JE UNAO
UHAKIKA UTANYAKULIWA NA YESU KWENDA MBINGUNI AU UTAACHWA HAPA DUNIANI?
BWANA YESU ASIFIWE, watu wote wa mataifa yote, MUNGU
anawapenda watu wake ila shetani hawapendi watu wa MUNGU sababu anajua
watarithi mbinguni ambapo ndipo ni pazuri na yeye atabakia katika shimo la
moto. Utasoma katika kitabu cha Yohana 14: 6-7; 6 YESU akamwambia,
mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. 7
Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Katika
somo hili nataka watu waelewe vizuri ili wapone roho zao na siku moja wafike
mbinguni na jambo hili linafurahiwa na MUNGU na serikali yake. Hapa utaona YESU
anasema yeye ndiye njia ya uzima wa milele na mtu yeyote hatafika mbinguni
pasipo kumjua YESU, lakini hapa watu wengi wametekwa na shetani sababu ya
mafundisho ya uongo, neno ni lile lile tu ila tafsiri zimeletwa za uongo na
watu wakaufwata uongo wengine wakijua na wengine pasipo kujua ila utakapo
uelewa ukweli hapo utakuwa umemjua YESU pia umemjua MUNGU.
Mimi Hebron hapo mwanzo nilikuwa ni mkristo ambaye
niliporithi udini ambao niliukuta kwa wazazi wangu na niliamini kabisa nitaenda
mbinguni lakini kumbe ilikuwa nisingeenda mbinguni kwa sababu nyingi ambazo
niliziamini na zilinifunga nisimjue YESU wala MUNGU wa kweli. Hapo utaona YESU
anasema katika mstari wa 6-7, ina maana ili umjue YESU ni lazima umwamini na
ukisha mwamini upokee alichokileta yaani wokovu na ukishapokea wokovu wa kweli
sasa hata hapo utamjua MUNGU, lakini ikiwa wanajiita wewe ni mkristo lakini
haujaokoka nakutangazia sasa bado haujamjua YESU wala MUNGU na zaidi huu ni
mtego uliowekwa na shetani kuwapiga watu upofu waone wapo na YESU lakini wapo
na mpinga kristo au yesu wa uongo. YESU huyo ambaye alisema mwenyewe
alipokuwepo hapa duniani kuna wengi watapotezwa na kudanganywa kwa kupitia jina
hilo.
Tazama sasa haujadanganyika na kama umedanganyika basi
uelewe unamwamini mpinga kristo na haumjui MUNGU wa kweli bali unaijua miungu
ila wewe haujijui wala haupendi ila unatekwa na shetani kwa kufwata elimu ya
uongo. Tunajua kuwa shetani ndiye baba wa uongo na unapouamini uongo tayari
yeye anakuwa ndiye baba yako uliyemwona na ukiwa unaufwata ukweli kama neno
lilivyo basi umemwona MUNGU na yeye anakujua na siku moja utafika alipo yeye
mbinguni na ikiwa umepokea uongo yaani mafundisho ya uongo basi uelewe hiyo
ndiyo njia yako ya kwenda jehanamu sasa uanze leo njia ipi utaifuata, ifuate ya
kweli mkatae shetani.
YESU anasema ukiniamini usiniamini kuwa ni mwana wa MUNGU
kama vile mashetani yanayoamini, unatakiwa uamini na uokoke na ubatizwe kwa
maji mengi, imani bila matendo imekufa, huko ndiko kufa kiroho watu wengi
wamemwamini YESU kama vile mashetani yanavyoamini. Mashetani hayaokoki, na wewe
mkristo, unajiita mkristo lakini hauokoki? Basi uelewe umekufa kiroho na
haumjui YESU wa kweli na MUNGU wa kweli. Sasa ni wakati wa mataifa yote kumjua
YESU wa kweli na MUNGU awe BABA yenu, msifikirie mnamfurahisha MUNGU mnapojiita
ni wakristo lakini hamuokoki, nawaeleza mnamfurahisha shetani sababu anakuwa
amekuteka wewe na wewe ndiye mtumwa wake katika ufalme wa giza.
Zaidi ukisoma katika kitabu cha Yakobo 2: 14-20, 26 utaona
Ibrahim alihesabiwa haki kwa matendo yake na wewe unajiita ni mkristo halafu
hauokoki, je MUNGU atakuhesabia haki
gani mbele zake? Imani pasipo matendo imekufa na hata sasa ndivyo ilivyo katika
ulimwengu wote shetani amefanya kazi yake ya kuua roho za watu kwa kuwazuia
watu wasiokoke na wajiite wao ni wakristo na watu wanaridhika. Amenituma YESU
niwaeleze ukweli, watu wa namna hiyo hawapo upande wake wapo upande wa mpinga
kristo. Ni mamilioni ya wakristo nilionyeshwa wakijiita ni wakristo na wakakataa kuokoka na wakazikwa
na makanisa yao ambayo yaliwazuia wasiokoke sasa wapo kuzimu kwa sababu waliifuata na kuitii injili ya uongo.
