Pages

Thursday, November 10, 2016

DHAMBI YA KUFIRA...INAKUZUIA KWENDA MBINGUNI!

(Warumi  1:26-27, 1 Wakorintho 6:9-10)

Hii ni dhambi moja wapo ambayo shetani anawatekea watu wengi, katika ulimwengu huu na hawaogopi na zaidi baadhi yao hupenda sana. Kule kuipenda sana maana yake ni kumchukia Mwenyezi MUNGU sawa na unapofanya hiyo dhambi unakuwa na wewe katika ulimwengu wa roho ni mke wa mashetani au mapepo au majini na kuunganishwa kuwa ni mwili mmoja na hayo mapepo iwe ni mwanaume anafanya au mwanamke tayari mnakuwa ni mwili mmoja na mashetani hivyo mashetani hayaendi mbinguni na unayefanya hivyo na wewe usipotubu upo katika mkumbo huo huo na mpaka uache na utubu uokoke.

Unazini na kahaba au yeyote yule unakuwa umefunga ndoa na yeye. Ukizini mara 30 uelewe umeunganishwa mara 30 katika mwili wa wanadamu na matatizo yao yote, na ukienda kinyume na maumbile unakuwa umeunganishwa katika ndoa na majini, shetani, mapepo katika ulimwengu wa roho na kuwa mwili mmoja.

Hii ni dhambi ya kufanya mwanadamu awe hekalu la shetani na MUNGU hawezi kabisa  kuishi ndani yake zaidi nimewaandalia kitabu, (Madhara ya uzinzi) kinapatikana katika makanisa yangu  ukikipata nimeelezea kwa undani zaidi na utapata uponyaji hivyo ikimbie zinaa, maangamizi yanakuja mabaya.

Dhambi hii inafanya mtu awe mke wa majini awe ni mwanamume au mwanamke na wanaofanya hivyo au kupenda sodomite mpaka awe na jini Jube, au Waibadati au Sharifu au Abubakari, Maimuna na mengineyo.

Binadamu mwenye akili timamu hawezi kufanya tendo hilo kwa akili yake alioumbwa nayo na MUNGU ila atafanya tu pale atakapoingiliwa na majini hayo au kutumiwa na waganga na wale wanaotafuta mali au vyeo kwa njia za giza hupewa hilo sharti, pia ikiwemo na mengineyo.

NABII HEBRON.