Pages

Tuesday, July 21, 2015

USHUHUDA KUPITIA YOUTUBE: JINSI TULIVYOISHI  KUZIMU PART 2.

ISAYA: BWANA YESU ASIFIWE, karibu tena ndugu mtazamaji katika kipindi kingine  kutoka  katika kanisa la  YESU NI BWANA NA MWOKOZI  WA MATAIFA YOTE, siku ya leo nitakuambia na mimi niliyekuwa kiongozi wa ngazi ya tatu kutoka katika ufalme wa shetani lakini kwa sasa sipo tena huko nipo kwenye ufalme wa MUNGU namtukuza MUNGU , namshukuru sana

Siku ya leo tutakuja kuwaelezea pia nitakuwa na yule aliyekuwa ni mwalimu wangu wa kule kuzimu ambaye alikuwa akiitwa Wariambora lakini kwa sasa anaitwa Debora. Naye tutawaelezea siku ya leo kwa upande wa maisha ya kuzimu na vitu ambavyo shetani alivipanga kwa ajili ya, yani mbinu za shetani kwa ajili ya kupoteza wana wa MUNGU ni namna gain alizipanga, tutakuelezea pia pamoja na vitu vingine vingi vingi.. ili mwana wa MUNGU uzidi kufunguka, ili uifuate njia ambayo YESU anaitaka kwa maana  kanisa limekwisha kutekwa na shetani, na shetani analimiliki kanisa kwa hiyo utoke huko  ili uje kwa  YESU.
Nitamkaribisha pia ambaye alikuwa ni mwalimu wangu wa zamani na yeye aweze kuongea chochote kabla hatujaanza kufundisha.

DEBORA: BWANA YESU ASIFIWE, Haleluya ninawapenda wasikilizaji, watazamaji.. jina langu ninaitwa Debora hapo mwanzo nilikuwa naitwa Wariambora.

Ninamshukuru MUNGU kipekee kwa ajili ya siku ya leo kuweza kuwaletea maisha ya kuzimu, tutaendelea  kueleweshana  zaidi nini ambacho tulikuwa tunafanya, na mipango ya shetani aliyokuwa amepanga ili kuweza kuangamiza kanisa.

BWANA YESU ASIFIWE, nitamkaribisha Isaya aendelee.

ISAYA: BWANA YESU ASIFIWE, nitaanza kuwaelezea kwa upande wa mbinu ambazo shetani alizipanga ili azitumie kwa ajili ya kutesa wana wa MUNGU, BWANA YESU ASIFIWE,

DEBORA:  Amen,

ISAYA: Kwanza kabisa shetani alikuwa anajua kwamba MUNGU ameumba binadamu ili wote mwisho wamrudie MUNGU waende  Mbinguni. Na shetani alijua kwamba binadamu wote wanatakiwa kumrudia MUNGU mbinguni, kwa sababu nimejiwekea uadui na MUNGU, sasa na mimi ngoja nipoteze watoto wake nay eye pia siku ya mwisho apate hasara. BWANA YESU ASIFIWE,

DEBORA: Amen,

ISAYA:  Baadhi ya mbinu ambazo shetani alizipanga kwanza aliamua kuleta ubatizo wake, ambao pia Mtume na Nabii Hebron    huwa anaelezea. Moja wapo .. zipo aina nyingi za ubatizo lakini ukiangalia zote sio ubatizo ule MUNGU ameutaka, ubatizo ambao aliuleta Yohana na sio ubatizo ambao YESU mwenyewe alibatizwa kwa kupitia ubatizo huo.
Pili shetani akaingia makanisani akakamata watumishi, ijapokuwa wapo watumishi ambao waliamua kabisa kufuata kazi ya shetani
 Kabisa kuifanya pasipo kuitwa na MUNGU, wapo ambao waliitwa na MUNGU, lakini wakaachabnjia wakafuata na kuanza kufanya kazi ya shetani, na wapo ambao wao kwa kutokujua ni watumishi wa MUNGU lakini kwa kutokujua kwa kuiga wakaanza kufuata yale ambayo watumishi wa shetani wanayafanya. BWANA YESU ASIFIWE..

DEBORA: Amen,

ISAYA: Kwa kupitia ubatizo lengo ambalo shetani alileta ubatizo ni kwamba binadamu wote wasiende mbinguni, na pia aliplan kwamba akajua endapo watu wote hawataenda mbinguni inamaana ni watakuja kupata adhabu ya milele katika ziwa la moto na mimi huku kuzimu.

Kuzimu watu wamesikia sana kuna kuna kitu kinaitwa kuzimu, watu wametoa shuhuda kwenye maredio kwenye makanisa mbali mbali lakini kuzimu kazi yake ni kupoteza wana wa MUNGU wote wasimfuate MUNGU, wote wafuate njia ya shetani na yale yote  ambayo shetani anayataka.  BWANA YESU ASIFIWE..

DEBORA : Amen,

ISAYA: Lengo pia la shetani kuleta watumishi wake kwa ajili ya kuja kutangaza Injili ya uongo ni kwamba, mwana wa MUNGU, utakaposikiliza mafundisho yao, inamaana tayari umejitoa kwenye mikono ya MUNGU, na unakuwa umeshajisajili kwenye kitabu cha shetani na unakuwa umeshajisajili tayari kwenye ulimwengu wa shetani pasipo wewe mwenyewe kuelewa na pasipo wala wewe mwenyewe kufahamu kitu ambacho unafanyiwa au kitu ambacho kinaendelea wakati huo. Unaweza ukajiona upo mahali sahihi au kwa mtumishi sahihi ambaye anaongea kweli ya MUNGU anatenda miujiza mingi anatoa unabii anatabiri vitu vingi lakini mwisho wako unaweza ukawa unakuta ni kurudi kuzimu kwa sababu kwanza huwezi kujua kwa wakati huo huwezi kujua anafanya kazi ya nani anafanya kazi  ya MUNGU lakini anafanya kazi ya shetani.

Ninachotaka kuwaambia kwamba, siku hizi watumishi wengi sana wamekuwa ni watoto wa shetani na wale wa MUNGU wamebaki wachache kidogo  akiwepo na Mtume na Nabii Hebron, Moses Kulola ambaye kwa sasa hayupo tena hapa duniani yupo mbinguni kwa Baba yake amepumzika na pia shetani alifikiria ni namna gain anaweza akasababisha watu wasiifuate njia ya mbinguni waifuate njia yake ambayo yeye mwenyewe anaitaka ndio nilivyosema akaamua kuleta ubatizo wake akaleta watumishi wake hata akaleta biblia zake, vitabu vyake, akaleta vitu vyake tofauti, unaweza ukakuta mtumishi anakuwa mpaka anakurupuka anasema na mimi naanza kufanya kazi ya MUNGU bila yeye kuelewa anakuwa ni mtumishi wa shetani na anafanya kazi ya shetani na pia kwa upande wa mambo hay ohayo shetani ameyapanga kwa ajili ya kupoteza wana wa MUNGU, wasiende mbinguni zipo janja nyingi za shetani ambazo amekuwa akizitumia alivyokuwa anafikiria mpaka akafanya na kiukweli wanadamu wengi  sana wamepotea kwa kufuata mambo ya shetani kwa kujua au kutokujua kwa kupenda na kwa kutokupenda pia. BWANA YESU ASIFIWE..

Nitamkaribisha na aliyekuwa mwalimu wangu ili aweze kuendelea kidogo kwa upande huo, aweze kuendelea kasha nitawaeleza maisha ya  kuzimu. Karibu

DEBORA: BWANA YESU ASIFIWE,

ISAYA: Amen,

DEBORA: Aa nitaendelea kuelezea, BWANA YESU ASIFIWE, mwenzangu ameelezea habari ya ubatizo, na ni kweli watu wengi wamedaanganywa, wamebatizwa ubatizo wa kisima na hata mimi kivuli changu kilivyokuwepo hapa duniani pia kilikuwa kina hangaika huku na kule kupelekwa labda angalau kikibatizwa labda kitapona, kikabatizwa kwenye maji ya kisima na pia nilibatizwa kwenye maji siyo ya mtoni, ni ya ziwa. BWANA YESU ASIFIWE.. lakini pia hapo  haikusaidia. Ubatizo wa kweli ni ule ubatizo ambao unabatizwa   kwenye maji ambayo yanatirirka maji yautakaso. BWANA YESU ASIFIWE, na pia shetani aliiga ubatizo wa mbinguni  tunajua kwamba ubatizo wa kweli ni wa Yahana na pia BWANA YESU alibatizwa kwenye maji mengi  na maji ambayo ni mengi  yanayotembea sio maji yanayokaa tu yanatulia  wala sio maji yanayowekwa kwenye kisima. BWANA YESU ASIFIWE, na BWANA YESU alibatizwa pale ili kutuonyesha njia ya kweli ni ubatizo upi tunaotakiwa tubatizwe.

