Pages

Thursday, November 3, 2016

KWANINI BAADHI YA NCHI ZINARUHUSU SHERIA YA USHOGA KWA WANANCHI WAKE ?  IPO SABABU UTAENDA KUIJUA.....

BWANA YESU wa Nazareti asifiwe, katika somo hili napenda kuujulisha ulimwengu na kumwaibisha shetani na uovu wake na kuharibu hili agano sodomite ambalo utashangaa hata bunge la nchi fulani linakaa na kujadili kuwa sheria hiyo inafaa inamaanisha shetani anafaa na MUNGU hatakiwai hapo .
Kila mtu anajua ameumbwa na Mwenyezi MUNGU  na ndiye MUNGU na BABA pekee hakuna kama yeye, yeye ametoa sheria zake na akijua  kuwa ukizifuata utakuwa salama,   ila usipozifuata utaangamia.

 Naongelea ushoga au tendo la  kujamiiana  kinyume na mambile au kufira  utasoma Kitabu cha Warumi 1:24-32 inaeleza madhara yake  ni kukubali mauti na kukataa uzima wa milele;   na unaposoma 1 Wakorintho 6:9  kila anayefanya dhambi ya ufiraji hataenda mbinguni soma.  Sasa basi kama hii  dhambi inafanya mtu asiende mbinguni ina maana dhambi hii ni ya kukufarakanisha na MUNGU  na kukupatanisha na shetani.

Ushoga unaporuhusiwa katika nchi kama au halali  na ni ruhusa  japo utasema wanasimamia haki za  binadamu,  napenda kusema kuwa hizo sizo haki za binadamu bali ni haki za shetani anazozileta kwa wanadamu ili wanapozipokea  yeye  ndiye anakuwa mungu wao, ila chanzo chake ni uongozi  au kiongozi  wa nchi au chama pale anapotegemea nguvu za shetani zimweke madarakani au nchi yake au chama chake kiweze kutawala au ufalme wake utawale , shetani kawapa agano ambalo ndilo hilo, japo yapo mengi ila naelezea hili la Ushoga (Sodomite) na nchi itakapolipitisha sheria iyo basi yale mapepo ya ushoga yanawaingilia wananchi na kuwatawala na kuwabadili kufanya uzinzi kuwe kinyume cha maumbile  na kwa njia hiyo wanafanya huo ushoga wanakuwa wametolewa sadaka kwa shetani.

Kupitishwa kwa sheria hii  nchi inaunganishwa na mungu shoga kupitia maagano ya hao viongozi waliofanya au kwa maana nyingine ni kusaini mkataba wa  kuyadumisha mambo ya Sodoma na Gomora  halafu wa waangamie, hivyo ushoga , ufiraji ( Sodomite) ni mbaya na muupinge na watu wote na waukatae  na cha ajabu  utashangaa na hata wapo baadhi ya wachungaji ambao ni mashoga na wanaongoza makanisa,  hao wachungaji wa jinsi hiyo wanafanya kazi chini ya utawala wa mungu shoga ambaye yeye yupo uzimu hata hao waumini na wao anawapeleka kuzimu  hapo ni mahali pa Jehanamu.

Nilipokuwa  nimeitwa na YESU ili nimtumikie mimi Hebron  nilimwambia nahitaji kwenda Chuo cha Biblia (Bible College) sababu sikujua pa kuanzia,  akanikataza akaniambia atanifundisha  yeye peke yake na pia kunifundisha jinsi ulimwengu ulivyopotea na njia sahihi ili wapone wanirejee mimi YESU, wakati wangu wa kurudi umefika ila sina watu wengi, watu wengi wapo katika upande wa shetani  wakiwemo na wanaofanya ushoga  wa jinsia yote,  iwe mwanamume au mwanamke  anayefanya tendo la ndoa kinyume na alivyopanga MUNGU yeye haendi mbinguni hata kama amefunga ndoa takatifu kanisani, hayo ni machukizo mbele ya Mwenyezi MUNGU kabisa.

Huyo mungu shoga anataka kutawala kwa kupitia viongozi wa nchi mbalimbali na huwasaidia kutajirika (Freemason ) na agano hili ni nguvu ya freemason (free mason power)  au mikataba (or agreement)  (na hulazimisha nchi nyingine waingie  na wakiona nchi imekataa na ili waweze kuwaingiza kwa lazima huwatishia  kuwanyima msaada (hao viongozi au hizo Nchi) nawaeleza viongozi wote wa dunia yote mnaompenda mwenyezi MUNGU kataeni kabisa mpango huo na MUNGU atawabariki tu.

MADHARA KWA WANAOSHIRIKI USHOGA UFIRAJI

(Madhara haya ni ya watu wote anayefanya na anayefanyiwa)
Kwanza kabisa unajinyima kwenda mbinguni  na kuwa adui wa MUNGU sababu zaidi soma biblia  na usome vitabu hivi vifuatavyo Walawi 18:22, Walawi 19:23………
Hivyo utubu na uache hiyo dhambi sababu kila anayefanya hivyo yeye ananuka harufu mbaya mbele za MUNGU na kwa serikali yake sababu umeingia agano la kumtukana, kumlaani yeye, na zaidi fahamu za wafanyao hivyo huwa na jini linaloitwa Jube na Waidabarati, hivyo  hilo jini likatae kwa jina la YESU wa Nazareti aliye hai.

Uliyeanguka katika ushoga uwe ni mwanamume au mwanamke,  uzinzi ni hatari, kusagana, ndoa za kike kwa kike au kiume kwa kiume mtu ni Ushoga (ufiraji).

Tubu – Sema
BWANA YESU naomba unisamehe, naomba uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele mbinguni, natubu, sitaki ushoga tena kuanzia sasa na mengineyo niongoze YESU nakupenda,  Amen.

NABII HEBRON.