Hebron: BWANA YESU asifiwe, Karibu tena ndugu
mtazamaji katika kipindi hiki cha mahojiano kati ya Nabii Hebron, Leo ninaye
ambaye alikuwa co ordinator wa shetani ambaye sasa ni mwana wa MUNGU hapo
mwanzoni alikuwa akiitwa Wariambora kwa sasa hivi anaitwa Debora, naye
tutahojiana kwa utukufu wa MUNGU, ili mzidi kufunguliwa maana alinituma YESU na
yeye nikamtoa.
Hebron: Bwana
YESU asifiwe! Haleluya!
Hebron: Karibu
Debora
Debora:
Asante: Bwana YESU asifiwe!
Bwana YESU asifiwe! Jina
langu naitwa Debora kwa sasa hapo mwanzo nilikuwa ninaitwa Wariambora,
Ninampenda YESU, YESU ameniokoa, YESU ana nguvu, YESU anaweza,
Debora: Bwana
YESU asifiwe!
Hebron:
Haleluya! Sasa huyu ndiye Debora,
ambaye leo tutakuwa na mahojiano naye, kuhusu maisha ya Kuzimu alikaa huko muda
mrefu.
Hebron: Nafikiri
miaka mingapi! Thelathini na mbili eeee
Debora: Thelathini
na mbili na miezi minane
Hebron:
Na miezi minane!!! atatueleza
yeye alivyofanya maana yeye alizaliwa lakini hakumbuki alivyopelekwa lakini, ila
mimi MUNGU alinifungulia, jinsi alivyopelekwa akawa anatumikishwa mpaka
alipofika kanisani nikamfungua,
Hebron: Bwana
YESU asifiwe!
Hebron: Karibu
Debora
Debora:
Asante,
Debora: Bwana YESU asifiwe, ni kweli kama
mtumishi wa MUNGU alivyosema, mimi kuanzia nivyozaliwa, nilipelekwa kuzimu
nilitumikishwa na shetani maana sikupenda mimi mwenyewe kwenda kule, na kama
nilivyosema kuwa niliweza kukaa miaka thelathini na mbili na miezi minane.Nilikiwa namtumikia shetani,
Bwana YESU asifiwe, na
nilikuwa na vyeo vingi kule kuzimu, cheo cha kwanza nilikuwa co ordinator
Hebron: Co
ordinator!!
Debora: Co
ordinator ndio, na cheo cha pili nilikuwa mwalimu
Hebron: Mwalimu!!!
Mwalimu wa kufundisha lugha mbalimbali!
Hebron: Kwa
hiyo kule kuzimu wana lugha mbalimbali mh!!
Debora: Ndio
Hebron: Unaweza kukumbuka ni lugha ngapi
ambazo ulikuwa unafundisha na za nchi ngapi?
Hebron: Unaweza
kutaja baadhi
Debora: Ninakumbuka
chache
Hebron: Ehee!
hebu zitaje
Debora:
Moja ya kwanza ambayo
ninaikumbuka ni lugha ya kuzimu yenyewe
Hebron: Kuzimu
wana lugha yao wenyewe???
Debora:
Ndio
Hebron: Unaweza
kuiongea mpaka sasa hivi?
Debora: Ninaweza
ndio
Hebron:
Hebu ongea kidogo, alafu unitafsirie
umesema nini kwa lugha ya kuzimu maana watu wangependa kuelewa maana yake
Hebron:
Maana pia mnajua watoto wa MUNGU
kuwa mbinguni wana lugha yao na kuzimu pia wana lugha yao.
Hebron: Hebu
unaweza kuongea kidogo!
Debora: Ndio
Hebron: Alafu
utatutafsirie
Debora: Ndio
Hebron:
MUNGU akutie nguvu.
Debora:
BWANA YESU asifiwe! Lugha mmoja
wapo ambayo ilikuwa inatumika kule kuzimu, ambayo hata watumishi wa kipepo na wale ambao
wamepewa nguvu na shetani ambao wanapenda sana kuitumia hiyo lugha , hapa dunia
inaonekana, wanaponena inaonekana kwama wananena kwa lugha lakini sio wote
wanaonena kwa lugha.
Lugha
nyingine wamepewa na baba yao ambaye ni shetani, ambazo baadhi ya lugha hizo
zipo ambazo pia wanapenda kuzitumia hapa duniani na wanapozitumia zile lugha
watu wanafikiria kuwa wananena kwa lugha ambayo zinatoka mbinguni lakini sio
hivyo.
Hebron:
Mimi kama Nabii Hebron hiyo lugha
ya kuzimu siijui lakini yuko ambaye alikuwa naye kule kuzimu ambaye sasa ni
mtoto wa Kanisa la YESU ni BWANA na Mwokozi wa Mataifa yote kwa jina Isaya,
anaitwa Isaya, pia walikuwa naye kule kuzimu na wanaongea kwa mawasiliano
kabisa:
Hebron:
Mda si mrefu nitamkaribisha Isaya
na yeye, watakuwa wakiongea maana huyu pia (Debora) alimfundisha Isaya
Hebron: Bwana YESU asifiwe wataongea hiyo
lugha ya kuzimu na watu wapate kusikiliza
Hebron: Usiogope
lakini, Amen
Debora:
Bwana YESU asifiwe, baadhi ya
lugha hizo nitaongea na mwenzangu ambaye na yeye pia alikuwa kuzimu lakini kwa
neema ya MUNGU, ameweza kutoka,
Debora: Bwana
YESU asifiwe, Baadhi ya lugha hizi ni:
Debora: shaboroseke
shindorobosai?
Isaya: Akaramaiska
mafias
Debora: Shiraboboko
sendaraibaksi
Isaya: Shanta
marka makass
Debora: Shuto
senndere book sosi
Isaya:
Rika meuasi
Debora:
whichu bokosi ndasi
Isaya: Kos
mandesrsmis
Debora: Roko
shinda mandotos
Debora: Bwana
YESu asifiwe!
Debora: Baadhi
ya lugha hizo ambazo tumeongea nitazitafsi kidogo! Mwenzangu atakuwa anaongea
na mimi nitazitafsi kwa Kiswahili
Isaya: Taridosi
Debora:
Ndivyo ilivyo
Isaya: Kar
tarasi mat saba
Debora:
Wamwabudu MUNGU wetu
Isaya: Ritmalakruksiii
Debora:
Walale chini
Isaya: Kar
taraa mat saba
Debora:
Wamwabudu MUNGU wao peke yao
Isaya: Radhu
madfass
Debora: Wamwabudu
shetani
Isaya: Sikur
mafitarsi
Debora: Waabudu
miungu
Isaya: Sarmakka
Debora:
Waabudu misalaba
Isaya: Deor
madabass
Debora: Waabudu
mungu jiwe
Isaya: Samsakar
makass
Debora: Waabudu
mungu ambaye yuko kuzimu ambaye ni joka kuu
Isaya: Sarkdur
mamkasma
Debora: Wamtolee
sadaka ambazo ni nyama za watu
Isaya: Deur
mata makasi
Debora:
Wamwabudu yeye peke yake
Isaya: Saur
mau mata mau
Debora: Wamwabudu roho mtakatifu
Isaya: Ti aumar mamtaks
Debora: Wamtolee sadaka peke yake
Isaya: Au
mar makamata
Debora: Tuwafunge
fahamu zao
Isaya: Ribo
tol maka mamtiss
Debora: Ili wasimwelewe MUNGU wa kweli
Isaya: M
kairu mamtasasi
Debora: Tuchukue na utayari wao
Isaya: Ribo
for Mauro mamtass
Debora: Tufunge
na fahamu zao
Isaya: Ribo
toll makkaqa mamtiss
Debora: Tufunge
na vinywa vyao
Isaya: Sikar
matassa
Debora: Tufunge
nguvu ya maombi
Isaya: Sikor
malatassa
Deabora: Tutengeneze
mabomu kwenye ulimwengu war oho
Isaya: Rediko
fo mamtassess
Debora: Tuwavuvie
roho ya kuwalewesha usingizi
Isaya: Ro
of amamtakasssasss
Debora: Tuwavuvie
roho ya kumwabudu mungu jiwe
Isaya: Re
outor malamtakasasa
Debora: Tuwapatanishe
fahamu zao na bahari ya hindi
Isaya: Kreopatriao
Deabora:
Kuna kijana mmoja ambaye yuko Tanzania
anakiherehere sana tunataka tupange mbinu za kwenda kumwangamiza
Isaya: Tormakasi
Hebron
Debora: Anaitwa
Hebron
Isaya:
Teur mamtassi mam deur YESU
NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE
Debora: Tukaangamize
na huduma yake
Isaya: Reu
koll ma san mau massi Moses Kulola
Debora: Na
baba yake alikuwa anaitwa Moses Kulola
Isaya: Teuorr
mamkassi mamdersea Serengeti
Debora: Ma
huyu kijana alikuwa anafanya kazi Serengeti
Isaya: Te markasi te assize ker mau hebron
Debora: MUNGU alimwita alivyokuwa huko katika
kazi yake ambayo alikuwa anaifanya
Isaya: Te
rranamau de mass YESSU
Debora:
YESU akamtoa akamwambia ukanitumikie
Isaya: De
teur markassii oo kore mattasisi
Deabora:
Akasema ndio Baba nitaenda
Isaya: Creopratio
Debora: Lakini
vita vuliinuka
Isaya: Treo
marapratatissi
Debora:
Wakataka kumuua
Isaya: Reokal
matasasa
Debora:
Lakini neno la MUNGU
Isaya: Reo
malakasa
Debora:
Lilitimia
Isaya: Reobotasisisii
Debora: Haikuwezekana
Isaya: Reo
kall matasisi max
Debora: Na alitumwa kuzimu kwenda kumtoa Max
Isaya: Treo
makasisi waria boraa
Debora: Na
pia kabla ya max alitumwa kwenda kumtoa Wariambora
Isaya: Creombota
rmaraksii
Debora:
MUNGU alimpa mtume na Nabii
Hebroni huduma ambayo ni ya dunia nzima
Isaya: Keo
mapatiss marpatasao
Debora:
Ili akaziokoe roho za wana wa
MUNGU ambazo zimepotea ili aweze kuwaokoa
Isaya: Creomaba
datapass
Debora: Alitumwa kuwaokoa wale ambao hawamju
MUNGU na waliotekwa na shetani
Isaya: Tika
bakosi
Debora: Ili wamrudie MUNGU, kwa kuwa sasa
hivi wako wengi wanadanganya wana wa MUNGU
Isaya: Dreo mamtababsaa
Debora: Hawasemi
kweli, bali wanasema uongo
Isaya: Reol
mamkassi
Deabora: Na
wanatumia biblia za uongo
Isaya: Reol
makasi dreomapal sapa
Debora: Na
wanawapa watu neno la uongo
Isaya: Rol
makatatisso mapatsi
Debora: Lakini
yeye amenituma kuharibu ufalme wa shetani
Isaya: Reo
mapasisisisiii
Debora: Wakati
wa YESU umefika
Isaya: Reokul
mapatamsisi
Debora: Wa yeye kurudi
Isaya: Reomampatass
Debora: Kuchukua kanisa
Isaya: Reo
mapatarada
Debora: Na
watu wataujua ukweli
Isaya: Krisu
masasa
Debora: Na
wakati umefika
Isaya: Reo
maksasisa
Debora: Ijapo wengi wanampinga Hebron
Isaya: Reo
makala masisi masa
Debora: Lakini
MUNGU akiamua ameamua
Isaya: Reol
mall keo ormaadotobo martaba ai :
Debora: Na shetani amewateka watu wengi
wakiwemo wanawake, wametekwa kwa kuambiwa watoe fedha, waweke fedha kwenye
miguu na wakanyage, biblia na sivyo neno la MUNGU linavyosema
Isaya: Reol matasi
Debora: Amentumwa
ili kuangamiza ufalme wa shetani
Isaya: Dreol
mataka
Debora: Waje
kwa MUNGU
Debora: Bwana YESU asifiwe!
