HAYA NDIYO
MADHARA YA KUABUDU PICHA ZA WATU WALIOACT SINEMA ZA YESU!
BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote, YESU
anawapenda na pia MUNGU anawapenda na ROHO MTAKATIFU anawapenda vile vile na
leo amenituma niwaletee habari njema za uponyaji wa roho na mwili ili miili
isike ikaangamia na roho kuhukumiwa siku ile ya hukumu. Napenda kuwashukuru
watu wote ambao waliamua kufundisha kuhusu maisha ya YESU kwa njia ya sinema,
walifanya vizuri wameelimisha watu wengi zaidi. Ila katika jamii na dini na
imani wamefanya kosa kubwa sana na MUNGU amelichukia sana jambo hili na
ninasema ukweli kutoka moyoni wangu bila unafiki kabisa sababu msema kweli ni
mpenzi wa MUNGU na msema uongo ni mpenzi wa shetani.
Ukisoma kitabu cha Kutoka 20:4-6; 4usijifanyie
sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala
kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5usivisujudie
wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA,
MUNGU wako, ni MUNGU mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata
kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao. MUNGU anasema usivisujudie wala
kuvitumikia mimi ni MUNGU mwenye wivu wote ambao watakao vitumikia ntawapatiliza wana maovu yao na kizazi chao. Point
hapa ni utaona amri ya MUNGU amekataa kitu chochote kisisujudiwe kikafanywa.
Sasa shetani amewateka watu fahamu zao na kuwafanya watu
walaaniwe na MUNGU na kutengwa na MUNGU kwa njia hizi za picha za mafundisho ya
YESU, cha ajabu ujue fahamu zimetekwa na shetani watu wameacha kumwangalia YESU
mbinguni wameanza kuangalia zile picha za walioact sinema hizo na kuwafanya
ndiyo YESU katika ulimwengu huu na cha ajabu hata katika fikra za wanadamu
ukiwauliza mnaijua sura ya YESU watakuambia ndiyo na kumbe ni sura ya mtu ndiyo
ipo kwenye fahamu, katika eneo hilo shetani amewateka wengi sana ikiwemo mimi
Hebron hapo mwanzoni nilijua ndiyo hiyo hata nilipokutana na YESU 2009,
Serengeti national park ilikuwa ni vigumu kumkubali YESU kwa jinsi sura yake
nilivyoijua mpaka aliponielimisha kuhusu ukweli huu na sura ya picha ya YESU
haupo katika ulimwengu huu kabisa, hivyo nawaeleza watu wote wa mataifa
unapozipamba katika nyumba hizo picha au katika kanisa tayari unakuwa umemkosea
MUNGU unampa mwanadamu nafasi ya kumwabudu ukiwa unajua au haujui na matokea
yake unakuwa umevunja amri moja wapo ya MUNGU.
Ikiwa ni kanisa linapamba hizo picha katika nyumba hiyo au
picha za wanafunzi wa YESU hata Petro tayari kanisa linakuwa limevunja
amri ya kwanza na ya pili na ya tatu. Sasa kama kanisa lenyewe limeshamvunjia
MUNGU amri zake je kanisa hilo litakuwa na uhusiano na MUNGU wa kweli tena? Jibu
hapana litakuwa na uhusiano na miungu hata waumini ndipo wanapopelekwa katika
ulimwengu wa roho. Huu ni wakati wa watu kutubu na kumrejea YESU wa kweli
katika hizo picha unapoziabudu zitafanya usiende mbinguni, wengine wanazilalia,
wanazitolea sadaka wakifananisha na YESU. Nawaeleza yeye ni mwana wa pekee
hafananishwi na chochote kile na unapozitolea sadaka na ibada haina tofauti na
picha yako, rafiki yako au mtu yeyote? Je ulimwengu huku ndiko kwenda mbinguni?
Jibu ni kupelekwa jehanamu, sasa usishiriki na hizo picha ile hasira ya MUNGU
isiwe juu yako, sababu nawaeleza nilivyokuwa naongea na YESU jambo hili linamuumiza
sana na shetanni anafurahia sana watu wanavyoacha kuweka fahamu zao katika roho
ili wamwone YESU lakini inashindikana sababu katika nafsi zao tayari wanawaweka
wale walioact sinema hizo wakiwa na nia njema ya kuelimisha jamii.
Na hata kama mtaupata ujumbe huu najua mnampenda YESU sasa
mwatangazie ulimwengu waache kuwaabudu nyie sababu nyie siyo MUNGU wala YESU
ili mataifa yapone na MUNGU atawabariki sana kwa sababu mtakuwa mmeshiriki
kumwaibisha shetani na mafundisho yake ya uongo na watumishi wake
wanaowadanganya watu kuwa ni sura ya YESU wakati ni uongo mkubwa na jamii
mmeipokea na kuamini hivyo katika ulimwengu wote 95% watu wote wanajua Brian ni
YESU na Robert hivyo hana watu wamepotea na huu ndio ukweli na kwa jinsi hii
inaonyesha wapo chini ya miungu hawa watu wote pasipo kujua sababu ya
mafundisho ya uongo.
Hivyo basi ili upone na usimuuzi MUNGU usiabudu tena hizo
picha, zitoe ndani mwako hata katika pete unaufikiri ni sura ya YESU hapana,
watu wanampenda YESU na ndiyo sababu wakisikia ni picha ya YESU wanaamini ila
wangefundishwa siyo hawa wameact tu hili tatizo lisingekuwepo, na mimi
amenituma kwa mataifa yote nieleze ukweli ili watu wapone. Msiabudu picha za
sinema, hakuna sura za YESU, wala za mitume wa YESU, wala ya malaika,wala ya
Maria na wengineo. Hizo ni acting tu. Na zaidi hata Mama Maria yeye siyo MUNGU,
kina Petro na wale mitume, hata malaika wote hawastaili kuabudiwa na hawaabudu
mwezi, wala jua, wala nyota, wala picha ya kiumbe chochote wao wanastahili
kumwabudu MUNGU pia na ndivyo wanavyofanya mbinguni niliwaona wanamsujudu MUNGU
mbinguni ila cha ajabu huku ulimwenguni watu wanawasujudu hawa watu, hawa ni
kama wewe tu ila tofauti ni kuwa wao tayari wameishinda ulimwengu na sasa wapo
mbinguni na wewe jitahidi utafika. Acha kuwaabudu, kuwasujudia ni dhambi
unakuwa unasujudia miungu na mwisho utaenda huko kwa miungu.
NABII HEBRON.