UNABII WA
MUNGU WA KWELI KUHUSU UCHAGUZI WA URAIS 2015 UMETIMIA NA TANZANIA MPYA (EDENI)!
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE! Au kwa jina lingine anaitwa
Nabii Issa. Kama nilivyokwisha elezea katika makala yangu ya Nabii Hebron
kuhusu unabii wa Tanzania tokea 2012, 2013, 2014, 2015 mtaona yaliyotimia
katika kila kitengo nilichokielezea kabla ya
muda hata na watu baadhi yao waliona nimechanganyikiwa kwa sababu ya
yale niliyoyaelezea. Watu baadhi waliona haiwezekani, ila jambo lolote MUNGU
akisema ni lazima kitokee na halipingiki wala kubadilika. Nitaelezea mambo
machache ila mengine mtayasoma katika blog hii.
a.
KUHUSU RAIS
ATAKAYECHAGULIWA NA MUNGU 2015
Kama nilivyoelezea nilivyokuwa naongea na MUNGU kama vile
alivyokuwa anaongea na Ibrahim, Musa na baadhi ya manabii wake kwa sababu wapo
wanaoota ndoto, wapo wanaoongea na yeye mdomo kwa mdomo na kujibiana na ndivyo
ilivyokuwa kwangu tokea aniite aliniita kwa kinywa chake nilikuwa Serengeti nikahojiana mpaka nikamwelewa na ndivyo afanyavyo mpaka
sasa. Nilipoongea na yeye miaka mitatu na miwili iliyopita katika siku tofauti
yapo mengi ila naelezea kwa ufupi katika swala la uchaguzi wa 2015 na mimi
niliyasema kama alivyonieleza ila kibinadamu watu wanafikiri ni maneno
yaliyotokea katika kinywa changu na fahamu zangu, akaniambia wewe Nabii wangu
na ninakuweka katika nchi hii ambayo nataka kuinua kwa ajili ya utukufu wangu hivyo
lazima uyajue haya na pia uelewe pia na shetani na yeye anao manabii wake hivyo
hivyo wakitumia jina la mwanangu wakati hata hao siyo wangu ila itajulikana na
kusudi langu Hebron mimi MUNGU nikisema ni lazima litokee na halizuiliki ila
kusudi la shetani analoongeaga na wafuasi wake waliojificha kwa kutumia jina
langu kumbe ni wa shetani, nakueleza Hebron, hayatapita maneno hayo ni yako
uyahifadhi mpaka nitakapokuruhusu na sasa ameniruhusu ninayasema.
Kuhusu Rais John Magufuli kama nilivyosema atakuwa ni rais
ambaye yeye jina lake halikutazamiwa na watanzania au nilisema nanukuu atakuwa
ni rais ambaye watu hawakutazamia kabisa na ndivyo ilivyokuwa katika yale
majina tokea mwanzoni kwanzia kwenye chama chake hata wakati wa kufuatilia fomu
katika ule ushindani kwa macho ya kibinadamu matumaini ya watu idadi kubwa
hawakumtazamia yeye angechaguliwa kuwa mgombeaji na akapitishwa.
Pili hata katika ushindani wa kampeni ukiangalia ulivyokuwa
na ushindani na akapita. Hivyo ninathibitisha tu katika unabii nilioutoa kuwa
Rais ajaye atakuwa ni mtu asiyetazamiwa na wengi na ndivyo ilivyokuwa na maneno
haya aliponiambia MUNGU aliniambia Hebron na wewe ukiwa ni Nabii wangu usiombe
lolote katika uchaguzi omba mapenzi yangu yatimie na siyo mapenzi yako ikiwa
namaanisha nampatia jina la mtu ninayemtaka na ndivyo ilivyo na wengine baadhi
wachache walioomba hivyo na wengine waliomba kwa kupeleka majina ya mapenzi yao
na fikra zao. Wengine waliomwomba shetani na akawaahidi uongo na ndiyo sababu
wanashangaa haijatokea ila mwishoni katika makala hii nitaelezea utapata jibu.
