Pages

Monday, December 21, 2015

TANZANIA MPYA!
THE BEGINNING OF A NEW TANZANIA!

NCHI YA KIFALME BAADAE!
A ROYAL COUNTRY IN THE NEAR FUTURE!

Kama nilivyokwisha kuelezea tokea MUNGU aliponiita 2009-2010 nilikuwa nafanya kazi ya professional tour guide Serengeti nilipokutana na yeye maana nilikuwa simjui namsikia tu  YESU kwa jina na nimeelezea katika vitabu vyangu na makala mengi katika blog yangu na katika YouTube zangu miaka ya nyuma kuanzia 2010-2014. Yapo mengi ila nitaelezea kuhusu Tanzania mpya au Tanzania ndiyo Eden ya sasa. Maneno haya aliniambia YESU akaniambia uwaeleze na watu wote na sikukaa kimya japo wengine waliniona nimechanganyikiwa lakini namshukuru MUNGU pia kwa ajili ya hayo utukufu umrudie yeye.

Akaniambia Hebron mimi nimekuumba wewe kwa lengo langu maalum uje unitumikie na nilipanga muda ukifika iwe na ndiyo sasa ila nilikuficha kama  nilivyomficha Musa kwa sababu shetani angekujua pamoja na maajenti wake wangekuua mapema lakini pia hata hayo yote mabaya yaliyokuwa yanakufwata ni mimi MUNGU niliyaondoa na kukuepusha wala siyo mwanadamu aliyekusaidia. Yapo mengi ila nitaelezea kuhusu Tanzania na mengine yameshatokea na mengine yote yaliyobakia wakati wake ndiyo sasa kutimia sababu MUNGU ameniamuru niyaseme japo sitayamaliza, nitaendelea kuyasema kila mara na kusudi la MUNGU lazima litimie ila la shetani halitatimia tena katika nchi ya Tanzania mpaka YESU atakapokuja kulinyakua kanisa lake.

Kama nilivyokuisha elezea Tanzania ipo katika mikono ya YESU au dini nyingine wanamwita Nabii Issa kwa kingereza anaitwa JESUS. Ninaposema Tanzania mpya ina maana ile ya umasikini ya zamani sasa haipo tena, Tanzania ya kuwa ya nyuma, omba omba na ufisadi hiyo haitakaa iwepo tena, maneno hayo amenieleza MUNGU December 2015. Hivyo mabadiliko yote haya ni MUNGU ndiye anayeyafanya na atawatumia wanadamu hawa hawa. Nilishasema uchawi hautafanya kazi katika nchi hii, katika wizara, uchaguzi na mengineyo YESU anakaa hapo anawaongoza watu ili ainyanyue nchi hii mwenyewe na kusudi lake la nchi iwe Edeni litimie yeye ndiye afanyaye na utayaona kila siku tofauti. Zaidi usome kuhusu Tanzania nilielezea kuhusu bandari na mengineyo tayari yameshatokea nilielezea three years ago.

MUNGU aliniambia rais ni yeye ndiye atakayemweka na siyo mwanadamu wala malango ya kuzimu na atamwongoza yeye na atamshauri yeye peke yake na rais atakayemweka atakuwa ni wa kuigwa mfano katika ulimwengu wote na hata nchi baadhi zitatamani wapate rais kama huyu wa Tanzania lakini haitawezekana. Haya ni maandalizi ya mwanaye YESU WA NAZARETI kurudi na katika ule ujio wake na mwisho aliniambia atashukia kwa miguu yake katika nchi ya Tanzania hivyo anasafisha mwenyewe sababu nchi zote na nitu vyote ni vyake ila ameichagua Tanzania kwa kusudi lake yeye mwenyewe na siyo la mtu au wana maombi yeyote ni mpango wake kabla ya kuumba  kwa dunia hii ataifanya Tanzania kuwa ndiyo Edeni yake ya mwisho, alichokifanya aliniambia nitamweka kiongozi wangu wenyewe na nitamtumia mimi mwenyewe na kupitia yeye nchi yote itabadilika sababu jinsi alivyo kiongozi na ndivyo watu wake watakavyokuwa kwa kumwiga yeye  katika kufanya mambo ya nchi hii kutoka moyoni.

