BWANA YESU
asifiwe, watu wote wa mataifa yote, au kwa jina lingine huyu YESU anaitwa
Nabii Issa.
Katika makala
hii ya Nabii Hebron, nitaelezea na kuweka kweli kwa watu wote, ili hii kweli
iwaweke watu huru na siku moja mfike mbinguni sababu hata mimi sikuujua ukweli hadi
YESU mwenyewe alivyonifundisha kama Mtume wake kwa ajili ya kazi yake atakavyo
yeye na siyo mapokeo ya watu. Mambo hayo alinifundisha miaka minne iliyopita
(2011) kuhusu watu wavyopokea na kufundishwa
uongo japo hawajui na wengine wanajua. Aliniambia hivi Hebron, hivi mimi nipo
kaburini au mbinguni? Nikajibu upo mbinguni. Akaniuliza swali lingine, hivi
mimi jina langu ni kaburi au ni nani? Nikamjibu wewe ni YESU. Akaniambia, Hebron,
mimi sipo pale kaburini, na siishi pale, wala hakuna kitu changu chochote,
hivyo itafika wakati utaenda, ila usisujudu pale, nenda katembee kama vile
mtalii na
ukajifunze.
Usifanye ibada wala kuabudu kaburini kabisa, akaniambia na mimi kwenda kutembea
Israel, ila usivisujudie vitu hivyo iwe ni makaburi ya mitume, na maeneo yote, ukienda
tofauti na hivi utakuwa umepotea na utakuwa umevunja moja ya amri ya MUNGU; usiabudu
chochote, wala kukisujudia chochote kwa mfano wa kitu.
Akanieleza,
huku Israel ni mahali pa historia na kumbukumbu za mitume na hata mimi katika
maisha
tuliyopitia, mimi nipo mbinguni, ila sipo kaburini sasa watu wanafanya sala
pale kaburini; maombi yale yanabadilishwa katika ulimwengu wa roho,
yanachukuliwa na yesu wa uongo na kuunganishwa na mpinga kristo na shetani
anakuwa anao uhalali sababu imeandikwa katika amri zile kumi
"usisujudie". Sasa pale kaburini ni kama sanamu. Au nikuulize wewe, je,
unaposali pale kaburini; je, shetani
akikuuliza hilo swali, utamjibuje? Ni nani unamsujudia hapa kaburini? Je,
anaishi hapa? Jibu ni hapana, na kama haishi hapa, sasa unamsujudu usiyemjua
pasipo kujua au kwa kujua. Hivyo basi, kama kwamba YESU katika eneo ambalo
hayupo uelewe umemwabudu shetani na watu wengi
wanafikiria eti walienda katika kaburi la YESU na hata katika makaburi
yote ya mitume na manabii, elewa pia, nataka uelewe kuwa hata shetani na yeye
anao mitume wake hivyo hivyo na MUNGU
anao wa kwake na wapo hapa duniani wanaendeleza kazi walizotumwa. Nataka
muelewe ukuu wa YESU hata kimwili, kwani YESU katika kaburi lake angekuwapo au
baraka zake au nguvu zake, nawaeleza hivi, aliyefika pale angebadilika kiroho
na kimwili. Cha ajabu walevi, wachawi, watumishi wa uongo wanaenda kila siku,
cha ajabu hawabadiliki na zaidi hata
waabudu sanamu wanaenda hakuna mabadiliko ya utakatifu. Hiyo ni ishara YESU
hayupo kaburini hivyo msifanye maombi
katika kaburi la YESU. Utakayesikia elewa ili upone, utakayekaza shingo, ujumbe
umeupata na YESU anajua umeujua ukweli hivyo utubu na uwache. Wewe nenda
katembee tu na kujifunza. Yeye yupo
mbinguni na atarudi kulinyakua kanisa ambalo ni mtu aliyeokoka na asiyefanya
matambiko, YESU hana matambiko. Niliogopa sana maana na mimi sikuyajua haya.
Mimi YESU nipo mbinguni, natafutwa katika roho na kweli, njia nilishaionyesha
ifuatwe; na hata katika Biblia haijaruhusu watu wakaabudu katika kaburi langu
mimi YESU. Katika kaburi kuna mizimu,
hivyo ukifanya sala kaburini unakuwa unaungana na mizimu, na mizimu inakuwa kwa
shetani. Jitengeni na mizimu.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina
langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Sitarudia wala kujaribu kusujudu
katika kaburi lako kwa sababu wewe haupo
pale.
Nabii Hebron.