KWA
NINI YESU AMEGAWANYWA NA WANADAMU WAKATI YEYE NI MMOJA NA HAGAWANYIKI!!!!!
(WAEFESO
4: 4-5)
BWANA
YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote. YESU wa Nazareti anawapenda na yeye ni
yule mmoja tu ambaye ndiye mwana wa pekee wa MUNGU aliyeumba viumbe vyote.
Ukisoma
katika kitabu cha Waefeso 4: 4-5;
“4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa
katika tumaini mmoja la wito wenu.
5 BWANA mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.”
Nilipoitwa
na YESU nikamtumikie mimi Hebron ilikuwa ni ngumu kumwelewa sababu nilishapokea
mafundisho ya yesu wengi na nilijiona mimi ni mfuasi mkamilifu wa YESU kumbe
siku zilipozidi kusogea nikazidi kujielewa nilikuwa ni mfuasi batili (fake), lakini nashukuru kwa neema yake
imeniwezesha nikamjua yeye wa kweli na pia niweze kuwaeleza mataifa na wapone
kama mimi kwa wale wanaopenda kuwa na YESU mmoja, imani moja na ubatizo mmoja.
Cha kustaajabisha,
hili si jambo la siri bali shetani akishirikiana na wafuasi au wakala wake
wakawaleta mayesu mbali mbali ambao hawajulikani wakaleta viapo vyao na watu
pasipokujua na wengine wakijua wakayafuata na kuyatii na kwa tendo hilo basi
kila aaminiye kiimani na kimatendo anakuwa ni mfuasi wa upande wa yesu wa aina
nyingine, au kwa maana nyingine mpinga kristo.
JINSI YA KUMJUA yesu ALIYELETWA
NA WANADAMU BADALA YA MUNGU; YUPO HIVI: -
Waefeso
4:5
1.
BWANA
MMOJA- Huyu ndiye BWANA YESU aliyeletwa kutoka mbinguni lakini
ukiona sheria zake zimechanganywa na sheria za wanadamu (mapokeo) basi uelewe
huyo ni bwana aliyeletwa kwa mapokeo ya wanadamu. Mfano utasikia katika ibada
watu wanaanza kuchangishwa pesa au harambee na hapo hapo linatajwa jina la
bwana au ukitoa unaambiwa bwana akubariki sana….halleluya….!!!!!
Nataka
ukumbuke huyu BWANA YESU wa mbinguni yeye alivyokuwepo hapa duniani aliingia
hekaluni; ukisoma kitabu cha Marko 11:
15-20 utaona aliingia kanisa akakuta biashara akasema mahali pangu hapako
hivyo akawafukuza, akakaa yeye na jambo hili la kufanya nyumba ya MUNGU kuwa
soko la biashara halikuanza leo, tangu YESU alivyokuwepo duniani aliyakataa,
sasa ameenda mbinguni baadhi ya watumishi wenye shingo ngumu au wanaomdharau
MUNGU na sheria yake wanayaendeleza katika ulimwengu wote, na watu pasipokujua
wanaona wanamfanyia BWANA wa mbinguni na kumbe ni bwana aliyeletwa na wanadamu.
Jambo
lingine, makanisa yamekuwa ni uwanja wa
siasa au kampeni za kutafuta wagombea wa uongozi wa nchi mbali mbali, kanisa la
jinsi hiyo muelewe mpo na bwana aliyeletwa na wanadamu. Ukikuta unatozwa pesa
ndio uombewe uelewe umekutana na bwana wa wanadamu na siyo yule MUNGU wa kweli,
kwa sababu MUNGU wa mbinguni anaponya bila malipo, yeye anao upendo kwako.
Hivyo basi unaweza ukajiona upo na BWANA YESU wa mbinguni kumbe upo na bwana
yesu wa mapokeo ya wanadamu ambaye yeye hutumia mizimu, nguvu za giza au kufanya
ibada kwa elimu za kusomea na akili yake pasipo kuitwa na MUNGU na kufanya
mtumishi awe ni wa pesa au mnyang’anyi.