Nitaiinua Tanzania juu sana katika kila jambo kwa utukufu wangu mimi MUNGU wala hakuna atakayeweza kunizuia mimi MUNGU. Akaniambia nilishasema na viongozi baadhi yao waliopita ila walinikataa mimi MUNGU wakafwata njia zao na mimi MUNGU nimewaacha na nilishawaeleza wanisikilize kabla mambo hayajakuwa mabaya kwao na taarifa wanazo na sasa ndiyo aibu sababu waliona MUNGU hana uwezo au ni utani na ataendelea kuwaaibisha yeye ajua mwenyewe MUNGU. Akaniambia waeleze kila anayempinga rais John ajue ananipinga mimi MUNGU niliyemweka ili kumtumia mimi MUNGU na atakyemfanyia yoyote mabaya hatafanikiwa siku zote. Akaniambia mimi ndiye niliyemshika mkono na ninamlinda na jicho langu liko juu yake. Nitamtumia kusafisha nchi huu ndiyo wakati sasa wa yale yote niliyokueleza na hata wale walioiba pesa za nchi hii zitarudishwa zote.

Kutakuwa na maendeleo yasiyo ya kawaida kwa akili za kibinadamu, na miaka michache ijayo nchi hii ya Tanzania itakuwa ni nchi ya kifalme, maneno haya ameniambia MUNGU peke yake aliyeumba mbingu na nchi na maneno yake yatatimia, yeye peke yake ndiye anayejua itakavyokuwa, mambo yatabadilika hata siasa zitabadilika, bunge litabadilika sana. Nimeelezea katika makala na vitabu vyangu Nabii Hebron Wilson na mengi yametokea.

LOLIONDO GAME RESERVE KURUDISHWA KWA WATANZANIA WENYEWE.

Jambo lingine ambalo MUNGU atafanya njia ni kuhusu loliondo game reserve atairudisha katika nchi na ataitoa katika mikono ya hao ambao wanaimiliki sasa hivi. MUNGU hafurahishwi na jambo hilo kabisa. Kibinadamu mtaona haiwezekani lakini MUNGU yeye kwake inawezekana. Na itakaporejeshwa itakuwa ni mali ya watanzania wote na haitabadilishwa tena wala kupewa mtu aimiliki itakuwa chini ya serikali ya nchi hii.

Wanyama wa Serengeti itafika wakati hawahami tena sababu mvua zitakuwepo kipindi kirefu Serengeti.

Nilisema elimu itakuwa bure 2015 sasa imetimia. Na sasa uthamani wa mazao yaliyopotea katika nchi ya Tanzania mfano katani (sisal) kuanzia sasa zao hilo litashamiri kuliko zamani miaka ya 1980 kurudi nyuma. Kahawa na yenyewe itastawi sana na kurudi kushika nafasi ya kwanza duniani kwa kuzalishwa kahawa hayo mtayaona MUNGU yeye dniye afanyaye na mazao mengine kwa ujumla.

Nchi itakuwa ni ya amani na hawatavamiwa na nchi yeyote ila jeshi limeinuliwa sana pia na usalama wa taifa. Japo kuwa uovu uliyofichika katika yale aliyonieleza MUNGU katika jeshi yatafichuliwa, kila kitengo kitatengenezwa upya. Katika baraza hili wapo baadhi ambao wasipobadilika na wao watatolewa muda siyo mrefu, MUNGU ndiye anayeijua mioyo yao ikiwa pamoja na wa kwako. Ni vizuri kuwa na hofu na MUNGU kwa kila mtu

Mbarikiwe, mengine nitaendelea kuyaelezea wakati wake. MUNGU ibariki nchi yako Tanzania. Amen.


NABII HEBRON WILSON.