Ilipofika mwezi April 2015 aliniita MUNGU kwa sauti yake
akiwepo Malaika Gabriel kwa sura yake mbele yangu tukaongea mengi, akaniambia
Tanzania ni nchi yangu nimeiteua kuwa ndiyo Edeni yangu ya sasa kama
nilivyokueleza tokea 2010, nimeishika katika mkono wangu mimi ndiye
nitakayemweka kiongozi wa nchi hii ninao watoto wangu baadhi yao wanafaa na
wengine hawafai kabisa na wneigne wananipenda ila wanakataa kusikiliza sauti
yangu bali wamewafuata wale ambao mimi siyo baba yao bali wanao baba yao wa
uongo na walitumia jina la mwanangu, lakini mwisho wao umefika na hii itakuwa
ni kwa uliwmengu wote, utukufu wangu wa mwisho umerejea sasa na mkubwa kuliko
wa kwanza. Akaniambia Hebron nakufundisha uelewe hata kina Musa niliwafundisha
na wakaelewa na wewe sasa umeshanielewa mimi MUNGU niliyekuumba nakupenda kwa
sababu unasema kweli na katika ukweli watu wengi wanaponywa na kufunguka na
kutolewa katika magereza ya shetani yakiitwa kwa jina lla kanisa na kumbe siyo
yangu yanajificha kivuli cha jina la mwanangu, lakini usiogope Hebron,
yalikwisha andikwa katika vitabu vitakatifu hivyo ni lazima yatokee na sasa
yametokea katika ulimwengu wote.
Akaniambia Hebron utasikia watu wengi wakitabiria viongozi
kuwa ni mimi nimewaambia mfano mtu fulani na fulani ni mimi ndiyo nimemteuwa au
nimewateuwa. Hebron mimi MUNGU wako na BABA yako na pia ni mama yako nimekuumba
wewe nilijua itafika utakuwa Nabii wangu
ila nilikuficha miaka yote ili shetani asikujue sababu nilichokifanya kwako ni
kuharibu kabisa ufalme wake na ufalme wangu wa mbinguni usimame katika dunia
hii na wakati ni sasa. Akaniambia hao watu mimi sijawatuma, siongei nao ila
tayari walishaenda kuzimu baadhi yao wakaelezwa na walikuwa wanaelezwaga mengi
na watu wakielezwa wananona yanatokea akasema ni mwisho wao sasa nawaaibisha,
mwanangu karibu anarudi na kundi la waongo ndilo lenye wafuasi wengi na hata
hao wafuasi hawajijui wanapigwa upofu sasa nawafungua mimi mwenyewe wanijue
mimi .
Hivyo ndugu msomaji natumaini umepata picha kidogo ni nini
kilichotokea. Watumishi wakatabiri uongo, hao waliopewa taarifa hizo za uongo
na baba yao wa uongo na akijua itakuwa ndiyo sababu watu wakapokea uongo,
wakauamini, wakautendea kazi baadhi wakaupigia kura na matokeo yake
walichotabiriwa n kuhubiriwa kumbe ni taarifa za uongo na hata kusababisha kuwanajisi
wagombea. Ukisoma katika kitabu cha Yeremia 23:28-33. MUNGU anasema mimi
sikuwatuma ndiyo sababu wametabiri uongo yeye ni kweli. Nataka mjue Nabii ni
kinywa cha MUNGU (Hesabu 12:8), lakini pia shetani pia anao manabii wake ambao
hutumia vinywa vyao hivyo inavyokuwa hivyo uelewe kibywa cha Nabii asemaye
uongo ni kinywa cha shetani.
Nilipokuwa naongea na MUNGU, akaniambia ninao watoto wengi
tena wazuri wenye hofu ya MUNGU ya kweli ambao wanafaa kuwa Rais wa Tanzania
2015 na akaniambia kuanzia sasa mpaka atakapo rudi mwanangu kulinyakua kanisa
yeye mwenyewe ndiye atakayewaanda na nitakujulisha sababu hata neno langu
lasema sitafanya lolote bila kumjulisha Nabii wangu hivyo nakujulisha. Akaniletea
picha za watu watatu alikuwepo Samwel Sitta, John Magufuli, Harrison Mwakyembe
nikabakia nikishangaa, kisha akaniaga anaondoka kurudi mbinguni nikabakia na
Malaika Gabriel, akasema kusudi la MUNGU ni lazima litimie na yeye akaniaga
akarudi mbinguni. Nilikaa wiki nzima nikitafakari lakini bado kinywa kimefungwa
siwezi kumweleza mtu hadi ilipofika mwezi wa sita 2015 akaniletea jina moja akaniambia huyo ndiye mapenzi yangu na jina
hilo ni la John Magufuli, akimwandaa yeye MUNGU na ndiye alimwongoza na kumpa
kibali hicho na kumfanya yeye ni Joshua wa kweli wa kutoka katika mapenzi yake.
