Pages

Saturday, November 5, 2016

JE UNAMJUA YULE AMBAYE KUJA KWAKE NA KUTENDA KWAKE NI KWA MFANO WA SHETANI (NDANI YA KANISA LOLOTE).

BWANA YESU wa Nazareth asifiwe, katika somo hili nitafundisha kwa ufupi ili umwelewe yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake shetani kwa uwezo wote na za ishara na za ajabu za uong,  ukisoma katika kitabu cha 1 Thesalonike 2:9 kinaeleza vizuri,  japo mamilioni ya watu katika dunia hii hawaelewi maana yake.

Ukisoma na utakapoelewa huyu shetani hatakuweza labda wewe umkubali mwenyewe, kwanza elewe kwamba biblia inasema;  kuja kwake ni kwa mfano wa shetani ? na ni wapi? na je!  hizo ishara za uongo zinatokea wapi? Jibu ni katika baadhi ya makanisa, ataingia na alishaingia sehemu nyingi,  akishuhudiwa na watumishi baadhi yao wanaitenda hiyo kazi,  ya kwanza  wanachanganya ukweli na uongo na injili ya namna nyingine, (Wagalatia 1:6) Huyu anayekuja ndiye shetani usifikirie kuwa utamwona shetani akija kabisa kimwili,  jibu anaingia kiroho kwa njia nyingi nitaelezea chache na mtu pasipo kujua wanafikiria  wanaongozwa na  YESU kumbe shetani  na anataka mfanye yake .

Zipo njia baadhi nitawaelezea

KWA NJIA YA NENO
a.      Hubadilisha neno mfano imeandikwa  nimewapa bure – lakini  mnachangishwa pesa katika maombi, ubatizo uliouagaza umebadilishwa,  YESU yeye alibatizwa mtoni imebadilishwa  ikiwapo na kuomba ...... .kubatizwa kwa jina la mchungaji, huyu ndiye shetani aliyekuja kwa mfano: wa neno la MUNGU la kubatizo wa maji mengi , yeye ametumia jina la YESU na akaleta wa kwake wa uongo huyo ndio shetani.

b.     Kuwaambia watu wasiokoke wakati ukristo ili ukamilike ni mpaka aokoke,  shetani amejifanya yeye ndie kristo hakuna kuokoka na watu hawataki wokovu  sababu wamfuata aliyekuja kujifanya yeye ni mungu na kumbe yeye siye na ukimfuata na wewe meunganishwa katika mfumo huo huo.

c.      Imendikwa usiabudu sanamu lakina utashangaa mkristo bila aibu amejikuta yeye ni mfuasi wake, YESU ambaye  Baba yake   alikataza watu wasiabudu  sanamu,  wanaabudu wafu, unapoenda tofauti na Neno la MUNGU basi na wewe unakuwa umemabudu shetani japo haupendi au hujui au unajini hapo dhambi ipo juu yako.

d.     Imeandikwa nyumba a MUNGU ni mahala pa sala basi, YESU kipindi kile alikuta wakiuza ndani ya hekalu yeye aliwafukuza hekaluni,  sasa sala hizi wanamtaja YESU na hapo hapo utakuta michango ibadani, harambee wote watu wameshatoa sadaka zao hiyo inaisha,  sasa hayo yanapofanyika hapo ndipo shetani hufanya na akakubaliwa na mengineyo yapo mengi.

e.      Mfano sadaka ni siri yako na Unaambiwa adika jina na unapewa risiti hapo huyo ni shetani anatenda kazi au unasomwa jina na unapewa vyeti vya hongera umetoa sadaka sana,  huyo ndiye ajaye yaani shetani na amekuja  na yupo sehemu nyingi
f.       Imeandikwa usichaji riba, kanisa lina Bank  -- (yaani benk  inamilikiwa na kanisa) ina maana MUNGU anafanyaga hayo na hufilisi? Sasa huyo sio mungu bali ni roho ya huyo ajaye yaani shetani kwa njia ya mafundisho  ya uongo  na yeye amebakia kuzimu anazitoa roho zake kwasababu akija kwa sura yake ataeleweka hivyo shetani  anatuma roho za uongo,  huziingiza katika baadhi ya makanisa ambalo hajasimama katika kweli ya MUNGU na mengineyo  na mengine yanakuwa kuzimu kabisa baadhi ya makanisa yaliyopo   duniani  bali  yamejificha nayo huleta mafunuo ya uongo ambayo huitwa mapokeo ya mwanadamu badala ya kupokea  ya MUNGU tu.

MIUJIZA

a.      Miujiza ya kichawi mfano kutolewa vitu katika mwili,  na ukaviona,
b.     Kufufuliwaa watu (kipepo) ambao haujawaona  kama walikufa (yaani wafu hewa)  YESU alimfufua Lazaro na wengine
Na zaidi  fungua youtube ya naabii Hebron inaelezea  vizuri kuhusu huyo ajaye sasa kwa kutenda,   shetani na soma vitabu na CD na DVD utaelewa zaidi ingia katika website www.prophetebron.org ingia katika link ya youtube na blog
Soma Kitabu cha Wagalatia kitabu cha 1  mpaka kitabu cha 6
Mwenyezi MUNGU akubariki sana.

NABII HEBRON.