NINI
MAANA YA KANISA LA KIROHO?
BWANA YESU ASIFIWE!
Napenda kufundisha kuhusu neno “KANISA
LA KIROHO”. Neno hili lina maana gani? YESU alisema muenende katika roho katika
kuomba na kusoma neno, hiyo roho alimaanisha tuongozwe na ROHO MTAKATIFU ambaye
ndiye aliyemtuma awe msaidizi wake asimamie kazi yake pale ambapo wapo na YESU
wa mbinguni, lakini napenda kuwaeleza muwe makini sana sawa sawa na alivyonieleza
YESU maneno haya miaka iliyopita.
Mimi hapo awali nikisikia mtu
anasali katika kanisa la kiroho nilijua kweli ameamua na anaongozwa na ROHO
MTAKATIFU, lakini kupitia hili jina baadhi ya watumishi wanaziangamiza roho za
watoto wa MUNGU, sababu mtu anajiaminisha anaenda kukutana na ROHO MTAKATIFU na
anaokoka na anatii anayofundishwa kumbe ni kinyume na matokeo yake anakuwa
ameenda katika “kanisa la maroho”. Ninaposema maroho ina maana ni roho za
shetani au mambo yasiyo ya MUNGU au kwa maana nyingine ROHO wa MUNGU hayupo
mahali hapo; na kama hayupo ina maana aliyepo hapo ni roho wa shetani au mpinga
kristo. Mfano mfupi; jiulize kama ni kanisa la roho MTAKATIFU mbona hawaelezi
ubatizwe kama YESU katika maji yanayotembea? Utakuta ubatizo wao ni aidha wa kisima,
kikombe au kwa jina la mchungaji (kitendo hicho kinakufanya wewe uwe muumini wa
maroho na anayekuongoza anaongozwa na maroho na ndiyo sababu unabatizwa tofauti
na ilivyoandikwa katika biblia).
Maroho pia yana nena,
yanatabiri na yanaona, roho ni moja hiyo hiyo tu kama ya mganga. Utakuta sehemu
hizo zina michango, waumini kulazimishwa kuahidi pesa, unyang’anyi, ufisadi,
miujiza ya kuwatoa watu vitu katika mwili mfano mawe na mengineyo, hapo ni kwa
maroho. Ukisikia unadaiwa pesa ndio ufanyiwe maombi uelewe hapo hayupo ROHO
MTAKATIFU wa mbinguni ambaye yeye anasema “mmepewa
bure, toa bure” funguka ufahamu, haya yote hayapo katika biblia, hayo ni
maroho na ndio yanayochukua pesa zako na mahali hapo ni makazi ya maroho.
Ukikuta mtumishi anasema saini
kwenye nguo yake na utoe kiasi fulani cha pesa uelewe anaongozwa na maroho,
haijalishi hata kama analitaja jina la roho mtakatifu; imani pasipo matendo
imekufa, hamna imani ya mbinguni. Mtawajuaje wanaongozwa na maroho badala ya kuongozwa
na ROHO MTAKATIFU wa mbinguni? Ni kwa matendo yao.
Ukisoma kitabu cha Yohana 4:
23-24; “23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo
halisi watamwabudu BABA katika roho na kweli. Kwa maana BABA awatafuta watu
kama hao wamwabudu. 24 MUNGU
ni roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
Sasa YESU alisema tumwabudu
yeye katika ROHO MTAKATIFU na kweli katika kulifuata Neno Lake, sasa imekuwa
tofauti sehemu nyingi ulimwengu wote wapo wanaoabudu katika roho na uongo,
kivipi?
Ubatizo batili, mapokeo ya
wanadamu, neno limechanganywa na uongo. Mwenye akili na afahamu, aelewe,
afunguke, atoke kwenye maroho kwa sababu yanamtengenezea njia ya jehanamu;
maroho hayapeleki watu mbinguni.
Soma, 2 Wakorintho 4:1-4, usiwe
muumini wa miungu ya dunia hii.
ANGALIZO:
Makanisa
haya ya kiroho yapo ya aina mbili katika ulimwengu wote;
1.
Kanisa la kiroho na kweli halisi.
2.
Kanisa la kiroho na uongo umechanganywa na
ukweli (ni ya maroho).
Wapo watumishi wa roho wa MUNGU
wa kweli halisi pia wapo watumishi wa roho wa uongo wakichanganya neno la MUNGU
na uongo. Sasa katika matabaka hayo ndipo utawakuta watumishi wa pesa,
waliojiita, wachawi, wanyang’anyi, matapeli, walevi, wazinzi, wauza madawa ya
kulevya na zaidi hata wengine wanavuta bangi ndio wanahubiri na mengine machafu
ya aibu, (ni watumishi wa maroho).
SALA
YA TOBA:
Naomba unisamehe BWANA YESU,
kuanzia sasa nasema maroho yote potea ndani yangu, toka kwa Jina la YESU.
Uniandike jina langu mbinguni katika kitabu chako cha uzima wa milele. Amen.
NABII
HEBRON.