Pages

Thursday, June 25, 2015

JE UMEKULA MANA YA MBINGUNI AU MANA YA SHETANI?
MANA YA MBINGUNI NI IPI?
MANA YA SHETANI NI IPI?

BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE, yeye bado upendo wake juu yako upo anakupenda yeye hajabadilika bado yeye ni yeye jana na hata milele. Katika somo hili au mafundisho nitafundisha somo kuhusu mana ni nini? Nitaelezea mana ya mbinguni ilivyo na mana ya kutoka kuzimu ambayo hata sasa watu wengi baadhi yao ni wakristo pasipo kujua wanalishwa mana ya kuzimu badala ya mana ya mbinguni. Haleluya! Ukisoma katika kitabu cha injili ya (Yohana 6:27-39) msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na BABA, yaani MUNGU. Basi wakamwambia, tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za MUNGU?  YESU akajibu, akawaambia, hii ndiyo kazi ya MUNGU, mwamini yeye aliyetumwa na yeye.

Wakamwambia, unafanya ishara gani basi ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. YESU akawaambia, Amin , amin, nawaambieni, siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali BABA yangu anawapa ninyi chakula cha MUNGU ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. Basi wakamwambia, BWANA, siku zote utupe chakula hiki. YESU akawaambia, mimi ndimi chakula cha uzima, yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini. Wote anipao BABA watakuja kwangu, wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja bali nimfufue siku ya mwisho.

Hapa utaona YESU anakataza tusikitendee kazi chakula kilichoharibika sababu unapo kitendea kazi basi na wewe unaharibika ila chakula chenyewe ni mafundisho ya uongo ambayo nitaelezea japo kwa ufupi natumaini utapata picha na utaelewa zaidi ingia katika website ya www.prophethebron.org, ingia katika link ya you tube nimeelezea vizuri hili somo la mana na chakula kilichoharibika utafunguka zaidi. Aliponituma YESU kufanya kazi yake sikumuelewa hapo mwanzoni ila siku baada ya siku alinifundisha kwa jinsi ajuavyo yeye mwalimu wa waalimu wala hakuna mwalimu kama YESU. Nilicho kuja kugundua nilikuta YESU anaijua kila elimu, kila ujuzi, hata ni mwana sayansi anajua kila kitu na elimu zote na ujuzi na kila utaalam ambao unawaona wataalam wanafanya jambo fulani YESU anajua hayo yote nilishangaa sana.

Mana ni chakula cha mtama au ni vyakula ambavyo wana wa Israeli walishushiwa na MUNGU kutoka mbinguni wakati wakiwa katika safari ya kuelekea katika nchi ya ahadi kupitia mtumishi wa MUNGU nabii Musa na walikula kwa miaka arobaini hadi wakafika katika nchi ya ahadi. YESU akaniambia Hebron wewe ndiye Musa wa sasa wa kuwapeleka watu katika nchi ya ahadi yaani mbinguni kipindi kile cha kwanza Musa aliwatoa kwa Farao utumwani hadi nchi ya ahadi wakavuka na bahari ya Shamu na MUNGU aliwalisha yeye mwenyewe, alishusha chakula kutoka mbinguni wakala siku zote na sasa wewe Hebron ni Musa wa kumalizia kipindi hiki cha mwisho cha kulinyakua kanisa hivyo pokea mana ya kuwalisha watu wote wa mataifa kuwaelekeza katika safari ya mbinguni na mana hii ni neno la MUNGU uwalishe katika roho, chakula hicho ndicho YESU mwenyewe ambacho ni neno la MUNGU lililopigwa muhuri na MUNGU mwenyewe, akaniambia katika safari ya kwenda mbinguni kila atakayekula mana yangu atafika katika nchi ya ahadi ambayo niliwaahidi naenda kuwaandalia makao hata sasa yapo tayari. 

Ila Hebron nataka uelewe shetani nay eye anaye Musa wake na anayo safari yake ya kuwateka watu kuwapeleka katika nchi ya ahadi yake ambayo ndiyo jehanam sasa uwaeleze mataifa yote wafundishe wale watakao kusikiliza watapona na wale watakao kataa kitakachotokea ni kama vile wakati wa Musa wale wana waisrael waliompinga walifia jangwani, hata kwako asiyekusikiliza na kufanyia kazi ataangamia sababu maneno hayo ni yangu mimi YESU WA NAZARETI nasema  na ulimwengu wote kupitia mwili wako, kama vile kipindi cha Musa MUNGU aliutumia mwili wake na hata yote yaliyotendeka ni MUNGU ndiye aliyeyafaya kupitia mwili wa Musa.

