Pages

Sunday, December 20, 2015

DALILI ZA UJIO WA YESU ZIMEANZA DECEMBER 2015…HAYA NDIYO ALIYONIELEZA MUNGU MWENYEWE.

BWANA YESU ASIFIWE. Kila mtu anajua kuwa siku moja YESU atakuja kulinyakua kanisa lake yaani wewe uliyookoka na kuishi katika utakatifu. Ukisoma katika kitabu cha ufunuo kinaelezea habari za ujio wa YESU mara ya pili na ya tatu na hivi sasa ni ujio wa YESU mara ya pili.

Mnamo tarehe 7.12.2015 MUNGU aliniambia Hebron huu ni wakati sasa wa maandalizi ya ujio wa mwanangu kuja kulinyakua kanisa. Ninayokueleza uyaseme kwa watu wote wa mataifa yote na mimi ninamtii.

A.    MABADILIKO YA HALI YA HEWA YASIYOREKEBISHIKA KWA AKILI ZA KIBINADAMU.

Kwanza zitanyeesha mvua za ajabu ambazo hazijawahi kuonekana katika macho ya watu katika dunia hii na zitafanya uharibifu mkubwa sana katika maeneo mbali mbali katika dunia yote. Itafika wakati ardhi itapasuka na kugawanyika na itafika wakati milima itapasuka kati kati baadhi yake. Yatatokea magonjwa yasiyotibika mabaya zaidi ila watapona wale tu watakaomkimbilia YESU wa kweli na kwa watumishi wake tu. Matetemeko yataanza katika dunia nzima kwa vipindi tofauti na yatafanya uharibifu na kuangamiza.

Sehemu nyingine mvua zitakatika kabisa na jua litashuka au kusogea katika sehemu yake na kushuka katika dunia kwa kiwango fulani kutakuwa na joto kali, sehemu nyingine chemchemi za maji zitakauka. Dunia nzima itasikia sauti ya MUNGU na ukuu wake. Mateso yataanza kuwa mengi ila hayatawaweza wale waliomkimbilia YESU. Mapepo ya ajabu na malaika wa shetani wataonekana katika ulimwengu huu katika mwili wakitembea. Kutatokea maafa mengi zaidi duniani kote.

B.    YATAKAYOWAPATA WATUMISHI WA SHETANI NA WALIOMSALITI YESU.

1.     Wengine maisha yao yataharibika kwa ghafla na kuporomoka na hawatainuka tena.

2.     Wengine mtaona ghafla wamekuwa ni vichaa.


3.     Wengine watakufa vifo vya aibu na vya mateso.

NOTE:

Haya ni baadhi tu ya yale aliyonieleza MUNGU na mambo haya ni kwa ajili ya ulimwengu wote hivyo mtakapoyaona msiogope hayanabudi kutokea ni MUNGU kayaruhusu na wala hayatabadilika. Watakaopona ni wale waliookoka hivyo basi tubu sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nakurejea wewe. Uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na kazi zake zote. Amen.

Zaidi soma katika blog hii yapo mengi na nitaendelea kuyasambaza kwa utukufu wa MUNGU wa kweli.


NABII HEBRON WILSON.