Lakini pia shetani nae aliiga ubatizo wa mbinguni unajua shetani naye alitupwa  alitoka mbinguni akatupwa moja kwa moja kuzimu, BWANA YESU ASIFIWE, na pia shetani naye aliiga, kule kuzimu pia kuna mto ambao unabatiza, BWANA YESU ASIFIWE, unabatiza mapepo, unabatiza watu ambao wanahitaji kupata vyeo mbalimbali,  BWANA YESU ASIFIWE,  hata mimi pia nilibatizwa kwenye ule ubatizo nilipokuwa bado mchanga. Nikisema mchanga inamaana kwamba tukumbuke kipindi kilichopita niliwaeleza kwamba nilienda kule nikiwa bado mchanga, nilipozaliwa tu nilienda kule lakini pia hata mwenzangu nay eye aliyekuwa akiitwa Max kwa sasa Isaya  naye pia alibatizwa ule ubatizo wa kule , na unapobatizwa huo ubatizo wa kule ndio pale ambapo unatumika na nguvu nyingi na wana wa MUNGU kusababisha wasiweze kubatizwa kwenye maji mengi waendelee tu kubatizwa kwenye maji ya kikombe na visima. BWANA YESU ASIFIWE, na ninamshukuru MUNGU kwa kuwa ule mto Baba yetu wa Kiroho alipoenda kule pamoja na jeshi la malaika ule mto uliweza kukaushwa.

ISAYA: BWANA YESU ASIFIWE, kama mlivyokuwa mmesikia amesema kwamba ubatizo pia upo ubatizo ambao ni wa shetani, lakini ameiga copy yake toka kwenye ubatizo wa mbinguni na ubatizo wa Yohana ambao YESU alibatizwa kupitia ubatizo huo.
Nitaelezea kuhusu huo mto ni kitu gani kinachokuwa kinaendelea.

Huo mto huwa watu wengi wanaotaka kufanya kazi ya shetani hata wale manabii wa uongo ambao huku wanaacti kama vile wanafanya kazi ya MUNGU, kumbe unashangaa mtu anatoa mapepo mara anatoa misumari, sijui anafanya nini kwenye mwili wa mtu.

Huo ubatizo unapoenda kubatizwa katika huo mto kule kuzimu kwanza unapewa  tayari utayari wa kufanya kazi ya shetani pasipo kujua, pasipo  kutafakari wala pasipo kujiuliza itakuwaje nitafanya nini. Ndio ujasiri ambao shetani anakuvika kupitia huo ubatizo.

Watu wengi wameenda kwa ajili ya kufanya kazi ya shetani kule kuzimu. Hauwezi kufanya kazi ya shetani pasipo kubatizwa kwanza katika huo mto.
Na unapobatizwa wanakuwepo watu wengi wanafanya sherehe nyingi uwe especially  mtu labda amepanga kabisa  toka kwenye moyo wake anataka kabisa kufanya kazi ya shetani. Ndio  unakuta anabatiwa katika huo ubatizo, anapangiwa  siku yake maalum, anakuwa anafanyiwa sherehe, na  vitu vingi ambavyo shetani atajisikia kumfanyia sababu amekubali kumtumikia shetani pasipo kujihoji wala kulazimishwa.

Na pia kazi ya MUNGU inafanywa na mtu ambaye yupo tayari amejikana na yupo tayari kwa ajili ya kuifanya kazi ya MUNGU.
Ndivyo shetani nae ameiga hivyo hivyo wana wa MUNGU ndio napenda kuwaambia kwamba mtu aliyeamua  kuifanya kazi ya shetani kwa kujikana na mtu ambaye yupo tayari kuifanya kazi ya shetani bila  kulazimishwa wala nini ndiye anyekuwa anabatizwa kwenye huo mto kwanza. Na pia anapokuwa  anabatizwa kwenye huo mto huku duniani  umebatizwa kwenye maji labda ya kisima ujue kabisa na kule kuzimu nafsi yako inakuwa imebatizwa kwenye ule mto wa shetani kule na mtu ambaye haitaji cheo chochote cha shetani wala hahitaji kufanya kazi ya shetani, lakini ukibatizwa katika mto maji ya kisima, maji ambayo ni mengi lakini hayatembei umebatizwa kwenye maji ya kikombe unatakiwa ujue kwenye ulimwengu war oho unabatizwa kwenye ule mto kule kuzimu. Na unapobatizwa kwenye huo mto ina maana unachukua nuksi, unachukua balaa, unachukua yani vitu vingi vya shetani ambavyo vitakusababishia wewe kutokuenda mbinguni unakwenda kuvikumba katika ule mto pasipo wewe kujielewa. BWANA YESU ASIFIWE.

DEBORA: Amen,   

ISAYA: Na pia huo mto umeigwa kutoka mbinguni kwa sababu shetani kama tunavyoelewa amekaa mbinguni ndio, lakini alipotaka kujifananisha na MUNGU na kutaka madaraka kama ya MUNGU akatolewa akarudishwa kuzimu. BWANA YESU ASIFIWE, unapokuwa unabatizwa kwenye maji mengi yale ambayo MUNGU anataka, unatakiwa ujue kwamba unabatizwa na mto wa mbinguni na unakuwa umepatanishwa na mto wa mbinguni. Lakini ukibatizwa kwenye maji ya kikombe,umebatizwa kwenye maji mengi ambayo hayatembei ujue kabisa umebatizwa katika ule mto wa kuzimu ambao ni kwamba ujue hata ufanye nini ujue MUNGU hawezi kukutaka, labda Neema yake MUNGU mwenyewe ameamua kukusaidia, ameamua kukutuma  ndio utatoka kule, lakini kwa akili zako kwa mtumishi ambaye hana nguvu za MUNGU, hawezi kukutoa kule kwa sababu pia mnakuwa mmejumuika wote na pia kwenye huo ubatizo wapo wengi wanaenda kwenye ubatizo huo wakiwa nai manabii wa uongo, wakiwa ni marais na watu wenye vyeo mbali mbali huku duniani wanaojulikana. Pia kwenye huo mto zipo siri. Unapoenda kubatizwa kwenye huo mto na huo mto ukishajua kwamba utakuja kukombolewa na MUNGU, utakuja kutoka kule ujue kwamba tayari utakufa katika ule mto, wala hautaishi duniani kwa muda mrefu kama ukienda katika mto ule ukienda kubatizwa halafu shetani akajua utakuwa ukipinduka pinduka huwezi kuifanya kazi yake kama anavyotaka, utalaanika katika ule mto na utakufa.

Kama vile tunavyojua ya kwamba, ukienda kinyume na  amri za MUNGU, MUNGU  anakuwa hana furaha na wewe, ndivyo ilivyo kule kuzimu ukienda kubatizwa kwenye huo mto shetani anakuwa hafurahishwi na wewe lakini akiwa hafurahishwi na wewe kitu ambacho atakufanyia rafiki yangu inamaana kitafuata ni mauti au kipigo au kitu chochote ambacho kitakufanya ujute ni kwa nini ulienda kumfuata shetani. BWANA YESU ASIFIWE,

DEBORA: Ameen,

ISAYA: Na pia watu wengi sana pasipo wao kuelewa walikuwa wakienda huko kubatizwa unajua shetani anauwezo wa kukuteka kama sio wewe kutaka  na pia shetani anaweza kukuteka kwa kutaka wewe mwenyewe ukaamua kuifanya kazi yake ndivyo shetani anapokuwa anakukontroli na kukumiliki yeye mwenyewe kwa mapenzi yake atakavyotaka. BWANA YESU ASIFIWE,

DEBORA:  Ameen,

ISAYA: Ukienda kubatizwa kwenye huo mto kama shetani amekuchukua kibabe, akakuteka yeye mwenyewe kwa kutaka halafu ukaenda kubatizwa kwenye huo mto wake, ina maana kwamba hata ukifanywa nini, hata huo mto ukakuvalisha nini, siku ya siku utakuja kutoka tu. Watu wote ambao  walitekwa na shetani kule kwa nguvu wakabatizwa kwenye huo mto, siku ya mwisho ni lazima watakuja kutoka. Siku ambayo MUNGU ameamua mwenyewe watakuja kutoka pasipo wale watu kujielewa.

Lakini wale waliokubali wenyewe na wakaamua kuifanya kazi ya shetani wenyewe na wakaenda kujipeleka kwa shetani wao wenyewe wakaenda kubatizwa katika ule mto kwa miguu yao na kwa vichwa vyao na kwa ufahamu wao, wenyewe na kwa akili zao, yaani hao MUNGU hataki awajue wala yani anakuwa hatamani hata kusikia majina yao. Lakini siku ya mwisho atakuja kuwaingiza katika adhabu katika ile adhabu ya moto ambao hata shetani atawekwa katika ule moto siku ya ya mwisho. Labda aendelee Debora, Debora unaweza kuendelea kuelezea kwa upande huo.

