BWANA YESU asifiwe. Tunajua
kabisa hakuna, na tunaheshimu; na zaidi ya vitu vyote duniani na mbinguni,
hakuna zaidi ya MUNGU aliyetuumba sisi na vitu vyote. Mwaka 2015, hapa Tanzania
kuna jambo baya sana lililofanyika la kuipindua ile siku ya BWANA ya Jumapili ambayo
MUNGU ameifanya ni siku yake maalum ya yeye kuabudiwa, aliumba vitu vyote kwa
siku sita, na ya saba akapumzika. Na pia, Mwenyezi MUNGU katika amri zake zile
kumi amesma; ikumbuke siku ya BWANA, uitakase. Jamani YESU anarudi kama
nilivyoelezea, kanisa limetekwa na shetani 98% katika ulimwengu wote. Na utajua
kwa matendo yake, Neno la MUNGU linasema, katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana
22:18-19, usiliongeze wala kupunguza wala kubadilisha yeye alishapiga mhuri. Na
endapo mtu ataenda tofauti, basi ataondolewa sehemu yake ya uzima.
Jambo hili ni mfano hai,
nashangaa ni Biblia ipi inasema watu wasisali Jumapili, wafunge makanisa wasali
Jumamosi, Jumapili wakapige kura? Haya ni makosa ya viongozi vipofu, na huko
ndiko kuwapoteza watu sababu huo siyo mwongozo wa MUNGU wala Biblia, MUNGU akapinduliwa
na watu wakawatii pasipo kujua, hii ni dhambi; inawahusu walioipindua siku ya
BWANA. Muulize, ni wapi imeruhusiwa tusifanye maombi, tukafanya mambo
mengine? Hapa kila mtu atachukua mzigo
wake mwenyewe, hasa viongozi iwe ni Nabii, Pastor, Mtume, Mwinjilisti, Mwalimu.
Niwaulize, haya ndiyo yameandikwa katika Biblia? Huu ndio upofu, au ndio kuwa
kiongozi asiyeongozwa na MUNGU wa kweli, akafuata ya mapokeo, na waumini wakafuata
ya mapokeo ya wanadamu, badala ya Neno la MUNGU. Hii ni dalili tosha ya kuwapotosha
watoto wa MUNGU.
Uchaguzi bila MUNGU bila MUNGU
kwanza ni kazi bure. Ila wapo waliokataa hiyo kauli, na Jumapili walifanya
ibada na kisha wakaenda kupiga kura tena kwa furaha pasipokuwa na dhambi ya
kuvunja amri ya MUNGU. Nikuulize swali; Je, siku ya ibada ya YESU yaweza ikatenguliwa
Jumapili ifanyike Jumamosi? Jibu haifai. Umevunja mpango wa MUNGU, hata watu
dunia yote msikubali kuivunja siku ya saba ya ibada. Madhara yake soma Ufunuo
wa Yohana 22:18-19. Umepotezwa na mapokeo ya wanadamu na umeyapuuzia maneno ya
Mwenyezi MUNGU. Ikitokea hivyo msikubali, cha ajabu hata serikali inayo hofu ya
MUNGU, haikatazi watu wasiende kanisani jumapili ili wakapige kura, cha ajabu
watumishi ndiyo wamevunja amri ya MUNGU. Kila mtu anajua, hii ni dhambi, na
viongozi wa juu hao ndiyo wale ambao wamekuwa wapinzani wa Neno la MUNGU, au
kumpindua MUNGU mpango wake.
Nabii Hebron.