Pages

Wednesday, February 10, 2016

NINI MAANA YA KUBATIZA KATIKA KISIMA NDANI YA KANISA?

Maana ya ubatizo huu wa kisima kinachojengwa ndani ya kanisa ina maana hii kuwa lengo la kuzimu ndilo linaloongoza hiyo madhabahu, haijalishi jina la YESU linatumika hapo tayari neno linakuwa ni kinyume sababu linapindishwa. Kiongozi YESU yeye alionyesha njia ni mtoni, akaja mpinga kristo kuliteka kanisa akabadilisha katiba ya MUNGU na ndivyo ilivyofanywa. Sasa uliza imekuwaje au yanatokea wapi? Yanaletwa na mapokeo ya elimu za wanadamu wakaona MUNGU yeye hajui kupanga mambo yake vizuri kumbe MUNGU yeye mambo yake anayahakikisha na yanafaa hayo ambayo hajayaruhusu hayafai yameletwa na shetani kwa mbinu zake kuhakikisha  tuu anawapata wanadamu wasiende mbinguni huu ndiyo ukweli kutoka mbinguni, na katika biblia ya mbinguni.

Watu wengi hawaelewi na sasa nawaeleza ili mpone, ni uhuru wako wewe kutaka kwenda mbinguni au jehanamu, ubatizwe upya utengwe na lengo la kuzimu ndani ya madhabahu. Na zaidi siyo jambo jipya ukikuta watumishi wanafukia watu kanisani mfano makafara, picha za watu, pesa, majina yao. Nataka muelewe vinapelekwa katika malango ya kuzimu na ndilo agano la mchungaji ili apewe nguvu na shetani ni lazima afanye hivyo na watu hawaelewi ukweli. Yaliyofanyika gizani sasa ni wakati wa kuwekwa wazi ili kila mtu aujue ukweli na umwekee uhuru MUNGU akufurahie.

NOTE:

Na pia kisima ikiwa nje ya kanisa hapo lilipojengwa ndipo panapokuwa ni lango la kuzimu. Pale tu unapoingia katika maji hayo unakuwa umeingie mwenyewe kwa hiari yako kwenye lango la kuzimu pasipokujua au kujua ili watumishi walioanzisha ubatizo huu wanaelewa wanachokifanya kwa shetani na pia hata wao hutumia hicho hico kisima wakati wa usiku kwenda kuzimu pasipo watu kujua, na zaidi hata kama mtumishi wewe unaiga ukajenga kisima na wewe utavutwa tu kwenda kuzimu sababu roho mchafu alikuteka fikra zako akakuongoza ukajenga. ROHO MTAKATIFU angekuwepo angekukataza kabisa sababu hiyo siyo njia ya mbinguni.


NABII HEBRON.