo hayo siyo ambayo MUNGU aliyoyaagiza yatendeke au watendewe
watoto wake ila ni ya miungu, haijalishi
kuwa wanalitaja jina la MUNGU hata miungu ni aina ya mungu vile vile ila wewe
utawajua kwa matendo yao ambayo yapo tofauti na biblia, yamechanganywa na
uongo.
Soma: Wagalatia 1:6-8 kila anayeabudu tofauti
na MUNGU alivyopanga ameshalaaniwa sasa tazama watumishi baadhi yao walivyolaaniwa
na MUNGU, wengine hawajui na wengine wanajua, watubu waache ujangili, najua
wapo baadhi yao wanaochukia na wapo ambao wanafurahi na kupata uponyaji ila haijalishi
wanadamu watachukia sababu ya kusema ukweli
ni bora kupendwa na MUNGU kuliko kupendwa na shetani, wapo wapendwa wa
shetani wengi wanaomfurahisha shetani kwa kutumia jina la YESU kuwachaji watu
pesa za maombi nataka mataifa muelewe kuwa kilichomjaa mtu katika moyo wake
ndicho kimtokacho, hivyo basi mtumishi akiwa amejaa MUNGU wa kweli atasema
kweli, atatenda haki, kwa sababu aliye ndani yake ni MUNGU wa haki. Utajiuliza
ni kwa nini YESU alipigwa, tena na hao hao watumishi kipindi kile? ni kwa sababu
YESU alimbeba MUNGU ndani yake, na hao waliibeba miungu, haiwezekani kuwa MUNGU ampige MUNGU, ila zikiwa na roho tofauti zitapingana na sasa
mtambue hayo ili mpate kuwa huru na MUNGU aliyewaumba na awe ndio BABA yenu.
KWA
BAADHI YA NJIA HIZI ZIFUATAZO UTAMJUA MTUMISHI AMBAYE ANAONGOZWA NA MUNGU
MWIZI AU MNYANG’ANYI:
- Ukiweka appointment na yeye unadaiwa pesa za kuonana na yeye.
- Kila tatizo lazima kutozwa (to be charged) pesa tena bila aibu anaweza akakuambia tatizo hili ni kubwa itabidi utoe pesa nyingi zaidi huyo ni jangili, umekutana na pepo lake.
- Kuandika sadaka majina na kupewa risiti.
- Kusimamishwa madhabahuni na kuambiwa uahidi kiasi fulani kwa ajili ya kanisa (limekuwa pango la wezi YESU alikataa) Je! Hayo yametokea wapi sasa? Kwa mungu mnyang’anyi ndiye anayetenda kazi hiyo na kwa njia hiyo uelewe basi yapo makanisa mengi duniani ni ya mungu mnyang’anyi au mwizi.
MUNGU
MNYANG’ANYI WA UBATIZO:
- Huyu ni aina ya mungu mwenye kazi ya kuzimu aliyetumwa hapa ulimwenguni kupinga ubatizo wa kweli ambao uliletwa na Yohana uliotoka mbinguni, na yeye akaleta wa kwake ili kila anayeamini na kushiriki basi na yeye anakuwa mwana wa miungu na mwanafunzi wa miungu ya mpinga kristo, na kukufanya usiende mbinguni, kwa sababu ulishaingia nao agano la hiyo miungu mfano: soma katika biblia je ubatizo wa kikombe, ubatizo wa kisima, ubatizo wa kubatizwa kwa jina mchungaji ( Pastor) na nyinginezo za uongo. Je! Ndizo alizozileta huyu MUNGU aliyekuumba? Jibu ni siyo, sasa kwa nini kama unampenda MUNGU wa kweli upokee viapo vya miungu na kukufanya wewe uwe na uhalali wa kwenda jehanam kwa kujua au pasipo kujua? sasa uelewe na uamuzi ni wako, nakusihi umrejee MUNGU wakati wa neema ni sasa mda siyo mrefu giza litaanza.
- Huyo mungu ubatizo akaiba na kuificha ile kweli ya neno la ubatizo kwa mataifa yote akaleta ubatizo wa uwizi na usio halali na watu wengi wakaupokea nikiwapo na mimi niliupokea , ninamaanisha kumwagiwa maji na wala sijaona nimepewa story ila nimemkataa sitaki miungu na wewe kataa, wakikubishia waulize ni nani kawaambia wabatize watu hivyo jibu hawatakuwa nalo.
MUNGU MWIZI WA IMANI
- Huyu huiba imani na kuuwa kweli akaleta imani za giza, mfano: Unakuwa mkristo lakini hutaki kuokoka au umeokoka lakini upo katika madhabahu ya miungu Mfano: utasikia kuwa huduma ni ya wokovu lakini watu wamebatizwa katika kisima, au wamebatizwa kwa jina la Mchungaji ( Pastor ) au wanachangisha pesa au kanisa linachaji riba, lina benki au linakuwa na mapatners, watu wenye pesa ndio wanashikiliwa na wachungaji (Pastor) na wale wasiokuwa na uwezo hawana mpango nao, anapenda pesa au kwa lugha nyingine mali za watu na siyo kuponya roho.
- Mchungaji (Pastor) au mtumishi anakuwa ni wakala wa shetani na ni siri yake ila anajifanya anafanya kazi ya YESU, mfano: Kila freemason iwe ni nabii, apostle, pastors na mengineyo mpaka waimbaji wa kwaya hao ni mawakala wa shetani moja kwa moja wako. Wapo wengine ambao walikuwa wameitwa na MUNGU lakini wakamwacha MUNGU, wanaendelea kuuharibu ufalme wa MUNGU.
- Ameleta imani mfu eti ukifa utaombewa, soma neno la MUNGU linasema MUNGU yeye siyo MUNGU wa wafu, sasa iweje wakristo na wengineo mtu ameshakufa mnaenda kutubu kwa ajili yake, kakuambia nani? Ukatubu kwa ajili ya maiti kakuambia nani? Kwani alivyokuwa hai hakujua kuwa kunakutubu na kumrejea MUNGU? Imeandikwa mtu akikata roho basi kama alitubu au hakutubu hayo ni siri ya MUNGU, MUNGU amempa mda kila mtu amrejee akiwa hai na siyo mzoga, mizoga inanuka. MUNGU anataka uwe fresh umrejee ukiwa hai na siyo ukiwa mzoga. Kila watu wanapofanya ibada hizo yule mungu wa wafu anakuja kuwaletea mauti watu wote wanaoshiriki na kuwapiga mihuri katika ulimwengu wa roho ya kuwa ni watu wake na anao uhalali nao kwa sababu wamemsujudia na kumnyenyekea.
Note:
Zaidi nitaendelea kukutumia masomo na yako mengi fuatilia katika blog hii,
BWANA YESU atakufungua.
Sema
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote,uandike jina langu katika kitabu
chako cha uzima wa milele ulitoe jina langu na vitu vyangu kwa huyu mwizi (jambazi)
sikutaki mwizi (jambazi) potea kwa jina la YESU wa Nazareti aliye hai mbinguni.
Amen.