Lengo la
YESU ni watu wamwamini na kuokoka, ikiwa unamwamini YESU tu wewe hauna tofauti
na mashetani kwa jinsi wanavyoamini kuwa ni mwana wa MUNGU. Nawasihi muokoke
YESU anarudi kwa mara ya pili atamnyakua yule ambaye amemwamini akaokoka na
kubatizwa katika maji mengi ya mto, siyo ya kisima, ya tenki wala ya kubatizwa
kwa jina la mchungaji au kubatizwa kwa kikombe, katika batizo hizi YESU
alivyoonyesha njia katika mto Yordani ndivyo tufwate hivyo hivyo na kama umebadilishwa
basi uelewe umepoteza njia na kujizuia kwenda mbinguni sababu hizi batizo za
tofauti na kwenye biblia ni chapa za shetani na kila mwenye chapa za shetani
haendi mbinguni hiyo basi ni lazima uokoke upya na ubatizwe upya utolewe
satanic nembo au alama upokee alama za mbinguni takatifu.
NOTE:
Na jambo lingine ambalo shetani aliona ni jinsi gani atawawekea
alama za shetani hata wale walioamua kuokoka akaungana na wanadamu ambao ndiyo
watumishi baadhi yao wamefundishwa na shetani jinsi ya kubadili neno la MUNGU,
wakaanzisha baadhi yao mtu ameokoka halafu amebatizwa kwenye kisima au kwa jina
la mchungaji, na hao wanakuwa wametiwa alama za shetani na mauti na kufungiwa
kuwa na uzima wa milele wa mbinguni bali watakuwa na mauti milele. Na wengine wanasema YESU alibatizwa katika maji tele, ndiyo
ni kweli maji yalikuwa tele yamejaa mtoni na sisi tufwate hivyo hivyo sababu
wangekuja kubadilisha watu wangebatizwa mtoni hata pasingekuwa na maji ay
wangebatizwa kwa kuwaeleza watu katika mto usio na maji na kuwamwagia vumbi. Ukisoma
katika Yohana 22: 18-19, ipo laana ya kuzuiwa kwenda mbinguni unapobadilisha
neno. Hapo ndipo mlipofungiwa na shetani watu waliookoka wakabatizwa tofauti na
mtoni zaidi usome kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE cha Nabii
Hebron utaelewa zaidi, nimeelezea utapata majibu zaidi, hii yote nakupenda wewe
uliyewekewa alama ya shetani katika roho itoke na upokee ya YESU wa kweli ili
akija unyakuliwe.
Zaidi siri ambayo ipo ndani ya watumishi wanaobatiza huu
ubatizo wao wanaelewa kabisa wanafanya agano na shetani kukuzuia usiende
mbinguni na shetani anawasaidia kiuchumi katika mambo yao ya kimwili, lakini
hapa duniani watu wanawaona ni watumishi wa MUNGU ila katika ulimwengu wa roho
MUNGU anawaona ni watumishi wa shetani na hata baadhi ya wenye macho ya rohoni
wanaonyeshwa na ROHO MTAKATIFU pia. Na madhabahu ya jinsi hiyo siyo ya MUNGU wa
kweli imebadilika ni ya miungu na ndiyo sababu unafuata mambo ya miungu badala
ya kufuata biblia na kuwafanya mamilioni ya watu wapotee pasipokupenda wala
kujua. Ninakusihi uokoke ili ukristo wako ukamilike na umjue YESU na MUNGU pia.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya
kwa kujua na kutokujua, niliamini miungu, nilikuwa mgumu kuokoka, sasa
nakukubali wewe uwe BWANA na mwokozi wa maisha yangu. Uliandike jina langu
katika kitabu chako cha uzima wa milele. Uniongoze na roho wako mtakatifu na
umtoe roho mchafu katika imani yangu akaniteka nikakukataa. Nakupenda YESU. Amen.
Sasa umeokoka, zaidi fuatilia katika website www.prophethebron.org ingia katika link
ya blog na YouTube utajifunza mengi, roho wa MUNGU akuongoze. Nitaendelea katika
somo lijalo kuelezea zaidi somo hili ni refu bado. Natumaini sasa umepata picha
katika maisha yako ya kuwa yngenyakuliwa na YESU kwenda mbinguni au ungeachwa. Watumie
na wengine ujumbe huu ili wengine wafunguke wasije wakaachwa na YESU au hata
wakifa wasije wakaachwa kwenda paradise wakaenda jehanamu.
Mathayo 24: 34-35, Mathayo 23: 23-28, 13, 14.
NABII HEBRON.