Pages

Thursday, May 28, 2015

JINSI MKRISTO WA KWELI ANAVYOULIWA KIROHO PASIPO YEYE KUJUA!!!


BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote kwa jina la YESU wa kweli aliye ndiye mwana wa MUNGU aliye hai. Katika makala hii napenda kuwajulisha wakristo mliookoka na ambao mtaokoka leo hii kuwa shetani anazo njia nyingi za kuhakikisha wewe uliyeokoka unakufa kiroho, tena pasipo hata wewe kujua, mimi Hebron nilishafanyiwa hayo kabla ya kuitwa kumtumikia YESU peke yake. Nitaelezea kwa kifupi katika jambo la kuwekewa mikono kichwani na baadhi  ya watumishi waliomuasi YESU au ni manabii wa uwongo. 

Njia kubwa zaidi ni pale watu wanapowekewa mikono na watumishi wachawi, freemason, wasio safi au unapowekewa mikono na mtumishi ambaye yeye anachangisha  pesa kanisani, hiyo mikono yake inakuwa inayo laana ya uwizi na unapowekewa na wewe unanajisika na kudumaa, au unapowekewa mikono na watumishi ambao hawajabatizwa kama YESU ina maana roho iliyo ndani yao ipo kinyume na YESU japo watumishi wengine hawajui na wengine wanajua kabisa wanacho kifanya.

Ukiwekewa mikono na mtumishi anayekunywa pombe basi uelewe unapokea na wewe udhaifu alionao yeye anakupandia na wewe pasipo kujua hasa watoto wa kipaimara wanapandikizwa vitu vya ajabu, sababu katika biblia hakuna suala la kipaimara, ukiwekewa mikono na pastor anayezika biblia, kuzika majina ya waumini na vitu vyao, kubatiza watu kwa jina lake, kubatiza kwa kisima, kuabudu sanamu, kubatiza kwa udongo na mengineyo yote yaliyo kinyume na biblia basi uelewe unauwawa kiroho na usipo shituka itafika wakati unaishiwa hata nguvu za kuomba au kusoma neno au kukosa muelekeo, jichunguze hao  wanaokuwekea mikono wakoje?

Zaidi ingia katika website ya Nabii Hebron www.prophethebron.org  ingia katika link ya youtube na blog na usome kitabu cha Nabii Hebron JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI na MKRISTO USIKUBALI KUWA MPUMBAVU na vinginevyo utayakuta mengi ya kukusaidia na utapona roho yako na maisha yako, zaidi karibu sana katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Arusha Tanzania, nitakuombea na utafunguliwa matatizo yote yaliyokutesa na kuwa huru milele bila kuchajiwa malipo yeyote yale.

Sema BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, naomba unisafishe ufahamu wangu na kichwa changu pale ambapo niliwekewa mikono na watumishi au mtumishi ambaye ni wa uwongo akaninajisi ukristo wangu nikafa kiroho, naomba unifufue na uniongoze mahali ulipo wewe YESU wa kweli nisije nikauwawa tena kiroho. Amen

KARIBU SANA TANZANIA ARUSHA , YESU ATAKUBARIKI SANA.

NABII HEBRON.