Kwa hiyo utaona kuwa baadhi ya lugha wapo
ambao wamejiita na wanasema wametumwa na MUNGU kwamba ni za uongo, lakini kama
haujafunguliwa ufahamu na kumwelewa MUNGU hutaweza kuelewa na watu wengi sana
wamedanganyika sana kupitia hizi lugha
na kupitia hizi lugha wengi wametekwa na shetani
Debora: Bwana YESU asifiwe!
Wametekwa na shetani kivipi,
unapoenda kwa mtumishi ambaye anatumia nguvu za giza na ambaye amepewa hizi lugha na ambaye amefundishwa hizo
lugha aje kuwadanganyia wana wa MUNGU unapoenda tu pale, na kuwekewa mkono ama unaposikiliza hizo lugha ni pepo ni nguvu ya
roho mchafu, ambaye roho mchafu tayari
tunamshukuru MUNGU kwamba alishatolewa unaposikiliza hizi lugha na zinakuvuvia na ile nguvu inakuingia, kwa hivyo
na wewe tayari unakuwa umeshaingiwa na ile lugha ya kunena kwa lugha bila wewe
mwenyewe kujua na hiyo lugha yenyewe sio ya mpango wa MUNGU bali ni mpango wa
shetani kuharibu wana wa MUNGU ili waende kuzimu ambapo ni kwa shetani
mwenyewe.
Bwana YESU asifiwe!
Kwa hiyo ninawasihi na ninawashauri muwe makini na
mahali mnapoenda, watu wananena , watu wanaongea, wengine wana tafsiri, lakini wengi
wao sio lugha ya Mbiguni, sababu lugha ya Mbinguni inakuja automatic na
inakuja mahali ambapo yupo mtumishi wa
kweli na ambaye amesimamia kweli, lakini wengi wamechukua huko kuzimu na
aliyekuwa anafundisha hizo lugha ni mimi
ambaye nilikuwa ninafundisha. Nilikuwa nafundisha hizo lugha kwa aina
tofautitofauti kwa kiwango ambacho mtumishi mwenyewe labda anataka akazitumie,
hizo lugha ndio maana na unaweza kukuta huyu anaongea lugha hii na huyu hii, na
mwingine lugha hii, lakini zote zinajumuisha kitu kimoja.
Kama vile kwa MUNGU,
tunavyoombewa, tunapokea nguvu za Roho Mtakatifu
utasikia kila mmoja ananena kwa maneno yake mengine lakini kinamaanisha kitu
kile kile.
Isaya: Bwana
YESU asifiwe!
Debora: Amen
Kwa jina naitwa Isaya ni
mtoto wa madhabahu ya YESU ni Bwana na
Mwokozi wa Mataifa yote, ndimi ambaye nilikuwa kiongozi wa ngazi ya tatu kwenye
ufalme wa shetani, ndimi nilikuwa roho
mchafu wa kuzimu, ndiye ambaye nilikuwa kiongozi
wa vikosi vya vita vya shetani,
Nilikuwa nikiongoza watu mbalimbali
lakini siku ya leo pia nipo na ambaye alikuwa ni Mwalimu wangu kwa upande wa
silaha, alikuwa akinifundisha, ndiye aliyenifundisha kutumia silaha zilikuwa
silaha za aina nyingi ambazo alinifundisha kuzitumia na kama ni kwa upande wa
vita, kwa kutumia silaha yeye ndiye aliyekuwa zaidi kiukweli mimi nilikuwa ni bado
mdogo sana kwake kwa upande wa silaha za kupigania vita.
Na pia yeye neema ya MUNGU
ilikuja kumwokoa akawahi kutoka kabla yangu, lakini pia MUNGU alikuwa na kusudi
lake akaamua kumtoa yeye kwanza, yeye ambaye alikuwa akinifundisha mbinu za
vita ili kwanza kasi iweze kupungua, ili
nisiweze kupigana kisawasawa.
Pia namshukuru MUNGU kwa siku ya leo kwa maana
tumeweza kueleza upande wa Lugha ambazo watu huwa wanaziongea; kwa kweli kabisa
ziko lugha ambazo watu wanaziongea, pasipo nyie wenyewe kuzielewa mnakuwa mnasema,
MUNGU wewe ni mjinga , kwanza hujibu maombi yetu, tunakudharau hatukitaki, ndio maana yunatoa
machozi yetu, ndio unaona mtu anakuwa anaomba au naongea anatoa machozi mengi pasipo
kupigwa au amefanyiwa kitu chochote au unaweza ukawaona hata waumini katika
makanisa ambayo ni la mtumishi, labda mtumishi wa kipepo, wanakuwa wanaongea kwa lugha ambayo labda
wanajisifia na kujisifu kuwa wanaongea kwa lugha pasipo wao kujielewa. Mda mwingine wanakuwa wanatukana watumishi
wao, mda mwingine wanakuwa wanasema maisha yetu na yawe mabovu, hatutaki maisha
mazuri siku zote.
Namshukuru MUNGU pia kwa kuwa
siku leo yapo mengi ambayo pia tutayaeleza
nikiwa na aliyekuwa mwalimu wangu zamani kama teacher, lakini siku ya leo wote
tuko katika mikono ya MUNGU na mikononi mwa Mtume na Nabii Hebron, namshukuru sana
MUNGU kwa ajili ya hilo.
Debora: Bwana YESU asifiwe!
Debora:
Ah! Kama alivyosema mdogo wangu
Isaya ni kweli lakini tunamshukuru MUNGU kwa kuwa kwa sasa tumetoka na tunamtukuza
MUNGU
Bwana
YESU asifiwe!
Ah
nitapenda kuelezea kazi ambazo nilikuwa nikizifanya kule kuzimu,
Bwana
YESU asifiwe!
Mimi
nilikuwa kama mwalimu nilikuwa ninafundisha kama nilivyosema, lugha mbalimbali
lakini katika ulimwengu ulimwengu waroho, nilikuwa nafundisha vyuo mbalimbali vikiwepo
vya hapa duniani kabisa.
Bwana
YESU asifiwe!
Kwenye
ulimwengu waroho nilikuwa ninafundisha, nilishaingia vyuo vingi, vingine viko
Dar vingine viko mikoani, vingine Arusha lakini pia vipo vingine nchi
mbalimbali nilikuwa ninaenda kule inaweza kuwafundisha kwenye ulimwengu wa
roho.
Bwana
Yesu asifiwe!
Nilikuwa
ninafundisha walimu ambao na wao pia wanafundisha wanafunzi, Lakini neema ya
MUNGU imeweza kunitoa huko na lingine nilikuwa kama nilivyosema nilikuwa
mwalimu wa lugha kule kuzimu mfano wa lugha hizi za kunena kwa lugha, nilikuwa
nawafundisha wale ambao walikuja kuzimu na walikuwa wanahitaji kufundishwa zile lugha nilikuwa
nawafundisha ila sikupenda mimi bali nilitekwa na shetani.
Bwana
YESU asifiwe!
Niliweza
kuwafundisha nyingi sana, na nilikuwa na uwezo wa kuwafundisha lugha nyingi
sana, na kupitia hizo lugha wana wa MUNGU wengi walitekwa kupitia hizo lugha.
Lakini
namshukuru MUNGU kwa kuwa amenitoa kule na “Aliyekuwa anafundisha hizo lugha
sasa ameokoka na anampenda YESU” Na
kingine nilichokuwa nafundisha nilikuwa mwalimu, mwalimu wa kwaya, unaweza
ukaona kwaya mbalimbali zinaimba unasema kweli hizi kwaya zinaimba ama ukaona kwamba
wanamuziki wa nyimbo za injili mfano, akiwepo mmojammoja unaweza na ukaona wanaimba unashangaa
labda wanaimba vizuri sana, au mtu anasauti nzuri , mimi ndio nilikuwa
ninawafundisha, nawafundisha na kuwaelekeza sauti nikiwepo nashirikiana na roho
mchafu ambaye na sasa ametoka ambaye sasa ni mwana wa MUNGU sasa ni Isaya
Lakini
ninamshukuru MUNGU sana kwa kuwa hakuna tena, kule kuzimu mtu anayefundisha
hizo lugha. Na pia nilikuwa ninafundisha kiswahili nilikuwa nina uwezo mkubwa
sana wa kufundisha lugha ya kiswahili kwenye ulimwengu wa roho lakini kimwili
mtu hawezi akafahamu.