2.
IMANI
MOJA-
Tunajua ili uwe mkristo ni lazima imani yako iwe moja wala usiifuate imani
nyingine tofauti na jinsi ilivyo katika biblia bila kuongeza neno wala kupunguza
(Ufunuo 22: 18-19). Ni ajabu utakuta
mtu au watu wanajiita ni wakristo lakini hawaokoki hapa duniani inapokuwa hivyo
basi asiyeokoka hana imani moja ya YESU wa mbinguni yeye anayo imani ya yesu wa
mapokeo.
Imeandikwa
usiabudu sanamu lakini sanamu zinaabudiwa, imeandikwa usifanye ibada za wafu,
kuombea watu bure wewe unawatoza pesa, imeandikwa nyumba ya MUNGU ni mahali pa
sala lakini sasa imekuwa ni soko, michango, siasa, harambee, na mengine maovu.
Imeandikwa utoapo sadaka ni siri yako; wewe unaandika jina, unatoa anwani (address), namba ya simu na unapewa
stakabadhi (receipt). Hii ni kinyume
na neno linavyosema, hivyo basi hilo neno halina ushirikiano na imani ya neno
la MUNGU bali maneno hayo yana ushirikiano na imani ya yesu aliyeletwa kwa njia
ya mapokeo ya wanadamu na kuwafanya watu wamsaliti YESU wa mbinguni pasipokujua
au kupenda kwa kushiriki imani ya kulipinga NENO la mbinguni lilivyo na
kuwafanya watu wengi zaidi kuwa wafuasi wa yesu mwenye mapokeo ya imani ya
wanadamu na wakamkosea MUNGU kama ilivyo sasa katika ulimwengu wote watu wengi
hawana imani ya YESU wa kweli bali wanayo imani ya yesu wa mapokeo ya wanadamu.
Hata kama unakataa jichunguze utapata jibu kamili wewe upo katika imani ipi?
Soma
Waefeso 5: 5-13, kwa kufunguliwa zaidi endelee kusoma makala za blog hii na angalia YouTube na kusoma vitabu mbali mbali vya Nabii Hebron utapona imani
yako. Iwapo upo kinyume basi uelewe imani imekufa, hivyo mkristo bila imani
yenye muunganiko (connection) na
mbinguni ni kazi bure. Chunguza kiimani, kimatendo, kiukristo wako utapata jibu
kuanzia kuokoka.
3.
UBATIZO
MMOJA- Luka 20: 3-7
Hapa
ndipo pako wazi kabisa katika kukufundisha wewe na mengineyo. Huyu YESU wa
mbinguni yeye alibatizwa katika mto Yordani maji yanayotembea, kijito cha
utakaso na ukisoma yeye ndiye njia ya kweli, tuifuate, tumfuate alipo yeye
katika roho na siku moja tuungane naye mbinguni. Ubatizo maana yake ni
kuzamishwa na kama ingekuwa ni tendo la YESU kuzamishwa mradi ni maji tu basi
Yohana mbatizaji angebatiza kwenye visima sababu alikuwa jangwani na kulikuwa
na visima, lakini hakufanya hivyo alitii alivyoelezwa mbinguni ili amtengenezee
YESU njia. Hivyo ubatizo siyo uambiwe tu ni ubatizo, utapokea ubatizo wa yesu
aliyegawanywa na wanadamu au wa mapokeo ya wanadamu. Mimi Hebron nilibatizwa
ubatizo sijui uitwe namba 2 au 3 au 4 hapo mwanzo na kunifanya niukose ubatizo
mmoja aliobatizwa YESU mmoja, imani moja.