Sasa shetani na yeye ameandaa mana yake vile vile ambayo watu hawaelewi na unapoila tu na wewe tayari roho yako imekufa na ndiyo mtego anaoutumia kuwateka watu sababu ni chakula kiharibikacho yaani kimetoka kwa shetani, lengo lake ni kuharibu maisha ya watu na wasifike mbinguni na wasimwone MUNGU ila sasa uwaeleze na mimi nimewaeleza tuyashike. Nitaelezea mana ya mbinguni ni ipi?

a). Mana ya mbinguni ni nini?

Mana ya mbinguni ni neno la MUNGU ambalo linatoka mbinguni na halijachanganywa na uongo au linaongezwa au kupunguzwa. Hicho ndicho chakula kisicho haribika na unapokila na wewe hauta haribika au kuangamia au kwa maana nyingine unapokitumia utaurithi uzima wa milele na atafanya ndani yako ya kukupa uzima mpaka ile siku ya unyakuo uende katika nchi ya ahadi ya mbinguni au unaweza ukasema mana ni neno la MUNGU la kweli.

b).Mana ya shetani au kuzimu ni nini?

Mana hii ya shetani au ya kuzimu ni mafundisho ya uongo au neno lililochanganywa na uongo na linahubiriwa makanisani au katika mikutano baadhi ya injili, na watu wakayapokea hayo mafundisho na unapoyapokea tu  tayari nao wanaunganishwa katika safari ya nchi ya ahadi ya kuzimu ambako ndipo alipo shetani, nitaelezea kwa ufupi na utaelewa bila wasi wasi na hakika utamtambua YESU sana kwa kukufunulia siri hii ya mana ya kuzimu ilivyo, na ninatumaini sio ajabu hata wewe au mwingine ulisha ila na haujui kuwa ni sumu ya kuuwa roho yako, kwanza hata mimi Nabii kabla ya kuitwa na YESU niliila hiyo mana ya shetani ila kwa neema yake  YESU akaitoa na kunitapisha nikawa huru. 

Mana hii ni haya yafuatayo japo yapo mengi hayajatokea mbinguni mfano mana ya kuzimu ni ubatizo wa kikombe, ubatizo wa kisima,kubatizwa ubatizo kwa jina la mchungaji, tafuta katika biblia mambo haya hayapo na kama hayapo basi hayajatoka mbinguni na kama hayajatokea mbinguni basi yamekupeleka hukohuko yalipotokea yaani kuzimu na ili uende au ufike katika nchi hiyo ya ahadi aliyowaandalia shetan ni lazima ule chakula kiharibikacho ambacho ni neno la uongo, mafundisho ya uongo haijalishi unajiita wewe ni mkristo angalia je hayo uliyoyapokea yametokea mbinguni? au hayajulikani yalipotokea.

Yapo mambo mengi sana sasa hivi injili kupitia jina la YESU watu wanatafuta pesa baadhi yao na watumishi wengine wametokea kuzimu 100% na wengine waliitwa na YESU  baadaye wakamsaliti YESU na sasa  wapo upande wa shetani, ila watu hawaelewi ila mtawajua kwa matendo yao, mfano, ukisikia kanisa linachangisha mchango uelewe hayo ya mbinguni (mana) MUNGU  hajaruhusu na watu hawaelewi wanaona wanaona wanamfanyia YESU lakini kumbe  unaposhiriki kufanya michango kanisani tayari yale wanayoyatenda ni wamekula mana za shetani, na matokeo yake wanafia jangwani katika ulimwengu wa roho hawatafika mbinguni kama vile wale wana waisraeli kipindi kile walivyofia jangwani kimwili mpaka leo hii wenzao wakafika. 