Lakini
pia namshukuru MUNGU kwa kuwa hiyo roho
ya shetani imeondoka na nimekuwa mtoto mzuri
wa YESU, nitaelezea vitu ambavyo pia nilikuwa ninavyo kule kuzimu, kama nilivyosema kuwa mimi nilikuwa co
ordinator. Cordinator ni mtu ambaye nilikuwa na cheo kikubwa
sana pia nilikuwa nikiheshimika sana nilikuwa na ofisi zangu lakini
zimeshachomwa moto na mtu ambaye aliyetumwa kule kuzimu kwenda kunichomoa huko
na pia nilikuwa nina nyumba na pia nilikuwa nina hospital, hospital zilikuwa
hospital za kutibu mapepo na malaika wa shetani ambao walikuwa wamejeruhiwa
ambapo malaika wa MUNGU walipokuwa wanakuja kupigana kule kuzimu ili kuharibu
ufalme wa shetani, walivyokuwa wakiumia
walikuwa wale wanakuja kwenye hospital yangu naweza kuwatibu, na huo uwezo
nilikuwa nimepewa na shetani na sio kwamba ni uwezo ambao nilikuwa nao mimi
mwenyewe, Namshukuru MUNGU kwa kuwa kwa kuwa uwezo huo pia MUNGU ameuondoa huo, uwezo wa shetani.
Bwana
YESU asifiwe!
Na pia nilikuwa na ofisi
nyingi lakini tu zimeshachomwa moto, pia nilikuwa nina wafanyakazi, madereva
pia nilikuwa na ndege.Namshukuru MUNGU kwa kuwa ni MUNGU.
Bwana YESU asifiwe,
Licha ya kuwa na ndege pia
nilikuwa na ninauwezo mkubwa sana wa kuweza kupaa, nilikuwa naweza kupaa
sekunde moja nikaweza kuizinguka Tanzania, naweza nikazunguka pia nchi kadhaa
na pia nilikuwa na nguvu, hiyo nguvu ilikuwa kwenye mkanda.
Bwana YESU asifiwe!
Nilikuwa na nguvu kwenye mkanda na nilikuwa na
nguvu kwenye saa, ambayo hiyo saa ndiyo ilikuwa inanielekeza na ule mkanda
nilikuwa ninauvaa kama mwanajeshi unafungwa kama mwanajeshi anavyovaa( kuanzia
begani na kuzungukia kiunoni) na nilikuwa na kofia lakini hiyo kofia ilikuwa ina
upanga pia ile ilikuwa ni nguvu kubwa sana kwenye ulimwengu waroho.
Bwana YESU asifiwe!
Lakini namshukuru MUNGU kwa
kuwa ameweza kuniokoa na ameweza kunibadilisha
Pia nilikuwa na nguvu ya
kuweza kuua nimeangusha magari,
Bwana YESU asifiwe!
Lakini MUNGU ameniokoa na
MUNGU amenisaidia na nilipokuwa nipo Co ordinator nilikuwa nahakikisha kwamba
kazi zote za kuzimu zinaenda salama,kama ambavyo zinatakiwa na kama hazijaenda
salama nilikuwa ninaenda kwa aliyekuwa namba tatu ambaye alikuwa roho mchafu,
anieleze kwa nini kazi hazijaenda sawa na nikisha enda kwake, na yeye pia
anaenda kwa wale ambao waliokuwa wanahusika na kile kitengo, na nilikuwa pia na
nguvu nyingine ya kuzuia wana wa MUNGU wasiwezekuomba nilikuwa naweka giza nilikuwa
ninachafua anga, nilikuwa nikitaka tu kuzuia maombi, mimi mwenyewe nilikuwa na uwezo
wa kupaa na nilikuwa ninaweza kujitanda kwenye anga ili maombi ya wana wa MUNGU
yasiweze kupenya na nikijitanda angani makanisani hawataweza kuomba, inakuwa ni
vurugu inakuwa ni faraka, kwa mtu mmoja mmoja na pia hata kwa familiawanakuwa
hawaelewani, hata kama ni wanandoa
walikuwa wanaomba au kikundi cha maombi wanakuwa hawawezi kuendelea sababu ya
kile ambacho nimekiachilia kule, na pia nilikuwa na wafanyakazi kama
nilivyosema, pia nilikuwa na mtumishi mmoja ambaye sitamtaja jina, yeye ndiye
alikuwa kama mfanyakazi wangu ni mtumishi wa kike anajulikana yupo Arusha,
lakini sitamtaja jina lake, maeneo ya Ngaramtoni. Yule pia alikuwa ni kama
mfanyakazi wangu wa kunipokea mabegi na kuhakikisha kama nimekula vizuri na
kufagia nyumba na kufanya vitu vingine ambavyo vinahitajika kufanywa kwenye nyumba, na ninamshukuru MUNGU kwa sababu hayo
yote nilikuwa nikiyafanya ni kwa sababu nilikuwa nimetekwa na shetani kama vile
wakati mwingine mtu yeyote na yeye anaweza akatekwa, lakini namshukuru MUNGu
kwa kuwa nimeweza kutoka.
Kule nilikuwa nina magari
lakini ninamshukuru MUNGU alivyoshuka
mtumishi wa MUNGU kule aliteketeza na yale magari kule, niliyokuwa ninayatumia
kule kuzimu pia nilikuwa nina ndege, pia namshukuru MUNGU kwa kuwa zile ndege na
vitu vyote vya shetani niliviacha kule na nikatoka kama nilivyokuwa
Bwana YESU asifiwe
Nitaelezea kuanzia nilivyozaliwa
na mpaka ilipokuwakuwaje nikapelekwa huko kuzimu mpaka nilivyotoka.
Bwana YESU asifiwe
Nakumbuka kwamba nilivyozaliwa,ijapokuwa nilikuwa mdogo, lakini ukishatekwa na shetani
hata kama ni mdogo unakuwa na ule uwezo wa kuelewa kwa sababu unakuwa sio wewe
tena bali umebadilishwa ufahamu
Bwana YESU asifiwe!
Ninakumbuka nilivyozaliwa tu
mimi nilikuchukuliwa nikiwa bado mdogo na mimi kivuli changu kikafanywa mfano
wangu mimi, Bwana YESU asifiwe!
Bwana YESU asifiwe!
Kwa hivyo, nilivyozaliwa nikachukuliwa na pepo ambaye huyo pepo alikuwa kama baba
yangu, na alikuwa anaitwa Tikiko, na
nilipokuwa kule kuzimu nilijua kuwa ndiye baba yangu
Bwana YESU asifiwe!
Na nilipokuwa kule kuzimu
kivuli changu kilikuwa kama vile ndio mimi kikawa na sura yangu Kamili na mama
yangu aliendelea kunilea akifikiri kwamba analea mtoto,
Bwana YESU asifiwe,
Lakini kwa kweli sikuwa ni
mimi kilikuwa ni kivuli tu kile na kile kivuli hakikuwa ni kivuli tu cha
kawaida bali kiliambatanishwa na pepo
Bwana YESU asifiwe!
Na nilivyokuwa huku duniani
kile kivuli kilikuwa kinateseka na magonjwa ya mbalimbali,
Bwana YESU asifiwe!
Magonjwa yasiotibika,
ugonjwa wa moyo, ukitibiwa huu, unakuja huu, ukitibiwa huu unakuja huu
Bwana YESU asifiwe!
Na nilikaa kama nilivyosema
nilikaa kule kuzimu, nilikaa miaka thelathini na mbili na miezi nane, kama
nilivyosema hapo awali, wakati huo wote nilimtumikia shetani
Bwana YESU asifiwe!
na nilimtumikia shetani bila kupenda na
nilitekwa na shetani, na nikaweza kumtumikia shetani nikawa naishi kule kama
vile mtu anavyoishi huku duniani lakini maisha ya kule kuzimu naya huku ni
maisha ya hapa duniani, kwa sababu ni maisha ambayo kila saa upo hatarini
Bwana YESU asifiwe!
kwa sababu kila saa ni kupigana, Chakula kikuu
kule ni nyama za watu na damu za watu ndio vitu ambavyo nilikuwa nakula, pamoja
pia na wengine ambao ndio wako kule, niliweza kuishi na mapepo bila kujua maana
unajua unapokuwa mdogo, hauelewi kwa hiyo niliishi nao , niliishi nao kule kama
vile ambavyo sasa ninaishi na wanadamu huku duniani tofauti ya maisha ya kule
ni maisha ambayo ya taabu, kwa sababu ni maisha ya ubabe kila saa kupigana
Bwana YESU asifiwe!
Na mda wote ambao nilikuwa
nikiishi kule nilivyokuwa nasema kwamba huku duniani nilikuwa dhaifu ,
naonekana kama asiyefaa, nilikuwa sipendi sana kukaa na watu, na nilikuwa
sipendi kuongea kila mara nilikuwa napenda kujitenga nikae peke yangu , peke
yangu, lakini ni kwamba sikuwa bali mimi kile kilikuwa ni kuvuli na mimi
mwenyewe sikuwepo.
Na nitaeleze jinsi ambavyo
niliweza kutoka kule kuzimu ambapo nilikuwa na nilivyokuwa aah ilifika wakati ambapo
MUNGU mwenyewe alipenda nitolewe kule
Bwana YESU asifiwe!
