MAANA YA
KUBATIZWA KWENYE KISIMA NI HII HAPA…
Unapobatizwa kwenye kisima pale unakuwa umejiingiza kaburini
nafsi yako na kupelekwa kuzimu pasipo wewe kujua au kujua. Shetani alitumia
ujanja huu kulibadilisha neno la MUNGU ili awateke na wale waliookoka badala ya
kufunguliwa baraka za mbinguni na kuwekewa chapa ya YESU wa kweli, shetani
akawafundisha watumishi wake, nataka uelewe kama ilivyo MUNGU anawatumishi wake
na shetani anao vile vile. Waalimu wa MUNGU na pia shetani anao waalimu wake
ambao amewafundisha hivyo hivyo. Kama ilivyo MUNGU anao ubatizo wake na shetani
anao wa kwake vile vile. Ili MUNGU aufikishe ujumbe wake kwa watu anatumia
mtumishi wake wa kweli na shetani hufanya hivyo hivyo. Pale ambapo watu
wamefuata ukweli na kutenda hapo wanakuwa ni watoto wa MUNGU na pale ambapo
unafuata elimu ya uongo tayari na wewe unafanyika kuwa mtoto wa baba wa uongo.
Siri hii shetani aliwafundisha watumishi wake na wakakubaliana
miaka mingi na sasa linasambaa dunia yote, watu wanafikiri wataenda mbinguni na
wanampenda YESU ila wametegewa katika ubatizo wa kisima. Nilionyeshwa na YESU
itakavyokuwa siku ile ya hukumu katika baadhi ya maeneo na jinsi shetani
atakavyofanya akisimamisha mawakili wake katika kukushtaki wewe ulivyookoka
ukabatizwa katika kisima, sawa ametenda utakatifu lakini je mbona hakubatizwa
kama wewe uliye njia ya kweli na uzima katika mto ya maji yatembeayo? Shtaka la
kwanza, shtaka la pili umepokea ubatizo ambao katika neno lake MUNGU ukisoma
katika Ufunuo 22: 18-19 atakayebadilisha na neno langu hataenda mbinguni, sasa
jiangalie utapona? Yapo maswali mengi na MUNGU ni wa haki atatenda haki,
ninawajulisha mataifa yote na hata sasa ninavyoandika ujumbe huu naona kuzimu
imekasirika yaani wamenifuata jeshi lote wananiambia usiyaseme. Mimi nayasema
katika jina la YESU sikuogopi shetani kabisa naufichua uongo wako na maagent
wako uliowaletea hizi batizo za chapa yako.
Shetani alibuni ubatizo huu wa kisima kule kuzimu wanauita
ubatizo wa kuwekwa katika jeneza wasitoke tena, sababu ni mipango ya
kuhakikisha wewe uliyeokoka ukamkimbilia YESU siku ile ya mwisho ukutane na
shetani, nawaeleza mfunguke, injili ya YESU siyo ya vyuo, au dini, ni injili ya
kweli ya MUNGU mwenyewe kama anavyonituma ndivyo nisemavyo, uyapokee upone roho
yako. Ubatizo huu ni agano lako na shetani na kiongozi wa madhabahu hiyo wala
YESU hayupo hata roho mtakatifu bali ni roho mchafu ndiye anayeyasimamia haya
mambo machafu ni ya upande wa shetani na unapobatizwa ubatizo wa kisima unakuwa
pia baraka zako zimezikwa na wewe mwenyewe pasipokujua au kupenda na ndiyo
sababu utakuta watu wengi sana wameokoka na walipobatizwa ubatizo huu wa kisima
maisha yao yameharibika, ndoa zimeharibika, kazi hata elimu za watoto, nyota
inakuwa imeibiwa na shetani au mchungaji na inatumiwa na freemason katika
ulimwengu wa roho na zaidi unakuwa unayo laana na namba 666. Yapo mengi
nitaendelea kuwafundisha mataifa yote kila mara ili mponywe roho zenu na
msidanganyike tena. Shetani amewavuna hata waliookoka kwa kupitia ubatizo wa
kisima, ubatizwe upya ili uponye roho yako na maisha yako yafufuke upya.
KWA
NINI WATUMISHI WALIOOKOKA WANABATIZA UBATIZO HUU WA KISIMA?
1.
Kwanza hawa watumishi hawajaokoka mbele za MUNGU
bali wamekuwa ni adui wa huduma ya ubatizo wa mbinguni na kusimamia kazi za
shetani na mpinga kristo.
2.
Ni amri wanayopewa na shetani jinsi
anavyowabatiza watu wengi katika ubatizo wa kisima, shetani anawabariki na
mali, miujiza na kumpa umarufu katika dunia hii ila mbinguni yeye haendi na
analijua hili.
3.
Anakuwa tayari ni msaliti wa YESU kama vile Yuda
na YESU anawajua kabisa.
4.
Anawateka fikra zao wawe wajinga wasijue kweli
na wamtii atakachosema au kulitaka mfano akitaka pesa yeyote utampa tuu, au
gari lako, hata viwanja, na kwa njia hii hutumia kuwanyanganya watu mali zao
sababu nafsi zao amezicontrol shetani na hazina uhuru kama za wale waliobatizwa
ubatizo anaoutaka YESU, wamekuwa na alama ya YESU hivyo wapo chini ya YESU na
ROHO MTAKATIFU anawalinda na kuwaongoza. Ila wakiwa chini ya shetani
wataongozwa na shetani atakavyo na kuwawekea madeni ya kujenga injili za kipepo
na siku ile ya mwisho watu wanafikiri wataikuta taji mbinguni bali hata
mbinguni hawaendi bali watavishwa taji ya mateso mbele ya shetani.
NOTE:
Uokoke upya na ubatizwe upya tena na mtumishi ambaye MUNGU
anamjua siyo asiyetambulika na MUNGU au aliyejiita au kujifanya. Sema BWANA
YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uliandike jina langu mbinguni, unitoe
katika kaburi la shetani yaani ubatizo wa kisima, sasa uniongoze ubatizo
mtakatifu. Amen.
Na wapo watumishi walioiga
haya mapokeo yakatae utubu uokoke upya sababu haukujua. Ila wako
walioshiriki na shetani sijui watamjibuje BWANA.
Mathayo 23: 34-35.
NABII HEBRON.