DEBORA:  BWANA YESU ASIFIWE, Haleluya.. namshukuru MUNGU kwa kuwa yeye ni mwema   ametutoa kule kwenye ule ubatizo,  na ninamshukuru MUNGU kwa kuwa ile chater ya ule ubatizo iliondolewa nilipoenda kubatizwa ndani ya Madhabahu ya YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Nilipoenda kubatizwa kwenye mto, kwenye maji tele yanayotembea. Na nina mshukuru MUNGU kwa kuwa aliyekuwa mwanafunzi wangu pia na yeye. Mimi nilitangulia kutoka lakini  ninamshukuru MUNGU na yeye pia ametoka, namshukuru MUNGU sasa tunafanya kazii ya MUNGU, tumeiacha kabisa kazi ya shetani, BWANA YESU ASIFIWE,

Na kingine kuna watu wengi wanabatizwa wanaambiwa wamebatizwa lakini ki ukweli hawajabatizwa, ninamshukuru MUNGU kwa kuwa maeneo mengi nilikopita kwenye ubatizo ilikuwa ni tofauti na nilivyokuja kubatizwa na mtumishi wa MUNGU, Mtume na Nabii Hebron, BWANA YESU ASIFIWE Na unapobatizwa kwenye ule mto kule kuzimu ina maana unaacha huko vitu vyako vyote unatoka box. Kwa hiyo wale watu waliobatizwa kule wanaojitambua na  nawasihi wamrudie MUNGU wabatizwe ubatizo wa kweli ili waweze kwenda mbinguni kwa sababu wakibakiwa na huo ubatizo hawataenda mbinguni bali watarudi kwenda kwenye kuendelea kufanya  kazi ya shetani sababu tayari wana chapa ya shetani. BWANA YESU ASIFIWE,

Na kuna watumishi wengi ambao wameenda kule wakabatizwa ubatizo wa lakini hapa duniani wanaonekana ni watu wakubwa  watu wenye vyeo na wanapokuja huku duniani sasa  kuanza kazi ya mungu wanakuja na nguvu ya kuwapofusha wana wa MUNGU fahamu zao ili wasiwaelewe na kingine sasa YESU amerudi wataendelea kuaibika kwa sababu hawaifanyi kazi ya  MUNGU ipasavyo bali wanafanya kazi ya shetani, wanaenda kinyume. Lakini ninamshukuru MUNGU kwa kuwa amemuinua mtumishi wake Nabii Hebron, na ataendelea kuusema ukweli ili wana wa MUNGU waweze kumrudia MUNGU na waweze kutoka kwenye hayo maji ya ule mto wa kuzimu kwa sababu kazi ya ule mto wa kuzimu ni kuhakikisha wana wa MUNGU, hawaendi mbinguni na kuhakikisha wana wa MUNGU hawasongi mbele mana ukishabatizwa kwenye ule ubatizo hutamuelewa MUNGU. BWANA YESU ASIFIWE, ile nguvu ya ule ubatizo inakuzuia wewe kumjua MUNGU,na inakuzuia wewe hata kwa mfano ukija kuokoka inakufanya mtu wewe uweze kushuka na baadae uache kumtumikia MUNGU na uache wokovu na uendelee kumtumikia shetani.

BWANA YESU ASIFIWE, ndio maana unakuta watu wengi wanabatizwa lakini baada ya muda wanaona wokovu hauwasaidii chochote, ni kwa sababu kwenye ulimwengu war oho, wana ile chatter, BWANA YESU ASIFIWE, kwa hiyo ambaye umeokoka mara nyingine unaanguka unatenda dhambi ujue kwamba kwenye ulimwengu war oho una ile chater ya ule mto wa kule kuzimu. BWANA YESU ASIFIWE, na watu wengi ambao wamebatizwa ubatizo wa kikombe pia wameunganishwa na ule mto wa kule kuzimu japo kuwa inakuwa ni kinyume na inakuwa ni ubatizo wa kikombe lakini wanakuwa tayari kwenye ulimwengu war oho wameunganishwa na ule mto wa kule kuzimu kwa hiyo wewe ambaye umebatizwa kwenye maji ya kikombe wewe ambaye umebatizwa kwenye maji ya kisima, wewe ambaye umebatizwa mfano tu kwenye bahari, au umebatizwa kwenye dimbwi tu hivi ujue tu umepotea mwana wa MUNGU, urejee ili uweze kubatizwa upya na uweze kuendelea na maisha ya wokovu na baadaye MUNGU akipenda kukuchukua uweze kwenda mbinguni. BWANA YESU ASIFIWE,

Lakini kubakiwa na ule ubatizo kweli nakuambia kwamba maisha yako ni bure, maisha yako ni ya kuzimu. BWANA YESU ASIFIWE.

NABII HEBRON: BWANA YESU ASIFIWE, ahaa..na mimi ningependa kuelezea kuhusu huo mto zaidi ufuatilie kwenye masomo na vitabu nimeviandika na vitakusaidia kuuelewa ukweli maana unapoelewa ukweli ni unamuelewa MUNGU, BWANA YESU ASIFIWE.

Jambo moja napenda kukuambia kwamba wewe msikilizaji ubatizo wa Yohana, Yohana alitoka mbinguni, na mbinguni kuna mto wa ubatizo ambao kwenye Biblia haupo, ndio mana unasikia Yohana alileta ubatizo wa mbinguni, sasa ulishawahi kufikiri wa mbinguni kivipi!  Lakini hayo ni mambo ya mbinguni ninakueleza na wale wote wanaobatizwa kwenye mto kama vile BWANA YESU anavyotaka wanaunganishwa naule mto wa mbinguni, lakini tutarudi sasa, kwenye huu mto ambao na mimi niliukuta kuzimu nilishangaa sana, BWANA YESU ASIFIWE, ule mto hapa duniani unapobatizwa kinyume unakuwa unaunganishwa na ule mto wa kuzimu ambao kazi yake ni kudhoofisha, kuharibu maisha yako, halafu unakuwa mjinga unajiona wewe ni mkristo kumbe ni Taahira mbele za MUNGU.

BWANA YESU asifiwe na makanisa mengi yamepigwa upofu na shetani akaingia namna hiyo MUNGU amekuwa akiinua watumishi ili waseme siri hizi miaka nenda miaka rudi, watumishi wanageukana wenyewe wanaungana na shetani wanamuasi MUNGU na kumkataa. Mwenyezi MUNGU amenituma kwako wewe, BWANA YESU ASIFIWE,  sawa sawa alivyoniambia nenda ukawabatize mataifa wote wawe huru, wawe wanafunzi wangu. Sasa ubatizo unaobatizwa kwa maji mengi ni ule unaounganishwa na BWANA YESU sio wa kisima, ukiwa wa kisima tayari umeunganishwa na ule, upo ubatizo wa wokovu wa kuzimu ambao umewekwa kinamna namna BWANA YESU ASIFIWE, ninataka nikuweke sawa maana unapobatizwa, ubatizo tofauti na wa BWANA YESU, unakuwa sio ubatizo tena na wewe unakuwa mwanafunzi wa shetani pasipo kujua, au unajua lakini wale manabii wa uongo wanajua wale wachawi washirikina wanajua maana, katika ule ubatizo wanaenda kuwekewa vitu, kule ambavyo wanakuja kusambaza huku duniani, na hao sasa wanauendeleza huku ili kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa shetani iwe wanafanya watu kuwa wanafunzi wa shetani iwe wanajua au hawajui BWANA YESU ASIFIWE,  nataka unielewe.

Na unapoona watu wamebatizwa ule ubatizo hata umwambiaje rafiki yangu ni bure hakubali kuokoka, ni mgumu kukubali kubatizwa ndio maana ninakuambia na wewe hapo ndio maana mpaka sasa hivi baadhi yenu hamtaki kubatizwa ubatizo wa maji mengi ili muwe huru, muwe wanafunzi wa YESU. Mkaridhika na ule ubatizo ambao unaunganishwa na mto wa kuzimu.

BWANA YESU ASIFIWE, ambapo hawa niliowatoa huko ni wanadamu ambao MUNGU aliowaumba na  MUNGU makusudi yake anayajua mwenyewe na kwenye Biblia mahali imeandikwa katika Ufunuo nitamtoa mwanadamu aliyekuwa ametekwa huko ili aje atoe siri za shetani ndio huyo Nabii Hebron alitumwa kwenda kumtoa huko kumchomoa yupo hapa sasa  ninakueleza ili vitu view vyepesi upate kuelewa makanisa sasa hivi wanabatiza kwa maji ya kikombe nawaambia hivi, nyie watoto wa MUNGU mmefanywa kuwa wanafunzi wa shetani, wanafunzi wa mpinga kristo. Ujue ukweli upate kuelewa uwe ni mtumishi ni askofu ni nani ukweli ndio huo. BWANA YESU ASIFIWE.