Kivuli hichi ambacho
kilikuwa duniani kilikuwakihangaika hangaika, unajua shetani , unajua ili
shetani aweze kupumbaza watu akikuteka ni lazima akuwekee kitu ambacho kitakufanya
wewe uonekane kuwa ndio udhaifu wako kwa hiyo mimi kitu ambacho kilikuwa
kimewekwa kenye kile kivuli ni magonjwa kwa hiyo wazazi walikuwa wanahangaika
huku na kule kwa hiyo hata ilifika kipindi ambacho nikatoka kwa wazazi wangu
nikaenda kukaa na ndugu mkoa Fulani lakini hali ilizidi kuwa mbaya kadri
ambavyo miaka inaenda ndivyo ambavyo magonjwa yalikuwa yanaendelea ndani ya
mwili wangu na mimi mwenyewe bila kujielewa na niliendelea pia kwenda kutibiwa
maeneo mbalimbali nikiwa nasumbuliwa na ugonjwa wa moyo ndio ulinitesa sana
lakini bila mafanikio yeyote
Bwana YESU asifiwe!
Lakini huku duniani
nilionekana ni mimi, nilionekana ni
mgonjwa Na niliweza pia kwa sababu
nilisoma, nilisoma nilivyokuwa mdogo kwa sababu kile kivuli kilipelekwa shule
nilisoma mpaka darasa la sita, darasa la saba kile kivuli kilisoma lakini
kilisoma kidogo sana kwa sababu ilikuwa inafika wakati kile kivuli chenyewe
kilikuwa kinachukuliwa linabakia pepo
moja kwa moja kuna wakati ilikuwa inafika kile kivuli kinashushwa kuzimu, kinaunganishwa
na mwili wangu kwa hiyo darasa la saba, nilisoma kidogo. Nilipoingia darasa la
saba kidogo nilishikwa na ugonjwa , ukaonekana kama ni ugonjwa wa Malaria
nikaanguka kwa hivyo nikaanguka nilivyoanguka pale kile kivuli kilichukuliwa
moja kwa moja napepo likawa ndilo limebakia
pale kwa hiyo kivuli changu nikawa nacho kama kawaida
Bwana YESU asifiwe
Kuanzia hapo kile kivuli
sasa kilipodondoka kikapelekwa kule kuzimu pale nyumbani likawa limebaki pepo
Bwana YESU asifiwe!
na lile pepo
liliendelea kuishi na wazazi wangu bila kujua lakini kulikuwa na tofauti
moja kati ya lile pepo na mama walikuwa hawaelewani kwa sababu niliingia
maagano mengi, mimi mwenyewe niliingia maagano mengi,Kwanza niliingia maagano
ya kuuwa na agano lingine lilikuwa agano la kutanda kwenye anga, nafsi yangu
ilikuwa inaganyika sana kwa hiyo kuna wakati mwingine nafsi yangu ilikuwa
inagawanyika inaenda inakaa kwenye anga, ili kuzuia maombi na hilo ni agano
langu la kwanza, kabisa ambalo niliingia kwamba hakuna ambaye atamwelewa MUNGU
na hata kuzuia watu wasiokoke na hata wakiokoka watu wasiweze kuelewa
Bwana YESU asifiwe!
Agano la pili lilikuwa ni
agano la kupandishwa cheo,
Bwana YESU asifiwe
Ni agano la kupandishwa cheo
cha coordinator pamoja na kuwa cheo cha ukoordinator kiendelee kupanda zaidi, na pia agano la tatu ni agano lingine la kuwa
malkia, lakini nilikuwa Malkia, lakini litakiwa niweze kuwa malkia mkubwa zaidi
wa kuzimu nzima kama vile tuseme katika nchi ya Tanzania awepo Malkia mmoja tu
au kama vile mfano mkuu wa Nchi mmoja tu anayesikika hivyo nilikuwa ndio
niingie agano hilo la kuwa malkia mkuu ilifika wakati sasa niliambiwa nikamtoe
mama yangu mzazi hapo ndipo ilipokuwa shida.
Bwana YESU asifiwe!
Ndio maana kuna mahali
nilisema kuwa lile pepo baada ya kivuli kuondoka lilikuwa mara kwa mara
halielewani na mama, sababu lile pepo lilikuwa limevaa sura yangu kwa hiyo
lilitakiwa kumuua mama yangu ili niweze kupandishwa cheo, zaidi lakini pale
haikuwezekana.
Bwana YESU asifiwe!
Na ndipo ilipotokea vita
kule kuzimu, kati yangu na baba yangu
ambaye alikuwa ni Tikito, lakini pia alikuwepo na lusifa, roho mchafu na
alikuwepo na joka kuu, lakini mimi nilikuwa, unajua wale walikuwa, sana sana Joka kuu na Lusifa
walikuwa kama mabosi wangu tulikuwa tunatembeleana, tulikuwa tunakaa tunapanga
mipango,
Bwana YESU asifiwe!
na ninamshukuru MUNGU kwa
kuwa haya yote MUNGU alinipitisha ili niweze kuja kusimama kuweza kumtumikia.
Ilipofika sasa wakati wa
kumtoa mama yangu, (Kafara) nilikataa nikaanza kupewa kibano(adhabu)
Bwana YESU asifiwe!
Nilikuwa napewa adhabu,
(kibano) ikawa mara nyingine nafungiwa kwenye sanduku nakunjwa kunjwa, unajua
kule kwenye ufalme wa shetani wanaweza
kukufanya mkubwa sana na wanaweza kukufanya kama mlima na pia wanaweza
kukufanya mdogo kama karatasi hivyo mara
nyingine nilikuwa nakunjwa nawekwa kwenye sanduku kwa sababu nilikataa kumtoa
mama yangu.
Unapokuwa Ukiwa umeenda kule kuzimu kuna maagano
mengi sana unaweza kuingia unaweza ukawa umeua watu wengi sana, lakini itafika
mahali utaambiwa kwamba umtoe mama yako au ndugu yako au mdogo wako kwa hivyo wakati hayo sasa yalipokuwa
yakiendelea ninatakiwa nimtoe mama yangu ndipo ulipofika wakati sasa alikuja
ghafla mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Hebron, akiwa na kikosi cha malaika
nilikuwa sijawahi kuwaona Malaika lakini siku hiyo niliwaona walivyo, walikuja
na vikosi vya farasi, walikuja na vikosi mbalimbali vya kupigana walikuwa
pamoja na Malaika akiwepo na Bwana YESU na akiwepo na Mtume na Nabii Hebron,
ndipo walikuja kunichukua kule ilikuwa
ni vita na ndipo ambapo mimi nilikuja kuchukuliwa, nilipokuja kuchukuliwa
nikajikuta niko kanisani kwake, kwa sababu jinsi ambavyo nilikuwa nateseka na magonjwa,
ni lile pepo sasa ambalo lilifanywa ndio mimi baada ya hospital kushindikana.
Nilianza kupelekwa maeneo
mbalimbali ya maombi nikapelekwa, lakini kwa kweli nilikuwa naenda tu kwa ajili
ya kuwatii wazazi lakini mimi mwenyewe nilikuwa naelewa ni nini ambacho
kilikuwa kinaendelea ila niliwewa agano la kutokusema na lile agano lilikuwa ni
la damu kwa hiyo ukishatekwa Unapokuwa na ile roho ya shetani imeingia unaweza
kufanya kitu chochote bila kujipenda.
Bwana YESU asifiwe!
Na baada ya kutoka kwa wazazi , baadhi ya ndugu ambao
pia nilikuwa naishi nao waliweza kunipeleka kwenye maombi sehemu mbalimbali na katika
kipindi hicho hicho lile pepo pia lilikuwa linafanya kazi katika shirika fulani
na alikuwa alikuwepo baba mmoja ambaye alikuwa akinishuhudia habari za
YESU, Na nilikuwa namkubalia naenda,
lakini mimi mwenyewe nilikuwa najua ni
nini kinaendelea ila sasa kusema ili niweze kufunguliwa nilikuwa siwezi kusema
sasa baada ya yule baba kuendelea
kunishudia, ilikuwa ni vigumu na alinishuhudia maeneo mbalimbali nikaenda
lakini aliponishuhudia kwa habari ya kwenda kwa Mtume na Nabii Hebron Kanisani kwake ilikuwa vigumu.
Alinishuhudia kama miezi nane, mwezi wa nane, lakini
nikakubali nikamwambia nitaenda, Lakini
kwa kweli ilikuwa sio mimi bali ni lile pepo ndio lilikuwa anaongea nae na bada
ya kufika pale lile pepo lilikutana za nguvu ya MUNGU, mahali pale, kwanza lile
pepo lilipofika pale, mahali pale walikuwa na malaika wako pale, wengine
walikuwa wamekaa kwenye viti kwenye anga, yeye mwenyewe (Mtume na Nabii Hebron)
nilikuwa nikimwangalia nilikuwa namwogopa kwa sababu alikuwa anawaka, alikuwa
na mng’ao ambao sio wa mwanadamu kwenye
ulimwengu wa roho.
Na nilipofika kwa mara ya
kwanza sikujielewa kwa kweli, nilikamatwa maana hata pia lengo la kwenda pale
ilikuwa niende nikapime nguvu aliyonayo, lakini mambo yalibadilika, nilikwenda
mara ya kwanza, nikashindwa lengo lililonipeleka pale nikashindwa maana
nilikutana na nguvu za MUNGU, hivyo nilienda mara ya pili.
Sasa vita vikawa vinaendelea kule kuzimu ndio
kwenye ulimwengu wa roho akashuka, Mtume na Nabii Hebron pamoja na vikosi vile ambayo nilivitaja na
mafarasi, wakawa wamebeba silaha mbalimbali ndipo ambapo vita vilianza kule
kuzimu magari yangu, yakachomwa moto, lakini ofisi zangu zikachomwa moto,
magari, ndege wasaidizi wangu pia
waliuawa na wengine wakakatwa vichwa,
mapepo yakaktwa vichwa, yakauwawa na ndipo ambapo mimi niliweza kutolewa na
nilivyotolewa, nilijishangaa nilijikuta nimerudi duniani, bila mwenyewe
kujielewa nini, kilitokewa lakini vita vilikuwa vinaendelea kule Malaika
walikuja wakanichukua alafu kwenye ulimwengu wa roho Mtume na Nabii akaniambia njoo! Basi ndipo ilipofika wakati
nakatolewa nikajikuta niko kanisani, nikajikuta niko na watu, ijapokuwa mimi
kipindi hicho kabla sijatolewa nilikuwa siwezi kuonana na watu; hilo pia ndio
agano ambalo nilipewa, hata mfano kama nilikuwa nimekuja duniani kufanya vitu
vibaya, nilikuwa kabisa sionani na watu nilikuwa napita anga kwa anga, hata
nikitoka chini napita anga kwa aga na nilikuwa sionani na mtu ana kwa ana.
