UBATIZO WA
MAJI YA KUCHEMSHA AU YA MOTO UNAMAANISHA NINI?
Katika ubatizo ambao nimesema ni ubatizo wa maji ya moto au
ya kuchemsha, huu ni ubatizo ambao ni wa kisima ambao pia ni chukizo mbele za
MUNGU kabisa na ni ubatizo ambao katika nchi za Ulaya wanautumia huwa wanayachemsha maji yanapata moto kama vile ya
kuoga kisha watu wanaingizwa katika kisima wanabatizwa kinyume na biblia na
mpango wa MUNGU.
Soma biblia yote hakuna ubatizo wa kuchemsha maji, huku
ndiko kutekwa na shetani tena zaidi, sasa tendo hili linapofanyika katika
kuchemsha maji kinachofanyika hapo katika ulimwengu wa roho unalaaniwa na MUNGU
na shetani pia na zaidi unakuwa umepatanishwa na moto wa jehanamu ambao baadaye
baada ya hukumu watachomwa na shetani, malaika zake na wanadamu waliomfuata
yeye na kwenda kinyume na MUNGU, na mtu unapobatizwa na maji moto kile ni kiapo
unachokuwa umekiingia cha kupatanishwa na moto wa jehanamu, nataka muelewe
mkatubu mkabatizwe upya sababu haujabatizwa bali mmepotea na MUNGU anawapenda,
amenituma mimi Hebron niwaeleze habari hizi njema za ukweli na zitawaweka huru
na siku moja mtafurahi na YESU mbinguni.
Shetani yeye alimkosea MUNGU peke yake lakini hakutaka
amkosee mwenyewe tokea mbinguni akiwadanganya thelusi moja ya malaika mbinguni
wakamtii yeye na akatupwa nao kuzimu na hata sasa 98% ya watu wote katika
ulimwengu huu ameiteka ili hao watu wakiwemo na wakristo baadhi yao siku ya
mwisho watahukumiwa pamoja na thelusi moja ya malaika walioasi mbinguni na
wanadamu wa sasa na watumishi wa uongo.
Tubu: BWANA YESU naomba unisamehe, uniondolee hili agano la
moto wa jehanamu wa ubatizo wa maji ya kuchemsha. Uniongoze YESU. Amen.
NABII HEBRON KISAMO.