YESU AMESEMA
MSIKITENDEE KAZI CHAKULA KILICHOHARIBIKA
MTAKUFA KIROHO!
BWANA YESU ASIFIWE, YESU wa Nazareti aliye
hai, ukisoma katika kitabu cha injili ya
Yohana 6:27 utaona YESU anasema msikitendee kazi chakula kilichoharibika, akiwa
anayo maana chakula hicho ni neno la uongo ni neno ambalo ni tofauti na biblia
na unapolipokea tu na kuliamini na kulishika hapo tayari umekula chakula
kilichoharibika cha kiroho, hata kibinadamu unapokula chakula chenye sumu mwili
unadhoofika au unaweza ukafa kabisa.
Na kiroho ndivyo ilivyo watu wengi
wanakula chakula kilichoharibika cha kiroho pasipokujua, na wengine wakijua
kabisa na jambo hili tayari limeua wana wa MUNGU kiroho na mbinguni hawaendi ni
mpaka neema ya MUNGU imfikie huyo aliyelishwa mafundisho ya uongo, akutane na
mtumishi wa kweli wa MUNGU, ndiye atakayeweza kumfufua tena kiroho na kumtenga
na hayo mafundisho hapo atapona. Je umeshajiuliza kwa nini YESU anawaonya
mataifa yote msikubali mafundisho ya uongo? Ni sababu anajua mtakufa kiroho na hamtamuona
yeye bali mtaenda kwake yeye aliyewaletea mafundisho hayo.
Mimi Hebron aliponiita YESU aliniambia mengi
hasa zaidi anahuzunika jinsi watoto wake wanavyolishwa sumu na baadhi ya
watumishi ambao wamemsaliti YESU na wengine hata YESU aliniambia yeye hawajui
wamejiita na wanatafuta pesa kupitia jina langu. Haya Hebron uwaeleze mataifa
yote wanijue, waonye wasile mafundisho ya uongo yanawaua na hata mpaka sasa
wale watu ambao wanayafuata ya uongo wajue wamekufa kiroho mimi sipo nao kabisa
sababu mimi YESU siyo chakula kilichoharibika, mimi ni chakula kitakatifu yaani
neno la kweli ambalo MUNGU amelipiga
muhuri yaani linafaa kwa watu wote.
Zaidi soma vitabu vya mtume Hebron
na ingia katika website www.propherhebron.org ingia
katika link ya youtube utafunguka katika mengi sana na hata huko ulipo kama
ulikuwa umekufa kiroho BWANA YESU atakufufua ikiwa pale utaamua kuyafuata haya
nikuelezayo sasa sababu na mimi siyo maneno yangu ni maneno ya YESU kutoka
katika kinywa chake nikufundishe wewe.
a.)
Mifano michache ya baadhi ya vyakula vya kiroho vilivyoharibika.
· Ubatizo wa
kikombe, ubatizo wa maji ya kisima, kubatizwa kwa maji mengi na kwa jina la
mchungaji.
· Makanisani
unachangisha pesa, au waumini unachajiwa pesa , mfano ili ufanyiwe huduma
unachajiwa pesa na tena pastor hana aibu anadhubutu kulitaja jina la YESU,
usimshangae huyo kasha kufa kiroho na yeye.
· Kuabudu sanamu,
kufanya ibada za wafu, kuruhusu pombe kanisani au hata kuzibariki tena
usidanganyike siku hizi hata watumishi wanaosema wameokoka baadhi yao baada ya
ibada wanakunywa pombe tena na waumini hata katika nchi ya America, Asia,
Europe, Africa, huko ni zaidi. Nawaeleza hamna MUNGU wa kweli majini na mapepo
ya ulevi na Roho Mtakatifu hayupo hata ibada mnazoshiriki enyi waumini
msitegemee kabisa mtamuona YESU wa kweli
hapo, hata kama kanisa linaitwa la MUNGU, HOLY SPIRIT, la YESU, pakiwa na
pombe, hicho siyo chakula kitokacho mbinguni, ni chakula kilicho haribika au ni
sumu ya roho ya kuwaua watu wafe kiroho na ndiyo sababu nawaona watu katika
nchi mbalimbali ninavyoandika ujumbe huu mnampenda YESU ila wengi mmekufa
kiroho na wala hamjielewi mnaomba sana, mnatoa sadaka sana, na mmeokoka
hampendi dhambi. Ila upo katika kanisa lenye chakula kilichoharibika umeshiriki
na wewe ukafa, unaomba sana hakuna majibu, umebakia kukata tama, shida haipo
kwa MUNGU wala YESU wala serikali ya mbinguni, shida ipo katika chakula kilicho
haribika.
Zaidi soma makala nyingine za Nabii Hebron utajijua zaidi na
utapona. Hii ndiyo njia nyingine ambayo shetani amewapiga watu upofu hasa
wakristo na hata waliookoka baadhi yao, wanaona wapo na YESU kumbe tayari ni
maiti katika ulimwengu wa roho pasipo kujua sasa ufurahi sababu YESU anawapenda
amenituma kwako na kwa wengine mkaujue kweli na ufufuke usile tena chakula
kilichoharibika, ni bora ukae nyumbani kuliko kwenda katika ibada ukashiriki
tena yaliyoharibika utakufa tena na hali yako itakuwa mbaya zaidi.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, unifufue
upya, sitaki tena chakula kilichoharibika, mafundisho ya uongo na mengineyo
machafu na dhambi, uniongoze wewe nikujue wewe YESU wa kweli na sikutaki yesu
wa uongo na mafundisho yako katika jina la YESU. Amen
Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA
YOTE, matatizo yote utaombewa na utalishwa chakula cha mbinguni na kubarikiwa
na kufunguliwa shida zako zote bila kuchajiwa pesa yeyote, sababu ni YESU
mwenyewe ndiye anayewalisha watu chakula chake. Yeye hachaji pesa bali shetani
anachaji pesa akiwatumia watumishi hao hao ambao ndani yao YESU wa kweli
hayupo, yupo yesu wa uongo na ndio sababu wanafundisha uongo wa huyo yesu wao.
NABII
HEBRON.