Kwa hiyo nilishangaa sana kutolewa kule kuzimu
ilikuwa ni kitu cha ajabu sana kwa sababu kitu cha kwanza mimi nilipitolewa
nilishangaa wanadamu kwa sababu nilizoea kukaa na mapepo, nilizoea kukaa na Joka
kuu nilizoea kukaa na watu wa ajabu ajabu sana lakini ninamshukuru MUNGU kwa
sababu siku hiyo ilikuwa ni ya ajabu sana na sitakaa niisahau maishani mwangu
kote kwa kuwa MUNGU ni MUNGU tu, Mtu anayesema MUNGU hayuko kwa kweli hajui anachokisema.
Kwa sababu kwanza
nilishangaa hii dunia, nikashangaa sana, nikashangaa watu wanavyoongea, mimi
nilikuwa nimekaa kimya naangalia lakini nawashangaa na nilipokuwa nimetoka hapo
sasa napelekwa nyumbani, maana bado ufahamu ulikuwa bado haujarudi, nilikuwa
nawashangaa watu, siongei lakini nilikuwa nawashangaa watu wanaongeaj !
nikaanza kupenda kukaa na watu nitaanza kuwa marafiki sasa na watu, ninapenda
nikae nao kwa hiyo ninamshukuru MUNGU aliyenitoa kule ilikuwa ni jambo la ajabu
sana, kumwelezea mtu hivihivi ni vigumu
lakini ndivyo ilivyokuwa lakini YESU anaweza, na wakati huu ni wakati wa Mwisho
na ninashukuru MUNGU yale yote niliyokuwa namtumikia shetani kipawa ambacho
MUNGU aliyaweka ndani yangu na shetani akakiwahi sasa kabla sijaanza kumtumikia
MUNGU sasa kimerudi na ninatumikia MUNGU na nimekuwa mtoto wa MUNGU na
ninawasihi watu wamrudie MUNGU na ninawasihi hata wale ambao wametumikishwa na
shetani kwa kujijua au kutokujijua
nawaambuiia waache wamrejee YESU, sababu YESU ni mzuri, na anaweza, sababu
wakiendelea kukaa huko watachomwa moto lakini wakimrejea YESU siku ya mwisho
wataenda mbinguni na pia nilikuwa nawafundisha baadhi ya watumishi ambao wako
huku duniani ambao wamtumikia shetani wengine wajijua na wengine hawajijui,
lakini nilikuwa hasa nawafundisha wale
waliokuwa wanajijua, jinsi ya kuhubiri, jinsi ya kunena kwa lugha, na pia jinsi
ya kufanya ishara na miujiza mingi
nilikuwa pia nahusika
Na kuna mtumishi mmoja
ambaye kule kuzimu ni rais mpaka sasa na
mimi mwenyewe nilikuwa ninashirikiana naye
na mimi mwenyewe nilikuwa raisi, na nilikuwa na hicho cheo kuanzia
nilivyoenda huko mpaka ile siku ambayo nilivyokuja kutolea lakini mpaka sasa
mtumishi huyo ambaye anajiita …. Hapo mwanzo aliitwa na MUNGU na baadae aliamwacha
MUNGU. Na kumtumikia shetani mpaka mimi nimeondoka kule yeye bado ni rais wa wa
kule lakini huku duniani anaonekana kwamba, ni mtumishi wa MUNGU na anaonekana
kwamba anafanya kazi ya MUNGU lakini kwenye ulimwengu wa roho ni kinyume bali
anatumikia shetani na anamtumikia shetani moja kwa moja anajitambua lakini ndio
hivyo tena ameamua kumtumikia shetani, na lakini hapa duniani anaonekana kwamba anamtumikia
MUNGU, watu wengi wanamkimbilia bila hata kujua lakini wakati MUNGU umefika
ISAYA: Huyo mtumishi nakumbuka alikuwa ni
pia alikuwa akikusafisha vyoo vyako, pia tulipokuwa kule chini, pia nakumbuka
alikuwa unampa adhabu mda mwingine alikuwa akienda kinyume na wewe, ulikuwa unampa
adhabu ya kudeki nyumba na kudeki vyoo na kusafisha viatu vyake kwa mate yake
Debora: Ndio
na pia alikuwa anakusaidia pia kubeba mabegi
mda mwingine alisimama badala ya yule mfanyakazi wako ambaye alikuwa
akikusaidia kubeba vitu zamani, ulipokuwa ukienda sehemu mbalimbali. Na huyo
mtumishi pia alikuwa ni mtumishi wa MUNGU kweli, alikuwa kweli anafanya kazi ya
MUNGU lakini ninaelewa historia ambayo ilimfanya mpaka akaacha kuifanya kazi ya
MUNGU
Kilichomfanya aache kazi ya
MUNGU …!!!!
Ndio maana hata kanisani
kwetu Mtume na Nabii Hebron huwa anasema
“Usipende sana kudadisidadisi sana vitu” sasa huyo mtumishi alikuwa
anadadisi dadisi mambo ya Mbinguni, na
kutaka kujua kuwa Mbinguni kukoje, kulikuwa kuna nini Mbinguni, wanaishi vipi, kwa
sababu unajua YESU akiwa amekuita anajua mwisho wako, kwamba utafanya kazi
yake, anajua kwamba utamsalitikwa wakati fulani anajua kama utaifanya kazi yake
mpaka mwisho akiwa kama anarudi.
Tazama wengi ambao walikuwa wameitwa na YESU
walikamatwa na shetani kwa sababu ya vitabia tabia Fulani Fulani tu, lakini ni
neema ya MUNGU siku ya leo tena ametuletea Mtume na Nabii ambae ni kwa ajili ya
kuturudisha Mbinguni tena, watoto wa MUNGu wote ambao tulikuwa tumepotea, hata
mimi na wewe.
Huyu mtumishi nakumbuka hiyo siku alikuwa
amekaa nyumbani kwake anajiuliza ni namna gani mbinguni kulivyo akawa anajipa
aidia (tathmini) yeye mwenyewe pasipo kuelezwa na Roho Matakatifu, na shetani
akamfuata hapo hapo kwa sura yake lakini shetani hakuwa na sura yake kabisa
kabisa, alimfuata kwa njia kama ya Malaika, akamwambia ee mtumishi wa MUNGU
nataka mimi nikuonyeshe jinsi kulivyo Mbinguni, asema bwana, unifuate mimi nami
nitakuonyesha jinsi njia ya Mbinguni
ilivyo, Yule Mtumishi kwa kuwa tayari alikuwa amekwishatekwa na shetani ufahamu
wake, mda ule ule na kwa kuwa shetani
alikuwa amekwisha mtumia, akakubali shetani akamshika mkono akapotea akaondoka nae
pasipo kuelewa kimiujiza miujiza tu na hiyo siku familia yake ilikuwa inamtafuta
lakini kikainuka kigezo kwamba sipo nipo hoo! Akapiga simu niko mjini nimekuja (akajutetea)
kutafuta vitu gani kwa ajili ya kazi ya Bwana, alivyo kuwa amefikishwa kwenye lango
la kuzimu shetani akamwacha hapo juu yeye akapotea (shetani) kisha akatokea
Malaika mmoja kule kuzimu akamweka muhuri wa moto ambao huo muhuri ukipigwa
wewe hata ufanye nini hata iwe vipi ni kwamba tayari MUNGU hatakujua.
Shetani ndio atakaye kutumia
sasasawa na vile atakavyotaka yeye mwenyewe baada ya hapo, MUNGU Hakuongea
maneno mengi ila alisema kwamba mia sita sitini na sita (666) maana yake ni
kwamba mimi tayari nimeshamchukua huyu
mtumishi sio wako tena ni mwanangu wa pekee ninayependezwa naye, YESU akamwacha kwanzia hiyo siku akenda na
baada ya hapo kitu kilichofuata juu yake
kilikuwa ni kipigo
Isaya: Sijui kama unakumbuaka??
Debora: Ndio, Nakumbuka
Debora: Ndio, Nakumbuka
Kilikuwa ni kichapo maana
alipewa kipigo hicho na shetani mwenyewe, na unaambiwa kipigo cha shetani
mwenyewe, na unaambiawa kipigo cha shetani ehhh kama unampiga kwa jiwe, siku
ambayo shetani atakupiga na jiwe lake rafiki yangu, utasuuzika na roho yako.
Alivyokuwa anapigwa na shetani ndivyo hivyo,
shetani akampa majukumu yake pamoja alikuwa
na jukumu mmoja wapo la kuwa mfanyakazi wa Debora ambaye zamani alikuwa anaitwa
Wariambora, kazi ali zokuwa akizifanya ndizo hizo alikuwa ni makamu wa Rais wa
ambaye nilikuwa naye kuzimu hapa lakini kwa sasa tunamshukuru MUNGU kwa kuwa
hatupo tena.
Na pia huyo mtumishi
anajulikana sana hapa Tanzania, kwa cheo chake alichonacho anajulikana kama
mwalimu, mpaka leo, hii watu wanajua kuwa bado ni mtumishi, lakini sio Mtumishiwa MUNGU akisema kuna
mkutano watu huenda kujazana hapo kibao lakini pasipo wao kuelewa ni kwamba
wanaenda kuhudhuria kwenye mkutano wa mapepo na wana vyohudhuria kwenye ule mkutano, wa mapepo,
shetani anakuwa anawa nyanyulia bango lake, sababu bango moja la shetani ni
likubwa na akiliweka mbele za MUNGU ni kwamba wewe tayari MUNGU anakuhesabia
kuwa tayari ni muovu na umeshamwacha MUNGU umeshamfuata shetani na kwa hiyo unapokuwa
umeenda kwenye hiyo mikutano wake shetani ananyanyua bango kwa MUNGU anasema
Tazama MUNGU hawa wamekuja kwangu kwa hiyo hawa sio wako tena , labda iwepo
neema ya MUNGU akikuhitaji anakuja
kukuchukua tu yeye mwenyewe, Utakuta tayari umeshafuata njia yake ya kwenda Mbinguni na kwenda kwa mtumishi aliye sahihi kama
alivyo Mtume na Nabii Hebron.
