Kama nilivyokwisha elezea katika makala ya Nabii Hebron
yaliyopita, nilishaelezea ni kwa nini Petro (yule mtume wa YESU) alivyouliwa
alizikwa ndani ya kanisa. Ile ina maana hii; Petro yuko na YESU wa kweli, yeye
amezikwa asiandike tena katika nyakati hizo na ndiyo sababu Injili ya kweli
ilifungwa na injili ya uongo ilisambaa zaidi hata sasa.
Katika kanisa pale ni mahali patakatifu, siyo mahali pa
kuwekwa mizoga au hata kuhifadhiwa mafuvu au mifupa ya watu waliokufa. Kila mtu
hata kimwili hapendi kukaa kaburini, ni sababu kaburi na mahali pa mateso,
pabaya natumaini hata wewe ambaye unajua siku moja utakufa ukaweka ndani ya
moyo wako haufurahii kufukiwa kaburini. Sasa tukija kiroho na ki-formula za
MUNGU, kanisani ni mahali pake yeye, na siyo mahali pa kuwawekea wafu au
kuwazikia wafu. Hii ni sababu MUNGU yeye siyo MUNGU wa wafu ni MUNGU wa wenye
uhai na uzima.Shetani ametumia mbinu hii kuwateka watu na hata imani zao pasipo
kujua japo wanaamini ni madhabahu hizo wasijue kuwa wao wanaabudu mungu wa wafu
au mungu mfu, na hii unaposhiriki tu katika nyumba ya ibada ambayo watu huzikwa
ndani, au wanyama, uelewe hapo unajipotezea muda wako, haupo na MUNGU aliye
hai, bado upo katika himaya ya mungu mfu, hivyo kama ni ukristo wako au na
mwingine ukristo huo ni mfu mbele za MUNGU wa mbinguni, wala sio ukristo hai
sababu YESU yu hai, yupo mbinguni, tunamwabudu aliye hai, na kama upo katika
madhabahu hiyo uelewe wewe ni mkristo mfu, YESU aliye hai anasema huu ndio
wakati wake, hakuna nyakati nyingine zaidi hata katika Biblia. Sasa tunasubiri
unyakuo, aliponieleza YESU habari hizi akaniambia, uwaeleze mataifa yote wajue
ukweli na watakaosikia wataponywa.
Hii yote ni kazi ya mpinga kristo, amelifanya kanisa ni
kaburi. Hata mimi YESU sikuzikwa katika madhabahu. Na ukiona madhabahu imezikwa
mtu ndani ya kanisa, madhabahu hiyo ni mfu na inaunganisha na matawi yake yote.
Alinieleza maneno haya akitoa machozi kwa ajili ya upendo alio nao kwa watu, na
wanapotezwa watu wengi wakijua wapo na MUNGU wa hao kumbe mungu mfu. YESU amesalitiwa
na watumishi baadhi yao katika ulimwengu, na alishasema mtawatambua kwa matunda
yao. Rejea sasa kwa YESU anakupenda na uokoke umrudie tena. Ndiyo sababu roho
ya mauti ina uhalali wa kuishi ndani yako na mateso.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe, dhambi zangu zote
nilizozifanya kwa kujua, na kutokujua, niliabudu katika kanisa lenye kaburi
ndani, nikawa mfu, naomba unifufue sasa, unishike mkono nisipotee tena,
uniongoze. Amen.
Zaidi tembelea website www.prophethebron.org
Nabii Hebron.