Kama hujui tubu uje nikubatize. Uje ubatizwe BWANA YESU ASIFIWE, ufanyike kuwa mwanafunzi wa YESU ili siku moja uende.
Ule ubatizo ndio umewashikilia na zaidi watu wametoa shuhuda kwa Hebron nimebatizwa tu nimekuwa mwepesi maisha yangu yamenyooka, ahaa!! Ule ubatizo wa kuzimu shetani akishakujua wewe ipo siku utaenda kwa MUNGU kwa hiyo atakuwekea mateso maisha yanaharibika ni mateso watu wanavifungo hawana mbele kwa nini?    Haujakuwa mwanafunzi wa YESU ni mwanafunzi wa shetani lakini haujui ni katika ulimwengu war oho. Njoo ubatizwe watu wengi nimewabatiza nimekupa ushuhuda maisha yao yamenyooka wanakuambia nimekuwa mwepesi lakini wewe kwa nini unamizigo upo bado umeketishwa katika ule mto. Sasa kwenye ulimwengu war oho, watu wanapobatizwa kama mimi ninavyobatiza kwenye mto wa maji mengi upo mto wa mbinguni ambao Yohana alitumwa kama mwanadamu maana kumuelewa  MUNGU ni vigumu. MUNGU yeye kwa ufahamu wake na uweza wake akaamua kumtumia mwanadamu, alimuonyesha kila kitu ili aje aseme maana sauti ya MUNGU ukiisikia una weza ukapasuka, au usimuelewe hata mimi aliponiita ilikuwa ni vigumu kumuelewa lakini hatua kwa hatua namuelewa hata nikisikia sauti namuelewa, MUNGU siri yangu mwenyewe alivyonifundisha. BWANA YESU ASIFIWE, na ujanja wote ili niweze kumpiga na kumpasua pasua sasa msidanganyike wana wa MUNGU.

Umebatizwa kwa maji ya kisima,  kwa jina la mchungaji, kwenye kikombe, kwenye dram wewe unaunganishwa na ule mto uliopo kuzimu. Wewe huoni ndio maana tunaenda katika roho, utazamishwa katika jina la Baba na Mwana… zaidi wakamuwahi motto mdogo sasa hao wanafanya kazi za shetani nawaambia ile siku ni kilio, ninawaambia ile siku ya mwisho watu watapigwa na mateso ambayo hawajawahi kuyapata na hao wengine wanaambiwa hakuna wokovu, BWANA YESU ASIFIWE, Biblia inasema sio wote wanaosema BWANA BWANA wataurithi uzima wa milele sasa wewe unafikiri ni watu wapi? Ni hao hao sasa ninakusihi umrejee..  BWANA YESU ASIFIWE, sasa nitamwachia coordinator aendelee aliyekuwa coordinator wa shetani BWANA YESU ASIFIWE, nimependa kuelezeakiufupi upate kuelewa. Haleluya..!

DEBORA: BWANA YESU ASIFIWE, nitaendelea kuelezea baada ya mwanadamu kubatizwa ni  nini ambacho kinaendelea baada ya ule ubatizo.

BWANA YESU ASIFIWE, aam..
Kipindi kilichopita nilieelezea kuwa nilikuwa nina nyumba, nitaelezea zile nyumba zilikuwa zina maana gani. BWANA YESU ASIFIWE, nilikuwa nina nyumba saba lakini zile nyumba saba lilikuwa ni agano la namba saba.

BWANA YESU ASIFIWE,  utakumbuka kwamba tulivyokuwa darasani tulifundishwa kuna namba shufa na namba tasa na ile namba saba, ilikuwa ni agano langu na shetani.

BWANA YESU ASIFIWE,lakini hakuna mwanadamu yeyote alijua bali ilikuwa ni mimi na shetani ambaye ni joka kuu na lusifa.BWANA YESU ASIFIWE, zile nyumba ambazo ni namba saba zinayo maana yake, BWANA YESU ASIFIWE, na ninamshukuru MUNGU kipekee kwa kuwa amenitoa huko nitaendelea kuelezea.

Zile namba saba ina maana mwanadamu, anapobatizwa baada ya ubatizo mtu anaombewa nguvu za Roho Mtakatifu soma katika kitabu cha Isaya utakuta kuna mahali pameandikwa kuna Roho saba za MUNGU. BWANA YESU ASIFIWE, kwa hiyo zile roho saba mwana wa MUNGU au aliyekubali kuokoka na kumpokea YESU na kubatizwa anapoombewa nguvu ya Roho Mtakatifu zile Roho saba zenyewe pia anaombewa zinakaa ndani yake. BWANA YESU asifiwe, ikiwepo moja wapo roho ya hekima, ikiwepo roho ya uweza, ikiwepo roho ya ushauri na nyinginezo. Ukisoma katika kitabu cha Isaya utakutana na huo mstari. BWANA YESU ASIFIWE.. kwa hiyo mimi nikakaa nikaunda nikisema kwamba nitawezaje kuwapa hawa watu wanaosema wameokoka ili wasiweze kusimama katika wokovu.

BWANA YESU ASIFIWE, na ndipo nilipokaa maana unapokuwa kule kuzimu unakuwa na ufahamu mkubwa sana wa kuweza kufikiri kitu na kuweza kubuni kila kitu na kikawa kama vile mtu anavyokaa na kuweza kufikiria na kusema kwamba naweza kufungua kampuni hii na inaweza kufanya kazi hii na hii..
BWANA ASIFIWE,
Ndivyo na mimi nilifanya, nilikaa nikasema okey hawa watu wanaokoka, na lengo langu au letu pamoja na mwenzangu, na wengine ambao tumewaacha kule pia na shetani mwenyewe lengo ilikuwa ni kuwafanya watu wasiweze kwenda mbinguni hata wakiokoka hata mmoja asiweze kwenda mbinguni.
BWANA YESU ASIFIWE,

Na ndipo nilipokaa nikapata wazo la kujenga hizo nyumba saba nilijenga nikiwa mtoto mdogo sana. BWANA YESU ASIFIWE, na ndipo nilipoanza kujenga zile nyumba nilikuwa na wafanyakazi mana kule kuna mapepo, nikiwa na wafanyakazi ambao ni wanadamu ambao wametekwa na shetani waliopo kule kuzimu kwa suala la kupata wajenzi ilikuwa sio shida. BWANA YESU ASIFIWE,
Na ndipo nilipobuni njia moja wapo ya kujenga kwa hivyo hizo nyumba saba nilizozijenga zilikuwa zimesimama badala ya zile roho saba za MUNGU. Mwanadamu anapookoka anazipokea anapoombewa zile roho saba zina kuwa ndani yake, ambazo ni roho ya maarifa na nyingine ambazo nimeshazitaja. Kwa hiyo kila nyumba ilisimama mfano nyumba ya kwanza ilisimama badala ya roho ya maarifa. BWANA YESU ASIFIWE!

 Kwa hiyo ndiyo maana unakuta mtu anaokoka anapookoka anakuwa mchangamfu sana katika kuomba katika kwenda kwenye mafundisho katika mkesha na katika kusoma neno, lakini baada ya muda unakuta mtu anakaa katika hali ya mazoea na anaweza tena kurudia dhambi au anakaa tu kama mtu aliyeokoka lakini hayatendi yale aliyoyapasa kuyatenda kama mtu aliyeokoka. BWANA YESU ASIFIWE!

Kwa hivyo zile nyumba nilivyozijenga kule na nikaandika kuna maneno Fulani niliyaandika kule katika ule mstari uliopo katika kitabu cha Isaya na lile neon likawa sio neno ni andiko nikawa nimelizika kule kwenye ule msingi. BWANA YESU ASIFIWE, nikimaanisha kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kusimama kwenye wokovu, hata kama amemkiri YESU hata kama ameokoka. BWANA YESU ASIFIWE, na nyumba ya pili hivyo hivyo nikaandika roho ya uweza nikaandika zile namba zote mpaka zikafika namba saba nikapiga na muhuri. BWANA YESU ASIFIWE,
Na zile ambazo nilizijenge ambazo zilikuwa saba nilibuni kutoka kwenye biblia ya shetani mwenyewe.

BWANA YESU ASIFIWE, kwa hiyo nikaandika maneno pale niliyoyaandika nikazidi yale maneno pale nikimaanisha zile roho saba za MUNGU hakuna mwanadamu yeyote zitakaa ndani yake na hata akiombewa ndani yake baada ya muda ziweze kuondoka. BWANA YESU ASIFIWE, na ninamshukuru MUNGU zile nyumba zilibomolewa hazipo tena nay ale niliyoyazika kule yaliondolewa, ninamshukuru MUNGU, sasa hivi watu wapo huru. BWANA YESU ASIFIWE, lakini wewe ambaye utakubali kwendelea na shetani na ukakubali tena kwenda kushuka kule kuzimu, BWANA YESU ASIFIWE,utakutana na kibano kwa hiyo nawasihi wana wa MUNGU mumrudie MUNGU ili MUNGU aweze kuwa baba yenu. BWANA YESU ASIFIWE.

Nitamkaribisha mwenzangu naye aweze kuendelea.

ISAYA:  BWANA YESU ASIFIWE, nitaelezea kwa upande wa vitu ambavyo vinafanyika kule kama ni kampuni, kama  ni kiwanda au kama kitu chochote shetani anataka kukifanya. BWANA YESU ASIFIWE.