Na pia yapo maisha ambayo
tulikuwa tukiyaishi, yako baadhi yake ambayo tumeyaelezea pia lakini tulikuwa
tunatembeleana, tulikuwa na sehemu nyingi za kwenda kutembelea tukiwa tunakula
, tukiwa tunapiga story za kupanga kazi za shetani.
Bwana YESU asifiwe!
Sasa nitakwenda kuwaelezea
ni jinsi gani tulikuwa tunatembeleana kwa ajili ya kupanga mipango ya kuendeleza kazi za shetani na pia
huku duniani tulisha wahi kwenda sehemu fulani, iko Dar es salaam
ISAYA: Sijui kama inakumbuka
DEBORA: Ndio nakumbuka
Tulienda
tukiwa peke yetu tulikuwa tunatokea nchi ya Uganda, tulivyotoka tulikuwa
tunadrive mpaka tulipofika Dar es salaam, kwa sababu mda mwingine pia tulikuwa
tunakuwa tuko kimwili, mda mwingine tunakuwa tunaingia kiroho, sasa hiyo siku
tulivyokuwa tumeenda kwenye hiyo hotel tulikuwa tumekaa, tulikaa kama nusu saa
kwa sababu tulikuwa hatukai sehemu moja kwa kipindi cha mda mrefu, tukivyotoka
katika hiyo sehemu,Nakumbuka tunasikia
watu wakawa wanasema sema Moses Kulola, Moses Kulola, Moses Kulola, mimi
nikamuliza mwenzangu hapa (Debora) unaelewa habari za huyu mtu anayeitwa Moses
Kulola? Akaniambia namfahamu ndio tulivyotoka hapo tukawa tunaendelea
kuwasikiliza watu waliokuwa wanataja jina la Moses Kulola, mimi nikashuka
kwenye gari, ndio nikauliza kuwa Moses Kulola anapatikana wapi? Pia nilikuwa
natafuta anapokaa ili niweze kufika kiwili pia wakanielekeza kanisa lake, mimi
nikaenda nilivyoenda pia nikatumia mbinu Fulani nikatumia mtumishi wa Moses
Kulola nikamwuliza huyo mzee anapatikana
sehemu gani, Maana nina shida kubwa
nataka nionane naye, kumbe kweli yule mtumishi akafikiri kweli nina shida kubwa
na kiu ya MUNGU kumbe walaa!!!!! Haikuwa hivyo, Akanionyesha sehemu ambayo
Moses Kulola anapatikana na pia nakumbuka siku ambayo nilienda kwa Moses Kulola
nilibahatika kuonana naye, ilikuwa ni Mwanza, nilivyoenda kukutana na Moses Kulola
Mwanza yupo mtoto wake ambaye pia nilimtumia kama kunipa kila kitu ambacho
kilikuwa kinaendelea kwa mda huo mahali ambapo Moses Kulola alikuwepo. Mtumishi
huyo wa Moses Kulola ndio ambaye pia alimwelekeza Mtume na Nabii Hebron kwa mara ya kwanza,
mahali ambapo Moses Kulola alikuwa
anapatikana.
Nilipofika
mahali pale mimi sikuingia ndani, yaani Moses Kulola alikuwa amekaa
sebuleni kwake lakini mimi sikuingia
sebleni kwake mahali alipokuwa amakaa, nilikaa sehemu moja nikawa namwangali,
tulivyotoka nikatoka nje nikaanza
kuongea na mwenzangu nikamwambia je huyu mtumishi unaonaje tukianza kumfuatilia
kuanzia sasa hivi …
Isaya: Unakumbuka jibu
ulilonipa? Akanimbia tupo tayari tuanza kazi sasa hivi,
Akaniambia tupo yayari
tuanze kazi sasa hivi!! Basi, tutakapotea
tu pale tukatokea kuzimu tulivyorudi, tukavaa nguo zetu za kijeshi tukavaa
silaha mbalimbali tukatokea tena duniani tukamfuata tena Moses Kulola, Kwa mda
huo tulipokuwa tunamfuata hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa anaona wala aliyekuwa
anaelewa kitu chochote kilichokuwa kinaendelea, kauli moja ambayo Moses Kulola
alisema, MUNGU mimi siongei lakini MUNGU shughulika na hao matakataka, Nikamuuliza
wewe mzee umetuita sisi matakataka, kwa kitu gani ulichonacho? ….. Kidogo ikashuka
nguvu ya MUNGU na alishuka Malaika Mkuu Mikael siku ile
Isaya: Debora unakumbuka??
Debora: Ndio
MikaEli alivyoshuka kwa
sababu tulikuwa na tabia moja kama tumeanzisha vita labda na serikali ya
mbinguni, tukiona labla wamekuja wengi wengi tunaanza kuwavuta kwa kukimbia,
tunakuwa tumejifanya kama vile tumeshindwa vita, tunakimbia tunawavuta
tunawavuta tukiona kuwa tunaona kuwa tumefikia sehemu ambayo tunaweza kupigana nao kisawasawa
tunasimama, Wakifika na wao kwa sababu
ni serikali ya mbinguni wana akili ya
Kiungu, wanaanza noa kupigana vita hapo
hapo pasipo kuuliza kitu chochote, hiyo
siku nakumbuka tukapigana mimi nikaotea kupigwa na rungu la mguu mmoja nilivyopingwa na rungu la mguu mmoja, huyu mwenzangu
alikuwa na mishale yake aliyochukua ile
mishale yake akaipiga chini kwenye ardhi, ardhi ile ikalipuka ikatoa kitu kama moshi
sisi tukapotea
Na baada ya hapo Moses
Kuloka akasema bahati yenu naye akaanza kutufuatilia nyendo zetu, lakini tukamtumia
mtu mmoja ambaye alienda kumloga Moses Kulola Akamloga mguu, akawa anaumwa mguu
baada ya hapo, haikupita mda mrefu ndipo MUNGU akamwinua Mtume na Nabii Hebron.
Baada ya hapo, ndipo na sisi tukaanza
kutangaza vita na Mtume na kumbuka siku ile ambayo YESU alikuwa anamwita Mtume,
mimi nilikuwa nazunguka zunguka tu onyo, Nilikuwa zangu peke yangu, nilipokuwa natembea
tembea Nikawa nasikia hali Fulani ambayo YESU akiwa mahali popote hiyo hali unakuwa
unaisikia, nikasema mahali hapa patakuwa na jambo mimi nikasogea nikakuta mtume
na Nabii anaongea na YESU nilichokifanya
nilichukua kamera yangu, nilikuwa na kamera Fulani, nikapiga picha lile tukio
halafu nitarudi zangu kule kuzimu.
Kwanza nilisikia yale Maongezi halafu nilivyomaliza
nakashuka zangu kuzimu nikawaambia jamaa kuna mtumishi mmoja ambaye anaitwa naona
kama kweli atakubali wito huu shughuli
itakayotukuta sio ya kawaida, wakakubali wote.
Hiyo siku tukaitana kikao,
huyu mwenzangu alikuwa amesafiri baada ya hapo akawa amepigiwa simu, akaambiwa
aachana na huko sehemu unayooenda, itakubidi ugeuze. Alivyogeuza akawa
anarudia, tukakaa chini sehemu tunayokaa hiyo meza moja ni mfano wa Mkoa wa
Arusha wote ndio meza moja ya makutano makuu tukiwa tunafanyia kuzimu, tukakaa
hapo ile picha nikaiweka kati nikaikuza, nilivyoikuza ikawa ni kubwa hivyo
nikaiweka kati, kila mtu akawa anaiona, na kila mtu alitoa neno lake mwingine
anasema huyu tumpake mavi, mwingine anasema tumfanye hiki, mwingine anasema
tumrudishe nyuma, mwingine tumpige misumari, mwingine anasema hivi, Mimi nikanyanyuka
nikasema kwa kuwa tupo sisi wawili ambaye ni mimi pamoja na Wariambora ambaye
kwa sasa anaitwa Debora kazi hii tunawezakuifanya sisi wenyewe, lakini mwenzangu akasema hapana
katika hilo mimi naomba usinishirikishe kabisa kama wewe utakwenda nenda
mwenyewe mimi naomba uniache kinyangu nikamwambia basi kama wewe hutahitaji
kupewa cheo kingine na shetani au kupewa pesa na shetani basi acha mimi niende
nikajaribu bahati nilivyotoka hapo nikaanza kumfuatilia Mtume na Nabii lakini
kila nikijaribu kwenda nikirusha vitu
vyangu ili vijaribu kumpata , kipindi kile bado alikuwa bado anafanya kazi
Serengeti, alikuwa bado hajaanza kuifanya kazi ya MUNGU sawasawa, vingine
vilikuwa vinaingia lakini YESU alikuwa anachomoa, na vingine vilikuwa haviingii
wakati mwingine nilikuwa naambulia makofi vile vile na ni kitu cha kushangaza sana na pia mda mwingine nilipokuwa nataka kusogea
nilisikia Malaika wakiniambia wewe uliyekuwa unamfuataga Moses Kulola, tunaomba
usisogee mahali hapa utakufa lakini kwa sababu nilikuwa na ujasiri na nilikuwa
ni kiongozi wa ngazi ya tatu na nilikuwa mtu wa Karibu sana na shetani nilikuwa
sioni hasara yeyote nikawa nawaambia mna kitu gani nyie kama mnaweza kuniua
njooni, lakini wakisogea wakitaka kuanza kupigana na mimi nakimbia.
