JE NI MKRISTO WA JINSI GANI ALIYEPO KATIKA GIZA NA HAJIELEWI?
ATAJIJUAJE?
BWANA YESU ASIFIWE, kwa watu
wote wa mataifa yote, YESU anawapenda sana yeye aliye ndiye Nuru ya kweli. Siku moja
nilipokuwa naongea na YESU, aliniambia jambo moja lililoniogopesha sana sababu
hata mimi Hebron nilikuwa nimepigwa upofu kwa miaka mingi nikajiona nipo katika
nuru ya kristo sababu nilikuwa nasali katika kanisa la wokovu na zaidi hata
niliitwa kwa jina la biblia kumbe ilikuwa tumepigwa upofu bado tulikuwa katika
giza.
Giza ninaloelezea ni giza la
kiroho, mahali panapoenda kinyume na biblia ilivyoandikwa na kufuatwa maagizo
ya MUNGU, ila tulisoma biblia ila yaliletwa mengine kutoka nje ya biblia, sasa
wakristo wengi sana katika ulimwengu wote hawajijui wapo upande gani au uliopo
salama sababu ya kuyapokea mafundisho ya uwongo au mtu anaokoka halafu katika
kanisa hilo hilo wanaruhusiwa kunywa wine, pombe, nawaeleza wote mfanyao hivyo
hamjaokoka hata huyo kiongozi wa kanisa hilo ila anawapeleka watu kwa shetani
wala yeye siyo mtumishi wa MUNGU kabisa na kama yeye siyo mtumishi wa MUNGU
basi hata hao anaowaongoza na kuwatunza
kiroho anakuwa anamtunzia shetani hao watu wasiende mbinguni.
Hata kama wananena hizo lugha
ni fake ambazo pastor yeye ndiye anayewatupia mapepo hao waumini pasipo kujua
na waumini wananena kupitia roho mchafu na kuzidi kuwaangamiza kiroho kabisa.
Nitaelezea kwa ufupi ili watu mpone ambao mpo kwenye giza ila mnaona mpo salama
katika nuru ya YESU kumbe mpo kwa yesu wa uwongo.
a) Mkristo
aliyebatizwa kwa maji ya kikombe, kwa jina la pastor, kwa kisima.
b) Mkristo
ambaye hajaokoka mpaka sasa.
c) Unayesali
katika kanisa la michango na kufundishwa mambo tofauti na neno la MUNGU.
d) Kuabudu
sanamu.
e) Kumwabudu
mtumishi kama yeye ndiye MUNGU.
f) Kanisa
linalokataza watu wasiokoke halafu wanajiita wakristo, niajabu sana YESU yeye
alileta wokovu na ili uwe mkristo ni lazima uokoke na kubatizwa kama YESU kwa
maji mengi. Kimbia hapo upo katika giza hapo hakuna nuru.
g) Unapoongozwa
na mtumishi wa mishahara, waliojiita, wanajifanya hata MUNGU hawajui, hawa ni
wengi sana kazi yao ni kunyang’anya watu pesa zao ni kuwafilisi na wengine
baadhi yao mwanzoni walikuwa ni watumishi aliowaita YESU ila baadaye wakamuasi
YESU wakajiunga na yesu wa uwongo, ndiyo sababu mafundisho yao kachunguze
utaona ni pesa tu, michango na mengine
ya aibu.
h) Makanisa
yanayofungisha ndoa za kishoga.
i) Na watu
wote wasiomjua YESU.
NOTE:
Nawashauri tokeni katika giza mje kwa YESU wa kweli yeye
aliye Nuru ya kweli ndiyo sababu unashindwa hata kuomba, na hata ukiomba
haupati majibu na zaidi haukui kiroho unazidi kushuka na hata nguvu za MUNGU
zinakuishia unabakia kama boksi tu na ule mwisho hilo giza litakutangulia
kwenda na wewe, sasa rejea katika mwanga wa kweli ambaye ndiye mwanga na kweli
YESU wa Nazareti peke yake ni msema kweli na utakapomfuata na wewe utaokolewa
na huo mwanga wa shetani hatakuweza, mpaka hapo umeipata picha unajielewa kama
upo katika giza, sasa fanya maamuzi uokoke, na zaidi ingia katika website yangu
www.prophethebron.org uingie
katika link ya youtube na blog
utafunguliwa zaidi, yote yaliyopo ndani ni YESU peke yake ndiye kanieleza na
mimi Hebron nimewaandikia watu wote wa
mataifa yote mnapoyasoma mnafunguka zaidi na hupona roho yako na siku
moja mtafika mbinguni.
Sema BWANA
YESU, naomba uniokoe unitoe katika giza niwe mkristo wa kweli mwenye nuru,
unisamehe makosa yangu yote nimeujua ukweli kumbe nipo katika giza, natoka
katika giza nasirudi tena katika ukristo wa jinsi hiyo nakufuata wewe YESU
uniongoze sasa na roho wako mtakatifu.
Amen.
Zaidi
matatizo, magonjwa uliyonayo karibu sana katika kanisa la YESU NI BWANA NA
MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, ufunguliwe utaponywa utafufuliwa na kurejeshewa vitu
vyako na kubarikiwa.
NABII
HEBRON.