Pages

Tuesday, February 2, 2016

NINI MAANA YA KUBATIZWA KWENYE VUMBI?

Huu pia ni ubatizo wa shetani ambao shetani amewaongoza katika dunia hii katika baadhi ya makanisa sehemu mbali mbali ila maana yake kwanza unakuwa  umepatanishwa na dunia hii ukitoka kwa mavumbi utarudi kwa mavumbi na kufungiwa usiende mbinguni kabisa kama ilivyoandikwa wale wa dunia hii  hawawezi kuyasikia ya mbinguni. Ndiyo maana kubwa ya ubatizo huu wa vumbi ila pia unapatanishwa na mauti na hii yote ni maagano ya shetani anayoyaingia na huyo anayembatiza hivyo msikubali kabisa batizo hizo. YESU ameniambia niwaeleze sababu hata mimi Hebron sikuyaelewa haya, amenifundisha niwafundishe myajue ili mpone na shetani asiwaweze tena.

Na pia maana nyingine utakapo kata roho, roho yako irudi kuzimu isiende mbinguni juu. Cha kufanya, ubatizwe haraka upone ufutiwe hilo agano, neema ya YESU bado ipo sasa kwa ajili ya kuwarejesha watu wake na kuangamiza ufalme wa shetani aliojenga ambao ndizo hizi batizo za uongo na mengineyo. Utaweza ukaona makanisa ni mengi sana kazi ya MUNGU imeshawiri kumbe ni kinyume makanisa mengi ni makelele ya shetani, utayajuaje? Ni kwa matendo yao.

Na zaidi nitaendelea kwa wakati mwingine ni somo refu sana la kufundisha ila tubu, sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniondolee na dhambi ya kubatizwa kwenye vumbi tofauti na neno lako ni kwenye maji ya mtoni, uliandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele mimi ni mali yako. Amen.


NABII HEBRON.