Naanza kuwapa mawasiliano wenzangu kuwa jamani
eeeh hali mbaya, tayari huku nawavuta ikifika mahali ambapo naona hapa naweza
ninajaribu kuwacontol, au kupiga nao, nasimama, hivyo hivyo naendelea kupigana
nao ikifika mahali nashindwa . mwenzangu anakuja ananisaidia ndivyo yaliilikuwa
hivyo maisha yetu.
Mda mwingine tulikuwa tunatoka tunaweza kwenda
kwenye nchi yoyote, tunaweza kutoka kuzimu tunaenda kwenye nchi yoyote tunakaa
kama wiki hivi, wiki mbili, ikiisha tunarudi zetu kuzimu kawaida.
Mwenzangu alikuwa na nyumba
yake,alikuwa na magari yake, alikuwa na ofisi yake, mimi pia nilikuwa na magari
yangu, nilikuwa na ofisi zangu na nilikuwa nina vitu vingi sana ambavyo, kama
tukitaka kuonana kule kuzimu labda kama kuna mtu anataka kwenda ofisini kwa
mwenzake, kwa shida Fulani au kwa ajili ya kufanya kitu fulani au shida fulani
ndio tulikuwa tunaenda na pia kupo mahali Fulani ambapo tulienda, ni hapa
duniani, nakumbuka ilikuwa ni nchi ya China:
Isaya: sijui unakumbuka
Debora: Nakumbuka
Isaya: ilikuwaje? Sijui mwenzangu labda anaweza
akaelezea safari yetu ilivyokuwa, mpaka
tulivyofika, kwa sababu China ndiko sehemu ambayo lango kuu la kuzimu lipo
hapo, katika sehemu fulani katika mlima
mkubwa sana katika nchi ya China tulikuwa tumetoka na tulikuwa na ndege yetu
moja. (Kwa sababu tulikuwa tuna ndege zetu kila mmoja alikuwa na ya kwake.)
tulivyotoka hapo tukafika katika hilo eneo pasipo watu kuelewa lakini tulienda
na tukaonekana kimwili lakini ndege haikuonekana kimwili labda kwa mtu mwenye
macho ya rohoni ambayo amepewa na MUNGU basi tukafika katika hiyo nchi
hatukukaa mda mda mrefu tulikaa kwa nusu saa tukazunguka zunguka tuliacha vitu
vyetu, na silaha zetu hapo, lakini
katika hiyo nchi kipindi hicho kulikuwa kuna mtumishi mmoja wa MUNGU ambaye
alikuwa anaitwa Kindaee
Isaya: Sijui nakumbuka!!!!
Debora: Namkumbuka
Tulipofika mahali hapo, tukakutana
nae, yule jamaa akaanza kutulipua sababu alishtuka tyari sisi ni kina
nani! Alivyoanza kutulipua sisi tukawa
tunamwamwalia, nikamgeukia na mwenzangu, nikamwambia huyu jamaa anaanza
kutafuta vita na sisi na sisi tuende nae kimwili, tukaanza kumfuatilia gari
lake alilokuwa anaendesha nae, jamaa na akapata wasiwasi nae akaanza kukimbia
ndio ile unakuwa mtumishi wa MUNGU bado huweki imani yako kwa MUNGU, kwamba
MUNGU anaweza kila kitu, sasa akaanza nay eye kutumia akili zake kimwili akawa
anakimbia na alivyokuwa anazidi kukimbia na sisi tukaanza kuongeza speed ya
gari ambayo tulikuwa tunaitumia ilikuwa aina ya
Range Sport, gari zetu nyingi ambazo tulikuwa tunapenda kuzitumia sana sana
zilikuwa ni range sport, sana sana ndizo tulikuwa tunapenda kuzitumia,hata huku
duniani ukiwa na Range anaonekana sana mtu mwenye hela, mtu tajiri.
Tulivyokuwa tunaendelea kungeza spidi ya gari,
tulivyokuwa tunamfuata jamaa tukamuotea sehemu, tukaenda tukaovateki gari yake,
akapata kihoro akaangukia sehemu nyingine kwenye mlima, huyo jamaa, sisi
tulivyomfuata tukampiga visu, tukamuua hapo hapo kimwili,
Isaya: sijui kama unakumbuka
Debora: Ndio nakumbuka
Baada ya hapo wale watu
wengine wakaenda kumfuata wakaenda kusema kifo chake kimetokana na ajali, na
baada ya hapo tukakamata roho yake, tukaichukua, tukaenda kuifanyisha kazi sisi
wenyewe, mpaka siku ya leo kazi ambayo anaifanya kule kuzimu ni kutawazisha
majini, wakiwa wametoka kujisaidia katika haja yoyote ile, kule chini.
Na pia, katika safari moja
ambayo ndio ilikuwa safari ya mwisho, ndio mwenzangu akapewa kazi ya kumuua
mama yake, kuna safari moja ambayo tulienda katika nchi ya Israel, tulikuwa
tumeenda katika kaburi ambalo watu walikuwa wanasema kuwa ni
kaburi la YESU, hiyo siku ambayo
tulikuwa tumeenda katika hiyo sehemu, tulivyofika tukaacha pale vitu vitu vyetu
kwa sababu hapakuwa na kitu chochote kile ambacho YESU alikuacha pale, YESU
alikuwa ameshatoka, baada ya kupaa kipindi kile alipokuwa na wanafunzi wake.
Tukaacha vitu vyetu pia,
tukakutana na mtumishi mmoja wa MUNGU, tulipokuwa kule Israel, hatukumbuki jina
lake, mimi simkumbuki kisawasawa
Isaya: Labda! Mwenzangu sijui kama unamlikumbuka
Debora: kwa sura ninamkumbuka lakini kwa jina silikumbuki,
Isaya: Na pia baada ya hapo sasa
tulivyokutana na huyo mtumishi, kwa sababu huyo mtumishi alikuwa na NGUVU za
ajabu , kiasi kwamba tusingeweza kupigana nae, ikabidi nimtafutie mwenzangu
njia namna ya yeye kurudi kule kuzimu, alafu mimi nione kama naweza kufanya
kitu chochote.
Na pia nataelezea kuwa ni
namna gani tulikuwa tunaweza kuwakamata watumishi, kuwafanyia kitu chochote,
kuwaangusha, au la kuwamaliza kabisa kutoa uhai wao. Ilikuwa inawezekana sisi
kufanya hicho kitu kwa sababu ya , unaweza ukute mtumishi mwingine bado imani
yake haijakaa sana kwa MUNGU, au anahofu au anajiuliza nitafanya kazi ya MUNGU, lakini kitu gani
kitakachoinuka kwa sababu kila ambaye ataitwa na MUNGU, kabisa kabisa kwanza
ataonyeshwa sura ya shetani, sasa hapo wengine, ile sura ya shetani, inakuwa
tayari amekwishapata hofu, akisikua sauti ya shetani yaani imani yao inaanza
kushuka, wapo watumishi wengine ambapo tulikuwa tunawaweza kwa tamaa, unaweza
kukuta mtumishi labda ameitwa na MUNGU lakini bado anakuwa na tamaa fulani, za
dunia dunia, ndipo na sisi tulikuwa tukipata mlango hapo hapo, tunafanya kitu
chochote ambacho tulikuwa tunakitaka.
Kama huyo mtumishi ambaye nilikuwa
nilimwuelezea kuwa tulimuua kwa ajali, huyo mtumishi kilichokuwa kinamsumbua ni
hofu, alikuwa anafanya kazi ya MUNGU
vizuri lakini akawa bado haamini kwamba MUNGU, yeye alichokuwa anakijua ni
kwamba MUNGU atasaidia kupigana na maadui zangu katika vita vya kiroho na
lakini vita vya kimwili lazima nitumie akili yangu, hapo ndipo tulipopata
mlango, ndipo shetani akamnyanyulia shitaka mbele za MUNGU, na MUNGU akakaa
pembeni, ndipo na sisi tukafanikiwa kufanya kile ambacho tulikuwa
tumekidhamiria. Na unapokuta kuwa mtumishi anaanguka, sio mtumishi anaanguka na kuacha kufanya kazi ya
MUNGU kama vile amependa, kipo kitu, ambacho kitakuwa kimesababisha mpaka
anaacha kufanya kazi ya MUNGU, kama hivyo nilivyosema ni imani, utakuta mtu
mwingine bado anayo hofu, hajiamini yaani, na hajamwamini sawasawa MUNGU ambaye
anakuwa amemwita.
Na pia wapo watumishi wa
MUNGU ambao wanafanya kazi ya MUNGU kweli lakini, kulingana na hao wengine
ambao yanafanya kazi za shetani, hawafanyi kama vile ambavyo MUNGU anataka nao
wakaiga, wakafanya mkumbo, wengine wakapotea na wengine, wanajijua na wengine
hawajijui.
Na pia nitaendelea pale
ambapo nilikutana na mtumishi huko Israel, ndipo ambapo nikaona kuwa huyu
mtumishi anakuwa na nguvu za MUNGU nyingi kuliko hata sisi ambao tunakuwa
tunafanya hizo kazi ya shetani, ndipo nikamtafutia mwenzangu mlango wa yeye
kutoka, kwa sababu mimi mda mwingine nilikuwa sitegemei sana silaha, nilikuwa
nategemea maneno, nilikuwa naweza kumjaribu mtumishi yeyote na kumpoteza kwa
maneno tu, basi huyo mtumishi nikaongea nae,
Isaya: Nikamuuliza je wewe kweli ni mtumishi
wa MUNGU akawa ananijibu!
Mtumishi: Ndio
Isaya: Nikamuuliza sasa umefuata nini
kwenye hili kaburi?
Mtumishi: Nimekuja hapa nimekuja kuomba
Isaya: Basi hapo ndipo nilipokuwa nimepata mlango, kwa
sababu kwenye kaburi lile la YESU hakuna kitu, YESU alikwisha kuzikwa tayari,
na tayari yuko zake kwa Baba yake Mbinguni, na tayari ameshapaa, pale inamaana hakuna kitu chochote.