Nataka nikuambie kitu kimoja kila kitu shetani anachokifanya, manabii wa uongo wanachokifanya wachawi wanakifanya waganga wanakifanya pia kimetoka kwenye biblia ya shetani. BWANA YESU ASIFIWE, ambapo ile biblia ya shetani yeye shetani amecopy maneno yake ambayo yalikuwepo kwenye kitabu cha biblia ya MUNGU, ambayo tuifahamu kama biblia na maandiko matakatifu. BWANA YESU ASIFIWE, kitu chochote shetani anachokifanya pepo anachokifanya hajakitoa kwenye biblia ya MUNGU kwa sababu kwanza biblia ya MUNGU ni kitabu kitakatifu na ni kitabu cha moto ambacho ni MUNGU mwenyewe alikiandika aliwapa maelekezo watumishi wake wakiandike ili watoto wake waweze kujifunza yale yaliyo yakena waweze kuifuata njia yake. BWANA YESU ASIFIWE,  nina maana kwamba kitu chochote ambacho shetani anachotaka kukifanya hawezi kufanya kitu, hawezi kukufuatilia bila ya kuisoma biblia yake na kuangalia ni mstari gani ambao nikiutumia ni neon gani nikitumia ambalo linaendana na kitu anachotaka akufanyie, BWANA YESU ASIFIWE,

Kama anataka kuvuruga maisha yako atatafuta mstari wa jinsi ya kukufanya kama anataka usisonge mbele ataangalia mstari unaoendana sawa sawa na kufanya kitu ambacho anataka kukufanya wewe kwa jinsi anavyotaka yeye mwenyewe.

Pia imeelezwa nyumba saba ambazo ni sawa sawa na roho saba za MUNGU na shetani pia ana roho saba ambazo pia nilishakwisha zielezea na Mtume na Nabii, hizo roho ikiwa ni hekima , ina maana ni hekima ya shetani, siyo hekima ya ki MUNGU. Hekima ya shetani pasipo kugombana naye, pasipo pukurushani na watumishi wake, pasipo kukosana na kitu chochote. Ukisema kwamba Tii ina maana kwamba utatii kitu cha shetani chochote ukienda kinyume rafiki yangu unakufa na shetani anakufanya kitu chochote ambacho anataka yeye mwenyewe akufanyie kwa sababu kama tunavyoelewa kwamba ukitaka kwenda na MUNGU inabidi uende na MUNGU ukiachana na MUNGU kidogo shetani anakushughulikia.

Na pia shetani na yeye ndivyo hivyo hivyo ukiachana na  mambo ambayo yeye anataka, baba yake joka kuu na roho mchafu anakutandika vile vile. BWANA YESU ASIFIWE, na pia unapoona labda unafanya kitu Fulani lakini hakiendi kama vile unavyotaka wewe mwenyewe kiende unashangaa kinaenda kinyume na vile ambavyo wewe unataka kiende, BWANA YESU ASIFIWE, ina maana kwamba shetani alishaingia kwenye biblia yake akachunguza mstari wowote utakaoendana na kitu chochote anachotaka akufanyie.
Roho saba za shetani sio kama zile za MUNGU, yeye alicopy  maneno tu kwamba kuna hekima, kuna nini  ambayo yapo katika roho saba za MUNGU. Lakini sio roho saba za MUNGU. BWANA YESU ASIFIWE, ni maneno tu ameyaiba kutoka yale ya zile roho saba za MUNGU ambazo na yeye pia alipoziiba yale maneno akachukua yale maneno akaweka vitu vyake vyote, hivyo wewe mwanadamu unayetaka kufanya kazi ya shetani anakupatia hizo roho. BWANA asifiwe,

Unataka kufahamu wanazipandaje hizo roho ndani ya mtumishi au ndani ya mtu yeyote anayetaka   kufanya kazi ya shetani. BWANA YESU ASIFIWE, Mtu yeyote yule anayefanya kinyume na MUNGU, tayari ni mtumishi wa shetani kwenye ulimwengu war oho pasipo yeye mwenyewe kujielewa,  mtu yeyote anayekwenda kinyume na maagizo ya MUNGU tayari wewe ni mtumishi wa shetani pasipo wewe mwenyewe kujielewa katika ulimwengu war oho na pia nitawaelezea ni namna gani shetani anavyozipanda hizo roho zake ndani ya waana wa MUNGU na ndani ya watumishi ambao wamekubali kuenda naye na kuifanya kazi yake. Haleluya..

Kwanza kabisa mtu ambaye anataka kupandiwa hizo roho saba za shetani, maana siwezi kusema ni roho saba za MUNGU na kumsifia shetani, BWANA YESU ASIFIWE, kwanza kabisa unakuwa unanawishwa miguu, ina maana unavalishwa utayari wa kuifanya kazi ya shetani, BWANA YESU ASIFIWE, Watu wanaonawishwa miguu na shetani kule kuzimu sio muumini sio mganga sio nani lakini nimekwisha kueleza ukiwa kinyume na amri za MUNGU anavyotaka wewe ni mtumishi wa shetani kwenye ulimwengu wa
roho.

Sasa nitaelezea ni jinsi gani hao watumishi wa wa shetani wanavyopakwa hayo mafuta. Mtumishi wa shetani anayeoshwa miguu na shetani ni yule ambaye amesimama madhabahuni huku duniani anasema anaihubiri injili ya YESU, analihubiri neno la MUNGU lakini anamtukuza shetani na anayafanya yale ya shetani.
Kwanza kabisa ndio hiyo unakuwa unanawishwa miguu, pili wanakuwa wanavalishwa taji. Taji ambalo ukivalishwa kule kuzimu na shetani, huku duniani ni kama mlima mkubwa hapa duniani ndio unakuwa umevalishwa hilo taji.

Na pia wanakuwa wanapewa biblia ya shetani ambayo tulishaelezea kuwa wanakuwa wanalala chini wanapigwa na ile biblia kichwani, BWANA YESU ASIFIWE, na pia wanakuwa wanapewa maji ya uzima na shetani.
Hayo maji ya uzima pasipo wao kuelewa kwamba ni maji ya mauti. Wao wenyewe wakienda kiroho kule na pia nafsi zao nafsi zao zinakamatwa na shetani anaingia agano kwamba ikifika wakati shetani anawataka zinasema Fulani niuwe, BWANA YESU ASIFIWE.

Na pia wanaanza sasa kupewa masharti ambayo shetani anayataka wao wayafuate, wakishapewa hayo masharti na wakiyatii ina maana kwamba tayari….

MTUME NA NABII HEBRON: BWANA YESU ASIFIWE, ninataka kuealezea hili jambo la maji, unasikia uzima huku duniani makanisani wanachota wanapewa, ndiyo maji hayo yanayo elezewa hapa. Kwa hiyo ndugu msikilizaji ninachokuambia, ukisikia kuna maji ya Baraka stuka! Mwenye akili na aelewe. Endelea ISAYA.

ISAYA: BWANA YESU ASIFIWE, na pia nitaenda kuwaelezea ni namna gani watu ambao wanataka kufanya kazi ya shetani ndio wanaopewa mamlaka ya kazi ya shetani na shetani mwenyewe, ndiye anayekuwa anawapa hiyo mamlaka. Kwanza kabisa ni lazima upite kwenye majaribu kama unataka kuifanya kazi ya shetani. Kama unavyoelewa kwamba ili uwe mtumishi wa MUNGU ni lazima pia upite kwenye majaribu, ili uwe mtu wa MUNGU lazima upitie majaribu. BWANA YESU ASIFIWE,

Shetani aliiga kama vile ilivyo mbinguni, ndio maana unaweza shangaa kwanza kabisa unaambiwa umtoe baba yako, mama yako, mtoe ndugu yako yeyote na shetani anapokuwa anakupa hilo jaribu tayari ameshakusoma ameshakuangalia anajua utaweza kufanya au hautaweza. Sasa anavyokupa hilo jaribu ukishindwa inamaana kama alikuambia uwa baba yako, mama yako, ukishindwa anakuua wewe mwenyewe pasipo wewe mwenyewe kutaka na kwa kutaka vile vile.

Labda kama ipo neema ya MUNGU, anapokuwa anakuambia ufanye kitu chochote, uue baba, uue mama, uue mtoto ufanye kitu chochote ambacho kitamfurahisa yeye mwenyewe, halitatimia hilo jambo lakini kama neema ya MUNGU haijakufikia na bado na wewe upo tayari kufanya kazi ya shetani ndivyo ilivyo utaanza kushangaa unaanza kutoa makafara, ndio unashangaa kama duniani hapa labda wapo watoto wanakuwa wanasababisha ajali mbali mbali zinatokea, mtu anavuka barabara gari linapinduka, mtu anafanya nini gari zina pinduka au ajali mbalimbali.

Labda nitaweza kuelezea, ulishakutana na ajali lakini hapo hapo hafi mtu hata mmoja ila damu, inakuwa imemwagika kwenye hiyo ajali, nataka nikueleze kwamba hicho ni kiapo cha damu shetani anakuwa anakitaka. Anasema mimi ninataka damu lakini asife mtu hata mmoja. Ikiwa inamaana umekosea inamaana anakuua wewe apo. BWANA YESU ASIFIWE, kwa hiyo msione hata hao watu wanaofanya kazi ya shetani nao pia wanapata shida vile vile lakini ni kwa vile shetani alishawapandikizia roho zake na alishawapandikizia mauti, ndio siri yake, ndiyo mtu anafanya kitu pasipo kutaka nao pia wanakuwa wanatumikishwa na shetani japo kuwa wanakuwa wanapenda na hata kutokupenda vile vile. Haleluya.

