SIKUKUU YA
MAVUNO NI SIKUKUU YA WANA WA MUNGU KUJILAANI WENYEWE KIUCHUMI KUPITIA KANISA.
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE,
katika makala hii ya Nabii Hebron natumaini watu wengi watanishangaa ninaposema
kuwa katika sikukuu maalum ambazo baadhi ya makanisa yanaitenga kama ibada
maalum kwa ajili ya mavuno yapelekwe kanisani na pasipo watu kuelewa wanafanya
jambo baya katika nyumba ya MUNGU sababu wanapoyapeleka yale mazao
kinachoendelea utafanyika mnada hapo kanisani, iwe ni ndani ya kanisa au nje ya
kanisa huo ni mnada na anayefanya huo mnada ni dalali, wakati kazi ya mtumishi
siyo kuwa dalali, hiyo tayari ni dhambi.
Na jambo hilo limeota mizizi sana
katika dunia yote kwa kiwango kikubwa pasipo watu kuelewa ni vibaya na shetani
amefunga fahamu watu wanajijua yapasayo kufanyika katika nyumba ya ibada,
ukirudi ukisoma katika kitabu cha agano la kale MUNGU alipowabariki wana wa
Israel katika mavuno yao na mifugo aliwaagiza wamtolee MUNGU, na siyo kufanya
mnada, zamani mazao yalichomwa moshi
ukaenda mbinguni sadaka zilipokelewa, baada ya kizazi cha Musa kupita, akaja na
yeye YESU akakuta katika nyumba ya sala wanafanya minada, minada ambayo ndio
kama haya haya katika sikukuu za mavuno makanisani, YESU aliyakataa sababu
unapofanya mnada tayari siyo nyumba ya MUNGU tena na shetani anao uhalali
kabisa ya watumishi au dhehebu hilo kuruhusu jambo hilo, shetani anamnyanyulia
bango MUNGU hapo sipo mahali pako pangekuwa ni kwako pasingekuwa na vitu vyangu
ambavyo ndivyo hivyo mfano sikuu ya mavuno.
a.)
Sadaka ya Mavuno ni nini?
Sadaka ya mavuno ni fungu la kumi unalolipata katika
mazao uliyoyavuna mfano umevuna magunia kumi ya maharage basi gunia moja ni la
MUNGU na kama ni la MUNGU basi ndiyo sadaka yake, sasa kama ni fungu la kumi umelitoa je linafanywa mnada?
Wewe
unapotoa sadaka yako ya mshahara wako au faida yako ukaipeleka kanisani je
huwaga unatoa nje halafu inauzwa kufanyiwa mnada? Jibu siyo, sasa basi uelewe
jambo hilo ni dhambi na ni laana na hata wewe unayetoa mavuno yako ukapeleka
kanisani yakafanyiwa mnada uelewe bado haujamtolea MUNGU 10% yake sababu 10% ya
MUNGU hainadiwi iwe kubwa au nyingi yeye anajua ulichokipata na anaridhika
nacho, wewe cha kufanya unauza hayo mazao unapeleka 10% yako na hapo
utabarikiwa na ikiwa ni kinyume na hapo unajichochea kujilaani kiuchumi na
ndiyo sababu mashamba mengi yamelaaniwa hata na wafugaji na zaidi hata ukiuza
ukayapeleka katika kanisa hilo hilo linaloendelea na mipango hiyo hiyo ya
minada ya mavuno bado uelewe utakuwa umetupa sadaka yako sababu hapo ni sokoni
siyo ibadani hata kama umetoaga katika mishahara au faida ya biashara yako pia
elewa haiendi kwa MUNGU sababu lipo pando la shetani, shetani ameitumia njia
kuliteka kanisa na hata baadhi ya watumishi hawaelewi wanaiga mafundisho potofu
na wengine kabisa watumishi baadhi yao wanajua kabisa ila hawasemi ukweli
wanaifurahia siku hiyo ili wazichezee sadaka za waumini kwa kuzinadi na
kumfukuza MUNGU kwa njia hiyo.
Hivyo sasa unayetaka kubarikiwa katika baraka za
mazao yako sasa umeujua ukweli, na pia uelewe sadaka yako ni siri yako sasa
inapofanyiwa mnada hiyo imekuwa siyo siri tena tayari imeharibika na kama
imeharibika huko ndiko kujilaani mwenyewe pasipo kujua au kwa kujua na kwa
kumfanya yeye alaye awe anao uhalali wa kukufilisi sababu ulipigwa upofu
ukaenda tofauti na YESU na neno la BABA yake linavyosema, pia muelewe kipindi
hiki ni kipindi cha agano jipya siyo cha agano la kale, YESU yapo mambo ya kale
aliyoyatengua mfano mtu akikosea usimpige mawe hadi afe kama zamani na pia hata
zamani walipotoa sadaka za mavuno hawakufanya mnada, walitoa kama vile sadaka
mazao yakachomwa basi, cha ajabu sasa wanayachukua na kuyafanyia mnada, mpaka
hapo hiyo ni dhambi na hata huyo kuhani amelaaniwa dhambi ya uwizi mbele za
MUNGU na pia waumini, sasa mmeujua ukweli, mambo haya yote ni shetani ndiye
aliyefanya ili kuwateka watu maana tofauti na biblia kama ilivyo na kuichafua
nyumba ya sala na kama nyumba ya sala ikichafuka basi hapo sipo mahali pake na
kama sipo mahali pake basi yupo mwenye kuishi ambaye ni shetani katika ulimwengu
wa roho.
Sasa ukatae kushiriki tena sema, Bwana YESU, naomba unisamehe dhambi
zangu zote uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele
uniongoze wewe YESU nisiende kutoa sadaka yangu ya mavuno katika sehemu hizo
sababu nitakuwa naendelea kujilaani kiuchumi na kiroho, Amen.
Zaidi ingia katika website www.prophethebron.org ingia
katika link ya youtube na blog utajifunza mengi.
NABII HEBRON.