Hayo ndiyo aliyoniambia na sasa yametimia leo ndiye Rais wa nchi ya Tanzania
2015 na mkono wa MUNGU upo juu yake, amemshika mkono yeye.
b.
KUHUSU JESHI LA TANZANIA
Nilielezea jeshi la Tanzania limeinuliwa na uthamani wake
ulioibiwa umerejeshwa mmeona jeshi la polisi lilivyofanya vizuri, hii haijawahi
kutokea katika nchi hii, MUNGU amewainua nilishasema na katika kitengo cha
jeshi ni jeshi lote la Tanzania. MUNGU yeye ndiye atoaye vipaji sasa vipaji
anawashushia na ndiyo sababu linakuwa ni mfano hivyo atukuzwe MUNGU wa
mbinguni, sifa zimrudie yeye na sasa msahahu madhaifu ya zamani siri mmeijua. Kuna
nchi ziliiba uthamani wa vitu vyetu mfano jeshi na jeshi la nchi zao linaonekana
ni bora zaidi, sasa wamenyang’anywa katika jina la YESU WA NAZARETI wa kweli.
c.
MATOKEO YA UCHAGUZI
Kama nilivyoelezea soma katika makala ya unabii wa Tanzania
2015 nilisema katika siku ile ya kura watu watabadilishwa fahamu zao na
kumpigia kura yule ambaye MUNGU anamtaka yeye na hii ndiyo ilivyotokea na wengi
hata mnaousoma ujumbe huu utashangaa siku ya kura ulibadilisha ukajikuta
unahama na ukampigia rais wa sasa. Haya nilishayasema na yametokea, nilisema
hivyo kwa sababu wapo watumishi watu
wamefikiri ni watumishi wa MUNGU wa kweli na wana umoja wao na wanapeana
hata upako wa shetani ili kazi ya mpinga kristo ishike h ila sasa huo upako wa shetani uliharibiwa
na YESU pamoja na serikali yake, na ndiyo sababu mnashangaa aisee imekuwaje
tena na upako wa kinabii walionao? Jibu unalipata huo ni upako wa shetani
hauwezi kushindana na YESU wa mbinguni,
na zaidi watu wengi walitekwa nafsi zao kupitia upako wa shetani wakahubiriwa
na kulazimishwa katika ulimwengu wa roho wamchague nani hilo YESU aliliona na alilitengua
sasa imebakia aibu ya baba yao wa uongo.
Nilisema YESU atasimamia uchaguzi na YESU akisimamia jambo
basi linakuwa na amani tu na ndivyo ilivyokuwa Amani. Nilisema wapo mawaziri
watapoteza nafasi zao za ubunge, imetokea, na wabunge wengi watakuwa ni wapya
na wengine wataachwa na vyama kabla ya uchaguzi baada ya vyama vyao kuwakataa
au kupitia kura za maoni watahama wengine watashinda na wengine watakosa
kabisa.
d.
KUHUSU VYAMA VYA SIASA.
