Pages

Monday, February 1, 2016

NINI MAANA YA UBATIZO WA KIKOMBE?

BWANA YESU ASIFIWE! YESU WA NAZARETI karibu anakuja kulinyakua kanisa lake ila muda na siku na dakika ndizo hazijui, anajua MUNGU peke yake na aliniambia ameshaelezwa na BABA yake muda wake umefika na mimi Nabii Hebron nakukumbusha uokoke na ubatizwe na uishi maisha matakatifu ili usije ukabaki hapa duniani au kuzimu. Nitaelezea kwa nini watu wanabatizwa ubatizo wa kikombe. Huu siyo ubatizo, maana ya ubatizo ni kuzamishwa, sasa jiulize je kikombe utaweza ukaingia ndani yake? Jibu ni hapana, na katika biblia ubatizo huo haupo na kama haupo huu ni ubatizo wa shetani au miungu au fikra za wanadamu na siyo ubatizo wa fikra za MUNGU ambao yeye aliyoufikiria ili ufanyike kwa watu wote na mwanae akabatizwa ili yeye njia tuige hivyo hivyo. Kwa kifupi ukiangalia hapa hata anayekubatiza ubatizo huu ukimuuliza unatoka wapi, hajui. Na ndivyo ilivyo, unapelekwa mahali ambapo haoajulikani, kwa mungu asiyejulikana.

Pia je ujiulize huyu roho mtakatifu aliyetumwa na YESU asimamie na atuongoze katika safari ya kwenda mbinguni haya ndiyo aliyoyaona mbinguni? Jibu, hapana. ROHO MTAKATIFU hawezi kuwa ni mnafiki kwa YESU wala MUNGU, jambo lao ni moja. Sasa ubatizo huu siyo wao wala hauna umoja mbinguni bali ni ubatizo wa umoja wa roho mchafu, mpinga kristo na shetani ndipo chimbuko la huu ubatizo ulipotokea na ukaletwa duniani ili wawekewe wanadamu alama ya namba 666 na wao wakifikiria wamepokea kitu kitakatifu kumbe ni kitu kichafu na mauti ya milele. Ili upone, uokoke, ubatizwe katika maji mengi yanayotembea mtoni, alama hiyo itatoka na utapokea alama ya mtoto wa YESU.

Na zaidi kile kikombe kina maana hii, kule kuzimu lipo kikombe cha mauti na mateso na yale maji yanapowekwa pale unamwagiwa, unapatanishwa na nguvu iliyopo kuzimu inakufuata na kukushikilia na ndiyo sababu unakuta mtu hataki kuokoka na anajiita yeye ni mkristo. Yeye anakuwa ameshakufa kiroho ni roho mwingine wa shetani anayemshikilia ila yeye hajijui na ndipo utashangaa mtu akiokoka anasema alikuwa wapi siku zote amepoteza muda mwingi ni sababu alikuwa katika giza sasa anaona mwanga na furaha. 

Ukiwa na MUNGU wa kweli unakuwa na amani bali ukiwa na shetani utajaa hofu na yale maji ya kikombe yanayomwagika chini yanakuwa yamekupeleka kwa shetani na kukushikilia wewe ni wa shetani na kukufarakanisha na MUNGU na utakatifu. Ndiyo sababu mtashangaa mkristo ni mlevi, mchawi, anatenda matendo ya giza na anaona ni kawaida tuu, sababu ni hili agano la kikombe linamwangamiza mtu badala ya kumwokoa na hata hao wanaofanya hayo hawataenda mbinguni labda waokoke na kubatizwa kwa maji mengi na kuacha kufanya hiyo kazi, sababu wamejenga ufalme wa shetani na kuupindua ufalme wa MUNGU. Wengine hawajui wamefundishwa kwenye vyuo vyao vya dini badala ya kufundishwa na chuo kikuu cha mbinguni Biblia takatifu au gombo, wakalishwa gombo la shetani badala ya gombo la MUNGU likachanganywa na uongo hilo gombo ni sumu na mbele ya wafanyao hivyo wategemee hukumu, sijui watamjibuje MUNGU siku ile ya hukumu. Matendo hayo yanarekodiwa mbinguni wataonyeshwa na sheria ya mbinguni itafanya kazi yake, katiba ya MUNGU inavunjwa na watu hawana hofu.

SOMA:
Ufunuo wa Yohana 22:18-19
Yakobo 2: 11-26
Isaya 10:1-11
Isaya 30:1-4
Isaya 29:15
Isaya 33:1
Mathayo 23:23-28, 13, 14

Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima uliondoe katika kikombe cha shetani na uniondolee mateso. Uliandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Uniongoze nikaondolewe hii chata ya shetani au miungu ambayo siyo wewe umeruhusu bali ililetwa na waharibiayo neno lako sawa sawa na Isaya 33:1. Asante BWANA YESU. Amen.

Mathayo 24: 34-35


NABII HEBRON KISAMO.