Na pia wapo watu wanaofanya kazi ya shetani, wapo wengi unaweza ukakuta labda mtu anaambiwa kule awe mke wa jini, awe mke wa shetani au unaweza ukashangaa mtu ni Nabii na ni mwanaume lakini kule kuzimu anakuwa ni mke wa jinni Fulani au pepo Fulani pasipo wewe kujielewa ina maana kwamba yule mtu kule anapokuwa ameolewa na shetani, kwanza kabisa, kama  ameolewa tayari kule kuzimu inamaana anatii masharti ya mume wake ambaye amekuwa amemuoa kule kuzimu kwa wakati ule.

Ndio unaweza kushangaa mtumishi huku duniani anajipaka paka mapoda anajichubua chubua ovyo ovyo pasipo kujielewa wewe mwana wa MUNGU, nataka nikupe siri hiyo uweze kuelewa. Ni kwamba anakuwa anaitii amri ya mumewake anachomwambia kule kuzimu, jichubue fanya nini vaa chupi za wanawake, vaa nguo za kike fanya nini huwezi kukataa. Lakini wa wa MUNGU mnaweza kusema mtumishi wetu anajipamba, anampendezesha MUNGU, halafu wanakuwa hawana adabu huku duniani wanakuja kuwaambia pendezeni wana wa MUNGU fanyeni nini lakini ni kwamba anakuwa anawachezea chezea akili ili ninyi wenyewe msijielewe na kama mtumishi akiwa huku duniani kama ameolewa na jini kule kuzimu, kwanza sio kama ameolewa atakaa tu atatulia kama vile duniani watu wanaokuwa wanaolewa.

Anaweza akaanza kufanya kazi za ajabu anaosha vyoo, anasafisha majini wakiwa wametoka kujisaidia anakuwa anakula mavitu ya ajabu ajabu, ambayo binadamu ukiletewa hautaweza hata kuangalia, unageuza shingo yako. Haleluya.

Na wapo watumishi wengi hata katika nchi ya Tanzania wapo wengi katika bara la Afrika bara la Asia, na nchi mbali mbali ambao unaweza ukakuta kwa mfano MUNGU amemwita Mtume na Nabii sasa hivi, lakini shetani anaanza kuwahubiria watu ambao wamekubali kufuata Neno la MUNGU la kweli kwa kanisa la mtume na Nabii Hebron. Unaweza ukaanza kushangaa hivi, ni mtumishi Fulani aliniambiaga kitu Fulani Fulani kikatokea. Ninachokuambia siku ya leo huyo unaweza kusema amenitabiria amenifanyia kitu gani na kimekuwa ni kwamba shetani anakuwa amempa story yako  wewe ambapo baadae atakuja kikakutokea. Ninachokuambia siku ya leo huyo mtumishi unaweza kusema amenitabiria amenifanya kitu gani na kimekuwa ni kwamba shetani anakuwa amempa story yako wewe ambapo baadae itakujakikutokee kila kitu utakachokuwa unakifanya atakuwa anamwambia yule mtumishi. Unashangaa anaanza kukuambia wewe ulizini, ulifanya nini ulitoa mimba ulifanya nini na nini pasipo wewe mwenyewe kujielewa ni mtumishi wa shetani, anakuwa ameshapewa kila kitu ulichokuwa unakifanya na shetani ndio kila  kitu ulichokuwa unakifanya kinyume na MUNGU shetani alishamuambia, sasa hapo utaanza kusema oho mtumishi wa MUNGU amesema kweli na mimi nimefunguka. Lakini ninachopenda kukuambia ndivyo ilivyo haifanyi kazi ya MUNGU ila anakuwa anamtukuza shetani. Ninaposema anamtukuza shetani anamtukuza vipi shetani?

Kwanza anapokuwa anakwenda kinyume na amri za MUNGU ina maana ameshamtukuza shetani amechangisha pesa kanisani amemtukuza shetani, akihubiri neno la uongo kwa wana wa MUNGU wala hafanyi ya kumpendeza MUNGU, ila anakuwa anamtukuza shetani anamtukuza vipi shetani?
Kwanza anapokuwa anakwenda kinyume na amri za MUNGU ina maana ameshamtukuza shetani amechangisha pesa kanisani amemtukuza shetani, akihubiri neon la uongo kwa wana wa MUNGU amemtukuza shetani. Na ndivyo ilivyo akiwa anahubiri maneno ya uongo na shetani anamuinua kule kwa kiwango  kingine kama leo nilivyosema mtu unaweza kukuta ameolewa na kama ameolewa mume na mume mmoja kivuko chake anachovushwa na shetani anapata mume mwingine, anaolewa na mwanaume mwingine kama alikuwa anafanya kazi kuwatawazisha watoto wa majini ataanza kutawazisha watu wazima kama alikuwa kazi yake ni kunywa mikojo itakuwa anakunywa mikojo ya majini wawili au watano kwa wiki au la kama alipangiwa kuua mtu mmoja kwa wiki atakuwa anaua watu wengi BWANA YESU ASIFIWE,

Lakini niachopenda kuwaambia wana wa MUNGU sipo mahali ambapo MUNGU anataka wewe uende hapo ila ni janja za shetani anakuvuruga tu ili na wewe uanze kwenda kwenye makanisa yao unasema ni mtumishi wa MUNGU na unasema tayari MUNGU amefanya sijui nini na nini lakini napenda kuwaambia MUNGU hayupo kwenye makanisa yao wala MUNGU hawatambui na wala MUNGU hataki wala hapendezwi na watu kama hao kwa sababu wanawapoteza wana wa MUNGU. BWANA YESU ASIFIWE.

Na sasa nitaenda kuwaelezea baadhi ya maisha ya kuzimu, BWANA YESU ASIFIWE, maisha ya kuzimu ni kama vile watu wanavyoishi hapa duniani.

MTUME NA NABII HEBRON: Ngoja nikuulize mlikuwa mnakula nini na nini na sahani zenu?

ISAYA: BWANA YESU ASIFIWE, sahani ya kuzimu ni kichwa cha mtu au fuvu la kichwa cha mtu.

MTUME NA NABII HEBRON: Kwa hiyo ulishakula kwa kutumia fuvu la kichwa cha mtu kama sahani?

ISAYA: Ndiyo.

MTUME NA NABII HEBRON: Na kijiko ilikuwa ni nini?

ISAYA:  Kijiko inakuwa ni mkono wa binadamu.

MTUME NA NABII HEBRON: Ndiyo umesema kweli. Na ulikuwa unakula chakula kiasi gani cha kuzimu kwa siku,

ISAYA: Aa, kule kuzimu kwa jinsi vile mtu anakuwa labda analimwili likubwa huku duniani labda ukiletewa chakula labda kilo moja huwezi kumaliza peke yako lakini kule kuzimu kwa ndani ya nusu saa mtu anakuwa anakula chakula kilo mia tano,

MTUME NA NABII HEBRON: Kilo mia tano? Kwa nusu saa?

ISAYA: Ndiyo kilo mia tano kwa nusu saa.

MTUME NA NABII HEBRON: Unakumbuka ulivyotolewa ulikuwa unapata shida ya kula sana, nini kilikuwa kinakusumbua? Ulikuwa unalamba lamba, lakini na kuona sasa hivi unafukia kweli.

ISAYA: Ni kwamba tayari nilishazoea kula vyakula vya kuzimu nilishazoea kuishi, kuishi ishi maisha ya kule yani, nikawa hata kula vyakula vya duniani naona kama mda mwingine nashangaa nakula kitu gani au ni kitu gani hichi nilicholetewa mbele yangu ndiyo mana nilikuwa siwezi.

MTUME NA NABII HEBRON: Aa sasa kile ulichokuwa unakula ulikuwa unakionaje kibaya au?

ISAYA: Vingi nilikuwa  naviona ni vibaya na vingine nilikuwa nikiletewa natamani hata kutapika

MTUME NA NABII HEBRON: Kama nini ulikuwa unataka kutapika nitajie unavyovikumbuka.

ISAYA: Vitu vingi vingi kama vile wali, ugali, machips haya nyama yani nilikuwa sipendi sipendi sana, maji majuice haya yani kitu ambacho nilikuwa nimejitahidi sana kula labda nimekunywa juice moja tena ya mtu ambaye naye alikuwa kuzimu kule ndiyo nilikuwa na kunywa.

MTUME NA NABII HEBRON: Ambaye alikuwa anakiwanda huko? Ndiye ulikuwa ukimuungisha?

ISAYA: Ndiyo.

