Pages

Monday, December 21, 2015

WISHING YOU A MERRY CHRISTMAS 2015 AND A HAPPY NEW YEAR 2016!

NAWATAKIA HERI YA KRISMASI 2015 NA MWAKA MPYA 2016!

BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote, Nawatakia heri ya Krismasi na mwaka mpya wa 2016. Katika Krismasi hii nawasihi watu muokoke mpe YESU maisha yenu ili aungane nanyi katika ile siku yake ya kukumbuka kuzaliwa kwake miaka 2000 iliyopita mjiandae kiroho na kimwili. Sasa watu wengine hujiandaa kimwili tu na siyo kiroho, inapokuwa unajiandaa kimwili na siyo kiroho basi uelewe wewe haushiriki Krismasi ya kweli na takatifu bali unakuwa unashiriki krismasi ya kuzimu kwa sababu na wao wanao yesu wao vile vile kupitia mpinga kristo na ndiyo sababu utaona katika ulimwengu huu yapo mafundisho ya kumpinga YESU wa kweli na neno lake kwa kulibadilisha au kulichanganya na uongo na unaposhiriki tu tayari unakuwa na wewe ni mfuasi wa yesu wa uongo either kwa kujua au pasipokujua ila ukijua ukweli utawekwa huru na YESU mwenyewe.

Mimi Hebron kabla sijaokoka nilikuwa siyajui haya na nilijiita ni mkristo bali sitaki kuokoka na ninapenda siku ya Krismasi, kumbe nilikuwa naunganishwa na krismasi ya kuzimu kwa sababu nilikuwa najiandaa kimwili bali kiroho, roho yangu ilikuwa inafungwa na elimu ya uongo niliyorithi ya mapokeo ya wanadamu kutoka kwa wazazi. YESU akaniambia ulikuwa hausherekei siku yangu kwa sababu ulikuwa haupo na mimi nikamuuliza kivipi? Akaniambia ili mtu awe na mimi ni lazima apokee wokovu kwanza aokoke ndipo na mengine yangu atayashiriki na mimi. Hivyo na wewe nakukumbusha uokoke na uishi maisha matakatifu ili ile siku ya Krismasi ushirikiane na mbinguni pamoja na BWANA YESU WA KWELI.

Ni swali la kujiuliza utaipendaje sherehe ya Krismasi wakati wewe hautaki wokovu wake? Na zaidi ni ya ajabu hata baadhi ya makanisa duniani yanakataza watu wasiokoke, hivi mnajua maana yake ni nini? Maana yake ni kuwakataza watu wasimpokee YESU WA KWELI bali wampokee yesu wa uongo kwa sababu yesu wa uongo yeye haokoki yeye hana wokovu.

Wengine wanajiandaa na pombe, ulevi, disco na mengineyo ya ufisadi. Nataka uelewe Krismasi haipokelewi na pombe au ulevi au disco au ufisadi, inapokelewa na wokovu na utakatifu. Ila krismasi ya kuzimu inapokelewa na pombe, ulevi, disco na matendo ya kifisadi na pia hauokoki. Unapoona dalili hizo sasa unapata picha halisi upo katika krismasi gani katika haki. Ukweli unaujua mwenyewe jipime kwa matendo yako likiwamo je umeokoka? Ni mtakatifu? Unashiriki kuabudu sanamu na umempamba father Christmas? Unaweka Christmas tree? Zaidi usome katika blog hii kuhusu father Christmas ni nini? Christmas tree ni nini? Utaelewa zaidi.

MUNGU azidi kuwaokoa watu wake wampokee YESU wa kweli na kumkataa yesu wa uongo ili wawe wafuasi wa kweli na YESU, na siku moja watafika mbinguni alipo yeye wafurahi na yeye milele.

SALA YA TOBA:
Sema BWANA YESU  naomba unisamehe pale ambapo nilisherekea Christmas ya kuzimu pasipokujua au kwa kujua. Naomba uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, shetani sikutaki kabisa katika maisha yangu. Amen.

Zaidi angalia katika YouTube ya Prophet Hebron Kisamo zikielezea Jinsi Christmas ya kuzimu inavyosherekewa na itakusaidia kuepuka navyo na utamfurahisha YESU wa kweli na MUNGU wa kweli peke yake.

Ubarikiwe.

NABII HEBRON WILSON.