Ulimwengu
wote napenda mjue siku atakapokuja huyu mwana wa pekee mmoja wa MUNGU wa
mbinguni yeye ataangalia ubatizo wake mmoja tu. Ukiwa unao wa kikombe au wa
kisima au wa jina la mchungaji atakuambia wewe siyo wangu mfuate huyo
aliyeletwa na mapokeo ya wanadamu, alama hii siyo yetu na BABA yangu mbinguni
hivyo sikujui sikujui, na ndipo itazidi kutimia, imeandikwa siku ile wengi
watalia wakisema BWANA mimi nilikutolea sadaka, nilikuwa naiombea kazi yako,
nimehubiria watu, naye atakuambia sikujui sikujui, yaani akisema leo ndio au
sasa hivi YESU anarudi mabilioni ya wakristo wataambiwa sikujui. Ameniambia
niwaeleze watu wote myajue haya. Hiki ni kipindi cha neema, bado giza halijaja,
batizwa upya haraka.
Katika imani nashangaa kuna watumishi mashoga, wanajulikana
kimwili na siyo siri. Sasa nauliza hivi YESU wa mbinguni yeye anao watumishi
mashoga? Wakati Neno lake linasema hivi “Ole
wao wafiraji” na wote hawatoenda mbinguni (soma 1 Timotheo 1:10). Sasa inakuwaje yeye akatae wafiraji halafu
tena wanadamu mnaona wapo watumishi wa kanisa, wapo mitume, manabii, wachungaji,
wainjilisti, waalimu na wengineyo ni wafiraji. Hii ni picha halisi uelewe kwamba
hao wanawaongoza watu kuelekea jehanamu; jinsi alivyo kiongozi ndivyo alivyo na
muumini wake, anarithishwa roho zake.
Pia
katika imani moja mimi nashangaa sana utasikia umoja wa makanisa, lakini katika
huu umoja wapo wanaomkataa YESU hawaokoki, wapo wanao abudu sanamu, wapo wanao batizwa
kwenye kisima, wapo wa ubatizo wa kikombe, wapo wa kubatizwa kwa jina la
mchungaji na wapo wenye miujiza ya kichawi, wapo wanaotoza watu pesa ili
waombewe, wapo waliojiita, waliojifanya, walio msaliti Yesu, wapo freemason,
wapo wachawi, wapo wanyang’anyi, wapo watoza riba, yapo makanisa yanayoendesha
biashara za benki, wapo wanaoabudu wafu, waabudu sanamu, wapo wanaomwabudu
mchungaji kwamba ndiye MUNGU au ndiye YESU, na mengineyo mengi. Sasa ukiniambia
kuna umoja wa imani moja, ubatizo mmoja, bwana mmoja katika dunia yote ule wa
kweli hautazidi 2%.
Umoja
mwingine utakuta ni tofauti na biblia, matokeo yake wakristo wanaanza kuabudu
miungu pasipokujua japo baadhi ya viongozi wanajua kabisa sababu wao wametumwa kuwapotosha
mataifa, wakawekewa roho za kuwaongoza za giza ambazo hazina nuru. Hili ni
giza.
Wapo
mashoga ambao kimwili hawajulikani ila kiroho ni wake za shetani, wapo wanawake
na wanaume, hawa ni wachawi. Watumishi wote wanaotumia nguvu za giza, wapo manabii,
mitume, wachungaji, walimu, wainjilisti, maaskofu na wengineo hata waimbaji
wanaotumia nguvu za giza na wamejaa katika ulimwengu wote, ila kibinadamu wana
wake/waume na watoto hivyo hivyo wao wanajielewa. Muwe makini sana nyakati hizi
ni za hatari, YESU wa Nazareti anakaribia kuja, sasa wewe utakuwa wapi?
Tubu
rejea uifuate njia ya kweli; Sema, BWANA YESU wa mbinguni, naomba unisamehe
dhambi zangu zote, uniandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa
mbinguni, nataka imani moja, ubatizo mmoja, Bwana mmoja wa kwako tu sitaki
wengine tena. Amen.
NABII
HEBRON.