MTUME NA NABII HEBRON: Pia hivyo ndivyo ilivyo hata hapa duniani viwanda vingi ni vya watu toka kuzimu na hata huyu alikuwa ni partner wake. BWANA YESU ASIFIWE,
Lakini ni wakati YESU sasa anarejea anawataka watoto wake warudi. Haleluya.. wewe unayehitaji urejee kwa BWANA YESU neema ipo bado. BWANA YESU ASIFIWE, wapo watu ambao shetani aliwaandaa kwa ajili ya kupoteza wana wa MUNGU. Vile vile kama hawa walivyoandaliwa kupoteza lakini hawa sasa waliwaandaa wengi sana na wengine wapo kuzimu huko, watakuja kwa wakati wake.  BWANA YESU ASIFIWE, mana MUNGU ni wa mipango ni wakati wa kuupindua ulimwengu watu wasifikiri labda itafanywa hivi, hapana, ni ufalme wa shetani kama hivi unavunjwa. BWANA YESU ASIFIWE,

Haya unaambiwa maji ya Baraka leo umeelewa. BWANA YESU ASIFIWE, utamkuta mwingine ana fimbo eehe muhubiri ana fimbo, inamaana yake, BWANA YESU ASIFIWE,  we unamuona kila anachoshika hapa ni copy ya kuzimu atatembea na mkuki ni copy ya kuzimu, mtumishi hutakiwi kushika mkuki wanadamu hawa sio maadui unawaua? BWANA YESU ASIFIWE, haleluya.
Embu endelea tena bwana,

ISAYA: BWANA YESU ASIFIWE, nitakwenda kuwaelezea sasa ni maisha gani ya kuzimu yalivyo ni namna gani maisha ya kuzimu yanaendeshwa na yanaendeshwaje? BWANA YESU ASIFIWE,

Kwanza kabisa maisha ya kuzimu huku duniani ikiwa ni dakika moja kule kuzimu tayari ni lisaa limoja. Duniani ikiwa ni wiki moja kule kuzimu ni mwaka mmoja. BWANA YESU ASIFIWE.
Lakini tofauti ya maisha ya kuzimu na maisha ya duniani ni kwamba huku duniani mnaishi binadamu wa kawaida, mnakula mnaabudu mnafanya vitu vingi vingi vya duniani.
Lakini maisha ya kuzimu kwanza kule ni ubabe ni kuendeshana, kitu unachokitaka usichokitaka kule ukiambiwa fanya lazima ufanye tu. BWANA YESU ASIFIWE,  lakini pia yapo majini yamewekwa kwa ajili ya kitengo cha ubabe tu kule kuendeshana. Unakuta labda mtu anakufuata kule kuzimu anakuambia mi nataka kitu Fulani ukikataa kumpa anaweza akakufanya kitu chochote kama ni kukupiga kama ni kukunyonga au kukuua.

Lakini namtukuza MUNGU kwa maana nimeshatoka kwenye hayo maisha maana kama ni ubabe mimi rafiki yangu, mimi hakuna mtu ananiambia kitu, kitu ambacho mimi nilikuwa nikikisema ndio hicho hakigeuki. Na pia maisha ya kuzimu kwanza kule hakunaga kitu kinachoitwaga mwanga. Kule ni usiku tu ni giza lakini huku duniani unaweza ukashangaa mtu anasema kule kuzimu nilikuwa nakaa asubui mchana na jioni, ni kwamba nawaambieni huyo mtu kwanza ni muongo.

Kule kuzimu hakunaga kitu kinachitwaga mchana wala mwanga hawaufahamu. Lakini ipo kitu inayoitwaga chemli ambayo Mtume na Nabii Hebron alishakwisha iongelea kuwa maana yake ni nini, ambayo ndiyo inayotumika kule kuzimu kama vile jua, kama vile taa ambazo binadamu mnaweka kwenye majumba yenu, mnaweka kwenye vitu vyenu mbali mbali kwa ajili ya kupata tu mwanga.

Na pia nitaelezea jua la kuzimu lipo vipi ambalo huwa linatoka kwa miaka sita linatoka mara moja tu, ambalo likitoka linatoka ndani ya dakika tano ambapo huku duniani ni sawa na miaka mitano ndio linatoka hilo jua.
Hilo jua sio kitu kikubwa wala sio kitu kidogo, nitataka kuelezea hilo jua huku duniani linakuja tu kwa ishara ni jinsi gani ilivyo lipo kama vile ni duara ambapo kwenye makanisa Fulani wanaitumia pia ni duara halafu inavikitu kitu kama vile vimstari kama vijiti vimechomekwa huko.
Hilo ndilo jua la kuzimu ndivyo lilivyo. Nadhani utakuwa umeshalifahamu wewe mwenyewe akili kichwani.

BWANA YESU ASIFIWE, lile jua linapokuwa linatoka ndio uzao wa shetani unazidi kuzaliwa, majini yanazaliwa, mapepo yanazaliwa, shetani anazidi kupata nguvu watumishi wa shetani wanainuliwa. Hilo jua mpaka wale watu waliopo kuzimu hua wanalipigia magoti wanaliomba litoke lakini wapi ndio kwa miaka sita, linatoka mara moja tu.
BWANA YESU ASIFIWE, lakini hilo jua linavyotoka wale mapepo yanavyozaliwa na shetani anapata nguvu ndio maana huku duniani wana wa MUNGU mnaendelea kupotea kama watumishi walikuwa elfu moja wanazidi tena mara elfu moja, jibu wewe mwenyewe unakuwa nalo kichwani unapata nini sawa sawa na ngapi.

Na pia kama huku duniani walikuwa wamefanya mfano kwa mtu mmoja ulikuwa unafanya dhambi labda kwa siku unazini mara moja lile jua linapochomoka huku duniani rafiki yangu unakuwa unazini hata kwa siku mara mia pasipo wewe mwenyewe kujielewa au kupenda, kama kwenye kile kitanda cha shetani ambacho nilishakielezea Altare, watumishi walikuwa wanazini mara moja watakuwa wanazini mara kumi  na moja pasipo wao wenyewe kutaka na kwa kutokupenda pia.
Lakini nitawaelezea pia wapo watumishi huku duniani wanapenda kwenda kuzini na majini kule kuzimu, ili mradi wazidi kupanda cheo kama vile huku duniani mtu unasikia unakihere here wewe, ndio kuzimu wapo hivyo hivyo. Wapo watumishi wanakuwa na kiherehere cha kwenda kufanya kazi ya shetani hii sasa ndio inakuwa ili wavushwe wanakwenda kuzini na mapepo na majini au nini. Na jinni mmoja kule kuzimu rafiki yangu ni kama likitu sijui likitu gani hapa duniani lilivyo likubwa.

Jicho moja la pepo wa kuzimu ni kama uwanja wa mpira lakini jiulize sasa mtumishi huku duniani jinsi mwili wake ulivyo na ninamna gani anakwenda kuzinishwa na lile pepo ni yeye anaenda kuzini na lile pepo kule kuzimu.
Sio anazini na mtu wala kitu cha namna gani ni makitu ya ajabu anayoenda kukutana nayo kule kuzimu.

Wapo watumishi wengine wanahubiri huku lakini muda mwingine akiwa anahubiri anasema nimechoka kufanya kazi yako shetani naomba uniache bila ninyi kuelewa mnashangaa anahubiri anasifu lakini anakuwa anamlalamikia shetani, lakini ndio MUNGU anakuwa hawataki kwa sababu walishakubali wao wenyewe kwa vichwa vyao kwa akili zao na kwa miguu yao wakaifuata njia ya shetani wakaenda kufanya mambo ya shetani.

Na pia maisha ya kuzimu kama ilivyo huku duniani watu wanaenda makanisani kwenye mafundisho na kule kuzimu ni hivyo hivyo.

Lakini kitu kimoja kule kuzimu hakunaga askari kule kuzimu hakunaga sijui katibu, sijui mbunge. Lakini wapo wabunge waliopo kule kuzimu kwa ajili kama ni nchi ya Tanzania kama tulivyokwisha elezea baadhi ya nchi ambazo zipo kule kuzimu.

Kama Tanzania na kule kuzimu pia kutakuwa na Tanzania sasa ile Tanzania ya kule kuzimu ndio huku unakuta kuna Raisi mbunge sijui kuna nani maaskofu maparokia sijui makitu gani ni watu wakubwa wakubwa tu hivyo hivyo kama ilivyo huku duniani.

Shetani aliiga duniani kama alivyoiga maisha ya mbinguni kama yalivyokuwa na akaweka malaika kuna malaika mkuu mikaeli, kuna malaika gabrieli kuna sijui wa sifa, kuna malaika wa mvua sijui kuna malaika wa nini..
Wapo yani mpaka biblia ya shetani akaweka ndivyo ilivyo na maisha ya kuzimu kama mnavyotembea binadamu na majini pia yanatembea kama binadamu ambavyo wanachelewa kurudi usiku mtu anatembea anazurura anarudi usiku, ndio binadamu maisha ya kuzimu yalivyo hivyo hivyo.

Labda nitamkaribisha na aliyekuwa coordinator wa kule kuzimu aendelee kuelezea maisha pia tulikuwa tukiyaishi kuzimu.

DEBORA: BWANA YESU ASIFIWE, nitapenda pia kuelezea kwa upande wa waimbaji. BWANA YESU ASIFIWE, haleluya..
Mnakumbuka kwamba kipindi kilichopita nilisema kwamba mimi mwenyewe pia nilikuwa mwalimu wa kwaya mbali mbali kwenye ulimwengu wa roho,  BWANA YESU ASIFIWE, na kuna baadhi ya waimbaji unakuta wanaimba wanasauti nzuri sana lakini baadhi yao wengi sauti hizo sio zao bali kuna kuwa na nguvu ya mapepo ya kuwasaidia kuimba. BWANA YESU ASIFIWE,

Na mimi mwenyewe ndiye niliyekuwa kiongozi nikishirikiana pamoja na mapepo ili waweze kuimba vizuri.
Na utashangaa wapo watu wanatabia za ajabu ajabu lakini wakiingia jukwaani wanaimba kwa sababu wanavyoimba vile wanavuvia watu ile nguvu yao ili wasiwaelewe unakuta wanawafunga fahamu zao unakuta watu wengi wanakimbilia pale.