Sasa yeye alipoenda inamaa pale
alienda kuabudu mizimu na kwenda kuabudu vitu vingine. Kwa sababu sehemu ambayo
shetani anakuwa amepakanyaga ina maana, ni mahali ambapo tayari shetani ana
uhalali napo, sasa sisi tulipoikanyaga hiyo sehemu nay eye akasema anaenda
kuomba ndipo mahali na mimi nilipomkamata,
Isaya:
Nikamuuliza yuko wapi Bwana
MUNGU wako ambaye alikuita uje kuifanya kazi yake?
Mtumishi: Akasema yuko mbinguni
Isaya: Nikamwambia kwa nini unakuja kuomba
katika kaburi?
Mtumishi: Akasema nimekuja kuomba kwa sababu
alishalala mtoto wake wa pekee!
Isaya:
Nikamwambia basi tayari nina
uhalali wa kukufanyia kitu chochote ninachotaka kuanzia sasa muite MUNGU wako.
Akaita
jina la YESU haikuwa, akaita mara ya pili haikuwa, akaita mara ya tatu,
haikuwa!!!
Isaya:
Nikamuuliza? Nikufanyie kitu
gani? Akaanzaa aa, yaani hapo tu kwa kumjaribu kwa hilo neno, akaniambia nisamehe. Basi ndipo na mimi nilipopata mlango, na mimi nikamuua
nikamchukua kabisa, nae pia nikashuka nae kuzimu kimwili, sikumfanyia kitu chochote,
tuliposhuka kuzimu, shetani akaanza, kumtandika, kwa sababu na yeye pia alikuwa anafanya kazi ya
kumpunguza nguvu shetani.
Alivyomaliza kumtandika
akamuua, mpaka na roho yake tayari ipo kule kuzimu.
Ninapenda kuwaambia kitu kwa
upande wa watu wale ambao mnapenda kwenda kuabudu na kusujudu katika lile
kaburi la YESU, ni kwamba pale hakuna kitu chochote, kama ni YESU ulikuwa ni
mwili wake tu ulikwisha kuwekwa pale, na tayari mwili wake umeshatoka kwanza
yeye yuko mbinguni, kwa hiyo kama wewe kweli una imani ya kumwabudu MUNGU, ina
maana unatakiwa umwabudu kwa imani kwa sababu yeye yuko mbinguni, na maombi yako yatakwenda mbinguni.
Unapokuwa unaenda pale ina
maana kwanza unaenda kuabudu mizimu kwanza, kwa sababu moja kati ya imani za
mizimu, ni mtu aende akaabudu kweny kaburi lao, unapoabudu kwenye kaburi lao
ina maana na tayari wewe umekwisha kufa, inamaana kwenye ulimwengu wa roho
umekwisha kufa pasipo wewe kujielewa na Imani yako inakuwa imekwisha kufa, sasa
mtu yeyote anayesema kuwa anaenda kuabudu, labla kwenda kuabudu katika kaburi
la mtu Fulani, au kaburi la mtumishi Fulani, huyo tayari anakuwa amekwisha
kupotea.
Lakini kwenda tu kutembelea
kama historia, kwenda kuangalia hilo kabuiri la YESU, sio mbaya ni vizuri kwa
sababu unakwenda kujifunza pia, vitu ambavyo, vilitokea hapo zamani, chanzo cha
kifo chake.
Lakini pia tukirudi kwenye neno
la MUNGU limesema kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU wako usiabudu miungu mingine,
wewe tayari ukishaenda kwenye hili kaburi, kualibudu, kulisujudu, ukisema
unashika mlango ambao Bwana YESU
alipopitishiwa, kushika mavazi ambayo YESU alifunikiwa, kwanza yale mavazi ya YESU yalishaondolewa,
yakawekwa mavazi ya mtu mmoja kule kuzimu,
ambaye alikuwa anaitwa Brian. Huyo Brian alikuwa mkuu wa uzinzi kwa hiyo
unavyooenda kushika lile vazi unaenda kushika uzinzi vilevile, ndipo unapotoka
pale unatoka na nuksi, balaa, lakini kama unaenda kuangalia kwa historia sio
mbaya, haikatazwi lakini ukienda pale kwa nia ya kwenda kuabudu, au kufanya
kitu kingine, kwa kweli unakuwa pia umeshaasi moja kati ya amri kumi za MUNGU,
Hebron: Bwana YESU asifiwe
Hebron: Hawa makomandoo ya shetani ya zamani,
bwana sasa ni watoto wa YESU, sasa ni watoto wa YESU wanamtumikia YESU.
Haleluya
Hebron: akamuuliza Isaya.Vipi Bwana
unamwambiaje shetani sasa?
Hebron: Mwageni kwa lugha yake ya kuzimu,
maana wako ambao wanasikiliza na wengine ni maajeti wake,
Hebron,
Isaya na Debora: haaaaaaaaa
wamecheka
Isaya: Crcomatau
makasi reotaimasctac reo matumarasctac marbata matao
Debora:
Shetani sikutaki na vitu vyako
vyote mimi ni wa YESU, nimetoka kwako, sina kitu chako chochote, mimi sasa hivi
ninamilikiwa na YESU
Isaya: Cicomasts trrcbccao maobata
Debora:
Unikome mimi sio wa kwako tena
Isaya:
Kcomastastams mastcbaco
Debora: Mimi
ni wa YESU peke yake
Hebron
na Debora: Amen, haleluya
Debora: Bwana YESU asifiwe, ninamshukuru MUNGU kwa kuwa sasa hivi
nimeokoka na ninampenda YESU, na pia nina wasihi wale ambao wamebakia kule, wako ambao wanajifahamu kabisa, ninawasihi
wamrudie MUNGU waache hayo ambayo wanayafanya maana yanamfaidisha shetani na
wala sio MUNGU,mimi nimeokoka na nampenda YESU na ninafurahia maisha ya wokovu.
Isaya:
Napenda kuwasihi watu wote
ulimwengu mzima, mataifa yote, makabila yote, rangi zote, mumrejee Bwana YESU,
mumrejee MUNGU, kwa maana kwake kuna kila kitu, kwake kuna raha, maisha ambayo
niliishi kuzimu na maisha ninayoishi nikiwa kwake kwa kipindi hiki, ni maisha
tofauti na sikuwahi kufikiri kuwa nitawahi kuishi maisha kama haya, kwa hiyo na
mimi nawasihi mmrudie MUNGU kwa sababu duniani hakuna kitu na nitawashangaa
sana wale ambao, wanaing’ang’ania dunia, kwa sababu sijui ni kitu gani ambacho
kitawafanya waing’ang’anie dunia, ninawasihi mrejee kwa YESU ndugu zangu wote,
ili siku ya mwisho tuende zetu Mbinguni tukamfurahie Bwana YESU.
Hebron:
Na mimi nakusihi ndugu mtazamaji
na msikilizaji, nchi yeyote mahali popote, nilipokuwa nikiongea na YESU, siku
moja alikuwa anatoa machozi, kwa ajili yako wewe na kwa ajili ya wengine hata
kwa ajili ya hawa ambao nimewatoa kuzimu, maana alikwisha kunipa habari zao,leo
hii wanamfurahia na wewe pia YESU anakutaka,
lakini tatizo haliko kwako, tatizo liko kwa watumishi ambao, wengi wao
wanawaongoza sala za toba kumbe ni waongo, wamewapumbaza watu, kuna watu wanalia,
wanamtafuta MUNGU lakini hawampati MUNGU wa kweli, hawapati injili ya kweli, injili
imekuwa ni biashara ambayo ni namna ambayo hata hawa walihusika kuharibu injili
hiyo na kwa wale waliokubali, wako watumishi wanaompenda mwenyezi MUNGU,
mumrejee mwenyezi MUNGU, nyie ambao mmeamua kumfuata shetani ninawaeleza mateso yanawasubiri sio ya kawaida. YESU
anarudi, Amerca najua mnateseka, Europe mnateseka, Africa mnateseka, India
mnateseka, Asia Mnateseka, mabara yote mnateseka, na nchi zote, lakini nina jambo
la kukwambia, nitakuja huko wakati wake
MUNGU ameshanituma.
Hbebron: Halelluya
Jiandae
wakati tutakapo onana utukufu wa MUNGU utakuwa kwako, na siku moja tutakwenda
mbinguni, hawa nimewatoa kuzimu mimi nawafahamu na mbinguni, wewe unasubiri
nini ni Mkristo lakini hutaki kuokaka unasubiri nini? Ili uwe Mkristo ni lazima
uokoe, usidanganyike na hizi injili eti hakuna kuokoka hao ni waongo nakuambia,
cha kwanza YESU ni mwokovu.
Bwana YESU asifiwe!
Hebu
jiulize! Wewe unakuwa Mkristo lakini
hujaokoka!
Simameni
imara watoto wa MUNGU, ninapokwenda kukuongoza sala ya toba rudi usigombane na
MUNGU, kama mpaka sasa hivi hujaokoka wewe umegombana na MUNGU, nachoona
wengine mmeshakwazwa katika maombi mnachajiwa pesa, haaaa hao ni waongo ni
majangili, nawaambia huyo sio YESU wa kweli.
Bwana YESU asifiwe!
Na wengine mmetoa mali mpaka mmefilisika,
mjiulize ni kwa nini mumtolee MUNGU mfilisike?
Ninakuambia dalili ya mvua ni mawingu, hayuko YESU hapo, ninakuambia
pokea injili ya YESU, zaidi ingia katika website ya www.prophethebron.org
ingia katika link ya blog utajifunza mengi, na MUNGU atakutengeneza, nakukaribisha
nikuongoze sala ya toba na siku moja tukae mbinguni tukae katika meza na Bwana
YESU,
Haleluya!
NA
KUANZIA SASA SEMA: Bwana YESU
naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua,
uniandike jina langu katika ufalme wako, siku moja YESU nitapata kuwepo na
wewe, ee YESU unilinde nisipotee. Amen.
Mbarikiwe
na MUNGU na MUNGU awatenge na maisha ya kuzimu siku zote za maisha yenu—Amen