Mana  ya kuzimu- kuabudu sanamu, kuwatoza waumini pesa ili wapate huduma ya kiroho, tazameni MUNGU yeye kasema nimekupa bure toa bure hiyo ndiyo mana ya mbinguni ila uliyechajiwa pesa na ukatoa ili ufanyiwe maombi uelewe umekula chakula kiharibikacho na wewe kwa kupitia tendo hilo tayari maisha yako yamekufa katika ulimwengu wa roho, sasa muelewe wewe unayetaka kufika mbinguni usikubali tena hao wanaochaji pesa wanayo roho ya shetani ya kuwapeleka watu jehanamu katika nchi ya shetani ambayo katika kitabu cha biblia ya shetani ndiyo inayoongezea hayo ili kukupoteza. Ukiabudu chochote tofauti na MUNGU, YESU na ROHO MTAKATIFU, uelewe unakula mana ya kuzimu na umeshakufa kiroho upo jangwani. Ukimfanya mtumishi yeye ndiye MUNGU tayari umekufa kiroho na umeshashika njia ya jehanam. Ukibusu sanamu hivyo hivyo umekula mana ya shetani, kanisa linalochangisha hapo hakuna mana ya mbinguni ni pango la shetani, MUNGU yeye hachangishi hata siku moja na alishaonya katika Neno lake Ufunuo wa Yohana 22:18 -19, utatupwa nje. Hii ni sababu umekula sumu ya kiroho. Yapo mengi sana zaidi ingia katika website yangu www.prophethebron.org ingia katika link ya you tube na blog na usome na vitabu utafunguka sana na utaona jinsi ulivyopotezwa pasipo kujua au kupenda na wengine ni watumishi wanaiga mafundisho hayo pasipokujua na yamewaua kiroho wameshakufa jangwani, leo utubu ufufuke neema yake YESU bado ipo. Kanisa lenye benki hapo hakuna mana ya mbinguni, MUNGU wa mbinguni ni yeye hachaji riba sasa uelewe. Na hata unaweza ukakuta mtumishi anafundisha labda somo la  mana lakini cha ajabu utashangaa na yeye anachangisha pesa za kuifanya hiyo kazi unapoona hayo ujiulize urudi katika mana ambalo ndilo neno la MUNGU yaani biblia. 

Ukiangalia dunia katika siku ya jumapili watu wengi huwa wanaenda kula mana ya shetani ili wafe roho zao na wao hawajui sasa uwe makini epuka mafundisho ya uongo, unapoyapokea au kukaa katika madhabahu hayo ndivyo inavyozidi  kukupa sumu ya chakula kiharibikacho na ndiyo sababu utashangaa makanisa mengii sana kila mahali lakini watu ni waovu na hata hawataki kuokoka na hata wakiokoka hudumaa kiroho hii ni sababu ya  kula chakula cha kuzimu yaani mafundisho ambayo hayajotokea mbinguni, sasa ni hatari sana unaposhiriki tu uelewe na wewe tayari umekufa kiroho upo jangwani, hizi ni mbinu alizozifanya shetani akiwatumia wale watumishi ambao wapo upande  wa shetani na watu hawajui ila ni siri yao na viapo vyao vya kujificha, sasa nimekufunulia hayo uelewe hata ukiwauliza maswali kwa nini mnatufundisha mambo hayo ya uongo hawatakuwa na jibu na uwaulize mbona mafundisho hayo  hayapo katika mana ya mbinguni yani biblia. 

Hiyo ni njia rahisi ya kuwajua watumishi wanao walisha watu mana ya shetani ili waende jehanam japo wapo wanaojua kabisa wanaziua roho na wengine hawajui wanawaiga katika kuwaiga wengine na wao wakatekwa na kama wametekwa basi na hata hao waumini wote wametekwa. Nataka muelewe MUNGU yeye ni wa haki na shetani  amemnyanyulia bango MUNGU, wewe uliwakataza wasile chakula kiharibikacho na sasa wanakula hivyo nina uhalali kabisa na wao niwaulie jangwani msifike mbinguni wafike katika nchi ya kuzimu. Pia usione makanisa, watumishi, wakristo wengi wanaenda makanisani wanashiriki huko katika maeneo ya ibada za uongo hao wote wameshakufa kiroho wamebakia jangwani hivyo sasa uokoke upya ufufuke ule mana ya mbinguni utoke ukatengwe nao na usikanyage tena huko ili uende mbinguni.

Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniandike katika kitabu cha uzima sababu niliokoka nikaongozwa sala ya toba kumbe jina langu likaandikwa katika kitabu cha shetani kwa ajili ya mana ya kuzimu niliyolishwa ikaniua, nishike mkono YESU uniongoze sasa nisife tena jangwani. Amen

NOTE:
Dalili ya kujua umekufa kiroho mambo yako hayaendi haijalishi umeokoka, unafunga sana, ni mateso matupu na yamekushikilia. Cha kufanya epuka hizo mana za kuzimu chakula kiharibikacho ndicho kilichoharibu maisha yako, ikiwa kweli unapata neno la MUNGU utastawi ni wengi mnaona MUNGU hayupo nawaeleza MUNGU yupo ila ni malisho ya uongo ndiyo yamekuuwa.
Zaidi soma vitabu vya Nabii Hebron utaona na pia ukiona watumishi wanapigania sadaka uelewe hao wana mana ya shetani.
Karibu sana katika Kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, ufufuliwe uwe huru. Ipo mana ya mbinguni kwa ajili ya mataifa wote wale wanaotaka kwenda mbinguni. Amen

NABII HEBRON