NINI MAANA
YA MTU KUZIKWA NDANI YA KANISA?
KATIKA
NYUMBA YA IBADA…
Ukisoma katika kitabu cha Mathayo 22:32 inasema mimi ni
MUNGU wa Ibrahim, na MUNGU Isaka, na MUNGU wa Yakobo. MUNGU si MUNGU wa wafu,
bali wa walio hai. Sisi sote ni kizazi cha Ibrahimu ambaye MUNGU wake ndiye
aliyekuwa MUNGU wa walio hai yaani watu wenye uhai na siyo waliokufa. Sasa ninachofundisha
hapa ni watu kuelewa ukweli wasipotee wakifikiri wanamwabudu MUNGU aliye hai
bali inakuwa ni upofu wa macho pasipo watu kujua au kuelewa waliabudu mahali
ambapo upo mzoga au mauti ndani ya kanisa. Inapokuwa mtu amezikwa ndani ya
kanisa au kupeleka maiti yake au mifupa basi tayari madhabahu hiyo inakuwa ni
ya mungu wa wafu ndiye atawalaye na watu wataongozwa na mungu mfu.
Ukisoma katika biblia baba yetu Ibrahimu mwenyewe
aliyembarikiwa yeye hajazikwagwa ndani ya kanisa au hekalu, pia YESU mwenyewe
mwana wa MUNGU maiti yake haikuzikwa kanisani alizikwa mbali sababu madhabahuni
ni mahali patakatifu pa MUNGU aliye hai na yeye ndiye hukaa pale, na
inapofanyika maiti inazikwa pale inabadilika mara moja anakuja kuishi mungu wa
wafu, na ukisoma biblia utaona MUNGU amekataa yeye ni MUNGU aliye hai maiti
izikwe pale iozee pale? Na zaidi ukisoma katika kitabu cha Marko 12: 27, neno
linasema yeye si MUNGU wa wafu bali ni MUNGU wa walio hai. Hivyo wapotea sana, maeneo haya aliyasema MUNGU ya
kuwa mwapotea sana yaani kupita kiasi na bila kujua katika ulimwengu huu. Ndiye
sababu hataki ibada za wafu ila leo zipo
na kama zipo zinafanywa basi waelewe wafanyao hayo wao wapo chini ya mungu mfu.
Sasa ni wakati wa kumrejea MUNGU wa kweli na siyo mungu wa wafu. Na wewe
unayependa kuwa chini ya MUNGU wa uhai inakupasa kujitenge na mambo ya wafu na
hata kuzikiwa vitu au makaburi kujengwa kanisani au katika madhabahu, inapokuwa
ni hivyo basi hapo shetani anapata nafasi ya kuwateka watu wale sababu tu ya
wafu
Kila mtu anajua ukisoma Marko 11: 15-18 hata YESU alipoingia
katika hekalu alikuta waliofanya mambo ya biashara, alijua tayari MUNGU siyo
mahali pake tena hivyo ili pawe na MUNGU aliye hai aliviondoa na kuwafukuza
hekalu likabaki safi na MUNGU akatukuzwa. Na zaidi hata kibinadamu mtu ukikaa
karibu na kaburi unaogopa linatisha, sababu katika kaburi inaishi roho ya mauti
na ikiwa ni hivyo basi uelewe na madhabahu hizo zinaishi roho za mauti na
mahali palipo na mauti anaishi mungu wa wafu. Hivyo unapoona hivyo uelewe ni
mahali pa mungu wa wafu asiye na uhai na wanaoabudu hapo watashikiliwa na mungu
mfu sababu anacho kibali, mahali unaposali ndipo na baraka za maisha yako
yaliopo. Ikiwa kuna uzima utapata uzima, ikiwa kuna wafu utapata umaiti na
kuhukumiwa usiende mbinguni.
NABII HEBRON WILSON KISAMO.