NINI
MAANA YA KUBATIZWA MTOTO MDOGO?
Katika somo hili ni kwa nini watoto wadogo wamebatizwa na
ilianzia wapi kusudi hili la shetani likatawala na la MUNGU kupingwa na matokeo yake watoto wadogo wakatengenezewa
laana mbele ya MUNGU pasipokujua au kupenda. Kwanza napenda mjue watu wote wa
mataifa yote MUNGU hakuwa ni mjinga asiruhusu watoto wadogo wabatizwe, alionyesha njia kwa mwana
wake wa pekee yaani YESU Luka 2: 29-32, utaona YESU hakubatizwa akiwa mtoto
mdogo bali alipelekwa kanisani awekwe wakfu na kutamkiwa baraka na kuwekwa
katika ulinzi wa MUNGU na ilifanyika hivyo. Wazazi wake Maria na Yusuph
walifanya hivyo. Je nyie wanadamu hamuoni huko ni kumdharau MUNGU? Jibu, ndilo
hilo. Shetani hapendi kabisa jambo hili sababu anajua watoto wakiwekwa wakfu basi
watakuwa na ulinzi wa MUNGU kama vile YESU na kisha atashindwa kuukamata
ulimwengu ila ili aweze kuukamata njia kubwa ni kuwabatiza watoto wadogo, pale
wanawekwa wakfu kwa shetani tangia utotoni mwao hivyo ni mpaka neema ya MUNGU
imfikie akiwa mkubwa amkubali YESU tena ndiyo aokoke na hata sasa wakristo
wengi usishangae hawataki kuokoka ni sababu ya ile chapa aliyewekewa akiwa
mtoto mdogo ya kumtenga na YESU na mbinguni.
Hivyo hizi kazi nyingi mnaona watumishi wanazifanya wengine
hawajijui na wengine wanajijua wanachokifanya ni kazi bure mbele za MUNGU,
wanafanya kazi ya kuujenga ufalme wa shetani na kuwafanya watu wawe mashetani.
Hivi ulishajiuliza iweje mtu aumbwe na MUNGU halafu amkatae MUNGU? ni sababu
ndani yake ipo roho ya shetani imetawala na ndiye baba yake sasa uelewe
unampinga MUNGU, wewe umepotea sasa mrejee yeye anakupenda tubu na usikubali
hata kubatiza watoto wadogo tena, unakuwa unamkufuru MUNGU unamtukuza shetani
na shetani ametukuzwa sana katika dunia hii. Ukiangalia vichwani ni wat wengi
wamebatizwa wakiwa watoto wadogo tena
bila kujua au kupenda. Amenituma nikufundishe na uelewe umrejee yeye. Sema
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote
na dhambi ya ubatizo nikiwa mtoto mdogo sijijui au nikijijua uliandike
jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele. Amen.
NABII HEBRON.