Nataka uelewe vyama vya siasa havina shida wala haipaswi kuviwekea
chuki yeyote ile, tatizo lililopo katika vyama vyote ni kuwa baadhi ya watu
wasiyo wenye hofu ya MUNGU, hivyo watu baadhi wasipokuwa na hofu ya MUNGU
wakatenda jambo baya hizo lawama zinakifanya chama kionekane ni kibaya mimi
Nabii nasema vyama vyote ni safi ila watu baadhi yao ni wachafu kimatendo na
hii ndiyo inayosababisha watu wavichukie vyama badala ya kuchukia tatizo na
yule atendaye. Mimi kama mtumishi wa MUNGU sitakiwi kuwa ni mshabaki wa chama
chochote bali ni kuwaombea wote hata sitakiwi niwe na kadi ya chama chochote. Inapokuwa
mtumishi wa MUNGU anayo kadi ya chama chochote hapo anafanya makosa ni dhambi,
huwezi kuwatumikia mabwana wawili na watumishi kazi yao ni kuhubiri injili siyo
kwenda kwenye majukwaa ya siasa au kuwanadi wagombea, hiyo ni dalili hawapo na
MUNGU wa kweli bali mtumishi anayeongozwa na roho ya shetani yeye anaruhusiwa
na baba yake wa uongo, mtawajuaje ni kwa matendo yao (soma 1 Yohana 4:1-6). Na shetani
katika ulimwengu wa roho alipoona kusudi la mapenzi ya MUNGU lazima linatimia
alitoa amri akasema nao wawasaidie katika mikutano ya siasa baadhi yao wakatoa
ushauri wakiwa wamepewa aina ya nguvu ya
kipepo inayoitwa sumaku za kuvuta watu na hilo pia YESU aliliharibu
halikufanikiwa. Ilikuwa ni vita kubwa ya kiroho kati ya mbinguni na kuzimu
lakini walishindwa hivyo muwe makini sana hata nchi nyingine, sasa hivi mambo
yameharibika YESU anarudi kulinyakua kanisa lake sasa jiulize wewe upo na
mtumishi anayesema ukweli au uongo? Hilo litakuwa ni jibu la wewe kukufanya
ujijue wewe upo salama au upo hatarini, lakini neema bado ipo, tubu uokoke
upya.
e.
WALIOTABIRIWA UONGO KATIKA UCHAGUZI.
Nataka waelewe wao hawana shida yeyote na wanampenda MUNGU
na MUNGU anawapenda ila hawakusikia sauti ya MUGNU wa kweli wengine walijua
kabisa lakini wengine hawakujua ila wameponzwa kuingizwa katika swala hili
sababu wengine hata wasingegombea kabisa ila walidanganywa eti MUNGU amesema
mfano wewe ndiye hivyo na wao wakatii sauti za manabii au watumishi pasipokujua
je ni MUNGU kasema kweli na tena wengine wakapakwa mafuta kabla ya uchaguzi,
nilishangaa sana mambo hayo ambayo hayakuwa ni ya MUNGU bali anasingiziwa
MUNGU, watu hawamwogopi MUNGU kwa kusema uongo hata kuwafanya watoto wa MUNGU
baadhi yao wanabakia na vilio ndani ya mioyo yao. Nataka uelewe ingekuwa kweli
kasema MUNGU na amemtuma aseme fulani na fulani ndiyo rais basi ingekuwa tu
MUNGU hazuiliki jamani wala hamna wa kumshinda MUNGU kabisa, ahadi zake ni za
kweli kwa watu wake, sasa iweje ahadi alizozitoa zisitimie jamani? Basi uelewe
ulipokea ahadi za uongo na Nabii akisema uongo na ikithibitika ni uongo basi
yeye ni nabii wa uongo ni mtoto wa baba wa uongo. Walipoona nabii zao za uongo
zimevurugwa na YESU wakatoa isingizio eti kura zitaibiwa embu jiulize wewe kama
MUNGU wa kweli kamweleza sasa itakuwaje ashindwe kuzuia kura zisiibiwe? Utaona tena
hapa ni tatizo hili.
