Pages

Tuesday, February 2, 2016

NINI MAANA YA KUBATIZWA KWA JINA LA MCHUNGAJI AU NABII?

BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote. Karibu tena katika mada ya ubatizo za uongo ambazo watu wengi katika dunia hii wameipokea tena wakiwa wameokoka pasipo kujua bali wasimamizi wa huduma hizo ndiyo wenye siri hizo za kujua wanachokifanya kama walivyofundishwa na shetani na sasa muelewe ili mpone sababu hata wokovu wako unakuwa ni wokovu mfu siyo hai wala MUNGU hautambui. Hivi embu jiulize wewe kama wewe je ni wapi katika biblia imeandikwa tubatizwe kwa majina ya mitume au hata ya wale wanafunzi wa YESU wa kwanza mfano kina Petro, Marko, Luka. Hawa wenyewe hawajabatizwa kwa majina yao iweje leo mnaokoka halafu mnakubali kubatizwa kwa jina la mchungaji au nabii? Nitakueleza maana yake na chanzo chake na lengo lake.

Katika biblia inasema tubatizwe (soma Mathayo 28: 19-20) basi enendeni mkawabatize watu wote kwa jina la BABA na MWANA na ROHO MTAKATIFU tu na ndivyo ilivyo mpango wa MUNGU na ndiyo mapenzi ya MUNGU. Natumaini umeshaona ukweli hapo na ndipo hao waliookoka halafu wakabatizwa kwa jina la mchungaji au mtume au nabii utaona hapa haujabatizwa na zaidi unafarakanishwa na MUNGU uvuruge katiba yake na neno lake na mpango wake, sasa muulize why anakubatiza kwa jina lake? Jibu, hana, sababu hayo ni maelekezo aliyopewa na shetani ili hao waliookoka wafanyike kuwa wanafunzi wa shetani. 

Lile tendo la kubatizwa kwa jina la mchungaji au nabii au mtume inakuwa katika ulimwengu wa roho umebatizwa kwa jina la shetani na inafanyika hivyo sababu likitajwa jina la shetani wewe utakataa au kujua hivyo imetumika mbinu hiyo ili ujione upo sawa na unaendelea na wokovu na siku moja utaenda mbinguni kumbe umeshamkubali shetani awe ndiye baba yako, pale tu unapobatizwa kwa jina la mchungaji haijalishi akaongezea kwa jina la Baba na Mwana na roho mtakatifu, huo ni kukupiga upofu utaona tayari wamekuwa wanne je nikuulize swali, je MUNGU anao umoja na wanne au watatu tuu? Hili ni somo refu sana ila endelea kufwatilia makala ya Nabii Hebron na vitabu vyangu mbali mbali utjifunza ukweli kama alivyonifundisha YESU na hata mipango yao wanayoyafanya kuzimuna wakawateka wengi ila sasa amenituma kwa mataifa yote kuharibu falme za shetani na elimu yake ili watu wawe huru!

Katika mafunuo ya shetani anapomwinua mtumishi wake ni lazima ampe elimu yake na mbinu zake  na uweza wake wa  kutenda kazi yake ili kuwateka watu waliookoka na wasiookoka. Na nataka muelewe kama ilivyo yapo makanisa ya wokovu wa MUNGU wa kweli hivyo hivyo yapo makanisa ya wokovu wa mpinga kristo vile vile ikiwemo moja wapo ni yenye kubatiza kwa jina la mchungaji au nabii au mtume au mwinjilisti au mwalimu au askofu. Hapa umetekwa na shetani, anza upya na ubatizwe upya, na pia kubatizwa kwa jina la mtumishi unakuwa umeingia agano ya kuwa wewe ni wa shetani na ni wa huyo mtumishi siku zote za maisha yako na YESU anakosa nafasi ya kukumiliki wewe na ufanyike kuwa mali ya shetani badala ya kuwa umemilikiwa na YESU na MUNGU na ROHO MTAKATIFU. Hivyo unakuwa umefungwa kila eneo kuhakikisha wewe umeingia agano na shetani na pia kutengwa na ufalme wa MUNGU mbinguni. Mathayo 23:13.

NOTE:
Mtumishi anapofanya hivyo kwa jina lake baraka zako anazichukua yeye ikiwamo na nyota yako, sababu ndani yake inakuwepo roho mchafu mfano pepo ubatizo, pepo mhubiri na nyinginezo zinafanya kazi hiyo, zinampa yeye na vingine anavichukua shetani, mfano utaona unakiu ya kumtumikia MUNGU kuimba, kuomba, moto wa ROHO MTAKATIFU utashangaa hivyo vitu havipo tena unabakia na kutamani tu au mipango lakini mambo hayatimii. Hapo umeshaibiwa nyota na macho ya rohoni na lazima yatobolewe pale tu unapoingia katika madhabahu yake katika ulimwengu wa roho ili usijue kuhusu jambo hili na mengineyo, na pia lazima upumbazwe na ndiyo sababu ukasahau neno lisemavyo Baba, Mwana na roho mtakatifu ukaongozwa na la shetani. Hivi ndivyo YESU akiangalia uliwmengu na watu wengi wanaona wameokoka ila wapo katika giza.

Sasa nawaeleza na wewe usambaze kila mahali ili wapone, waokoke upya, warejee kwa YESU na wabatizwe upya. Hao ni wapinga kristo wala hawaitaji kwenda mbinguni ndiyo maana wanawazuia wanaotaka kwenda mbinguni (Mathayo 23:13-23, Mathayo 24:5) ndiyo hawa watumishi ambao YESU  alisema watawadanganya wengi sasa utabisha nini hapa? Haujadanganyika?  Okoka wakati ni sasa sema BWANA YESU naomab unisamehe na uniondolee wokovu wa kipepo na jina la shetani katika maisha yangu naomba ulitoe na jina langu katika kitabu cha wokovu cha shetani huko niliko batizwa kwa jina la mchungaji au mtu yeyote yule, uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele, mimi ni wako YESU. Amen.

Na zaidi hata sala za toba ambazo watu wameongozwa na hawa wanaobatiza kwa maji mengi na kwa majina yao na pia kwa kisima na batizo nyinginezo chafu. Kawaida yale majina yao yameandikwa katika kitabu cha wokovu wa shetani na siyo mbinguni sababu kinywa cha huyo mtumishi kinawaongoza katika nguvu ya giza katika kinywa ili kujikabidhi kwa shetani pasipokujua kupitia njia ya roho mchafu. Zaidi fuatilia blog hii na YouTube za Nabii Hebron na vitabu utapata mengi na utaiona nuru.


NABII HEBRON.