Ujue unaposikiliza huo wimbo na ile roho tayari inakuingia. BWANA YESU ASIFIWE, na unaposikiliza vile nafsi yako na wewe inaunganishwa na zile nyimbo kwa hiyo unakuwa umeunganishwa moja kwa moja kuzimu na pia kuna watu mfano unakuta anaimba sauti nzuri nyororo ujue hapo hiyo sauti amefundishwa kutoka huko kuzimu. BWANA YESU ASIFIWE, lakini ninamshukuru MUNGU kwa kuwa sasa nimeacha hizo kazi na ninampenda YESU na nitaendelea kumuimbia MUNGU. BWANA YESU ASIFIWE,
Na pia kwa mfano utakuta watu wengine wamejiunga na freemason lakini unakuta pia ni waimbaji wanaimba nyimbo za injili lakini ujue kwamba hao sio waimbaji walioinuliwa na MUNGU bali kwenye ulimwengu war oho wameinuliwa na shetani ili waje kuharibu kazi ya MUNGU, BWANA YESU ASIFIWE, nitamkaribisha mwenzangu aweze kuendelea.

ISAYA: BWANA YESU ASIFIWE, nitakuelezea kwa mtu ambaye unakuta ni mwanaume lakini sauti yake anayoimba unaweza kusema labda ni mwanamke, halafu duniani mnavurugwa fahamu mnasema sauti ya kwanza, sauti ya pili sauti ya ngapi.. unakuta ni kwamba mtu anaenda kule kuzimu kwanza wanakuwa wanafanya kabisa practise,  BWANA YESU ASIFIWE, kama huku duniani mtumishi anakaa lakini kule anajifunza vile vile namna gani atakuja kuhubiri kama vile anavyoweza kulegeza sauti ili mtoe sadaka zenu anakaa kule kuzimu naye anafanya testing nanma gani atakuja kuongea. Unashangaa ni mwanaume sauti yake akiwa anaongea kawaida ana li bass lakini akianza kuhubiri habari za michango kisauti kinabadilika kinakuwa kidogo kidogo, haleluya, haleya.. ni ili mradi tu achukue pesa zenu. Ni kwamba ipo hivi, kwanza ukienda kule kuzimu, ipo kitu inakuwa kama vile ni chuma halafu katika ile chuma kuna kitu kinatembea pale kati kati kama vile karpet sauti yake inakuwa anakatwa koromelo lake kwanza anakatwa shingo, akishakatwa shingo, ile kichwa yake na shingo yake vinapitishwa pale kana kitu kimekaa pale kama vile upanga. Akishapita pale kichwa chake kinakatwa, kinabaki kichwa na shingo pale kuna kuwa na sehemu inaingia chini ikishaingia chini kuna maji unaenda kukutana nay ohayo maji  yana rangi ya blue, ambapo akishakutana na hayo maji, anaenda kuchukua sauti ya Yesebeli akisha toka kule sauti yake ikirudishwa duniani anakwenda kuunganishwa na sauti za umoja wa makahaba kule kuzimu.

Halafu ikija huku duniani ndio sasa nay eye anaanza kubadilisha sauti. Unashangaa mtu anabadilika kasauti, mara matendo yake yanakuwa kama vile motto wa kike, yani ni mambo mengi pasipo ninyi wenyewe kujielewa hata hao watu ambao wanakuwa wanaitwa huku duniani,  mnawaita mashoga ni kutokana na mbegu za uzao wao hao watumishi wanaojibadilisha sauti.  BWANA YESU ASIFIWE,

Na pia kwa upande wa hao waimbaji huku duniani, hivi nikuulize labda swali mwana wa MUNGU, inawezekanaje mtu huku duniani anavuta bangi anavuta madawa ya kulevya ni jambazi anasema mambo ya uongo ambayo siyo ya kweli ya MUNGU halafu anakaa chini eti ana muimbia MUNGU.
Anasema utamu wa YESU, anasema sijui nini mara nimemuona BWANA, sijui kitu gani ninachopenda kuwaambia wana wa MUNGU ni kwamba anakuwa kwanza anamtukuza shetani. Pia anakuwa hafanyi lile la MUNGU analolitaka.

Na katika mda unakuta mtumishi anaimba, anakatika kama vile sijui kitu gani mnaweza kusema ni Roho Mtakatifu kumbe ni roho mchafu anakuwa ameshaenda mahali pale, anakuwa anaimba yeye na pia ni yale mapepo yanakuwa yanaenda kucheza naye pale.
Mtu unaweza ukamshangaa labda mtu anaimba anaimba anafanya vitendo vya ajabu ajabu mara anakatika mara sijui nini ni kwamba anakuwa anamtukuza baba yake ambaye ni shetani mwana wa MUNGU, na pia ningependa kuwasihi vile vile hizo nyimbo pia haziwafai wewe mwana wa MUNGU ambaye umepata neema ya Wokovu, na pia unakuta huku duniani labda  mtu kwanza anaimba nyimbo za duniani, mtu yale manywele yake ameyaweka kajogoo kakubwa hivi, kama kitu gani sijui halafu akikaa naye unashangaa nay eye anamuimbia MUNGU anamuimbia YESU anamtukuza MUNGU. Ni MUNGU gani anaye mtukuza?

Napenda kuwaambia kwanza kule kuzimu wana miungu yao ambayo mtu akiwa anaimba huku anarap labda anaimba nyimbo za MUNGU anaimba eeeeeee!!! Ninachokuambia kwanza anasujudu yule mungu aliyeko kule kuzimu, pasipo ninyi kujielewa labda sijui mtu yani,

MTUME NA NABII HEBRON:  Kwa hiyo Isaya unaposema wanaporap mbinguni najua hakuna rap. Rap imeanzia wapi?

DEBORA NA ISAYA:   Kuzimu,

MTUME NA NABII HEBRON: Mkaifundisha, mkaileta Rap kwenye makanisa, na leo hii vijana wanajifanya ni nyimba za kisasa za kileo wana anza kurap. Embu hapo elezea ina maana gani?

ISAYA: Ina maana kwamba, akiwa anarap huku duniani ni kwamba kule kuzimu anakuwa anafanya ishara ya kuinama na kuinuka kwa ishara ya kwamba anakuwa akisujudu MUNGU wake.

MTUME NA NABII HEBRON: Unawaambiaje makanisani na waimbaji wanaoimba kurap sijui kucheza, shetani utafanya lelelele inamaana gani na makanisani wanawapenda kweli vijana.

ISAYA: Ni kwamba mimi ninapenda kuwaambia kwamba, kwanza kabisa yaani haitakiwi kuimba hivyo iwe unajijua haujijui kumbe kwa faida Fulani au kwa manufaa Fulani.
Ninachopenda kuwaambia haifai wala haitakiwi kabisa kuimba nyimbo za namna hiyo.

MTUME NA NABII HEBRON: BWANA YESU ASIFIWE, leo umejifunza mengi zaidi karibu katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE utakuwa huru. Ninachowaeleza, habari za miziki mimi huwa Rap halafu makanisani wanasema ni kizazi kipya, hicho ni kizazi kipya cha shetani nina waeleza. Hata nyie mnaoimba ni kizazi cha shetani kipya acheni kumchafua  MUNGU kumchezea BWANA YESU, mnamuinua mungu wa Rap kule kuzimu.

Mbinguni hakuna Rap, nyimbo zote za MUNGU ni za kisas hakuna za zamani. Unayetaka kupona upone uliyekuwa unaiga wacha! Hata kusikiliza hizo nyimbo nyumbani kwako, hapana ni balaa na mikosi mitupu, BWANA YESU ASIFIWE,
Lakini ninakusihi uokoke Neema ya YESU ipo najua umetenda mengi mabaya lakini YESU amenituma kwako na kwa wengine na kwa mataifa yote. Anataka umrejee nami nakuambia karibu mlango upo wazi bado haujafungwa. Neema yake ipo sasa usisubiri wakati wa usiku baada ya unyakuo mambo yatakuwa ni mabaya sana . BWANA YESU ASIFIWE,

Sema BWANA YESU ninaomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua, BWANA YESU ASIFIWE kuanzia sasa nishike mkono nisipotee tena.  Ninakushukuru kwa shuhuda na hayo yote yamenifungua.

Nami nakuombea uje uokoke, uje ubatizwe uje ukae na BWANA YESU umwambie shetani baibai na wewe unalo la kuwaambia wasikilizaji na watazamaji?

ISAYA: Sina kingine cha kuwaambia zaidi ya kusema MUNGU awabariki.

MTUME NA NABII HEBRON:  Na wewe?

DEBORA: MUNGU awabariki.

MTUME NA NABII HEBRON: Tutaonana muda mwingine karibu kanisani baiii


MWISHO.