Na wengine walisema asipokuwa mfano mtu fulani basi afe au
apate adhabu kama biblia inavyosema adhabu ya Nabii asema uongo, haya mapigo
hayazuiliki yatatimia tu, neno la MUNGU ni hai, ni kweli. Wengine walisomewa
mistari katika biblia ikitamkwa ni wao na bado haijawa. Hii inakuonyesha vinywa
vingi zaidi vya watumishi ni vinywa vya shetani na siyo vya MUNGU zaidi soma
kitabu cha JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI kilichoandikwa na Nabii Hebron
na pia sikiliza YouTube za 2013-2014 nilielezea uchaguzi utakavyokuwa na kuhusu
rais ajaye na jinsi watakavyoliwa pesa zao na jinsi watu wengi watakavyolia na
imetokea ni sababu ya kupotezwa na baadhi ya kauli za viongozi vipofu na hiyo
ni dalili hawaongozwi na MUNGU bali ni lusifa. Na hata kazi zao ni za kuua roho
za watoto wa MUNGU wasiende mbinguni. Hivyo nyakati hizi ni mbaya utaweza
ukaingizwa kwenye matatizo ya kukugarimu maisha yako kwa kuwasikiliza manabii
wa uongo na unapowasikiliza pia tayari unakuwa unamsikiliza baba yao na
ukikubali kuyafuata mambo yao tayari na wewe unanajisika, hivyo okoka, utubu
ili upone.
BAADHI
YA MAMBO YATAKAYOTOKEA KATIKA UONGOZI WA JOHN MAGUFULI KUANZIA 2015.
1.
Uchumi utainuka zaidi.
2.
Pesa ya Tanzania itapanda thamani na kuwa ya juu
zaidi Afrika mashariki na baadaye itapanda hadhi kuingia katika historia ya
pesa zenye thamani katika dunia hii.
3.
Walioibia nchi pesa au kuliingiza taifa katika
hasara watafilisiwa na wengine watafungwa kifungo kirefu na wengine watafia
gerezani kabla ya kumaliza kifungo chao, na baadaye wapo ambao baada ya kuwafunga na kufilisiwa na
serikali hii na rais huyu atawatoa gerezani kwa msamaha wake maalum na hii
itakuwa ni fundisho kwa watanzania, wafanya kazi, viongozi wa juu katika nchi
na wizara mbali mbali.
4.
Elimu na matibabu yatakuwa bure, unabii wa Nabii
Hebron niliyotamka miaka mitatu iliyopita unatimia.
5.
Air Tanzania itakuwa na ndege zake zaidi ya tano
very soon. Landing fee za ndege zitashuka bei, na ndege zitaongezeka nyingi
sana za mataifa mengi.
6.
Wapo watanzania walitaka kuwekeza katika nchi
hii mfano kununua ndege walinyimwa vibali sasa watapewa
na hata katika transport watapewa tena bila kudaiwa wapewe share ndiyo
wakubaliwe kuingiza vitu vyao kwa kuwekeza.
7.
Kesi za uwizi wa mali za serikali zitafufuliwa.
8.
Mikataba yote itapelekwa bungeni kujadiliwa upya
na sheria zitabadilishwa sana katika
vipengele vingi ili nchi ifaidike.
9.
Viwanda kufufuliwa, viwanja vya ndege vya
migodini vitafungwa.
10.
Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
11.
Bunge hili litakuwa moto zaidi la msimu
uliyopita, na wabunge wengi hawatakubali miswaada isiyo na maana upitishwe na
watafichue uovu zaidi. Na mengine mengi yatafanyika, nitaendelea kuyaandika kwa
wakati wake na muda wake. Na amani ya Tanzania itaendelea kudumu zaidi na zaidi
na hata wanaosema kutatokea vita nawaeleza hakuna vita itakayotokea ndani ya
nchi, hayo ndiyo aliyonieleza MUNGU na mtayaona.
NOTE:
Yapo mengi aliyonieleza MUNGU na ni MUNGU mwenyewe ndiye
atakayemwezesha na mtayaona kama nilivyoyatabiri yote ya nyuma mmeyaona na
serikali itasafishwa katika vitengo vingi na atapewa mwongozo na MUNGU na siyo
wachawi na wanajimu.
Nakusihi uokoke YESU anawapenda sana watu wote yeye siyo mwongo ila wengi wameongozwa sala ya toba na Nabii
wa uongo basi uelewe jina lako lipo
katika kitabu cha uzima wa shetani sasa tubu; Sema BWANA YESU naomba unisamehe
dhambi zangu uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele wa
mbinguni. Amen.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA AHADI ZAKO ZITIMIE KATIKA JINA LA
YESU WA NAZARETI.
NABII HEBRON.